Wednesday, 15 March 2023 08:01

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 1

Share via Whatsapp

QUESTIONS

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi kutoka 1-15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manns.
Chagua jibu sahihi kati ya yale aliyopewa

__1__jamii humu nchini zilikuwa__2__majira ya mwaka badala ya miezi. Kwa mfano,majira ya mvua kubwa yaani__3__jua kali, upanzi na mavuno. Jamii zingine nazo ziliweka__4__ ya matukio maalum kama vile tohara, njaa, vita, mafuriko na uvamizi wa nzige. Yasemekana kuwa jamii moja __5__ikiishi Kusini __6__ukanda wa Ikweta __7__ mwezi wa __8__ "Jua kali" na mwezi wa Desemba ukaitwa mpe mjombako maji.

  1.                        
    1. Baadhi ya
    2. Baina ya
    3. Fauka ya
    4. Licha ya
  2.                    
    1. zinatumia
    2. zimetumia
    3. zikitumia
    4. zilitumia
  3.                
    1. mchoo
    2. vuli
    3. kipupwe
    4. kifuku
  4.              
    1. kumbusho
    2. kumbukumbu
    3. mafanikio
    4. madaftari
  5.                  
    1. iliyokuwa
    2. iliokwa
    3. waliyokuwa
    4. waliokuwa
  6.                      
    1. ya
    2. mwa
    3. na
    4. la
  7.                    
    1. waliuita
    2. iliita
    3. iitwa
    4. iliuita
  8.                
    1. Oktoba
    2. Octomba
    3. Oktomba
    4. Octobe

Hapo zamani za kale, __9__mtumwa mmoja ambaye alidhulumiwa sana na tajiri wake. Licha ya__10__kazi za sulubu kutwa kucha, alicharazwa__11__mijeledi. Mtumwa__12__kwa jina. Hasimu, hakuweza __13__tena mateso hayo.__14__akaamua kutorokea__15__kule, na liwe liwalo.

  1.                          
    1. kuliishi
    2. mliishi
    3. muliishi
    4. paliishi
  2.                
    1. kufanyishwa
    2. kufanyizwa
    3. kufanyia
    4. kufanyika
  3.                
    1. na
    2. ni
    3. kwa
    4. bila
  4.                
    1. buyo
    2. huu
    3. huo
    4. huyu
  5.                  
    1. kustahimili
    2. kudhamini
    3. kukabiliwa
    4. kukabidhi
  6.            
    1. Alipiga jeki
    2. Alipiga moyo konde
    3. Alipiga chafya
    4. Alipiga domo
  7.                
    1. kokote
    2. kwakwote
    3. popote
    4. momote

