Monday, 27 February 2023 06:48

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 3

Share via Whatsapp

 INSHA

Anzisha insha yako kwa maneno haya:

Siku tuliyosubiri kwa hamu na ghamu iliwadia, hivyo basi sote .........

QUESTIONS

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi hadi 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Kuoga ni ___1___ shartyi mtu ___2___kila wakati au kila siku. Hasa watoto ___3___kuoga ama kuogeshwa mara kwa mara. Watoto ___4___ jasho ___5___ wanapocheza. Jasho ___6___ huchanganyika na vumbi___7___ mahali ___8___. Nao wanapata ushafu. Baada
ya kupata uchafu ___9___ , ni lazima waoge. Tusipowasaidia watoto kutunza usafi ___10___ mili ___11___hawatakuwa na afya bora. ___12___magonjwa kama vile upele na harara ya ngozi. Usafi si muhimu kwa watoto tu ___13___ pia kwa watu ___14___. Hao ___15___
wasipooga ni hatari zaidi kuliko hata watoto wadogo

   A   B   C   D 
 1.   hiari   faradhi   kutaka   ngumu 
 2.   haogi   kuoga  aoge  anaoga 
 3.  hupasa   hupasua   hapaswa   hupaswa
 4.  hutoa  hutoka  hutia  hutokwa
 5.  mingi  nyingi  jingi  mengi
 6.  hilo  hiyo  huo  hizo
 7.  ya  za  la  vya
 8.  wanacheza   wanauchezea   wanapochezea   wanapocheza 
 9.  huo  hiyo  hilo  hizo 
 10.   ya  za  wa  la
 11.  zao  yao  lao  cha
 12.  watungua  wataugua  wataangua  watapungua
 13.  mbali  bali  wala  ili
 14.  wazima  wazimu  wasafi  yeyote
 15  ndipo  ndiye  ndio  ndivyo

 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, chagua jibu lililo sahihi.

  1. "Sabalkheri wanafunzi," Mwalimu aliwasalimia wanafunzi wake. Huo ulikuwa wakati wa
    1. adhuhuri
    2. asubuhi
    3. jioni
    4. alasiri
  2. Chagua sentensi yenye kivumishi kiulizi
    1. Mashubaka haya yalitengenezwa lini?
    2. Leo wameapishwa wangapi?
    3. Wasusi, wanaelekea wapi?
    4. Huyu atavikwa pete gani?
  3. Andika sentensi hii kwa wingi
    Mtume huyo ana tunda hili
    1. watume hawa wana matunda haya
    2. Mitume hao wana matunda hizi
    3. Watume hao wana matunda haya
    4. Mitume hao wana matunda haya
  4. Miongoni mwa sehemu hizi za mwili ni sehemu ipi iliyo tofauti na zingine?
    1. Paja
    2. Kiganja
    3. Pafu
    4. Goti
  5. Methali inayofaa funzo kuwa;
    Mtu anaposababisha shida huishia kuwahusisha watu wake au jamaa yake ni 
    1. Kikulacho ki nguoni mwako.
    2. Mwiba wa kujichoma huambiwi pole.
    3. Mla nawe hafi nawe ila mzaliwa nawe. 
    4. Mchuma janga hula na wa kwao.
  6. Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri
    1. Lo? Amefika?
    2. Viti vyenu ni vipi?
    3. njoo nikutume!
    4. "mimi sisemi na mtu"
  7. Tumia kivumishi '-enye-'kwa njia sahihi
    Mbuzi____________madoadoa ni wangu.
    1. lenye
    2. chenye
    3. yenye
    4. mwenye
  8. Kamilisha methali hii
    Hakuna ____________________________________ yasiyo na mbu.
    1. masika
    2. vuli
    3. kiangazi
    4. kipupwe
  9. 'kazi ya kijungu jiko, 'ni kazi gani?
    1. kupika jikoni
    2. kukupatia riziki pekee
    3. kupika na kupakua
    4. kupika na jiko moja tu
  10. Nomino habari iko katika ngeli ya
    1. U-ZI
    2. I-I
    3. U-I
    4. I-ZI
  11. Chagua sentensi sahihi
    1. Viluwiluwi vile vilimezwa na samaki
    2. Mikebe hizo zimetupwa katika moto
    3. Ng'ombe hiyo ilikamuliwa maziwa
    4. mengi
    5. Wanajeshi wale walikuwa watiifu na wapole
  12. Wageni walikuja wakati ______________ tuliowangoja
    1. huu huu
    2. uo huo
    3. uu huu
    4. uo huu
  13. Ni saa ngapi sasa?
            C8MathT1BMQ28
    1. Saa kumi kasoro robo
    2. Saa nne kasoro robo
    3. Saa tisa kasoro robo
    4. Saa kumi na robo
  14. Andika kwa maneno tarakimu hii 8,000,001
    1. Milioni mia nane na elfu moja
    2. Milioni nane na moja
    3. Milioni mia nane na moja
    4. Milioni mi anane na mia moja
  15. Kipindi cha miaka mia huitwa
    1. muongo
    2. majira
    3. karne
    4. milenia

