Wednesday, 05 July 2023 13:16

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 3 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo.

Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kuzinduliwa kwa katiba mpya ___1__ sana mtoto msichana. Hapo awali jamii tele sana ___2__ sana. Kuna vyakula kama mayai ambavyo ___3___ wanaume. Hata ___4__ zinazohitajika nguvu nyingi ziliachiwa wavulana.__5____ hapo awali, siku __6__ hadhi ya mtoto msichana ___7__ sana. Wakati huu elimu ya mtoto msichana inaenda __8___ na ile ya mvulana.

 
 1  ilimsaidia  zilimsaidia   mlimsaidia  kulimsaidia 
 2  ilimyanyasa  zilimyanyasa  ulimyanyasa   lilinyanyasa 
 3  ziliachwa  kiliachwa   iliachiwa   viliachiwa 
 4  kazi za sulubu  kazi za ujima   kazi za shokoa   kazi za gunda 
 5  Licha ya  Bighairi ya  Mbali na  Kinyume na 
 6  huu  hili   hizi   imevikwa 
 7  imeenezwa  imetia fora  imekwezwa  imevikwa vilemba
 8  mtawalia  mkabali   sadakta   sambamba 


Zamani __9___ zilimtweza msichana na alichukuliwa kama kitega uchumi. Alisubiri akomee ili __10__ na wazazi wake kupokezwa mahari. __11___ jamii hata ziliwatuma ___12__ kupeleka habari za posa pindi tu msichana __13___. Dunia imebadilika na ___14__ anayejifanya hajui kila kitu kiko wazi. Atajionea. Kumbuka ___15__.

 
  9  nyingi  mingi   wengi   mengi 
 10  aoe  aozwe   aoleshwe   ndoa 
 11  Kati ya  Baadhi ya   Miongoni mwa   Katikati ya 
 12  washenga  manyakanga   wahandisi   makuli 
 13  alipozaliwa  alikozaliwa   alimozaliwa   aliyezaliwa 
 14  yeyote  wowote   wote   yote 
 15  Bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi  Kinga na kinga ndipo moto uwakapo   huwezi kulificha jua kwa ungo  mwana wa ndugu kirugu mjukuu mtu wa mbali 


Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu sahihi.

