Thursday, 03 February 2022 13:23

Kiswahili Questions and Answers - Class 6 End of Term 3 Exams Set 1 2022

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua lifaalo zaidi

Kuna njia 1                za kuhakikisha kuwa tuna afya bora. Kwa 2               , tunashauriwa kula chakula 3                , kufanya mazoezi, kujiepusha na 4                na kutafuta matibabu tukiwa wagonjvva. Mtu akiwa mgonjwa, 5                kufanya kazi wale kusoma kwa njia inayofaa. Kipindupindu, kichocho na kuendesha ni baadhi ya 6                ambazo husababishwa na 7                usafi wa mwili na mazingira. Kila 8                ana jukumu la kuhakikisha kuwa mwili wake ni safi, anakula chakula safi na kuishi mahali safi. Wadudu hatari kama vile 9                nao hushambulia vidole vya mtu anayeishi mahali penye uchafu. Sote tujiepushe na uchafu.

 1.      
  1. ambazo
  2. mengi
  3. mingi
  4. nyingi
 2.        
  1. vile
  2. kuwa
  3. sababu
  4. mfano
 3.        
  1. inayofaa
  2. kinachofaa
  3. linalofaa
  4. vinavyofaa
 4.        
  1. madawa ya kulevya
  2. dawa ya kulevya
  3. dawa za kulevya
  4. madawa za kulevya
 5.        
  1. anaweza 
  2. hawezwi
  3. hawezi
  4. hawawozi
 6.        
  1. magonjwa
  2. ndwele
  3. ugonjwa
  4. maradhi
 7.        
  1. kutozingatia
  2. kuzingatia
  3. kujua
  4. kutojua
 8.        
  1. moja
  2. kimoja
  3. umoja
  4. mmoja
 9.        
  1. tekenya
  2. mende
  3. kunguni
  4. chawa

Asubuhi 10                , wazazi wa Kajua 11                kuelekea shuleni iii wajue kwa nini mtoto wao alirudishwa nyumbani. Walianza safari hata biia kunywa 12              yao kama ilivyokuwa kawaida. Walipofika 13                waliarifiwa kuwa Kajua alipatikana akicheza na simu wakati wa masomo. Wazazi walishangaa na 14                sana. Walimpa 15                kali na kumpokonya simu hiyo Nadi akamiIishe masomo yake. Kajua aliomba msamaha na kubadilika kabisa.