Kutoka swali la 16-10. jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa

  1. Ni uunganishi upi unaofaa zaidi wa sentensi hizi mbili?
    Mimi nitakuwapo. Wewe hutaniona.
    1. Mimi nitakuwapo halafu wewe hutaniona.
    2. Mimi nitakuwapo lakini wewe hutaniona.
    3. Wewe utakuwapo halafu mimi sitakuona
    4. Wewe utakuwepo lakini mimi sitakuona.
  2. Ki katika sentensi "Wageni wakifika watavalia kitamaduni," imetumiwa kuonyesha
    1. masharti, namna
    2. wakati, udogo
    3. masharti, nomino
    4. namna, nomino
  3. Ikiwa jana ilikuwa Jumapili, kesho kutwa itakuwa
    1. Jumatano
    2. Jumamosi
    3. Jumatatu
    4. Jumanne
  4. Kalamu ni kwa kuandikia, meno ni kwa
    1. kulia chakula
    2. kusagia chakula
    3. kutafunia chakula
    4. kukatia chakula
  5. Ni sentensi ipi sahihi?
    1. Huree! Tumeshindwa.
    2. Ng'o! Naomba maji.
    3. Hamadi! Amefaulu.
    4. Wallah! Watoto hawa wataadhibiwa
  6. Kamilisha: Baidika kama
    1. ardhi na mbingu
    2. mchuzi na ugali
    3. maziwa na tui
    4. pua na mdomo
  7. Chagua maelezo sahihi
    1. Susu-kifuniko cha chungu
    2. Ufu-nazi iliyokunwa
    3. Ukoko-chakula kilicholala mpaka asubuhi
    4. Bariyo-chakula kilichoganda kwenye chombo
  8. Chagua sentensi yenye kiwakilishi.
    1. Mwalimu anatembea kijeshi.
    2. Gari limeegeshwa kando ya barabara.
    3. Cha mlevi huliwa na mgema
    4. Watoto hawa ni watiifu
  9. Joka la mdimu ni kwa inda ilhali kutokuwa mwaminifu katika ndoa ni kuwa na
    1. mpango wa kawaida
    2. kisebusebu
    3. mkono mrefu
    4. jicho la nje
  10. Mtu anayehamia nchi nyingine na kuifanya makao yake huitwa
    1. mlowezi
    2. mkimbizi
    3. Mmtoro
    4. kibaraka
  11. Nyambua kitenzi 'tokota' katika hali ya kutendesha
    1. tokoza
    2. tokosha
    3. tokosa
    4. tokesha
  12. Akisami, kwa maneno ni
    1. subui kumi
    2. ushuri saba
    3. ushuru saba
    4. subui saba
  13. Chagua sentensi yenye kivumishi cha idadi katika orodha
    1. Mgeni wa mwisho amewasili.
    2. Daktari amewatibu wagonjwa watano.
    3. Waliingia wawili wawili kwenye jukwaa
    4. Vitabu vingi vimechafuka.
  14. Geuza sentensi katika kauli ya taarifa: Mwalimu aliwaambia wanafunzi, "Viwekeni vitabu vyenu safi kila siku."
    1. Mwalimu aliwamuru wanafunzi kuviweka vitabu vyao safi kila siku.
    2. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa anataka waviweke vitabu vyao safi kila siku.
    3. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa angetaka waviweke vitabu vyao safi siku zote.
    4. Mwalimu aliwaambia wanafunzi kuwa yeye hutaka waviweke vitabu vyao safi kila siku.
  15. Chagua kundi lenye wadudu pekee.
    1. Kipepeo, sigi, mende, panzi
    2. Bandi,nzige,nzi, njiwa
    3. Kiwavi, nyigu, kumbukumbi, kiroboto
    4. Mbu, utitiri, mkunga, kipepeo 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40
Nyangi alikuwa na furaha isiyo na kifani. Alikuwa ameyakamilisha masomo yake ya uzamifu huko Uingereza. Alikuwa mwenye buraha na furaha kwani ndiye aliyekuwa kijana wa kipekee katika familia yao aliyesoma.
Siku ya kurudi kwake humu nchini, jamaa yake na marafiki wachache walijitokeza kumlaki katika uwanja wa ndege. Hakuna aliyempa Nyangi raha kumwona kama Farida aliyekuwa mchumba wake ambaye hawakuwa wameonana kwa miaka sita mtawalia. Ndoa yao ilikuwa imepangwa kufanyika mwezi wa Agosti baada ya Nyangi kupumzika siku sitini na tano. Farida alikuwa amemsubiri mpenzi wake kwa ustahimilivu kweli, mara nyingi alikuwa na wasiwasi kuwa angepata mchumba mwingereza. Sasa alipata uhakika na kuamini ya wahenga subira huvyaa mwana. Aidha, subira ni ufunguo wa faraja. Sheria ya kanisa lao ilihitaji kwanza wafanyiwe uchunguzi wa ukimwi. Hakuna kati yao aliyekuwa na tashwishi kwa kuwa walikuwa waaminifu. Kwa hivyo, walichangamka vilivyo pale walipoendea matokeo na cheti cha kupimwa. Farida ndiye aliyepatiwa matokeo kwanza na kama walivyotarajia, yalikuwa sawa kabisa. Wakati wa matokeo ya Nyangi, daktari alisitasita, "Samahani, sina habari njema kwako!" "Unamaanisha nini daktari?" Nyangi aliuliza kwa mshangao. Alipoarifiwa eti alikuwa na virusi vya ukimwi, alikataa katakata.
Farida alibaki kuduwaa. Walitoka pale bila maongezi. Hata walipoachana, Nyangi alizidiwa na mawazo chungu nzima, kuwa na ukimwi kwake lilikuwa fumbo ililohitaji kufumbuliwa. Alijijun mwenye nidhamu ya hali ya juu. Mara wazo likamjia. Lazima ilikuwa simimi. Alikumbuka vyema walikuwa pamoja kitambo sana. Alijiuliza maswali yasiyo na majibu. Mbona mabaya yalikuwa yakimlenga yeye ambaye aliishi maisha ya uaminifu na kujinyima raha akiogopa karaha? Lilikuwa jambo la kumkera kuona kuwa wengi ambao waliishi maisha ya kiholela na anasa walikuwa wazima kama vigongo wakitembea mzofafa bila athari yoyote. Laiti angalijua! Angalikuwa mbembe na kuzini kama vijana wengine pengine asingalijuta hivyo! Mawazo yake hata yalimwongoza aanzie pal kasambazia wengine, ili asife peke yake, lakini fikra za kuwa tabibu zikamwambia hivyo ni vibaya.
Asubuhi iliyofuata wakati wa staflahi, hakuwa ameamka. Ilibidi aitwe lakini hakujibu. Mlango wake ulibishwa kwa nguvu, lakini hakufungua. Ulipovunjwa, kila mmoja alishangaa kumpata ni maiti. Alikuwa amejitia kitanzi. Hakuna aliyeelewa hadi walipoisoma barua aliyoandika kusema "Poleni wavyele wangu, siwezi kuishi katika hali hii. Singeweza kumchukua mchumba wanga akiwa anajua ninaishi na ukimwi. Nilitenda kosa moja tu, nalo limeniua. Nawaomba radhi. Ninawapenda!
Vilio vilitanda kote. Daktari yule aliyewapima naye alishindwa kufungua kinywa alipofika pale kutaka kuongea naye. Alikuwa ameenda huko kwao kumweleza kuwa alikuwa amefanya makosa. Jibu alilokuwa amepeana awali kuwa la Nyangi kumbe lilikuwa la mgonjwa mwingine! Afanalek!