 1. Kanusha sentensi ifuatayo:
  Barabara iliyokarabatiwa haijaharibika tena
  1. Barabara ambayo ilikarabatiwa haikuharibika tena
  2. Barabara isiyokarabatiwa haijaharibika tena
  3. Barabara iliyokarabatiwa haijaharibika tena
  4. Barabara iliyokarabatiwa haijaharibika tena
 2. Chagua usemi wa taarifa ulo sahihi "Mkutano utaanza saa tisa jion kesho," Kinara alisema.
  1.  Kinara alisema kuwa mkutano ungeanza saa tisa jioni siku ambayo ingefuata
  2. Kinara alisema kuwa mkutano ulianza saa tisa jioni siku iliyotangulia
  3. Kinara alisema kuwa mkutano unaanza saa tisa jioni siku ifuatayo.
  4. Kinara alisema kuwa mkutano ungeanza
 3. Unganisha sentensi zifuatazo:
  1. Unaweza kulinunua gari
  2. Usimalize akiba yako
   1. Unaweza kulinunua gari lolote angalau usimalize akiba yako
   2. Unaweza kulinunua gari lolote mradi usimalize akiba yako
   3. Unaweza kulinunua gari lolote ilhali usimalize akiba yako
   4. Unaweza kulinunua gari lolote seuze usimalize akiba yako
 4. Andika wingi wa:
  Baraza la mtihani la taifa limetoa tangazo
  1. Baraza la mtihani ya taifa limetoa matangazo
  2. Mabaraza ya mitihani ya mataifa yametoa matangazo
  3. Baraza za mitihani za mataifa zimetoa matangazo
  4. Mabaraza ya mitihani ya kitaifa yametoa matangazo
 5. Chagua sentensi iliyotumia -amba- kwa usahihi:
  1. Karai ambalo lililopotea ni lake
  2. Miguu ambazo zilizojeruhiwa ni za jirani
  3. Ujumbe ambao uliwafikia ni wa kweli
  4. Kitabu ambacho kilichopatikana kimechorwa simba
 6. Kutokana na kitenzi ‘iga' tunapata nomino
  1. Mwigo
  2. Igiza
  3. Igika
  4. Igizeni
 7. Chagua sentensi yenye kielezi kinachoelezea mengi kuhusu kivumishi
  1. Daktari alimtibu vyema mwathiriwa huyo wa ajali
  2. Tulihuzunika zaidi baada ya timu yetu kushindwa
  3. Mwanamuziki hodari zaidi atatuzwa zawadi nyingi
  4. Yeye ni mzuri kama jamaa hao
 8. Chagua aina za maneno yaliyopigiwa kistari.
  Wageni wale walialikwa tena lakini wengine hawakualikwa.
  1. Kivumishi, kielezi, kiwakilishi
  2. Kiwakilishi, kihusishi, kielezi
  3. Kielezi, kihusishi, kiwakilishi
  4. Kihusishi, kivumishi, kielezi
 9. Chagua kitenzi kilichoundwa kutokana na nomino:
  1. Mvumilivu - uvumilivu
  2. Mwaminifu - aminika
  3. Mapishi - pikika
  4. Wacheshi - ucheshi
 10. Ni mpangilio upi ufaao kwa vifungu vifuatavyo ili kuleta maana kamili?
  1. sharti lishughulikiwe
  2. Uhifadhi wa mazingira
  3. na kila mzalendo
  4. ni jambo ambalo
   1. (ii), (iv), (i), (iii)
   2. (i), (iv), (iii), (ii)
   3. (iii), (iv), (i), (ii)
   4. (ii), (iii), (i), (iv)
 11. Chagua methali zenye maana sawa:
  1. Usipoziba ufa utajenga ukuta
  2. vyote vyowevu si maji
  3. Samaki mkunje angali mbichi
  4. Usidharau kiserema chalima kuliko jembe
   1. (i), (iv)
   2. (i), (ii)
   3. (i), (iii)
   4. (iii), (iv)
 12. Chereno na Rahma ni mabibi zake Rashidi..
  Je, ndoa ya aina hii huitwaje?
  1. Mkemwenza
  2. Mitala
  3. Mwanyumba
  4. Nasaba
 13. Chagua sentensi yenye ‘karibu' na 'takriban'
  1. Mjomba anaishi karibu na mji huo
  2. Darasa hilo lina karibu wanafunzihamsini
  3. Mruka viunzi alikuwa karibu kuanguka
  4. "Karibuni kwenye kipindi chetu," mtangazaji alisema
 14. Nomino mate, mawaidha na manukato ni nomino katika ngeli gani?
  1. LI - YA
  2. I - I
  3. YA - YA
  4. U - YA
 15. Eleza matumizi ya -ni- katika sentensi ifuatayo:-
  Juma alicheka kwa sauti nilipoanguka chini:
  1. Nafsi
  2. Sababu
  3. Wakati
  4. Mtendaji

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Tarafa ya Kwasi ilikuwa maarufu kutokana na bidii za mchwa za wakazi wake. Uchumi wa tarafa nzima ulitegemea kilimo licha ya kuwa wenyeji wa eneo hili hawakuwa na mashamba makubwa bali vikataa vidogo vidogo tu. Hata hivyo wanatarafa hawa walijua jambo moja, kuwa ukilima pantosha, utavuna pankwisha na kwa hivyo walifanya bidii kubwa katika kilimo chao. Licha ya udogo wa vikataa hivyo, waliweza kupata mazao ya kazole kila msimu wa kuvuna ulipowadia. Tatizo kuu walilopambana nalo lilikuwa usambazaji na uuzaji wa mazao yao. Lakini kwa bahati nzuri pale tarafani palikuwa na mkulima mmoja wa miaka mingi. Yeye alikuwa na shamba kubwa na alinuia kuoa na kumfunza mwanawe mbinu bora za kilimo. Lengo lake lilikuwa mwanawe awe maarufu katika zaraa.

Si miaka mingi sana iliyopita. Mkulima huyu alifunga harusi ya kukata na shoka na ua la moyo wake, Bi Maridhia. Baada ya kuishi miaka minne wakitafuta mwana wao, Mola aliwafungulia njia. Bi Maridhia akajifungua totoshoo, mtoto si mtoto. Hungemwangalia mara moja. Alikuwa mrembo kuliko huralaini wa peponi. Kwa jina walimwita Baraka. Ujio wa Baraka uliwapa furaha kuu.

Kwa furaha hiyo walimwangusha karamu ya kukata na shoka. Yakini si yamkini Baraka alianza safari yake ya maisha kwa furaha. Utotoni alikuwa danga la mwana. Alikuwa mwenye tabia bulibuli. Maadamu waliishi unono, alilelewa kwa tunu na tamasha. Chochote kile alichokitamani alipewa na hata kuongezewa.