 1.        
  1. hiyo
  2. hio
  3. huo
  4. huwo
 2.        
  1. walikata shauri
  2. walikata kauli
  3. walikata kamba
  4. walikata kiu
 3.        
  1. kiamshakinywa
  2. staftahi
  3. chamcha
  4. uji
 4.        
  1. ndani mwa shule
  2. katika shuleni
  3. kwa shule
  4. shuleni
 5.        
  1. kulia
  2. kushangilia
  3. kuhuzunika
  4. kusherehekea
 6.        
  1. adabu
  2. viboko
  3. adhabu
  4. heshima
 7. Kivumishi gani ambacho ni tofauti na vingine?
  1. zote
  2. wengi
  3. yeyote
  4. chenye
 8. Chagua maelezo ambayo si sahihi.
  1. Figo ni kiungo ambacho husafisha damu mwilini.
  2. Kiwiko ni sehemu ya mkono ambapo saa hufungwa.
  3. Mfupa ambao hufunika meno huitwa
  4. Mapafu huingiza hewa safi mwilini na kutoa hewa chafu.
 9. Chagua ukanusho wa;
  Unga umeletwa na mama.
  1. Unga hujaletwa na mama.
  2. Unga haujaletwa na mama.
  3. Unga umepelekwa na baba.
  4. Unga haukuletwa na mama.
 10. Tambua sentensi iliyotumia "ki" kuonyesha udogo.
  1. Ukimwona mwalimu shuleni uniambie.
  2. Magari yote yalikuwa yakioshwa na wafanyakazi.
  3. Kijibwa cha nyanya kimelala.
  4. Wacheni kucheza kijinga mtaumia.
 11. Neno eshukuru' lina herufi ngapi?
  1. 3
  2. 7
  3. 6
  4. 5
 12. Tambua usemi wa taarifa wa sentensi ifuatayo.
  "Kesho tutaenda Mombasa," mwalimu alisema.
  1. Mwalimu alisema kuwa wangeenda Mombasa siku iliyofuata.
  2. Mwalimu alisema kuwa tungeenda Mombasa kesho.
  3. Mwalimu alisema kuwa wataenda Mombasa siku iliyofuata.
  4. Mwalimu alisema kuwa tutaenda Mombasa kesho.
 13. Sentensi ifuatayo itaandikwaje katika wingi?
  Kuli ameweka chupa karibu na ukuta.
  1. Makuli wameweka chupa karibu na nyuta.
  2. Makuli wameweka vyupa karibu na kuta.
  3. Kuli wameweka chupa karibu na kuta.
  4. Makuli wameweka chupa karibu na kuta
 14. Rangi ya chini kabisa kwenye upinde wa mvua huwa ipi?
  1. nyekundu
  2. urujuani
  3. nili
  4. machungwa
 15. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari.
  Tulitembea polepole na kusimama chini ya mti.
  1. nomino, kihusishi
  2. kivumishi, kielezi .
  3. kielezi, kihusishi
  4. livumishi, kitenzi
 16. Sentensi gani iliyotumia kiashiria kisisitizi?
  1. Mkeka ule radio ulionunuliwa_
  2. Kinywaji hiki hiki kitapewa mtoto.
  3. Nguo yenyewe ndiyo iliyopigwa pasi.
  4. Baiskeli iyo hiyo itapelekwa kwa fundi
 17. Orodha ipi iliyo ria msamiati wa aina moja?
  1. funza, nzi, mbuni
  2. randa, msumeno, tarumbeta
  3. sabmarini, purutangi, machela
  4. dania, mdalasini, tangawizi
 18. Chagua sentensi ambayo ni
  1. Chaff ambacho kimeiva ni kitamu.
  2. Nyumba yenye imejengwa ni ya babu.
  3. Usinywe maji chafu, kunywa maji safe.
  4. Kutembea kunakopendeza ni kwa mtoto.
 19. 'Lima' ni kwa `mkulirria' kama vile ni kwa 'msomaji.'
  1. soma
  2. andika
  3. fundisha
  4. masomo
 20. Mpira wa kandanda huwa na umbo gani?
  1. tufe
  2. duara
  3. duaradufu
  4. tao
 21. Kiambishi kimetumikaje katika sentensi ifuatayo?
  Mtoto huyo amejiangusha chini.
  1. kirejeshi
  2. hall
  3. mtendaji
  4. ukubwa

Soma kifungu kifuatacho kisha ulibu maswali 31- 40.
Vita ni hall ya kukosa amani na utulivu. Hall hiyo husababisha kutoelewana na kupigana. Mara nyingi, vita husababishwa na ugpmvi. Vita huweza kutokea kila mahali na kwa kila umri. Pengine hata mahali unaposomea, shuleni au darasani, umewahi kuona wanafunzi wenzako wakipigana. Pengine hata wewe mwenyewe umewahi kuhusika katika vita. Je, umewahi kuona watu wakipigana njiani ukielekea nyurnbani kutoka shuleni? Kuna nyakati ambapo vita hutokea kati ya watu wazima kama vile wazazi au makabila mawili ambayo ni tofauti. Kiwango cha juu cha vita huwa ni vita katika nchi. Vita kama hivi huweza kutokana na kutoelewana katika jambo la kitaifa kama vile matokeo ya uchaguzi. Vita vina madhara gani?

Ifahamike kuwa vita husababisha kuumia kwa watu na mifugo. Watu walioumizwa wakati wa vita hulia kwikwikwi kutokana na maumivu. Wengine huishia kuaga dunia kutokana na majeraha katika vita. Mali nayo huharibiwa mno. Utapata kuwa maduka ya watu na nyumba zao huchomwa bila sababu maalum. Magari hupigwa na kuvunjwa vioo au kuchomwa. Uharibifu huu wa niali hurudisha nyuma uchumi wa taifa letu. Masomo, biashara na kazi haziwezi zikafanyika kwa kuwa ni vigumu kusafiri katika mazingira yaliyo na vita. Wanafunzi na walimu hubakia katika nyumba zao wakihofia kuangamizwa na wapiganaji. Hakuna awezaye kuuza wala kununua chochote kwa kuwa maduka yote hufungwa. Upendo na umoja katika nchi nao hurudi chini. Hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa umoja na ushirikiano ni muhimu sana.
Kunapotokea kutoelewana, njia ya pekee huwa ni kupigana ama kuna njia nyingine? Mwenzako anapokukasea shuleni ama nyumbani, unafaa kufanya nini? Jinsi tunavyojua, kupigana hakufai hata kidogo. Mazungumzo yanafaa kuwapo kati ya watu wawili waliokosana ama makundi mawili ambayo yamekosana. Kama hakuna kuelewana, husisheni mtu au watu wengine iii wasaidie kuleta utulivu. Aliyekosea hushauriwa kuomba msamaha na aliyekosewa amsamehe mwenzake. Tukumbuke kuwa kiln mtu hukosea. Hakuna mkamilifu ila Mungu pekee.