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kutoka 31-40.

Ni jambo la busara kwetu vijana kusikiliza mashauri tunayopewa na watu wazima kama vile wazazi na walimu kwani wametuzidi kwa maarifa. Ama kwa hakika,lolote lile wakuu wetu hutu.unbia yafaa tuzingatie tusije kufikwa na balaa iliyomfika kijana matatizo.

Matatizo alikuwa kijana mwenye sura nzuri na tabasamu ya kuvutia. Kwa nje aliweza kuwavutia wengi hasa wasiomjua. Hata hivyo, hakuna kizuri kisicho na dosari. Matatizo alikuwa na hulka mbaya isiyopendeza kwa watu wengi. Alikuwa mkali kama pilipili na mkaidi mfano wa mkia wa nguruwe. Tabia yake iliwashinda hata wazazi wake ingawa hawakusita kummwagia bahari ya maneno ya busara kwa tamaa ya kumwokoa.

Baadaye alipopelekwa shule angalau apate kisomo cha kumwekea nguzo maishani mwake, Matatizo alipatikana akishiriki visa vya ujeuri na kuwa mtundu. Visa hivi havikupungua, viliuma. Siku moja baba yake kijana huyu alishtuka alipojulishwa kuzidi kwa utundu wa mwanawe shuleni hasa alipoambiwa mtoto wake anapiga mtindi, hakosi sigara mdomoni na anashiriki wizi ili ajipatie pesa za kujitimizia haja zake. Matatizo alifukuzwa shule. Vitendo vya matatizo vilimtahadharisha mzee Toboasiri.

Wakati mmoja siku ya Jumapili alfajiri, mzee Toboasiri alijikuta ameshika mkongojo wake akienda kwake mzee Busara wakiwa na mzee Saidia.

Aliwaalika mkutano wa dharura nyumbani kwake siku iliyofuata. Wazee hawa wawili walipowasili, walimkuta Toboasiri na mtoto wake Matatizo wameketi kimya. "Wazee wenzangu," alianza huku sauti yake ikionyesha masikitiko, "Nimewaita hapa ili mnisaidie kumpa mawaidha kijana wangu. Nimejaribu niwezavyo kumkanya mwanangu dhidi ya matendo maovu lakini nimeshindwa. Nawaomba wazee wenzangu mnifanyie kazi hiyo."

Wazee hawa wawili walimshauri na kumshawishi Matatizo aache ile tabia yake mbaya. Kabla hawajamaliza, Matatizo alisimama huku akipandwa na hasira. Alifoka na kuwakodolea wale wazee macho huku amekunja uso wake na kuonekana kama jitu lililonyimwa chakula mwezi mzima.