Kwake msamiati 'sina' au hakuna hakuujua. Alipata kila kitu labda kiwe hakikupatikana madukani. Naye Baraka shuleni alikuwa wembe uliokata kuwili. Alifuata nyay za wazazi wake ambao licha ya kuwa na vyao hawakudekeza hisia zozote za ugoigoi masomoni.

Baraka pia alikuwa mcha mungu. Alikuwa ngoi aliyewafurahisha waumini wa kanisa lao. Alisoma msahafu kwa uaminifu. Isitoshe hata wakati mwingine alisimama mimbarini na kuhubiri.

Waswahili husikika wakisema kuwa muda hupaa kama ndege. Baraka alijipata amejiunga na shule moja ya kifahari huko ng'ambo. Akiwa huko alitangamana na wanafunzi wa matabaka mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia. Licha ya kuwa na furaha ya kupata nafasi hiyo ya kipekee iliyotamaniwa na wengi aligubikwa na huzuni. Kule alijipata katika kisiwa cha ukiwa na upweke. Nayo asilimia kubwa ya wanafunzi ilikuwa na mienendo iliyozorota. Mavazi ya wengi yalipwayapwaya, mazungumzo yasiyozingatia tasfida na nywele zilisukwa kivoloya.

Jinsi muda ulivyozidi kumsonga, ndivyo Baraka alivyozidi kuhusudu tabia za wenzake. Hii ni kwa sababu alichelea kuitwa limbukeni asiyetaarabika. Alishawishika kufuata rubaa. Haukupita muda mrefu ambako aliyazika maadili yake katika kaburi la sahau. Baraka alipotoka kitabia na kupoteza matumaini.

Baraka hakuona sababu ya kuwasiliana na jamaa kule nyumbani kama ilivyokuwa kawaida yake. Alijiona aliyekomaa. Hakujali la togo wala la jando. Chochote alichokiona au kusikia aliiga tu.

Maadamu alikuwa Mwafrika, aliamua kujimbambua ngozi ili awe kama wazungu. Alianza kujutia kuzaliwa Afrika. Yeye hakujali methali isemayo mwacha mila ni mtumwa. Isitoshe, alitamani kubadili umbo la kiwiliwili chake ili awe na kiuno cha nyigu cha kufungasha na nywele za singa. Yote haya aliyadhaminia mapenzi ya wavulana.

Baraka alibahatika kumpata daktari wa kutibu ugonjwa wake. Kwa kutumia karo alienda kufanyiwa upasuaji. Alipeusha rangi ya ngozi yake. Vilevile alifanywa kuwa na umbo la kuwapendeza aliowalenga. Akawa amefanana na wazungu wenyewe.

Anasa zilimnasa. Masomo nayo yakasukumwa mlango wa nyuma. Kazi yake ikawa ni kuzurura kutoka klabu moja hadi nyingine. Wakati akifanya haya, wazazi walijua kuwa alikuwa akibingirisha gurudumu la maisha. Laiti wangalijua kuwa Baraka kabadilika.

Ajabu huajabiwa. Kumbe Baraka alikuwa amejipalia makaa. Alianza kuugua saratani ya ngozi. Nywele, kope na nyusi zilimnyonyoka. Uso wake ulisawajika na kupata mabaka na makunyazi. Vidonda vilishika usukani. Akawa hatazamiki hata mara moja. Halimashauri ya shule iliamua kumrudisha nyumbani akiwa hali mahututi. Alikuwa hajiwezi. Wazazi wake walipomwangalia hawakumtambua. karibu hakuwa yeye. Kovu lililokuwa shingoni ndilo liliwafanya wamtambue. Baada ya muda mfupi, Baraka aliaga dunia. Mama yake naye kusikia hivyo, alizirai na kuipungia dunia mkono wa buriani. Ikawa huzuni si huzuni katika jamaa iliyokuwa na utulivu.