 1. Ufahamu unaeleza kuwa vita husababisha
  1. amani na utulivu.
  2. kutoelewana na amani.
  3. kutoelewana na kupigana.
  4. kupigana na utulivu.
 2. Ni kweli kuwa vita huweza kutokea wapi?
  1. Shuleni na njiani
  2. Sokoni na darasani
  3. Njiani na sokoni
  4. Kila mahali
 3. Kiwango cha juu cha vita kinahusu nini?
  1. Vita vinavyotumia bunduki
  2. Vita katika nchi
  3. Vita vinavyoleta kifo
  4. Vita kati ya watu wakubwa
 4. Ufahamu unaonyesha kuwa vita huongeza yafuatayo isipokuwu
  1. uchumi.
  2. vifo.
  3. umaskini.
  4. chuki.
 5. Maneno 'hulia kwikwikwi' ni mfano wa
  1. nahau.
  2. sitiari.
  3. tashbihi.
  4. tanakali ya sauti.
 6. Msimulizi anaeleza kuwa hall ya kukosana ikitokea watu wafanye nini?
  1. Wasigombane wala wasipigane sana.
  2. Wazungumze na kusameheana.
  3. Wapigane to ikiwa msamaha haupatikani.
  4. Aliyekosea anafaa kuombwa msamaha.
 7. Msimulizi ametumia maneno kuwa umoja na ushirikiano ni muhimu sana'.
  Methali gani inayokubaliana na maneno hayo
  1. Polepole radio mwendo.
  2. Mkono mmoja hauchinji ng'ombe.
  3. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo.
  4. Akufaaye kwa ndiye rafiki.
 8. Kulingana na ufahamu, hakuna mtu ambaye
  1. hana makosa.
  2. hukosea.
  3. huomba msamaha.
  4. husamehewa
 9. Nini ambacho huwa hakichomwi wakati wa vita kulingana na ufahamu?
  1. Nyumba
  2. Magari
  3. Maduka
  4. Vioo
 10. Ufahamu huu unahusu umuhimu wa nini?
  1. Vita
  2. Amani
  3. Mazungumzo
  4. Kutoetewana

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41- 50.
Katika cha Jikaze, paliishi kijana mmoja aliyeitwa Musa. Aiikuwa kijana wa miaka kumi na
mitano. Musa alipenda kufanya rnzaha na kuchezea wenzake. Wakati mwingine alipokuwa shuleni, alianguka chini na kuanza kulia. Walimu na wanafunzi waliingiwa na wasiwasi sana. Baada ya kuulizwa kwa mucla mrefur Musa alisema kwa sauti ya unyonge, "Mimi ni rngonjwa, ninaumwa na tumbo." Walimu walitafuta njia ya kumrudisha nyumbani kwao. Kula nyumbani alilala kidogo kisha akasimama na kusema kuwa amepona. Aliifanya hii kuwa tabia yake hasa alipojua kuwa hakuwa amefanya kazi yoyote ya mwalimu. Alijifanya mgonjwa kiasi cha kushindwa kutembea. Wanafunzi wengine walimsikia siku moja akimwambia mwenzake kuwa hiyo ilikuwa njia rahisi ya kutonaswa vvameiti tura' Wakati akiwa katika likizo ya Disemba, alikuwa akitumwa na wazazi wake kuwapeleka mifugo msituni wale nyasi. Kwa kuwa hakutaka kuifanya kazi hiyo, alitafuta njia ya kuwafanya wazazi waache kumtuma msituni. Baada ya muda mfupi wa kuwafikisha ng'ocr be malishoni, angeanza kupiga kelele, "Uuuuwi! Wooi! Weziii!" Wanakijiji walifika pale kwa kasi sana. Ajabu ni kuwa mifugo wote walikuwa wametulia tuti wakila nyasi. Musa naye alikuwa juu ya kitima fufani akiruka na kupiga kelele. Wanakijiji hao walikasirika na kuondoka. Wiki moja ilipopita, wanakijiji tena walizinduliwa kutoka katika shughuli zao na kamsa. "Jameeeni! Mungu wanguuu! Woooi! Mayoo!" Wanakijiji walifika pale kwa kasi ya umeme wakidhani kuwa amevamiwa na wezi au mnyama hatari. Waliondoka wakiwa wameudhika kwelikweli.
Siku moja, Jumamosi, Musa aliwasili malishoni wakati wa adhuhuri. Alijilaza chini ya mti na kutulia. Ghafia kama ajali, aliwaona wezi wakiondoka na mifugo wao. "Woooi! Mayoo! Woooi! Weziii!" Alipiga kelele na kuomba msaada. Hakuna aliyeonekana iii kumsaidia. Mwizi mmoja alimshika na kumfunga kwenye mti. Mifugo kumi walichukuliwa, watano wakauawa na wengine watano wakaachwa kwa sababu walikuwa wachanga. Mtoto wa watu akabaki akiwa amefungwa kwenye mti.

