Displaying items by tag: Kiswahili Lugha

Soma kifungu hiki Cha mazungumzo kisha ujibu swali la 1-5.

Onyango: Sabalkheri Lucia?
Lucia:       Aheri Onyango. Habari za likizo?
Onyango: Njema sana, labda yako.
Lucia:       Yangu pia ilikuwa njema. Wakati wa likizo wavyele wangu walinipeleka kwa nyanya.
Onyango: (Kwa furaha) Inaonekana kuwa likizo yako ilijawa na mema.
Lucia:       Naam! nyanya alinisimulia hadithi chungu nzima za kusisimua. Baada ya kila hadithi ningepata  
                 mafunzo mengi.
Onyango: Nami ningependa kujua mafunzo uliyopata.
Lucia:       Ngano ya sungura na fisi ilinifunza umuhimu wa kushirikiana na wengine.
Onyango: (Huku akitikisa kichwa) Likizo ijayo nami pia nitahakikisha nimeenda kumzuru nyanya.
Lucia:       Hakika sahibu yangu. Hilo ni wazo zuri sana. Naomba kwenda darasani. Kuwa na siku njema.
Onyango: Nawe pia Lucia.

Maswali

  1. Sabalkheri ni salamu za wakati upi?
    1. Jioni
    2. Wakati wowote
    3. Adhuhuri
    4. Asubuhi.
  2. Onyango na Lucia walipatana lini?
    1. Kwa nyanya yao
    2. Wikendi
    3. Baada ya likizo
    4. Disemba.
  3. Taja hadithi moja iliyotajwa kwenye kifungu hiki
    1. Onyango na Lucia.
    2. Nyanya na Lucia.
    3. Sungura na fisi.
    4. Nyanya na wavyele.
  4. Tambua kisawe cha 'wavyele' kama ilivyotumika kwenye mazungumzo
    1. Mama
    2. Wazazi
    3. Abu
    4. Rafiki.
  5. Lucia alifurahia nini alipokuwa kwa nyanya yake kulingana na kifungu?
    1. Hadithi za nyanya.
    2. Kulisha mifungo.
    3. Kupalilia mimea.
    4. Kupiga deki.

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 6-10. 

Dawa za kulevya pia huitwa mihadarati. Dawa hizi huwa na madhara mengi hasa kwa siha zetu. Dawa hizi husababisha vifo pia. Hivyo basi, tunapaswa kuepuka matumizi ya dawa hizi kabisa.

Baadhi ya njia za kuepuka matumizi ya mihadarati ni kusikiliza na kufuata ushauri tunaopewa shuleni na walimu wetu. Walimu huwashauri wanafunzi kuhusu madhara ya dawa za kulevya na jinsi ya kujiepusha na dawa hizi. Mwanafunzi pia anaweza kuingizwa katika matumizi ya dawa hizi na marafiki wapotovu. Ni vyema wanafunzi kuwachagua marafiki wao kwa uangalifu sana.

Wanafunzi pia hawapaswi kutazama filamu na vipindi vinavyopotosha mitandaoni. Vipindi hivi huonyesha wanaotumia dawa hizi kama mashujaa na ni kinyume na maadili.

Hatimaye vijana wanahimizwa kujihusisha na shughuli na michezo mbalimbali wakati wao wa mapumziko ili kujiepusha na fikra za kutaka kujaribu dawa hizi.

Maswali

  1. Kulingana na aya ya kwanza mihadarati ni nini?
    1. Dawa za afya.
    2. Dawa za kulevya.
    3. Dawa za nguvu.
    4. Dawa mbovu.
  2. Ili wanafunzi wajiepushe na matumizi ya dawa za kulevya, wanafaa kufuata ushauri wa nani?
    1. Mwalimu
    2. Marafiki
    3. Rika
    4. Mitandao.
  3. Wanafunzi hutazama wapi vipindi na filamu zinazohusu dawa za kulevya?
    1. Nyumbani
    2. Shuleni
    3. Mtandaoni
    4. Vitabuni.
  4. Ipi kati ya njia hizi itasaidia kuepuka matumizi ya dawa za kulevya?
    1. Kusikiliza ushauri wa mwalimu.
    2. Kuwa na marafiki wapotovu.
    3. Kutazama filamu na vipindi vinavyoimarisha matumizi ya dawa za kulevya.
    4. Kutumia muda wa mapumziko kutumia dawa za kulevya.
  5. Tambua mada inayofaa zaidi kwa kifungu hiki
    1. Dawa za kulevya.
    2. Maafa ya dawa za kulevya.
    3. Wanafunzi na dawa za kulevya.
    4. Ushauri.