  1. Kulingana na aya ya kwanza, Nyangi
    1. alienda Uingereza kusomea shahada ya pili
    2. alienda Uingereza kusomea shahada ya tatu
    3. alienda Uingereza kusomea shahada ya kwanza
    4. alienda Uingereza kusomea stashahada
  2. Ni kweli kusema kuwa
    1. Nyangi alikuwa kijana wa kipekee katika familia yao
    2. familia ya Nyangi haikuwa na mtoto mwengine kijana
    3. wazazi wa Nyangi hawakuwa na karo ya kuwalipia watoto hao wengine
    4. Nyangi ndiye tu aliyesoma katika familia yao
  3. Kwa nini Nyangi alifurahi alipomwona Farida?
    1. Walikuwa wamekaa miaka sita bila kuonana
    2. Alifurahi kurudi nchini
    3. Alikuwa mpenzi wake
    4. Aliandamana na wazazi wake
  4. Kulingana na kifungu, Nyangi alirudi mwezi wa
    1. Juni
    2. Mei
    3. Julai
    4. Agesti
  5. Methali 'subira havyaa mwana" mwema hailingani kimaana na
    1. mkono mmoja haupigi kofi
    2. papo kwa papo kamba hakata jiwe
    3. Zito hufuatwa na jepesi
    4. Baada ya dhiki faraja
  6. Neno mbembe limetumika kumaanisha nini?
    1. Mahindi ya kuchoma yaliyoza
    2. Kufutia hali aliyonayo mtu
    3. Mtu anayependwa sana na wengine
    4. Mtu msherati
  7. Ni sahihi kusema kuwa
    1. Simimi alimwambukiza Nyangi ukimwi
    2. Nyangi na Farida walioana
    3. Nyangi hakuwa na ukimwi
    4. Matokeo ya ukimwi ya Nyangi hayakuwa na makosa
  8. Nyangi alikuwa ameenda Uingereaza kusomea
    1. urubani
    2. uhasibu
    3. udaktari
    4. uhazigi
  9. Kwa nini Nyangi alijitia kitanzi?
    1. Hakuwa na ukimwi
    2. Simimi alimwambukiza ukimwi
    3. Aliamini alikuwa na ukimwi
    4. Alikuwa na ukimwi
  10. Kichwa mwafaka cha kifungu hiki ni
    1. Arusi ya Nyangi na Farida
    2. Kosa la daktari
    3. Simimi kumwambukiza Nyangi ukimwi
    4. Urafiki wa Nyangi na Farida 

