Wednesday, 05 July 2023 13:03

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 4

Share via Whatsapp

QUESTIONS

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Amadi alipojiunga na shule ya chekechea, walimu wake walishuhudia kuwa alikuwa na kipawa cha ...................1................... muhula mmoja baadaye, aliweza kujitokeza jukwaani kukariri mashairi ya ...................2................... yaani yenye mishororo mitatu katika kila ubeti, walimu na wanafunzi wenzake wakawa ndio ...................3................... yake. Walimu walimpa mazoezi zaidi ili ...................4................... Kadhalika, Amadi ...................5................... masomo kiasi kwamba katika darasa la nane aliweza kufahamu aina za vivumishi kama vile: ...................6................... pamoja na akisami kama tusui tano ambayo kwa tarakimu ni ...................7................... 

  1.                  
    1. kihalali
    2. kipekee
    3. kigeni
    4. kiasili
  2.                
    1. tasdisa
    2. tathlitha
    3. takhmisa
    4. tarbia
  3.                          
    1. hadhira
    2. halaika
    3. msoa
    4. shabiki
  4.                      
    1. waimarishe
    2. waimarike
    3. aimarishe
    4. aimarike
  5.              
    1. alizithamini
    2. aliyathamini
    3. alimthamini
    4. aliuthamini
  6.                      
    1. ajabu, tamu, refu
    2. kubwa, tena, kiasi
    3. zuri, dogo, lo!
    4. chache, kwetu, vile
  7.                     
    1. 5/6
    2. 6/5
    3. 9/5
    4. 5/9

Kwa ...................8................... lugha ya Kiswahili imetanda kote ulimwenguni. Wenyeji asili  ...................9................... wakiongea lugha hii  ...................10................... awali ni waarabu. Waarabu wamepatikana kote pwani mzima  ...................11................... pwani ya Afrika Mashariki. Kwa muda wa miaka Kiswahili  ...................12................... humu nchini lakini mambo yamegeuka. Lugha hii sasa imepewa hadhi kubwa ...................13...................nyanja mbalimbali nchini. Lugha hii  ...................14................... pakubwa kuwaunganisha wananchi na kudumisha amani. Wakenya wengi wamejitolea kukuza lugha ya Kiswahili na hawataki tena,  ...................15...................

  1.                  
    1. kweli
    2. hakika
    3. vile
    4. sababu
  2.                
    1. walikuwa
    2. wamekuwa
    3. watakaokuwa
    4. waliokuwa
  3.              
    1. tangu
    2. mpaka
    3. kufikia
    4. hadi
  4.              
    1. mwa
    2. la
    3. wa
    4. kwa
  5.              
    1. haki kuthaminiwa
    2. hakikudhaminiwa
    3. haikuthaminiwa.
    4. haikudhaminiwa
  6.                
    1. kuliko
    2. kati ya
    3. zaidi ya
    4. katika
  7.              
    1. imechangiwa
    2. imechangia
    3. imechangu
    4. imechanga
  8.              
    1. kuididimiza
    2. kuididimia
    3. kuizungumza
    4. kuitunza

