Monday, 27 February 2023 12:16

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 Term 1 Opener Exams 2023 SET 4

Share via Whatsapp

MASWALI

Imla

 1. ..............................
 2. ..............................
 3. ..............................

Andika wingi

 1. kitabu ..............................
 2. Mti ..............................
 3. Ua ..............................

Tumia "huyu" au "hawa"

 1. ..............................ni wasichana.
 2. ..............................ni mtoto.

Chagua jawabu sahihi kujaza nafasi

 1. Mgeni..............................amaingia leo.
  (langu, wangu, yangu)
 2. Matunda..............................yameoza.
  (yangu, wetu, yetu)
 3. Kiti ..............................kilivunjika.
  (kizuri, mazuri, wazuri)
 4. Watoto .............................. walichuna matunda yote.
  (mazuri, vibaya, wabaya)

Kanusha sentensi hizi

 1. Mimi ninasoma
 2. Sisi tunalima

Andika kinyume cha maneno haya

 1. Ingia ..............................
 2. Safi ..............................

Andika wingi wa maneno haya

 1. Kitabu hiki
 2. Tunda hili
 3. Mzazi huyu
 4. Chakula hiki

Chagua jibu sahihi kujaza nafasi

 1. Viti .............................. vitanunuliwa.
  (hiki, hivi, hili)
 2. Kichana ..............................kimevunjika.
  (hivi, huyu, hiki)
 3. ..............................nitafagia.
  (sisi, mimi, yeye)
 4. ..............................anavua nguo.
  (wewe, yeye, wao)
 5. Gari ..............................limeharibika.
  (hili, huyu, hiki)

Soma hadithi kisha ujibu maswali

Jamila anapoamka asubuhi anasugua meno. Kisha anaweka maji kwenye karai. mama yake humfunza kuoga vizuri kwa kutumia sabuni na maji. Yeye huoga sehemu zote za mwili. Nguo zake za shule hufuliwa na mama. Dada yake Sidi hanawi mikono vizuri.

 1. Jamila husugua ..............................anapoamka asubuhi.
 2. Jamila hutumia nini kuoga?
 3. Ni nani hufua nguo za Jamila za shule?
 4. Je, dadake Jamila huitwa nani?
 5. Jamila huweka maji yake ya kuoga kwa kifaa kipi?

Majibu

 1.    
 2.    
 3.   
 4. vitabu
 5. miti
 6. maua
 7. Hawa
 8. Huyu
 9. wangu
 10. yetu
 11. kizuri
 12. wabaya
 13. Mimi sisomi.
 14. Sisi hatulimi.
 15. toka
 16. chafu
 17. Vitabu hivi
 18. Matunda haya
 19. Wazazi hawa
 20. Vyakula hivi.
 21. hivi
 22. hiki
 23. Mimi
 24. Yeye
 25. hili
 26. meno
 27. sabuni na maji
 28. mama
 29. Sidi
 30. karai

KUSOMA

Soma habari hii

Omari ni mtoto. Baba yake ni Otieno. Mama yake anaitwa Kanini. Omari hukaa na dada katika kaunti ya Nairobi. Omari huletewa mayai na kaka yake Kimtai. Nyanya mkuu humpa mabuyu. Omari hutamani chakula kitamu zaidi ya mabuyu. Omari hupenda kucheza sana. Yeye ana mpira mzuri.

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 2 Term 1 Opener Exams 2023 SET 4.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.