 1. Kulingana na ufahamu, ni kweli kuwa
  1. Musa alikuwa mgonjwa mara mbili.
  2. Musa hakuwa mgonjwa wakati wowote.
  3. Musa alikuwa akiumwa na tumbo.
  4. Musa alipenda sana masomo.
 2. Kwa nini Musa alikuwa akisema kuwa yeye ni mgonjwa?
  1. Ndipo apelekwe hospitalini.
  2. Ndipo awasaidie wazazi kuwalisha mifugo.
  3. Ili asiadhibiwe kwa kutofanya kazi.
  4. Ili apate nafasi ya kucheza na wenzake.
 3. Mara ya pill Musa alipopiga kelele;
  1. alisema kuwa ameshambuliwa na wezi.
  2. alisema kuwa ameumwa na nyoka.
  3. alisema kuwa ameshambuliwa na mnyama hatari.
  4. hapakuwa na hatari yoyote iliyomkumba.
 4. Mara ya tatu, Musa aliwasili malishoni saa ngapi kulingana na ufahamu?
  1. saa na nane
  2. saa tano
  3. saa kumi
  4. haijulikani
 5. Ufahamu unaonyesha kuwa Musa alikuwa na tabia gani?
  1. mwerevu na mtiffu
  2. mjanja na mzembe
  3. mwoga na mchafu
  4. mzuri na mwenye heshima
 6. Unadhani kwa nini wanakijiji hawakwenda kurnwona Musa alipopiga kelele mara ya tatu?
  1. Hawakusikia akipiga kelele.
  2. Walitaka wezi hao wa mfanye abadilishe tabia.
  3. Walifikiri kuwa Musa alikuwa akifanya mchezo kama kawaida.
  4. Walijua kuwa wezi hao hawakutaka kumwua Musa.
 7. Mifugo wa akina Musa waliibwa siku gani?
  1. Jumamosi
  2. Ijumaa
  3. Jumapili
  4. Alhamisi
 8. Kifungu hiki kinatushauri tuache tabia gani?
  1. Ya kufanya mzaha na kuwachezea wengine.
  2. Ya kusema kuwa sisi ni wagonjwa.
  3. Ya kupiga kelele tukiwa na mifugo msituni.
  4. Ya kuwaita watu kwa sababu ya wezi.
 9. Musa alikuwa na mifugo wangapi msituni?
  1. Ishirini
  2. Kumi
  3. Watano
  4. Kumi na watano
 10. Kichwa gani kinachofaa kwa makala haya?
  1. Musa na wezi.
  2. Vituko vya Musa.
  3. Musa shuleni.
  4. Musa na marafiki take.

INSHA
Andika insha ya kusisimua inayoanza kwa maneno yafuatayo

Hayawi hayawi huwa. Siku tuliyokuwa tumeingojea kwa hamu kuu baadaye ilifika. Wanasoka wa shule yetu walikuwa wamejiandaa vya kutoshaMARKING SCHEME

 1. D
 2. D
 3. B
 4. C
 5. C
 6. B
 7. A
 8. D
 9. A
 10. A
 11. B
 12. B
 13. D
 14. C
 15. C
 16. B
 17. C
 18. B
 19. C
 20. B
 21. A
 22. D
 23. B
 24. C
 25. D
 26. D
 27. D
 28. A
 29. A
 30. C
 31. C
 32. D
 33. B
 34. A
 35. D
 36. B
 37. B
 38. A
 39. D
 40. C
 41. B
 42. C
 43. D
 44. A
 45. B
 46. C
 47. A
 48. A
 49. A
 50. B

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 6 End of Term 3 Exams Set 1 2022.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students