Soma kifungu hiki kwa makini kisha ujibu Swali la 11-15.

G5SwaT1SE23003P1

Mapambo ni vitu vinavyovaliwa mwilini ili kufanya mtu awe wa kuvutia. Mapambo huvaliwa katika sehemu mbalimbali za mwili. Kuna mapambo ambayo hutumiwa kwa kupaka. Mapambo hasa hutumiwa mtu anapohudhuria sherehe kama za harusi na kadhalika.

Kuna mapambo ya aina mbalimbali ya kike na kiume. Aidha kuna mapambo kama vile ushanga, pambo ambalo huvaliwa na wanawake shingoni. Mapete na vipuli huvaliwa sikioni na wanawake. Pete huvaliwa kwenye kidole cha pete na wanawake kwa wanaume. Hina nayo hupakwa mikononi na miguuni. Ni vizuri kuyatumia mapambo ifaavyo.

Maswali

  1. Kwa nini watu hutumia mapambo?
    1. Ili kuvutia
    2. Ili kusafiri
    3. Ili kulala.
    4. Ili kuchukiza.
  2. Mapambo hutumiwa kwa kuvaa na
    1. kuangalia
    2. kula
    3. kupaka
    4. hakuna.
  3. Taja pambo linalotumiwa kwa kupaka 
    1. Kipuli
    2. Hina
    3. Ushanga
    4. Mapete 
  4. Pete huvaliwa wapi?
    1. Shingoni
    2. Vidoleni
    3. Puani
    4. Mkononi.
  5. Tambua pambo linalovaliwa sikioni
    1. Mapete
    2. Ushanga
    3. Kipini
    4. Pete.

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 16-20 ukitumia jibu sahihi

Asubuhi hiyo watu wengi walikuwa ___16___kwenye ___17___cha polisi. Wanawake kwa wanaume walikuwa wakizungumza kuhusu ___18___waliokuwa wakiwavamia usiku na mchana kwenye kijiji chao. Sajini wa polisi aliyekuwa akiyapokea malalamishi ___19___aliyaandika kwenye shajara na kutuliza ___20___wa watu uliojawa na hasira.

   A   B   C   D 
 16.   anafika   wakifika   walifika   watafika 
 17.  kituo  shule   darasa   mahali 
 18.  watu  watalii   wanakijiji   wezi 
 19.  zao  yao   wao   yake 
 20.  umati  mlolongo   tita    halaiki 

 

Tambua aina za nomino zilizopigiwa mstari.

  1. Umati wa watu ulihudhuria mkutano.
    1. Nomino ya wingi.
    2. Nomino ambata.
    3. Nomino ya makundi.
    4. Nomino ya kawaida.
  2. Ipi ni nomino tofauti kati ya hizi?
    Maji, Maua, Manukato, Maziwa
    1. Maua
    2. Maukato
    3. Maziwa
    4. Maji.
  3. Andika sentensi ifuatayo kwa wingi.
    Sabuni ilinunuliwa jana.
    1. Masabuni yalinunuliwa jana.
    2. Sabuni zilinunuliwa jana.
    3. Sabuni ilinunuliwa jana.
    4. Sabuni yalinunuliwa jana.
  4. Tambua sentensi iliyoakifishwa vyema.
    1. juma alisafiri Jana
    2. wanafunzi wamenunua vibati kalamu na vifutio
    3. Kitabu kipi kilinunuliwa?
    4. mwalimu amefika shuleni.
  5. Kamilisha methali ifuatayo.
    Asiyesikia la mkuu huvunjika ______________________
    1. mkono
    2. shingo
    3. mguu
    4. guu
      Tumia maneno ya heshima.
  6. Mama ana mimba
    1. mawe
    2. mtoto
    3. mjamzito
    4. mlevi
  7. Mtoto anahara
    1. anatapika
    2. anaendesha
    3. anakimbia
    4. anazama
  8. Tumia amba- kukamilisha sentensi ifuatayo.
    Chakula ____________________ kimepikwa ni kitamu.
    1. ambayo
    2. ambacho
    3. ambalo
    4. ambao
  9. Tambua ngeli ya neno lililopigiwa mstari.
    Chupa imeanguka ikavunjika.
    1. I-ZI
    2. A-WA
    3. U-I
    4. LI-YA
  10. Mwezi wasaba huitwaje?
    1. Agosti
    2. Juni
    3. Julai
    4. Aprili.

