Thursday, 09 September 2021 08:39

Kiswahili - Class 6 End Term 1 Exam 2021 Set 2

Share via Whatsapp

DARASA LA 6, MWISHO WA MUHULA 1
KISWAHILI
JINA....................................................SHULE.............................

Soma vifungu vifuatavyo. Kina nafasi 1 hadi 15. Kwa kila nafasi, umepewa maneno manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa

Mtoto    1    aliacha mchezo    2    aliokuwa nao na akafuata maneno    3    akiambiwa afuate na baba yake. Alitokea     4     mtoto    5        6    wote    7    darasani    8    , kwa hivyo mtihani    9     yeye ndiye    10     wa kwanza.

  1. A. ule                           B. yule                         C. wale                  D. vile
  2. A. yake                        B. zake                        C. wake                 D. lake
  3. A. aliyokuwa                B. aliokuwa                 C. alizokuwa          D. alilokuwa
  4. A. kua                          B. kuka                        C. kuwa                 D. kukuwa
  5. A. mhodari                   B. hodari                     C. mbora                D. mshujaa
  6. A. kumliko                    B. kuwaliko                 C. kuliko                 D. kukiliko
  7. A. huo                          B. hilo                          C. hiyo                   D. humo
  8. A. mwao                       B. lao                          C. yao                   D. nao
  9. A. ulikuja                      B. ulipokuja                 C. uliyekuja           D. ilipokuja
  10. A. atakayekuwa           B. aliyekuwa                C. angekuwa        D. angalikuwa

Ama kweli, elimu ni bahari     11    haina mwisho. Kila siku, mja    12     jambo     13      ambalo hakulijua. Nayo elimu humfaa mmiliko wake kwa     14     na marefu. Mtu aliyesoma, kwa mfano, hupata kazi nzuri na hujua     15     na watu.

  1. A. ambalo                     B. ambao                     C. ambaye              D. ambayo
  2. A. amejifunza                B. anajifunza               C. hujifunza            D. atajifunza
  3. A. mpya                        B. jipya                         C. mapya                D. lipya
  4. A. mapana                    B. mengi                      C. machache         D. mageni
  5. A. Kutengana                B. kutengemana          C. kutangamana    D. kutegana

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi

  1. Kitenzi 'choka katika kauli ya kutendesha ni
    1. chokesha
    2. choza
    3. chosha
    4. chokea
  2. Tumia kiunganishi mufti kujaza pengo
    Niliweza kumwua ndovu ______ swara
    1. laiti
    2. ilhali
    3. sembuse
    4. lakini
  3. Udogo wa neno 'mwana' ni
    1. jijana
    2. jana
    3. Kimwana
    4. kijana
  4. Chagua kinyume cha neno lililopigiwa mstari katika sentensi ifuatayo
    Baada ya kutabasamu, alianza kuhutubia hadhira
    1. kucheka
    2. kununa
    3. kughafilika
    4. kulia
  5. Kamilisha methali ifuatayo
    Dua la kuku halimpati
    1. mjinga
    2. ndege
    3. mbwa
    4. mwewe
  6. Sehemu ya chini ya sikio huitwa
    1. ndewe
    2. masharubu
    3. paji
    4. mashavu
  7. Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
    Mti uzaao embe unaitwa mwembe.
    1. Miti zizaazo miembe zinaitwa maembe.
    2. Miti izaayo miembe inaitwa maembe.
    3. Miti izaayo maembe huitwa myembe.
    4. Miti izaayo maembe inaitwa miembe.
  8. Jaza pengo kwa kivurishi kilaache
    Mtoto _____ alianguka vibaya sana
    1. mwenye
    2. wenyewe 
    3. mwenyewe
    4. enyewe
  9. Mtu anayefanya kazi ya kujenga kwa mawe huitwa
    1. sonara
    2. mwashi
    3. hamali
    4. nokoa
  10. Tegua kitendawili hiki
    Njoo umwone umpendaye.
    1. Kioo
    2. Picha
    3. Runinga
    4. Filamu
  11. Malipo ya kuolewa huitwa
    1. nauli
    2. koto
    3. mahali
    4. mahari
  12. Kanchiri, shimizi, kaptura na kocho kwa jina moja ni
    1. nguo
    2. mavazi
    3. mapambo
    4. maumbo
  13. Bainisha akisami inayoonyesha subui
    1. 1/7
    2. 1/3
    3. 1/8
    4. 1/9
  14. . Tumia '-ingine kwa usahihi:
    Mama amenunua nguo _______ nyingi
    1. zingine
    2. ingine
    3. nyingine
    4. mengine
  15. Tumia 'amba' kwa usahihi
    Mwalimu aliyeingia na vitabu ni Bwana Mirobi.
    1. Mwalimu ambaye anayeingia na vitabu ni Bwana Mirobi
    2. Mwalimu ambaye aliyeingia na vitabu ni Bwana Mirobi
    3. Mwalimu ambaye aingiaye na vitabu ni Bwana Mirobi
    4. Mwalimu ambaye aliingia na vitabu ni Bwana Mirobi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Adili alijiandaa kwa safari ya kuitikia wito wa mfalme.