 1. Ni kauli gani isiyo ya kweli kulingana na aya ya kwanza?
  1. Wakazi wa Kwasi walitegemea kilimo licha ya udogo wa mashamba
  2. Licha ya mashamba haya kuwa madogo wakazi walipata mazao mengi
  3. Katika eneo la Kwasi ni mkulima mmoja tu alikuwa na shamba kubwa
  4. Licha ya wakazi kubarikiwa kuwa na mazao ya kutosha, soko liliwatatiza
 2. Hii ni tamathali gani ya lugha iliyotumika katika kauli hii:
  Alikuwa mrembo kuliko huralaini wa peponi.
  1. Chuku
  2. Kinaya
  3. Ishara
  4. Tabaini
 3. Danga la mwana ni
  1. mtoto aliyelelewa na kudekezwa
  2. mtoto anayepata masomo ya ng'ambo
  3. mtoto anayezaliwa baada ya wazazi kusubiri kwa muda mrefu
  4. mtoto anayelelewa vizuri
 4. Kulingana na aya ya tatu Baraka aliku mwerevu shuleni kutokana na
  1. vitabu vingi alivyonunuliwa na wazazi wake
  2. ukweli kwamba, wazazi wake walipenda mtoto mwenye bidii masomoni
  3. shida nyingi iliyokuwa nyumbani kwao
  4. ukweli kuwa wanafunzi wengi shuleni walipenda michezo kuliko masomo
 5. Kuhusudu tabia za wenzake ina maana ya
  1. kuchukia tabia za wenzake
  2. kuandama tabia za wenzake
  3. kuvutiwa na tabia za wenzake
  4. kusikia tabia za wenzake
 6. Si kweli kusema kuwa,
  1. Baraka aliionea fahari asili yake
  2. Baraka hakupendezwa na maumbile yake
  3. Baraka alitamani kuwa kama mzungu
  4. Baraka alitaka kuwa na umbo ambalo lingewavutia wavulana kwake
 7. Kulingana na kifungu ulichosoma
  1. wazazi wa Baraka hawakuwa na mwao kuhusu tabia za mwana wao
  2. baba yake Baraka alipata fadhaiko la moyo akakata kamba
  3. baada ya kusikia kuhusu kifo cha Baraka, mama yake alirukwa na kichwa.
  4. Baraka aliaga dunia pindi tu baada ya kufika katika uwanja wa ndege
 8. Kifungu chaonyesha wazi kuwa
  1. wazazi wake Baraka waliaga dunia
  2. Baraka aliwapa wazazi wake fahari kubwa baada ya kurejea kutoka ughaibuni. 
  3. lilikuwa kosa kubwa kwa wazazi kumpeleka Baraka kwa masomo ya juu
  4. Baraka aliwapelekea wazazi wake aibu kubwa
 9. Kulingana na kifungu ulichosoma, ni kauli gani ambayo si ya kweli?
  1. Wazazi wa Baraka walikaa kwa miezi arubaini na minane bila kujaliwa mtoto
  2. Kuzaliwa kwa Baraka kuliwapa wazazi wake furaha kubwa
  3. Baraka alikuwa msichana mrembo sana alipozaliwa
  4. Baba yake Baraka alimlaumu Bi. "Maridhia kwa kukawia kupata mtoto
 10. Ni methali gani mwafaka kujumlisha ujumbe wa kauli hii?
  Mama yake naye kusikia hivyo alizirai na kuipungia dunia mkono wa buriani.
  1. Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo
  2. Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
  3. Kifo ki karibu ki kisogoni pako
  4. Ajali haina kinga wala kafara.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50

Mengi yamesemwa kuhusu utiifu. Ukweli ni kuwa, watu wengi hudhani kuwa maisha yangekuwa mazuri ikiwa kila mtu angeruhusiwa kufanya atakavyo. Kulingana na mimi, ni makosa kufikiria hivyo madhali mienendo isiyodhibitiwa na sheria ni kiini cha vurugu na ukiukaji wa sheria nchini. Hebu fikiria hali ingekuwa vipi ikiwa mwendeshaji pikipiki angeiendesha kulia na kushoto katikati ya barabara na kupuuza sheria za trafiki? Hali kama hii huweza kusababisha msongamano mkubwa wa magari mjini, hivyo kuwafanya watu wachukue muda mrefu kabla ya kufika waelekeapo. Kutengenea au kuwa shwari kwa mambo hutokana na kila mtu kutafuta kanuni zote zilizowekwa.

Kila mtu hana budi kuelewa kuwa utiifu si udhaifu au woga. Ni hali ya kutambua kuwa kutii utawala wa kisheria huhakikisha kuwa kuna muumano na utangamano wa kijamii. Utiifu una maana ya kufanya yanayotarajiwa. Vilevile utiifu una maana ya kutambua na kukubali kuwa kufanya matendo mema ni bora zaidi kuliko kutekeleza jambo au matendo ya kibinafsi tu. Kwa hakika ni vyema kutafakari kuhusu tunayoambiwa na wenzetu au hata watu wengine. Hatufai kufuata kila maagizo tunayopewa bila kuyatathmini vizuri. Mathalani; ikiwa mtu atakuambia ujihusishe na ujambazi, unafaa kukataa.