INSHA

Ufuatao ni mwanzo wa insha. Iendeleze kwa maneno yako mwenyewe huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

Mvua ilinyesha sana siku hiyo. Mimi na rafiki zangu tulikuwa...

MARKING SCHEME

  1. D
  2. C
  3. C
  4. B
  5. A
  6. B
  7. A
  8. C
  9. A
  10. A
  11. A
  12. C
  13. B
  14. B
  15. A
  16. C
  17. A
  18. D
  19. B
  20. A
  21. C
  22. A
  23. B
  24. C
  25. D
  26. C
  27. B
  28. B
  29. A
  30. C

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 hadi 5.    

G5SwaT1SB23P1

Polisi:      Usijaribu! Unaendesha gari bila taa zote za mbele?
Utingo:    Niko hapa Afande. Hujambo mzee?
Polisi:      Nimemwita dereva. Sikukuita wewe. Kwa nini anaendesha gari barabara i ilhali halina taa zote za mbele? Tena mnabeba                          abiria wawili wanaosimama.
Utingo:     Lakini afande, hapa pana chui kidogo!
Polisi:      Usijaribu! Wewe huna aibu? Unajaribu kumhonga afisa wa polisi!
Dereva:    Lakini Afande ....................
Polisi:       Sitaki hizo lakini zenu. Nimewakamata wewe na dereva wa gari hil. Twende kwenye kituo cha polisi. Nyinyi mtamweleza                          hakimu hizo lakini zenu. Ala! Njia ya mwongo ni fupi!
Utingo:     Tafadhali ............
Polisi:       Abiria wengine shukeni mngojee gari jingine.
Dereva:    Tafathali. Tusamehe................
Polisi:       Hapana cha tafadhali. Nyinyi abiria wawili mliosimama pia twendeni kwenye kituo cha polisi.

  1. Utingo ni mtu gani?
    1. Afisa wa polisi
    2. Msaidizi wa dereva.
    3. Abiria.
    4. Mtu ambaye anachukua nauli
  2. Watu wangapi walishikwa na Afisa wa polisi?
    1. Wanne
    2. Wawili
    3. Watatu
    4. Watano
  3. Hakimu anapatikana wapi kazini?
    1. Kwenye kituo cha polisi
    2. Kortini
    3. Barabarani
    4. Kwa jela
  4. Utingo alisema, "hapa pana chai kidogo." maana yake ni:-
    1. Chai kwa kikombe
    2. Nauli
    3. Pesa
    4. Hongo
  5. Dereva wa gari alipatikana na hatia ngapi?
    1. moja
    2. mitatu
    3. hakuna
    4. mawili

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 11.            

G5SwaT1SB23P2

Hapo zamani za kale paliishi wazee watatu waliokuw marafiki. Wote walikuwa maskini. Siku moja waliamua kwenda mahali panapoitwa Kaunguni kutafuta mali. Kufika huko ilikuwa ni tabu kwa sababu iliwabidi kupita vijiji vingi na kuvuka jito kubwa sana.

Kwa vile safari ilikuwa ndefu, waliamua kutafuta farasi ili waweze kufika upesi. Kwa bahati mbaya, kila
walikokwenda kutafuta farasi hawakufanikiwa kwa sababu
farasi walikuwa safarini. Basi wazee hao waliendelea na safari mpaka wakafika kwenye kijiji kilichokuwa karibu na lile jito.

Hapa walibahatika kupata farasi watatu ingawa farasi hawa hawakuwa wa kawaida. Farasi hawa wakiwa wakila vyakula tofauti. Wa kwanza alikula nguo za binadamu, wa pili alikula nyama ya binadamu, na wa tatu alikula nyama ya farasi. Kwa hivyo wazee walikuwa na tatizo la kutafuta vyakula vya farasi hawa.

