Friday, 03 September 2021 08:54

Kiswahili: Lugha - Grade 2 End Term 1 Exam 2021 SET 2

Share via Whatsapp
  1. SEHEMU YA 1:
    KUZUNGUMZA NA KUSIKILIZA
    1. Hujambo?
      (mwanafunzi kujibu)
    2. U hali gani?
      (mwanafunzi kujibu)
    3. Jina lako nani?
      (mwanafunzi kujibu)
    4. Uko katika gredi gani?
      (mwanafunzi kujibu)
    5. Mwalimu wako wa darasa anaitwa nani?
      (mwanafunzi kujibu)
    6. Taja mfano wa somo unayosoma katika gredi yako
      (mwanafunzi kujibu)

      (alama 6)
  2. SEHEMU YA 2:
    KUSOMA KWA SAUTI
    Tamka sauti za herufi hizi
    r            j             g              d
    1. furahi
    2. chakula
    3. kufanya
    4. dereva
    5. wageni
    6. majengo
    7. pacha
    8. dhidi
    9. ghala
    10. kupata
    11. tulipiga
    12. juzi
    13. raha
    14. dhambi
    15. maziwa
      (alama 15)

      Kusoma sentensi
      1. Wewe ni Maria.
      2. Kuku ni wetu
      3. Mama anapika chakula.
  3. SEHEMU YA 3 :
    KUSOMA UFAHAMU
    Soma hadithi kisha ujibu maswali.
    Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Apesa na Sifa walikuwa shuleni. Usafiri ulitatizika. Jioni Apesa na Sifa waliamua kutembea. Mto ulikuwa umejaa na kufurika. Sifa aliteleza na kuanguka mtoni.

    Jibu maswali
    1. Apesa na Sifa walikuwa wapi mvua iliponyesha?
      __________________________________
    2. Jioni Apesa na Sifa waliamua kufanya nini?
      __________________________________
    3. Mto ulikuwa umefanya nini?
      __________________________________
    4. Nani aliteleza na kuanguka mtoni?
      __________________________________
      (alama 4)
  4. SEHEMU YA 4:
    MATUMIZI YA LUGHA
    1. Tumia "ako" na "enu" kujaza mapengo.
      1. Kalamu ________________________ imepotea.
      2. Walimu ________________________ ni wazuri.
      3. Kitabu _________________________ kimeanguka.
      4. Madarasa ______________________ yamefungwa.
        (alama 4)
    2. Jaza mapengo ukitumia "vizuri" na "vibaya"
      1. Mwanafunzi anafaa kuandika _________________________
      2. Mwalimu anafaa afundishe ___________________________
      3. Dereva asiendeshe gari ______________________________
      4. Nwanafunzi asiketi __________________________________
        (alama 4)
    3. Andika nambari hizi kwa maneno
      1. 10 __________________
      2. 6 ___________________

        (Alama = 35)
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili: Lugha - Grade 2 End Term 1 Exam 2021 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.