Ukweli ni kuwa katika maisha ya kila siku, tunatii kanuni nyingi bila kufahamu au kujua. Hakuna mtu kwa mfano anayetulazimisha kuzingatia lishe bora au kufuata maagizo ya daktari. Wengi wetu huhudhuria shule au kazini kwa wakati ufaao bila kushurutishwa. Ikiwa kwa mfano una gari unalomiliki, hakuna anayekukalifu kulipeleka kwenye gereji likatengenezwe au likakarabatiwe. Hebu jiulize hapo ulipo; je, kwa nini watu hufanya mambo kama haya bila a kuagizwa au kukahiriwa? Ukweli ni kuwa, tendo lolote lile la kutotii au kutotekeleza yale yanayohitajika litakuwa na matokeo mabaya au hata ya kuhatarisha maisha ya watu.

Wanafunzi shuleni wanatakiwa kuvaa sare nadhifu. Wabunge nao wanafaa kuvaa suti. Bwelasuti ni kwa makanika. Hata hivyo wengi hawatii wala kuheshimu uvaaji. Hapo awaliamii nyingi zilikuwa zikithamini maadili sana. Hata hivyo sasa maadili ya jamii zetu yanazoroteka kwa kasi kiasi cha kushangaza. Hali hii imeletwa kutokana na mwingiliano mwingi wa taifa letu na yale ya kigeni. Mwingiliano huu unaweza kuleta upungufu wa maadili. Kwa watu wengi na hususan vijana, kwao upotovu wa maadili ndio ustaarabu ufaao. Kusifu au kuiga nyendo mbaya huchangia upalilizi wa uozo wa tabia. Hali kama hii ikiruhusiwa kuendelea inaweza kuifuja nchi yetu.

Vijana wengi hawataki kutii sheria za uvaaji. Wafaa wakumbuke kuwa mavazi yanaweza kumtukuza au kumtweza mtu. Hali hii italingana na vazi lenyewe, hadhira lengwa, wakati na hata cheo cha mvaliaji. Hebu fikiria askari akivalia bombo na kizibao huku amebeba bunduki yake, mwalimu naye avalie chepeo, kaptura na ndara miguuni, mkunga naye avalie suruali ya kumkaba mwili na blauzi nyembamba katika zanahati yake. Zote nilizotaja ni nguo lakini wanaozivaa ndio hawatii mahali na kanuni za jamii.

Jamii zetu hutuzaini tuweze kuvalia nguo zetu za kijadi wakati wa sherehe. Kama nilivyokuelezea, wabunge wetu hawaruhusiwi kuingia bungeni bila suti na asiyetii hupigwa marufuku. Je, inamaanisha wakivalia fulana waheshimiwa wetu watakuwa uchi? La hasha. Ni vile tu kwa kuvalia fulana waheshimiwa wetu watakuwa wamekiuka kanuni za bunge. Bila vikwazo hivi, baadhi ya waheshimiwa wangekuwa na vibindo vya kutia pesa zao. Bunge ni jumba la heshima linalostahili heshima zake

Nilishasema vijana ndio hawataki kutii katika masuala ya mavazi. Hawa ndio walio katika mstari wa mbele kukosoa mavazi ya jadi. Wengi wao wamelewa na usasa na hawaoni chochote kizuri kutoka jadi. Ni vibaya sana kukosoa mavazi yetu ya kale kwa kuwa yangali na bado yako na mvuto wake. Joho, vilemba, shanga na migwisho ilikuwa na maana kubwa katika vyeo vya wazee wetu. Mzee angelia kigoda akiwa amevaa vazi la utawala, heshima ilikuwa ikiongezeka maradufu.

Siku hizi sote tumekuwa mateka wa kigeni. Mitindo yetu ya uvaaji ni shaghalabaghala. Si rahisi kumtambua msichana au mvulana, mzee au kijana aidha mwanaume au mwanamke. Wote wanadai kuwa chochote kinachoingia mjini ni halali. Hii ndiyo sababu utawaona wavulana wetu wakivalia vipuli, vikufu na hata kusuka nywele. Ya wasichana sisemi kwa kuwa niliyokutajia ya wavulana ni lele.