Kwa maswali 16-30, chagua jibu lifaalo kulingana na maagizo uliyopewa 

  1. Ni nini wingi wa sentensi ifuatayo: Ua mzuri umezingira nyumba yao.
    1. Nyua nzuri zimezingira nyumba zao. 
    2. Maua mazuri yamezingira nyumba zao. 
    3. Nyua nzuri zimezingira manyumba yao. 
    4. Maua mazuri zimezingira nyumba zao.
  2.  Ukiongeza robo kwa robo tatu utapata 
    1. robo 
    2. nusu 
    3. sudusi
    4. moja.
  3. Nomino uwele hupatikana katika ngeli gani?
    1. LI-YA
    2. U-ZI
    3. U-YA
    4. YA-YA.
  4. Ni sentensi ipi inayoonyesha kivumishi kimilikishi?
    1. Dawati lolote litakuwa la muhimu.
    2. Uzoefu wake ulimfaa zaidi.
    3. Mchezea tope humrukia.
    4. Chai hii ni tamu.
  5. Maana ya sentensi usingesoma sana ungefaulu ni
    1. ulisoma sana na haukufaulu
    2. ulisoma sana na ukafaulu
    3. kutosoma kwako kulikuwezesha kufaulu
    4. kufaulu kwako hakukutegemea kusoma sana.
  6. Ni sentensi ipi ambayo haijatumia istiara
    1. Mke wa kakangu ni kasuku.
    2. Ulafi wa fisi ulimdhuru
    3. Tutafaulu liwe liwalo.
    4. yeye ni mbwa koko.
  7. Chagua kundi la vihusishi pekee
    1. haraka, sana, asteaste
    2. baadhi ya, miongoni mwa, hali kadhalika
    3. mkabala na, nyuma ya, kando ya
    4. lo! kefle! lahaula!
  8. Bainisha matumizi ya karibu katika sentensi: Amejigonga ukutani karibu apasuke paji.
    1. Nusura
    2. Wakati
    3. Makaribisho
    4. Hali.
  9. Kipanga, korongo, mwewe na bata ni msamiati wa
    1. wanyama pori
    2. samaki
    3. vimelea
    4. ndege.
  10. Tunasema kitita cha pesa na numbi ya
    1. ndizi
    2. chokaa
    3. maua
    4. samaki.
  11. Kucheza ngoma goya ni
    1. kusakata densi bila malipo
    2. kufanya jambo lisilo la manufaa 
    3. kufanya mambo kinyume na sheria
    4. kuharakisha kufanya jambo.
  12. Abubakar amemwoa Aisha. Je, wazazi wa Abubakar na Aisha wataitanaje?
    1. Wacheja
    2. Mwanyumba
    3. Wakwe
    4. Kivyere.
  13. Kati ya magonjwa haya ni upi usio na chanjo?
    1. Polio.
    2. Kifaduro.
    3. Surua.
    4. Saratani.
  14. Ni pembe tatu ngapi ziko katika umbo hili?
    29 sfsfs
    1. Kumi na tatu
    2. Kumi na mbili
    3. Kumi na moja 
    4. Kumi
  15. "Ukitaka la waridi sharti udhurike." Babu aliniambia. Kwa usemi wa taarifa ni
    1. babu alinishauri kuwa ningetaka la waridi sharti ningedhurika
    2. babu aliniambia kuwa ningetaka la waridi sharti nidhurike
    3. babu aliongea kuwa ningetaka la waridi sharti ningedhurika
    4. babu alisema kuwa nikitaka la waridi sharti nidhurike. 

Soma kifungu kifuatacho kwa makini kisha ujibu maswali 31-40
Si siri kama jua la mchana kuwa demokrasia katika taifa letu la Kenya imekua haraka na kwa kiwango kikubwa. Bila shaka hili ni jambo la kujivunia kwani ina maana kuwa taifa letu liko miongoni mwa mataifa yanayoheshimu haki za binadamu duniani. Demokrasia ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu wenyewe. Tangu tulipojinyakulia uhuru miongo mitano iliyopita, taifa letu limepiga hatua kubwa na kuimarisha ulingo wa siasa na wanasiasa.

Mwanzilishi wa taifa letu hayati Mzee Jomo Kenyatta aliposhika hatamu za uongozi, alihakikisha kuwa amewaunganisha wananchi wote wa nchi hii na kuwapa sababu tosha za kuionea fahari nchi yao. Aliasizi falsafa ya Harambee, ambao ulikuwa mwito wa kuwahamasisha wananchi kushirikiana na kuchangia maendeleo yao kwa kuvuta pamoja. Mwito huo ulileta ari na mshawasho kwa wananchi wa Kenya na kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi yao. Aliposafiri pasi na nauli mnamo mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na nane, makamu wake, Daniel Moi alichukua hatamu za uongozi naye akashikilia uzi huo huo na kuanzisha mwito wa Nyayo ambao ulimaanisha ya kuwa angefuata nyayo za mtangulizi wake na kuhimiza wakenya kuishi kwa amani, upendo na umoja.

