Wednesday, 03 November 2021 06:43

Kiswahili Activities Questions and Answers - CBC Grade 2 End of Term 2 Exam 2021 Set 1

Share via Whatsapp

KISWAHILI
GREDI YA 2
MTIHANI WA MWISHO WA MUHULA WA 2

Soma sentensi hizi.

 1. Maziwa ya pakiti ni tamu.
 2. Pendo anapenda peremende.
 3. Roda anaruka kwa kamba
 4. Chatu na chui walikuwa marafiki.
 5. Hii ni risiti

Andika kwa maneno au nambari.

 1. 25 _________________________________
 2. 18. __________________________________
 3.  Arubaini na saba. ____________________________
 4. Themanini na nane _______________________________

Jaza pengo ukitumia kimilikishi sahihi.

 1. Pete_________________ ni nzuri. (wake, zake,lake)
 2. Vyoo _________________ vitaoshwa. (vyenu, vyenyu,chemu)
 3. Tumbo ___________ linauma. (-ake)
 4. Meno _________ yameoza. (-angu)

Andika maneno haya vizuri.

 1. Mueli ______________________________________
 2. Kiha ________________________________________
 3. kulacha _____________________________________

Eleza watoto hawa wanafanya nini.

 1.    
  KisG2et221q17
  ____________________

 2.    
  KisG2et221q18
  ______________________
     
 3.   
  KisG2et221q19
  _______________________

 4.    
  KisG2et221q20
  ______________________

Jaza nafasi ukitumia vizuri au vibaya.

 1. Alifukuzwa ____________________ na ndugu zake
 2. Mwalimu aliwafundisha ________________ wakafurahia.

Jibu maamkuzi haya.

 1. Shikamoo __________________________________
 2. Hujambo _____________________________________
 3. Hamjambo ___________________________________

Taja haki mbili za watoto.

 1. ___________________________________________________
 2. ____________________________________________________

Taja majina ya vifaa hivi vya usafiri.

 1.   
  KisG2et221q28
  ___________________________
 2.    
  KisG2et221q29
  ___________________________
 3.   
  KisG2et221q30
  ___________________________

Akifisha sentensi zifuatazo ukizingatia herufi kubwa na ndogo.

 1. mwalimu mkuu anaitwa bwana kamau. ____________________________________________
 2. sisi huenda kanisani jumatatu. _____________________________________________________
 3. kenya ni nchi yenye amani. __________________________________________________________

Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.

Bwana Katama alikuwa tajiri sana. Alikuwa na shamba kubwa alilokuwa akipanda miti ya matunda kama vile miembe, michungwa na minanansi. Alikuwa akiyauza matunda hayo na kupata pesa. Siku moja maafisa wa polisi walimtambelea shambani.. Polisi hao walishangaa walipowaona watoto wadogo wa umri wa miaka kumi wakifanya kazi shambani mwake.

Maafisa hao walimkamata Bwana Katama na kumshtaki kwa kuwaajiri watoto wadogo ambo walifaa kuwa shuleni wakisoma. Watoto hao kumi na wawili, akiwemo Ndoro na Mbeyu walirudishwa shuleni na kuendelea na masomo yao.

Hivi leo Ndoro ni daktari wa meno, naye Mbeyu ni mwalimu mkuu wa shule ya upili ya Niache Nisome. Si haki ya watoto kuajiriwa hata kamwe.

Maswali.

 1. Ni nani aliyekuwa tajiri mkubwa? __________________________________
 2. Utajiri wa Bwana Katama ulitokana na ______________________________(biashara, ukulima)
 3. Watoto waliokuwa wakifanya kazi shambani walikuwa na umri gani? _____________________
 4. Ni nani aliyekuwa daktari ? _____________________________
 5. Ni akina nani waliomtembelea tajiri shambani? _______________________________
 6. Bwana Katama alikuwa akiuza nini? ________________________________
 7. Ni watoto wangapi waliokuwa wakifanya kazi huko shambani? _______________________

Taja watu watano wa familia.

 1. _________________________________
 2. ________________________________
 3. ________________________________
 4. ___________________________________
 5. __________________________________

Unda maneno ukitumia silabi ulizopewa.

 1. Ny _________________________________
 2. Pa. ________________________________
 3. Ki __________________________________
 4. Gh _______________________________
 5. Dh _________________________________

MAAKIZO

 1. , 2,3,4,5(Mwanafunzi anapaswa kusoma sentensi alizopewa kwa usahihi)

 1. Ishirini na tano
 2. kumi na nane
 3. 47
 4. 88
 5. yake
 6. vyenu
 7. lake
 8. yangu
 9. elimu
 10. haki
 11. chakula
 12. kukimbia/ anakimbia
 13. kusoma/anasoma
 14. kucheza mpira/wanacheza/ wanacheza mpira
 15. kuomba/ wanaomba
 16. vibaya
 17. vizuri
 18. marahaba
 19. sijambo
 20. hatujambo
 21. haki ya kusoma/ elimu
 22. haki ya kulishwa/ chakula/ ulinzi wa mwili
 23. gari moshi/ gari la moshi/ treni
 24. meli
 25. ndege
 26. Mwalimu mkuu anaitwa Bwana Kamau.
 27. Sisi huenda kanisani Jumatatu.
 28. Kenya ni nchi yenye amani.
 29. Bwana Katama
 30. ukulima
 31. kumi
 32. Ndoro
 33. Maafisa wa polisi
 34. matunda kama vile miembe, michungwa na minanasi
 35. kumi na wawili
 36. baba/ mama
 37. ndugu/dada
 38. babu/nyanya
 39. shangazi/mjomba
 40. binamu
 41. nyanya/nyumba/ nyoka/onya - sahihisha neno lolote lililo na silabi 'ny' mwanzo, mwisho au kati
 42. pa- papa/ panya/ paja/ lipa -sahihisha neno lolote lililo na silabi 'pa' mwanzo, mwisho au kati
 43. ki- kiti/kitanda/ haki -sahihisha neno lolote lililo na silabi 'ki' mwanzo, mwisho au kati
 44. Gh- ghorofa/ lugha/ ghafla - sahihisha neno lolote lililo na silabi 'gh' mwanzo, mwisho au kati
 45. Dh- dhana/ baadhi/ bidhaa/ nidhamu/ - sahihisha neno lolote lililo na silabi 'dh' mwanzo, mwisho au kati

Download Kiswahili Activities Questions and Answers - CBC Grade 2 End of Term 2 Exam 2021 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.