Mavazi huvaliwa ili kujisetiri. Tuzipe kazi zetu heshima. Tuipe miili yetu heshima. Tukifanya haya yote na tusipokaidi wito, heshima itaturudia. Utiifu ni suala muhimu sana katika maisha ya binadamu.

 1. Aya ya kwanza imeonyesha wazi kuwa
  1. kufanya mtu atakavyo huliletea taifa furaha na ufanisi
  2. ni vibaya kudhibiti sheria za raia maadamu kufanya hivyo ni kuwanyima furaha
  3. uendeshaji ovyoovyo wa pikipiki husababisha kifo kwa mwendeshaji
  4. kufuata kanuni zote zilizowekwa hufanikisha mengi
 2. Ni methali gani mwafaka kuelezea ujumbe wa kauli hii?
  Kwa hakika ni vyema kutafakari kuhusu tunayoambiwa na wenzetu au hata na watu wengine.
  1. Enga kabla ya kujenga
  2. Cha mwenzetu kikinyolewa tia chako. maji
  3. Hakuna bahari isiyo mawimbi
  4. Habari ya nyumbani simfunulie jirani
 3. Aya ya nne imeonyesha wazi kuwa, kuzorota kwa maadili kunasababishwa na
  1. matukio na maisha ya kisasa
  2. kupenda na kuzifuata nyendo mbaya.
  3. kusifu na kuzifuata tabia zote za kigeni
  4. kufikiri tu kuhusu mataifa ya kigeni
 4. Kulingana na kifungu, ni nini hasa kinaharibu nchi yetu.
  1. Wananchi wachache wanaojivunia maadili yetu
  2. Vijana wengi wanaozidi kuiga maadili yafaayo
  3. Wazee walioshindwa kuwaongoza
  4. Kufuata ustaarabu wa kigeni na kupuuza maadili
 5. Vyote hivi ni vigezo vya kuzingatia mtu anapovaa ila
  1. watu unaolenga kukutana nao
  2. mtindo wa vazi lenyewe
  3. maneno yanayolengwa kuzungumzwa
  4. mamlaka ya anayevaa
 6. Kulingana na aya ya tano, ni kweli kusema
  1. kuna nguo nzuri na mbaya
  2. hakuna maana ya kuvaa nguo
  3. hakuna nguo nzuri au mbaya
  4. nguo nzuri ni zile zinazovaliwa katika shughuli maalum
 7. Kifungu kimeonyesha wazi kuwa,
  1. ukiingia makao ya bunge ujue lazima uvae tai na suti ya buluu
  2. makao ya bunge ni rasmi yenye utaratibu wake wa uvaaji
  3. makao ya bunge hushurutisha watu kuvaa kwa njia inayofanana
  4. katika makao ya bunge, bila suti afananishwa na aliye uchi
 8. Ni wazi kuwa vijana wanasahau
  1. mavazi ya kale ni vitambulisho vya nchi ya kisasa
  2. mavazi ya kale ni vitambulisho vya serikali kihistoria
  3. mavazi ya kale ni vitambulisho vya elimu kulingana na historia
  4. mavazi ya kale ni vitambulisho vya jamii kihistoria
 9. Zamani
  1. haikuwa rahisi kumtambua msichana katika kundi la wavulana
  2. wasichana na wavulana walivalia mavazi sawa
  3. mavazi yalivaliwa kulingana na jinsia
  4. watu walivalia mavazi sawa
 10. Fulana ni
  1. vazi linalovaliwa ndani ya shati
  2. vazi linalosukwa kwa nyuzi ambalo huvaliwa juu ya shati
  3. vazi linalofumwa kwa nyuzi kujikinga na baridi
  4. vazi lisilo na mikono linalosukwa kwa kutumia nyuzi

INSHA

Endeleza:

Tulipofungua mlango huo, hatukuweza kuzuia hisia. Tulitoa mayowe kwi!kwi!kwi! kwa yale tuliyoshuhudia...

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. D
 2. B
 3. D
 4. A
 5. D
 6. C
 7. C
 8. D
 9. A
 10. B
 11. B
 12. A
 13. A
 14. A
 15. C
 16. D
 17. A
 18. B
 19. B
 20. C
 21. A
 22. C
 23. A
 24. C
 25. A
 26. C
 27. B
 28. B
 29. C
 30. A
 31. C
 32. A
 33. D
 34. B
 35. C
 36. A
 37. A
 38. D
 39. D
 40. B
 41. D
 42. A
 43. B
 44. D
 45. C
 46. C
 47. B
 48. D
 49. C
 50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 3 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students