  1. Wazee hawa watatu walikuwa na uhusiano upi?
    1. walikuwa matajiri
    2. Walikuwa wajinga
    3. Walikuwa wajanja
    4. Walikuwa maskini
  2. Safari ya wazee hawa ilikuwa na nia gani?
    1. Kutafuta farasi
    2. Kwenda kutafuta utajiri
    3. Kuvuka jito
    4. Kuenda Kaunguni
  3. Farasi wa mwisho alikuwa yupi?
    1. Aliyekula nguo
    2. Aliyekula farasi
    3. Aliyeluka binadamu
    4. Aliyekuwa mzembe
  4. Ni farasi yupi alikuwa katikati?
    1. Alaye watoto
    2. Mlafarasi
    3. Mlanguo
    4. Mlawatu
  5. Ni kitu gani kilichofanyikia farasi hawa walipovuka mto?
    1. Waligeuka kuwa wa kawaida
    2. Walimea pembe
    3. Walipata mali nyingi
    4. Walitajirika
  6. Kichwa kifaacho taarifa hii ni:-
    1. Juhudi sio pato
    2. Mchagua jembe si mkulima
    3. Akili nyingi huondoa maarifa
    4. Baada ya dhiki ni faraja

Jaza mapengo kwa kutumia jibu bora zaidi kutoka nambari 12 hadi 16.

Dawa___12___ kulevya hutumiwa na baadhi ya watu na kufanya kuonekana kama 13. Miongoni ___14___dawa hizi ni kama vile bangi, aina fulani ya ___15___ za kumeza na dawa fulani za ___16___kwa sindano.

   A   B   C   D 
 12.   ya   la  za   cha 
 13.  welevu   warefu   waolevi   walevi 
 14.  kwa  ya  mwa  pa
 15.  tembe  tembo  mawe  muitingoi 
 16.  kutunga   kuchoma   kuweko   kujidunga 

 

Kutoka nambari 17 hadi 30, jibu kulingana na maagizo.

  1. Neno "kifaru" iko katika ngeli ipi?
    1. I - ZI
    2. KI - VI
    3. U - ZI
    4. A - WA
  2. Umbo hili huitwa?
    G5SwaT1SB23P3
    1. Mraba
    2. Mstatili
    3. Duara
    4. Mche
  3. Rafiki _____________________________ amefika.
    1. wangu
    2. yangu
    3. langu
    4. changua
  4. Anayejenga kwa mawe huitwa _______________________________
    1. mwashi
    2. sonara
    3. seremala
    4. mhunzi
  5. Humusi huandikwaje?
    1. 1/5
    2. 1/6
    3. ΒΌ
    4. 1/8
  6. Andika wingi wa:-
    "Uso mfupi"
    1. Macha mafupi
    2. Mauso fupi
    3. Nyuso fupi
    4. Nyuso mfupi
  7. Msimu wa baridi kali bila mvua huitwa:-
    1. Kiangazi
    2. Vuli
    3. Masika
    4. Kipupwe
  8. Samaki ___________________________ ni wakubwa sana.
    1. hizo
    2. hao
    3. zile
    4. hio
  9. Aliandika barua ____________________________ kalamu ya wino.
    1. na
    2. kwa
    3. la
    4. cha
  10. Kitenzi "cheka" katika hali ya kutendewa ni:-
    1. Chekwa
    2. Chekelewa
    3. Chekea
    4. Chekewa
  11. _________________________________ niazime kalamu yako, yangu imepotea.
    1. Pole
    2. Tafadhali
    3. Samahani
    4. Niwie radhi
  12. Pesa anazolipa abiria yeyote ni:-
    1. faini
    2. karo
    3. nauli
    4. kiingilio
  13. Tunapita mtihani _______________________ tulifanya bidii.
    1. na
    2. pia
    3. lakini
    4. kwa sababu
  14. Simu ya mkono huitwa? ____________________________
    1. Runinga
    2. Rununu
    3. Sare
    4. Kompyuta

INSHA

Andika insha ya kusisimua kuhusu

SHULE YETU

MARKING SCHEME

  1. D
  2. A
  3. B
  4. D
  5. D
  6. D
  7. B
  8. B
  9. D
  10. A
  11. D
  12. C
  13. D
  14. C
  15. A
  16. D
  17. D
  18. B
  19. B
  20. A
  21. A
  22. C
  23. D
  24. C
  25. B
  26. B
  27. B
  28. C
  29. D
  30. B

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1 hadi 5.     