Farasi watatu walitandikwa matandiko mazuri. Yeye alipanda farasi mmoja, na mmoja kwa kila nyani. Ikibali alipanda farasi wake mwenyewe. Farasi wa Adili na yule wa Ikibali walikwenda sambamba njiani. Nyuma yao waliandamana nyani juu ya farasi. Kila mtu aliyeona nyani wamepanda farasi alistaajabu. Mnyama kupandwa na mnyama! Ulikuwa mpeo wa miujiza kwa watu.

Vinywa vya umati wa watu vilikuwa wazi kwa kivumo cha lo salala! Wakati umefika wa mawe kusema, miti kujibu na wanyama kuwa watu! Ikibali aligeuza uso wake kwa Adili akasema kwa ucheshi, "Mbwa wanatubwekea kama walionusa kundi la wanyama wanaowindwa." Adili alikubali kwa kuinamisha kichwa akitabasamu. Walisafiri hivi mpaka nchiya mfalme. Baada ya kutua, Adili alipelekwa mbele ya mfalme na manyani wake.

  1. Adili alijizatiti kwenda
    1. kumsalimia mfalme
    2. kuonana na mfalme
    3. kumwua falme
    4. kuwatandika farasi
  2. Farasi watatu waliandikwa matandiko walikuwa ni wa kuwabeba
    1. Mfalme, Adili na Ikibali
    2. Adili, Ikibali na mfalme
    3. Ikibali, Adili na nduguze
    4. Adili na nyani wawili
  3. Farasi wa Ikibali na wa Adili walikwenda sambamba. Maana yake ni kuwa walikwenda
    1. mmoja mblele mwingine nyuma
    2. karibu karibu
    3. unyounyo mwendo wa asteaste
    4. sawasawa ubavu kwa ubavu 
  4. Manyani waliandamana nyuma ya Ikibali na Adili. Ndiko kusema Adili na Ikibali waliandamana na nyani
    1. sambamba
    2. unyounyo
    3. mkabala
    4. chapuchapu
  5. Kilichowashangaza watu zaidi katika habari hii ni
    1. Adili kuongozana na ikibali
    2. Adili kupanda farasi.
    3. Nyani kupanda farasi
    4. Mawe kusema, miti kujibu na wanyama kuwa watu
  6. kibali aliposema kwa ucheshi, bila shaka
    1. alinuna
    2. alighadhabika
    3. alinong'ona
    4. alitabasamu
  7. Mbwa alibweka. Je, wangekuwa fahali wangefanyaje?
    1. Wengeroroma
    2. Wangenguruma
    3. Wangekoroma
    4. Wangetetea
  8. Ikibali alipogeuza uso wake kwa Adili, bila shaka
    1. alimtazama Adili
    2. alimpa Adili kisogo
    3. alimkabidhi Adili
    4. hakumwangalia ana kwa ana
  9. Walipofika na kuwasili ughaibuni
    1. mfalme waliwalaki
    2. nyani walichoka
    3. Adili na Ikibali waliagana
    4. Adili alifikishwa maskanini pa mfalme
  10. Kauli ipi si sahihi kulingana na makara haya?
    1. Watu walishangazwa na nyani waliopanda farasi
    2. Watu walishangilia ili nyani wapande farasi
    3. Mbwa nao waliobweka walipowaona Ikibali na Adili
    4. Adili na nyani waliitwa na mfalme

Soma barua ifuatayo kisha ujibu maswali 41 hadi 50

Zera Ahmed.
S.L.P 27001,
MOMBASA
27-01-2001

Meneja wa Benki Kuu,
S.L.P 20101
NAIROBI.

