Thursday, 31 August 2023 09:37

Kusikiliza, Kuzungumza na Kusoma Questions and Answers - CBC Grade 3 Term 3 Opener Exams 2023 SET 1

Share via Whatsapp

SEHEMU YA A:

SEHEMU YA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Mwalimu asome hadithi na mwanafunzi ajibu maswali

Hapo zamani za kale paliishi mwewe juu ya mlima kwenye mti mrefu.Chini ya huo mti aliishi nyoka mwenye rangi nzuri sana.

Kila mara nyoka alipanda mtini na kula mayai yake mwewe. Nyoka alimwambia mwewe, "siku moja nitakutafuna wewe pia." Mwewe aliondoka kwa hasira sana. Alikwenda mpaka kwa rafiki yake fisi. Fisi alikuwa na akili kushinda wanyama wote. Alimwambia fisi habari yote.

"Nitamngoja nyoka alale. Kisha nitatoboa kichwa chake. Hataweza kufanya ujeuri tena. Mwewe alifafurahi sana.

  1. Nani aliishi chini ya mti?
  2. Wingi wa "mlima" ni?
  3. Nyoka iko na miguu mingapi?
  4. Kwa nini mwewe alienda kwa fisi?
  5. Je, nyoka alikuwa na tabia nzuri?
  6. Wanyama wangapi wametajwa katika hadithi?

SEHEMU YA 2: KUSOMA KWA SAUTI

Mavazi husaidia kufunika mwili. Mavazi niya aina nyingi. Mtu huvaa kulingana na mahali anapoenda au sababu nyinginezo.

Yapo mavazi rasmi kama ya shule yaitwayo sare. Mavazi mengine ni ya waogeleaji, nayo huitwa bikini. Mavazi ya wasanii wa sarakasi, ngoma na tamthila ni maleba.

Wachezaji kandanda huvaa majezi. Wanawake wanapotoka nje huvalia buibui. Mavazi huonyesha heshima, dini, ushule, uongozi na cheo. Mavazi hutunza, hivyo basi binadamu naye ayatunze.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kusikiliza, Kuzungumza na Kusoma Questions and Answers - CBC Grade 3 Term 3 Opener Exams 2023 SET 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.