Thursday, 01 September 2022 08:56

Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 2 End Term 2 Exams 2022 SET 2

Share via Whatsapp

ASSESSMENT RUBRIC

Learning Areas  Score  Exceeds Expectations  Meets expectations  Approaches Expectations  Below Expectations
Kiswahili          

QUESTIONS

Kiswahili

ZOEZI LA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

  1. Jibu maswali mwalimu atakayokuuliza kwa kutamka. (Alama 5)
    1. Tambua vokali zote. 
    2. Wingi wa neno 'mkoba' ni nini? 
    3. Unda neno ukitumia silabi 'cha'.
    4. Taja haki mbili za watoto. e) Chombo cha usafiri kinachopitia kwenye reli ni gani?

ZOEZI LA 2: KUSOMA KWA SAUTI

  1. Soma kifungu hiki kwa sauti. (Alama 10
    Chakula cha nyumbani ni kitamu kuliko cha barabarani. Chakula cha nyumbani huhifadhiwa vizuri. Kila adhuhuri, mama huchemsha maji ya kunywa ya nyumbani. Yeye huyachuja vizuri. Chupa yetu ya chai daima hung'ara kama dhahabu. Mama hapendi tununue chakula cha barabarani. Yeye hutupikia chipsi na chapati. Tunampenda mama.

ZOEZI LA 3: SARUFI

  1. Panga herufi hizi vizuri ili kuunda salamu. (Alama 3)
    1. qamraabh - ....................................
    2. Jewambaa - ....................................
    3. ahirba - ....................................
  2. Jaza pengo kwa kutumia a, e, i, o, u. (Alama 3)
    1. b_ st__n_
    2. ch_ _
    3. m_kt_b_
  3. Tumia vyenu' 'wenu' ai 'zenu' kukamilisha sentensi. (Alama 5)
    1. Wanafunzi ................................... wanaimba vizuri.
    2. Bendera ................................... zinapendeza. 
    3. Vifutio ...................................vimeanguka sakafuni. 
    4. Walimu ...................................wameingia darasani. 
    5. Nyuso ................................... zinameremeta.
  4. Andika majina ya vyombo hivi vya usafiri. (Alama 5
    6 q
  5. Unda maneno yenye silabi au herufi zifuatazo. (Alama 4)
    1. ny - ..................................
    2. me  - ..................................
    3. da  - ..................................
    4. ng  - ..................................
    5. pi  - ..................................

ZOEZI LA 4: UFAHAMU

  1. Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo. (Alama 5)

Tulifunga shule baada ya kumaliza masomo ya muhuld mwezi wa Aprili. Wazazi wangu walinipeleka kwa ami yangu. Ami yangu anaishi mtaa wa Dhahabu. Mtaa wa Dhahabu uko mbali na mjini. Tulienda a kuabiri matatu kuelekea kwa ami.

Njiani niliona pikipiki, baiskeli magari madogo madogo na hata malori.

Hatimaye, tulifika katika kituo cha matatu cha Dhahabu. Ami yangu alikuwa Tayari kunipokea. Alifurahi sana kutuona Tulienda nyumbani kwake kwa tuktuk. Alikuwa ametuandalia chakula kitamu. Nampenda sana ami yangu.

  1. Ami aliishi wapi?
  2. Ilikuwa likizo ya mwezi gani?
  3. Njiani niliona magari, malori, pikipiki na 
  4. Mtaa wa Dhahabu uko mbali na
  5. Ami aliwapeleka nyumbani kwake kwa kutumia nini?

ZOEZI LA 5: KUANDIKA

  1. Andika sentensi kumi kuhusu. (Alama 10)

DARASA LETU

MWONGOZO WA KUSAHISHA

  1.                        
    1. a,e,i,o,u
    2. mikoba
    3. chama, chanjo (neno lolote sahihi)
    4.              
      • Haki ya kuishi
      • Haki ya kuendelezwa
      • Haki ya kulindwa
      • Haki ya kushiriki
      • Haki ya kutobaguliwa
    5. treni
  2. Anaposoma kifungu, mwanafunzi anapaswa kupangiwa daraja kulingana na;
    • Kasi ya kusoma
    • Utamshi wa maneno katika kifungu
    • Usahihi
  3.                
    1. marahaba
    2. waambaje
    3. habari
  4.               
    1. bustani
    2. muktaba
    3. chai, choo, chuo (jibu lingine lolote husika)
  5.                    
    1. wenu
    2. zenu
    3. vyenu
    4. wenu
    5. zenu
  6.                
    1. lori
    2. ndege
    3. meli
    4. tuktuk
    5. treni
  7. Pea alama jibu lolote husika
    1. nyayo, nyaya, nyama
    2. mende, meno, meza
    3. dada, dakika, damu
    4. ngombe, ngamia
    5. pika, picha, pindua
  8.       
    1. mtaa was Dhahabu
    2. Aprili
    3. baiskeli
    4. mjini
    5. tuktuk
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 2 End Term 2 Exams 2022 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.