KUH: OMBI LA KAZI

Mimi nina umri wa miaka thelathini, nimesomea kazi hii ya kufanya kazi kwenye benki kama mhasibu. Niliupata waraka mliokuwa mmetuma mkitafuta mhasibu. Mimi ni  mmoja wa wahasibu wale bora na maarufu zaidi nchini.

Nimeisomea kazi hii katika mojawapo wa vyuo vikuu nchini. Nilikuwa katika chuo kikuu kisha nikajaribu kufanya kazi kwa miaka miwili kwani nilikuwa nikijua kuwa, haba na haba hujaza kibaba.

Mimi ni stadi katika hisabati na lugha nyingine nyingi kama vile Kiswahili, King'eng'e, Kifaransa, Kijerumani pamoja na lugha nyingine nyingi.

Sipendi mapendeleo labda katika kabila, aila au hata rangi ya sura.

Huu ndio mwanya peke yake ninao wa kupata kazi hii ya uhasibu. Tafadhali ninakusihi unipe kazi hii.

Wako mwaminifu,

Zena Ahmed.

  1. Barua ya aina hii huitwa
    1. barua ya kindugu
    2. barua ya kirafiki
    3. barua rasmi
    4. barua kuu
  2. Anwani ya pili katika barua hii ni ya
    1. mwandishi
    2. mwandikiwa
    3. Zena
    4. mhasibu
  3. Barua hii iliandikwa mwezi gani?
    1. Februari
    2. Machi
    3. Juni
    4. Januari
  4. Nia ya mwandishi huyu kuandika barua hii ni
    1. Kuwa meneja 
    2. kuenda chuo kikuu
    3. kuwa tarishi wa benki
    4. ombi la kazi katika benki
  5. Mwandishi amesomea kasi ya
    1. utabibu
    2. uhasibu
    3. ualimu
    4. ukadamu
  6. Kazi ya uhasibu ni ipi?
    1. Kazi ya kuhesabu pes
    2. Amali ya kuchunga pesa
    3. Riziki ya upelelezi
    4. Kazi ya ufundi
  7. Baadhi ya mapendeleo ambayo mwandishi hayapendi na yametajwa ni kama vile
    1. ukabila
    2. jinsia
    3. lugha
    4. elimu
  8. Mwandishi wa habari hii amesoma hadi
    1. shule ya msingi
    2. chuo kikuu
    3. shule ya upili
    4. chekechea
  9. Zena Ahmed alisomea kazi hii ya uhasibu wapi?
    1. Chuo kikuu 
    2. Shule ya upili
    3. Shule ya msingi
    4. Chuo cha ufundi
  10. Mwandishi wa habari aliandika barua akiwa wapi?
    1. Makerere
    2. Mombasa
    3. Benki
    4. Nairobi

INSHA
Andika insha kuhusu: SHEREHE YA SIKU YA KUZALIWA KWANGU

MARKING SCHEME

  1. A
  2. C
  3. A
  4. C
  5. B
  6. C
  7. D
  8. A
  9. B
  10. B
  11. D
  12. C
  13. B
  14. A
  15. C
  16. C
  17. C
  18. D
  19. B
  20. D
  21. A
  22. D
  23. C
  24. B
  25. A
  26. D
  27. B
  28. A
  29. C
  30. D
  31. B
  32. D
  33. D
  34. B
  35. C
  36. D
  37. A
  38. A
  39. D
  40. B
  41. C
  42. B
  43. D
  44. D
  45. B
  46. A
  47. A
  48. B
  49. A
  50. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili - Class 6 End Term 1 Exam 2021 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students