Thursday, 02 March 2023 07:55

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 3 School Based Assessment 2023 Opener Exams Term 1 Set 2

Share via Whatsapp

QUESTIONS

SEHEMU YA A:
SEHEMU YA 1:
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu atamwuliza mwanafunzi maswali yafuatayo, mwanafunzi ayajibu vilivyo

  1. Mzazi wa kike ni?
    (Mwanafunzi ajibu)
  2. Mama wa baba ni?
    (Mwanafunzi ajibu)
  3. Baba wa mama ni?
    (Mwanafunzi ajibu)
  4. Mwalimu hufunza akina nani?
    (Mwanafunzi ajibu)
  5. Mimi nina umri wa miaka?
    (Mwanafunzi ajibu)

SEHEMU YA 2:
KUSOMA KWA SAUTI
Soma hadithi hii kwa sauti
Lochita aliishi na wazazi wake Betei. Wazazi hao walimpenda sana. Wakati wa likizo, Lochita aliwatembelea shangazi na mjomba. Aliwanunulia binamu zake kalamu na vifutio.
Shangazi alimwambia Lochita abaki ili watembelee mbuga ya wanyama. Mbugani waliwaona wanyama wengi, waliwaona simba, ndovu na chui. Lochita alipiga picha ili awaonyeshe wazazi wake.

SEHEMU YA B:
SEHEMU Ya 1: KUSOMA UFAHAMU
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali
Ilikuwa ni siku ya Alhamisi, kulikuwa na mashindano ya kuimba nyimbo. Wanafunzi wa shule jirani walikuja shuleni kwetu. Tulienda kwenye gwaride. Bendera ilipandishwa tuliimba wimbo wa taifa, Baadaye tuliingia ukumbini. Gredi ya tatu iliimba vizuri. Tulipewa zawadi. Grace alikariri shairi. Naye pia alipokea zawadi.

  1. Siku ya mashindano yalikuwa gani?....................................................................
    (Ijumaa, Alhamisi, Jumatano)
  2. Mashindano yalikuwa ya nini?....................................................................
    (kukimbia, kuimba, kucheza)
  3. Baada ya kupandisha bendera tuliimba wimbo wa....................................................................
    (dunia, taifa)
  4. Wale walioshinda walipewa....................................................................
    (mkate, zawadi)
  5. Atieno pia alishinda?....................................................................
    (ndio, la)
  6. Walioimba vizuri zaidi walikuwa wa gredi....................................................................
    (ya nne, ya pili, ya tatu)

SEHEMU YA 2: SARUFI
Chora picha

  1. Miwani
  2. Kifutio
  3. Saa
  4. Nanasi
  5. Ufagio

Andika:

  Umoja Wingi
 Ua  
7 kengele  
8 mkono   
9 sahani  
10   mzee  

Tumia silabi kufanya neno
Mfano: ba
babu

  1. na.................................................
  2. ch.................................................
  3. M.................................................
  4. ki.................................................
  5. sh.................................................

Chagua jibu sahihi

  1. Mguu..................................................(hawa, huu)
  2. Kiti.................................................(huu, hiki)
  3. Wazee.................................................(hawa, hizi)
  4. Vyombo.................................................. (hivi, hiki)
  5. Mvulana.................................................(hii, huyu )

Jaza pengo

  1. s__m__k__
  2. msw__ki
  3. d__r__s__
  4. mp__ra
  5. __a

SEHEMU YA 3: KUANDIKA IMLA
(Mwalimu atakusomea sentensi, ziandike.)

  1. .................................................
  2. .................................................
  3. .................................................
  4. .................................................
  5. .................................................
  6. .................................................
  7. .................................................
  8. .................................................
  9. .................................................
  10. .................................................

MAJIBU

  1. Alhamisi
  2. kuimba nyimbo
  3. taifa
  4. zawadi
  5. la
  6. ya tatu

Sehemu ya 2: 
Andika

  1. ua  - maua
  2. kengele - kengele
  3. mkono - mikono
  4. sahani - sahani
  5. mzee - wazee
  6. nafasi, nakabu,.......................
  7. chakula, chombo,.......................
  8. mama, mkate, mkoba .......................
  9. kikombe, kitabu, kimbo, ...........................
  10. shule, sheria, .........................
  11. huu
  12. hiki
  13. hawa
  14. hivi
  15. huyu
  16. samaki
  17. mswaki
  18. darasa
  19. mpira
  20. ua

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 3 School Based Assessment 2023 Opener Exams Term 1 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.