Hapo alitoka nje, akawasha sigara kubwa na kupiga mikupuo miwili. Macho yakageuka na kuwa mekundu kami. pilipili. Akarudi na kumkabili mzee Busara. "Kwa vile unaitwa Busara, unadhani unahaki ya kunipa mawaidha, leo utanitambua. "Alimzaba mzee Busara kofi moja pa! Mzee huyu hakushimili kofi hilo na hapo akaanguka chini pu!

  1. Kulingana na aya ya kwanza, anayezungumza ni
    1. Toboasiri
    2. Matatizo
    3. Busara
    4. Mwandishi
  2. "Yafaa tuzingatie ya wakuu wetu tusije tukakumbwa na yaliyomkabili Matatizo" Ni methali gani isiyoambatana na maelezo haya?
    1. Usipoziba ufa utajenga ukuta
    2. Asiyesikia la mkuu hupatwa na makuu
    3. atangaye sana na jua hujua
    4. sikio la kufa halisikii dawa
  3. Kulingana na aya ya pili ni ipi si sifa ya matatizo?
    1. Alitemea mate nasaha za wazazi wake.
    2. Matatizo alikuwa mtanashati.
    3. Matatizo alikuwa mkaidi na mjanja.
    4. Tabia zake ziliambatana na sura yake.
  4. Lengo la Matatizo kupelekwa shuleni ni
    1. kupata masomo ili kuboresha maisha yake
    2. kuwafurahisha wazazi wake
    3. kuendelea kudumisha hulka yake
    4. kuelimika ili azidishe hulka yake
  5. Kulingana na kifungu hiki. Matatizo 
    1. Alibadilika alipoenda shuleni
    2. Alishiriki katika uvutaji sigara na kunywa pombe
    3. Alifanya bidii katika masomo yake
    4. Aliepukana na hulka ya wizi
  6. Baba yake matatizo ni
    1. mzee saidia
    2. mzee Busara
    3. Mzee Toboasiri
    4. Mwalimu mkuu
  7. Ni kweli kusema kuwa
    1. Baba yake matatizo alikuwa amefika mwisho
    2. Wazee walipoitwa hawakutoa nasaha
    3. Mkutano ulipangwa kwa siku nyingi
    4. Matatizo alitekeleza yote aliyoambiwa 
  8. 'kupiga mtindi' ni maneno yaliyotumiwa. Ni tamathali gani ya lugha?
    1. Istiari
    2. Nahau
    3. Methali
    4. Tashbihi
  9. Methali inayomlenga matatizo katika aya ya mwisho ni
    1. sikio la kufa halisikii dawa
    2. ushikwapo shikamana
    3. la leo litende leo
    4. aliyekalia kigoda mtii
  10. Neno 'foka' namna ilivyotumiwa katika kifungu hiki halima maana
    1. kughadhabika
    2. kuwa na mafutu
    3. kuwa na huzuni
    4. kupandwa na mori

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali ya 41-50.

Kulonga dhahiri shahiri Kiswahili ni mojawapo ya lugha za kimataifa zinazozungumzwa ulimwenguni. Hata hivyo inasikitisha sana sisi wenyeji wa eneo la Africa Mashariki ambao ni kitovu cha lugha hii, tumekuwa tukinyonga raslimali hii kwa ukatili mkubwa.

Ni aibu iliyoje kukitumia Kiswahili kiholela bila kuzingatia kanuni zake huku tukijidanganya kuwa sisi ni mahiri tunapokiporomosha Kimombo kwa usanifu mkubwa. Jinsi tunavyokitema kiingereza sawasawa. Kwa nini hali hii tusiizingatie katika lugha yetu tunu? Wageni kutoka nchi za ughaibuni waliopata fursa ya kuzuru eneo la Afrika Mashariki wametambua utamu wa Kiswahili wakajifunza wakajistawisha. Baadhi ya wageni hao wamekuwa walimu wa lugha hii.