Sama kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50
Kuwa na elimu ni jambo la busara. Tumefunzwa kwa kina hadi tukaelewa kinagaubaga kuwa masomo ni taa ambayo huangaza gizani. Aidha, elimu ndiyo ufunguo wa maisha mema ya mustakabali. Kutokana na ujuzi huu, wanafunzi wengine hujikaza kisabuni na kusoma kutwa kucha ili wafaulu katika mitihani yao.
Wazazi nao wametekeleza wajibu wao wa ulezi wa kuhakikisha wana wao wamezima kiu yao ya masomo. Wengi wamechukua mikopo minono kwenye benki huku wengine wakiuza mali na mashamba yao ili kulipa karo ambayo si mchezo siku hizi. Walimu kwa upande mwingine wanajizatiti kuwapa wanafunzi wao masomo ya kiwango cha juu.
Serikali haijasazwa. Masomo bila malipo ya msingi yametolewa kwa watoto wote maskini kwa matajiri. Kwa sasa, ni hatia kutompeleka mwana shuleni hata kama wewe ni maskini hohehahe.. Jukumu la watoto nao ni kusoma. Wengi wameyatwaa masomo na kuyakumbatia kiasi cha kualikwa katika vyuo vikuu kusomea taaluma mbalimbali. Kuna wale huendeleza masomo yao kwa bidii ya mchwa lakini kunao wakifika huko husahau kabisa kilichowapeleka chuoni.
Ni juzi tu kijana barobaro wa chuo kikuu alifyatuliwa risasi na kufa papo hapo baada ya kushiriki utekaji nyara wa mkuu mmoja wa polisi. Alipatikana chumbani mwa mwanafunzi huyu akiwa amefungwa miguu na mikono kwa kamba. Nao mdomo ulikuwa umezibwa kwa kitambaa. Polisi mwenyewe alikuwa na bahati ya mtende kuokolewa na mwanafunzi mwengine aliyemshuku kijana huyo baada ya kugundua hakutaka yeyote akaribie chumba hicho. Ilibainika kuwa kijana pamoja na genge lake walikuwa wakidai kulipwa shilingi milioni tano na familia ya polisi ili wamwachilie huru. Aibu iliyoje! Kikawa kisa cha tamaa mbele mauti nyuma.

  1. Wanafunzi wengine hujikaza kisabuni kusoma kutwa kucha. Hii inamaanisha kuwa
    1. wanafunzi husoma mchana na usiku 
    2. wanafunzi husoma usiku na mchana
    3. wanafunzi husoma asubuhi na mchana
    4. wanafunzi husoma jioni na asubuhi
  2. Neno 'mustakabali' kama lilivyotumika linamaanisha
    1. maisha ya kisogoni
    2. maisha ya baadaye
    3. maisha ya raha
    4. maisha ya utosini
  3. Ni nini maana ya "serikali haijasazwa?"
    1. Serikali haijabaki nyuma kimasomo
    2. Serikali imejitia hamnazo
    3. Serikali inachunguza masomo
    4. Serikali ina hatia kimasomo
  4. Kilichomfanya mwanafunzi kumshuku kijana ni
    1. tabia yake ya utekaji nyara
    2. tabia yake ya uongo
    3. tabia yake ya ukali
    4. tabia yake ya usiri
  5. Wajibu mkuu wa wazazi uliotajwa ni
    1. kuwaelea wanao, kuuza mashamba
    2. kuuza mashamba, kuchukua mikopo benkini
    3. kuwalea watoto, kugharamia masomo yao
    4. kugharamia elimu ya wanao, kuchukua mikopo benkini
  6. Kulipa karo si mchezo siku hizi kwa sababu
    1. si lazima mtu acheze ili aweze kulipa karo
    2. kulipa karo kwahitaji kujitolea
    3. ni lazima mtu acheze ili aweze kulipa karo
    4. kulipa karo na kucheza ni sawa
  7. Kulingana na kifungu, si sahihi kusema kuwa
    1. kijana na genge lake walilipwa milioni tano
    2. vyuo vikuu hufundisha mambo mbalimbali
    3. wana wengine hulaza damu chuoni
    4. kijana na genge lake hawakulipwa milioni tano
  8. Kwa mujibu wa kifungu
    1. si hatia watoto wa maskini wakikosa kusoma
    2. wazazi wanapenda kuuza mashamba na kuchukua mikopo
    3. walimu wanazuia wanafunzi kusoma vizuri
    4. watoto wa mkata wanafaa kusoma sawa na wa kizito
  9. Waliotajwa kushiriki masomo ni
    1. serikali, walimu, wavyele, wazazi
    2. watoto, serikali, wafanyikazi, askari
    3. watoto, wavyele, walimu, serikali
    4. askari, polisi, wazazi, watoto
  10. Methali iliyotumiwa mwisho ni mwa kifungu inaweza kulinganishwa na
    1. Yote yang'aayo si dhahabu
    2. Penye mawimbi na milango i papo
    3. Mwenye pupa hadriki kula tamu
    4. Kilicho baharini kakingoje pwani

Insha

Andika insha ya kusisimua isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukimalizia kwa maneno haya

................................................................................tulinadi kwa vicheko na bashasha.

 

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students