Monday, 27 February 2023 12:09

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 Term 1 Opener Exams 2023 SET 3

Share via Whatsapp

Maagizo ya mwanafunzi

  1. Karatasi hii ina mazoezi matano.
  2. Jibu maswali yote kulingana na maagizo uliyopewa.

Jedwali la Alama

Zoezi  Kusikiliza na kuzungumza Kusoma kwa sauti ufahamu wa kusoma sarufi  kuandika
Upeo 10  25  10 
Alama za mwanafunzi          
Kiwango cha utendaji          


MASWALI

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu aulize maswali. Mwanafunzi ajibu kwa sauti.

  1. Bendera ya nchi yetu ina rangi ngapi?
    Mwanafunzi ajibu.
  2. Taja rangi moja inayopatikana kwenye bendera yetu.
    Mwanafunzi ajibu
  3. Taja siku ambazo bendera hupandishwa juu.
    Mwanafunzi ajibu
  4. Bendera inapopandishwa watu wanaimba wimbo upi?
    Mwanafunzi ajibu
  5. Taja majina ya raisi wa nchi ya Kenya.
    Mwanafunzi ajibu

KUSOMA KWA SAUTI
Soma hadithi ifiuatayo kwa sauti
Leo ni siku ya Jumapili. Tunajitayarisha kwenda kanisani na watu wa familia yangu. Nimevaa mavazi ya rangi ya samawati na shati jeupe. Nimevalia soksi za rangi nyeusi. Mama yangu anataka nivae viatu vyangu vipya. Baba ndiye alininulia viatu hivyo. Baba amevaa suruali ndefu na shati ambalo ni ya rangi sawa na yangu. Amejifunga tai shingoni. Mimi na baba tumevaa mavazi yanayofanana.
Mama amevaa rinda la rangi nyekundu. Yeye anapenda rangi nyekundu. Amevaa viatu vinavyomotamota. Anapendeza sana. Kila siku ya Jumapili sisi huhudhuria ibada kanisani. Huwa tunavaa mavazi yetu yanayopendeza.

UFAHAMU
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali.
Mimi ninaitwa paka. Mimi pakasipendi uchafuchafu hufanya umbo lisokote. Mimi hujifuta mikono kila mara. Sirambi kucha zangu ovyoovyo. Huwa nasafisha kucha zangu vizuri. Ninapenda usafi. Ninapotaka kujisaidia ninachimba shimo. Nikimaliza kujisaidia ninalifunika. Nina kazi nyingine muhimu sana kwa binadamu. Mimi hufukuza panya nyumbani. Panya huharibu nguo za binadamu na mahindi waliyovuna. Binadamu hunipatia maziwa kwa kazi yangu nzuri. Mimi hufurahia kazi hiyo.

Maswali

  1. Paka anapenda nini?
  2. Uchafu hufanya tumbo lifanye nini?
  3. Paka hufanya nini akitaka kwenda haja?
  4. Paka hufanyia nini kucha zake?
  5. Paka hapendi nini?

SARUFI

  1. Andika jibu sahihi.
    Ni vizuri.........................kila siku. (kuoga, kucheza)
    ......................hutuzuia kupata magonjwa. (Usafi, Uchafu)
    Watu hupangusa kamasi kwa..............................(taula, hancifu)
  2. Chagua jibu sahihi kujaza mapengo.
    [Mwili   Kuoga   mswaki   Kukatwa]
    Kila mtu anafaa kufanya usafi wa.....4.......Kila asubuhi ni vizuri ....5......Kupiga....6....huua wadudu kwenye meno. Kucha pia zinafaa ....7.....ili zibaki fupi kila wakati.
  3. Jaza nafasi kuunda maneno ya heshima
    P_I_
    _s_nt
    s_m_h_n_
    t_f_dh_
  4. Andika sentensi ukitumia picha hizi
    4 bag............................
    4 aiygdiua............................
  5. Jaza mapengo kwa kuchagua jibu sahihi.
    Salam aleikum..........................................(aleikum salaam, vizuri).
    Shikamoo..........................................(salama, marahaba).
  6. Kanusha vitendo hivi.
    Keti..................................
    Lia..................................
    Inuka.................................
  7. Andika maneno haya kwa herufi kubwa au ndogo.
    mwalimu - .................................
    DAKTARI - .................................

Andika sentensi tano kuhusu;
UMUHIMU WA MAJI



Majibu

UFAHAMU

  1. usafi
  2. lisokote
  3. ninachimba shimo
  4. safisha kucha zake vizuri
  5. uchafu

Sarufi

  1. kuoga
    Usafi
    hancifu
  2. mwili
    kuoga
    mswaki
    kukatwa
  3.  pole
    asante
    samahani
    tafadhali
  4. Mtoto alibeba mkoba.
    Ufunguo ulianguka chini.
  5. aleikum salaam
    marahaba
  6. simama
    cheka
    inama
  7. MWALIMU
    daktari

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 Term 1 Opener Exams 2023 SET 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.