Tuesday, 08 February 2022 09:44

Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti - CBC Grade 3 End of Term 3 Exam SET 2 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

  1.  KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA      (Alama 5)
    Sikiliza hadithi nitakayokusomea kisha nitakuuliza maswali.
    Bi. Asha aliishi katika kijiji cha Bondeni. Yeye na mume wake walikuwa na watoto wanne. Waliwafunza watoto wao kuwa na maadili mema. Waliwafunza kuwa na heshima kwa wakubwa na wadogo wao. Watoto wao walipendwa na watu wote na walimu wao kwa sababu ya heshima.
    1. Bi. Asha aliishi katika kijiji kipi?
    2. Bi. Asha alikuwa na watoto wangapi?
    3. Bi. Asha na mume wake waliwafunza watoto wao nini?
    4. Ni nani aliwapenda watoto wa Bi. Asha? (alama 2)
  2. KUSOMA KWA SAUTI.         (Alama 10)
    Soma hadithi hii kwa sauti.
    Familia ya Kiprono iliishi jijini Nakuru. Kiprono alikuwa mtoto mzuri sana ambaye alipenda kuwasaidia wazazi wake kazi.
    Siku moja baada ya kumaliza kazi za nyumbani, aliondoka kwenda kucheza. Baada tu ya kufunga mlango, kulitokea mtu mmoja akamshika kwa nguvu. Mtu yule alimlazimisha amfungulie mlango. Kiprono alikataa na kupiga mayowe. Kwa bahati nzuri babake alikuwa ametoka kazini. Kwa mbali alisikia mayowe na kukimbia. Alimkamata mtu yule na kumpeleka kwenye kituo cha polisi.

Majibu

  1. Bondeni
  2. wanne
  3. kuwa na maadili mema
    kuwa na heshima kwa wakubwa na wadogo wao
  4. watu wote na walimu wao
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti - CBC Grade 3 End of Term 3 Exam SET 2 2022.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.