G6SwaT1SB23P1
Rozina:   Shikamoo Lawi?
Lawi:       Marahaba Rozina. U hali gani?
Rozina:    Njema. Nashuru "Mola" kwa kila hali ya leo. Habari za utokako?
Lawi:        Nzuri. Lakini nimechoka sana. Nimekuwa shambani kutwa nzima niking'oa magugu.
Rozina:    Pole sana kwa uchovu. Mwakani utalia kivulini.
Lawi:       Umegonga ndipo. Uzohali ni nyumba ya njaa. Bidii zangu zitanifaidi sana.
Rozina:    Hakika mimi nilimaliza kazi zote za shambani jana. Leo nikaamua kumtembelea bibi. Si unajua amekula chumvinyingi.
Lawi:        Naam, pia kazi hiyo ni nzuri.
Rozina:    Nimemsaidia kupiga deki na kuosha nguo zake. Amefurahi sana.
Lawi:        Umefanya vyema. Heko!
Rozina:    Tutaonana kesho kikaoni.
Lawi:        Inshallah! Asante Rozina.

  1. Kati ya Rozina na Lawi nani ako na umri nyingi?
    1. Rozina
    2. Lawi
    3. Hakuna
    4. Wote
  2. Nani alisaidiwa kulingana na mazungumzo haya?
    1. Ajuja
    2. Mke
    3. Nyanya
    4. Shaibo
  3. Kulingana na mazungumzo haya ni kweli kusema kuwa:--
    1. Lawi alimsaidia bibi
    2. Rozina alipenda kazi tofauti.
    3. Lawi na Rozina ni wakulima
    4. Lawi aling'oa kwekwe shambani
  4. Ni neno gani la adabu alitumia Rozina kwa Lawi?
    1. pole
    2. samahani
    3. karibu
    4. asante
  5. Neno "Mola" imetumika kwa mazungumzo. Maana yake ni:-
    1. Mazao
    2. Bidii
    3. Mungu
    4. Shamba

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 15.        

G6SwaT1SB23P2

Hapo jadi na jadudi paliishi mhunzi alikuwa na taaluma ya ufinyazi. Aliitwa Zuma. Alitegeneza sime, visu na hamadi kwa mhanga mwarara. Zilikuwa zana za hali ya juu. Aidha, vilimezewa mate na wengi. Kutokana na kipaji chake alizidi kutokuwa na jasho jekejeke kutokana na zaburi alizopokea kutoka kwa wateja wake. Kwa udi na uvumba alijifunga kibwekibwe kutimiza ahadi zake. Mchanga aliotumia Zuma ulikuwa wa kipekee. Ulipatikana tu katika nchi ya mbali.

Siku moja aliumaliza mchanga wake. Alimuaga mkewe aliyekuwa na jukumu la kumtunza mwana mtarajiwa. Nyathira hakutaka kuachwa peke yake. Zuma alimuuliza ninaye kumtunza akiondoka.

Ingawa mamaye Zuma alikuwa ajuza alikuwa mhariri na mwenye nguvu. Alimsaidia mkazamwana wake kwa kazi za nyumba kisha akawapeleka kondoo malishoni. Nyathira alipika na kuosha vyombo pasi kufanya kazi ngumu. Aliacha kuchota maji, kutafuta kuni na kupalilia mimea.

Jioni moja Bi. kizee yule hakurudi kutoka malishoni. Mwangaza ulipoondoka, Nyathira hakujua la kufanya kwani hakuwa na kurunzi nao mwangaza ulikuwa adimu. Alishikwa ma woga na akakata tamaa. Alijiloza katika kitanda kungoja kuche
akamtafute.