Aidha tunazidi kukitia kitanzi Kiswahili kupitia uchapishaji wa magazeti yetu. Bei ya gazeti la kiswahili inaashiria uduni wake. Habari zinazochapishwa katika magazeti ya kiswahsili ni za kiwango cha chini na ni chache mno cha kuudhi zaidi ni kuwa baadhi ya kaifa za magazeti ya kiswahili hujikuta katika masuala ya kijamii kwa kiasi kikubwa na kuyapa kisogo au kugusia gusia tu mambo kuhusu uchumi,siasa na dini. Hakuna mazito kuhusu matangazo ya biashara. Hakuna habari ya vifo. Hakuna habari za ajira na kadhalika. Si ajabu wakati mmoja niliulizwa mtaani, "Hili gazeti ulilo nalo umemnunulia babu yako?" Swali hili lilinijulisha kuwa fikra za waja wengi imejengwa na mtindo wa wakati mrefu wa kuchapisha magazeti kwa njia hii; hivi kwamba magazeti ya kiswahili yanapaswa kusomwa na wazee na labda wale walioshindwa na masomo skulini.

Nawasihi wananchi wa eneo lote la Afrika Mashariki wazinduke na kukiendeleza kiswahili.

  1. Kulonga dhahiri shahiri ni sawa na;
    1. kunena ukweli
    2. kuamba bila hadaa
    3. kupiga vijembe
    4. kuongea waziwazi
  2. Maneno tunavyo kitema kiingereza yamepigiwa mstari. Maana yake ni
    1. Tunavyokikaia kiswahili
    2. Tunavyokikata kiingereza
    3. Tunavyokiongea kimombo barabara
    4. Tunavyokizungumza kiingereza ovyoovyo
  3. Neno lipi katika taarifa hii lina maana sawa na kaifa
    1. picha
    2. habari
    3. kurasa
    4. vichwa
  4. Kwa mujibu wa taarifa ni kauli gani sahihi?
    1. Magazeti ya kiswahili yana bei ghali
    2. Magazeti ya kiswaili huwavutia wengi kuyasoma
    3. Bei ya magazeti ya kiingereza ni rahisi
    4. Magazeti ya kiswahili yamedunishwa
  5. Watu mahiri ni watu
    1. woga
    2. wajuzi
    3. walaghai
    4. washindani
  6. Tunazidi kukitia kitanzi kiswahili ni
    1. kukfrunga kiswahili
    2. kukipa sifa kiswahili
    3. kukiharibu kiswahili
    4. kukienzi kiswahili
  7. Visawe vya neno waja si pamoja na
    1. Mahuluki
    2. Adinasi
    3. Nswi
    4. Wanadamu
  8. Kulingana na taarifa hii asili ya lugha ya kiswahili ni
    1. nchi ya ughaibuni
    2. nchi ya Kenya
    3. Afrika mashariki
    4. Hatujaambiwa
  9. Mwandishi anawashauri wakazi wa eneo la Africa mashariki
    1. wasiitumie kiswahili hadharani
    2. waache kutumia kimombo
    3. wakipe kiswahili kipaumbele
    4. wakididimize kiswahili
  10. Kichwa kifaacho taarifa hii ni
    1. Lugha za Afrika-
    2. Mbinu za kuboresha Kimombo
    3. Historia za kiswahili na kiingereza
    4. Kiswahili kitukuzwe


MARKING SCHEME

  1. B
  2. C
  3. D
  4. A
  5. B
  6. B
  7. A
  8. C
  9. A
  10. C
  11. B
  12. B
  13. B
  14. A
  15. C
  16. B
  17. D
  18. D
  19. C
  20. D
  21. B
  22. D
  23. A
  24. B
  25. D
  26. D
  27. B
  28. A
  29. B
  30. C
  31. D
  32. C
  33. D
  34. A
  35. B
  36. C
  37. A
  38. B
  39. A
  40. B
  41. D
  42. C
  43. B
  44. D
  45. B
  46. C
  47. C
  48. C
  49. C
  50. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students