  1. Zuma alifanya kazi gani? Kazi ya:-
    1. kufinyanga
    2. uashi
    3. kuwinda
    4. usonaha
  2. Vifaa alivyotengeneza ni:-
    1. Ala za vita
    2. Vifaa vya upishi
    3. Vifaa vya usafiri
    4. Vifaa vya muziki
  3. Kutokana na habari hii ni kweli kusema:-
    1. Zuma alikuwa na wateja wengi.
    2. Zuma alikuwa kapera
    3. Zuma alikuwa na watoto wawili
    4. Zuma alikuwa mzembe.
  4. Si kweli kusema kwamba:-
    1. Zuma alitengeneza vitu vizuri.
    2. Mamake Zuma alimsaidia mkazamwanawe.
    3. Zuma alitumia mchanga wowote kufinyanga.
    4. Mamake Zuma alikuwa na nguvu.
  5. Kifungu "vilimezewa mate na wengi" ni kumaanisha kwamba:-
    1. watu walivitemea mate.
    2.  watu walitokwa na mate.
    3. walividharau
    4. watu walivitamani
  6. Mama Zuma alifanya kazi gani?
    1. Kuchunga kondoo
    2. Kuteka maji
    3. Kuvunja kuni
    4. Kufanya biashara
  7. Mkewe Zuma aliitwa nani?
    1. Mumbi
    2. Mfinyazi
    3. Nyathira
    4. Ajuza
  8. Nyathira angeenda kumtafuta mama yake lini?
    1. jioni
    2. usiku
    3. asubuhi
    4. hatujui
  9. Neno "taaluma" linamaanisha nini?
    1. ujuzi
    2. kutojua
    3. daktari
    4. kasoro
  10. Mke wa Zuma aliachiwa kazi zifuatazo isipokuwa:-
    1. kupalilia
    2. kuchota maji
    3. kutafuta kuni
    4. kufua nguo

Kutoka swali 16 hadi 20, jaza pengo na maneno chini.

Karai___16___hununuliwa dukakuu na dobi. Huwekwa maji___17___ ya___18___ nguo chafu. Dobi hutumia sabuni ___19___ katika duka la reja reja. Baada ya nguo kuwa safi, huanikwa na baadaye kupigwa ___20___.

   A   B   C   D  
 16.   ile   lile   yale   kile 
 17.  mingi   chache   mengi   ndogo 
 18.  kuvulia   kuvua   kufua   kufulia 
 19.  kinachonunuliwa   inunuliwayo   yanayonunuliwa   inayonunua 
 20.  bao  jeki    kitutu  pasi 


Kutoka nambari 21 hadi 30, jibu kulingana na maagizo.

  1. Tulienda kanisani kuimba kwaya. Neno kanisani ni:-
    1. Nomino
    2. Kivumishi
    3. Kiwakilishi
    4. Kielezi
  2. Gari ___________________________________liliharibika njiani.
    1. nzuri
    2. langu
    3. moja
    4. lile
  3. Wingi wa sentensi hii ni:-
    Msichana yule ni mgonjwa.
    1. Wasichana wale ni wagonjwa.
    2. Wasichana yule ni mgonjwa.
    3. Wasichana hao ni wagonjwa.
    4. Wasichana hawa ni wagonjwa.
  4. Umbo hili huitwa?
    G6SwaT1SB23P3
    1. Duara
    2. Mraba
    3. Mche
    4. Duara dufu
  5. Neno "ufahamu" lina irabu ngapi?
    1. mbili
    2. tatu
    3. nne
    4. saba
  6. Neno "ua" liko katika ngeli gani?
    1. I-ZI
    2. I-I
    3. LI-YA
    4. A-WA
  7. Jibu wa waambaje ni nini?
    1. vizuri
    2. vyema
    3. vibaya
    4. sina la kuamba
  8. Mtoto wa mjomba au shangazi ni:-
    1. kuzo
    2. mkoi
    3. shemeji
    4. wifi
  9. Tumia -enyewe kwa ufasaha.
    Shati __________________________ ni safi.
    1. lenyewe
    2. yenyewe
    3. enyewe
    4. mwenyewe
  10. Wageni walikula wali ______________________________________ nyama
    1. na
    2. pia
    3. kwa
    4. tena

INSHA  

Andika insha ya kusisimua kuhusu:

UMUHIMU WA MITI

MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. C
  4. A
  5. C
  6. A
  7. A
  8. A
  9. C
  10. D
  11. A
  12. C
  13. C
  14. A
  15. A
  16. B
  17. C
  18. D
  19. D
  20. D
  21. A
  22. B
  23. A
  24. D
  25. C
  26. C
  27. D
  28. B
  29. A
  30. C