Raisi Moi alikaa kwenye kiti cha enzi kwa miaka ishirini na minne. Isipokuwa hakuna kapu isiyokosa usubi, alifanya mengi ya kujivunia pia. Rais Kibaki alipochukua hatamu za uongozi baada ya kumbwaga mpizani wake wa karibu Uhuru Kenyatta, katika uchaguzi wa mwaka elfu mbili na mbili, taifa letu lilianza mchakato wa kujipatia katiba mpya. Katiba hii imebadilisha na kurahihisha uongozi wa nchi yetu. Mabadiliko mengi yamedhihirika hususan katika ulingo wa kisiasa. Siasa ya sasa ni tofauti na hapo miaka ya awali.

Kulingana na katiba mpya kuna nyadhifa zaidi ya tano ambazo mpiga kura atahitajika kuchagua. Nyadhifa hizi ni rais, gavana, seneta, mwakilishi wa wanawake bungeni, mbunge na mwakilishi wa wadi. Katiba hii imeimarisha viwango vya uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa.

  1. Demokrasia hujitambulisha vipi wakati wa uchaguzi katika nchini ya Kenya?
    1. Rais anapoteua viongozi mbalimbali wa nyadhifa za kisiasa.
    2. Wapiga kura wanapopewa nafasi kuchagua viongozi wa kisiasa katika nyadhifa mbalimbali.
    3. Vyama vya kisiasa vinapowateua viongozi wazalendo wa vyama.
    4. Spika wa bunge anapowateua viongozi kuwalalisha wananchi bungeni.
  2. Kiongozi anayechaguliwa kidemokrasia nchini ili kuongoza taifa ni
    1. rais
    2. gavana
    3. mfalme
    4. waziri mkuu.
  3. Maudhui makuu ya fulsafa ya Harambee yalikuwa?
    1. Kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kudumisha amani nchini.
    2. Kuboresha kiwango cha uchumi kwa kuwaruhusu raia wafanye biashara.
    3. Kuhamasisha raia kufanyia pamoja kwa ushirikiano na kuchangia maendeleo yao kwa kuvuta pamoja.
    4. Kuhakikisha kuwa viongozi wote wanaochaguliwa wanawajibika kwa kila namna.
  4. Ni kauli ipi si sahihi kwa mujibu wa taarifa uliyoisoma?
    1. Rais wa kwanza wa taifa hili alijinyakulia mali mengi kwa manufaa ya Wakenya.
    2. Takriban miongo mitano imepita baada ya Kenya kujinyakulia uhuru.
    3. Mwanzilishi wa taifa la Kenya alienda njia ya marahaba akiwa uongozini.
    4. Kenya ilipata uhuru kutoka kwa wakoloni zaidi ya miaka hamsini iliyopita.
  5. Ni nini maana ya msemo "..Aliposatiri pasi na nauli..."?
    1. Alipotembelea jongomeo.
    2. Alipoaga.
    3. Alipotembea kwa miguu.
    4. Alipofariki.
  6. Kulingana na taarifa
    1. kauli mbili ya harambee iliwafanya wanasiasa kuimarisha siasa zao
    2. rais Moi aliongoza nchi ya Kenya kwa miongo mitatu
    3. rais Kibaki aliboresha maisha ya Wakenya kwa kuleta katiba mpya
    4. katiba mpya imebadili mtazamo wa siasa nchini.
  7. Taifa la Kenaya lilijipatia uhuru mwaka wa
    1. 1961
    2. 1963
    3. 1962
    4. 1964
  8. Neno 'miongoni mwa' limepigiwa mstari katika ufahamu liko katika kitengo kipi cha sarufi?
    1. Kiunganishi
    2. Kivumishi
    3. Kihusishi
    4. Kielezi.
  9. Methali nyingine yenye maana sawa na *hakuna kapu isiyokosa usubi'ni
    1. hakuna masika yasiyokosa mbu
    2. hakuna kovu la masimango 
    3. mwenye pupa hadiriki kula tamu
    4. kila shetani na mbuyu wake.
  10. Katika aya ya mwisho tunadokezwa ya kwamba
    1. katiba mpya imewafanya wanasiasa pekee yao kuajibika
    2. ni lazima mpiga kura apigie nyadhifa tano za uongozi
    3. bunge litakuwa na wakilishi wa wanawake
    4. spika, rais na makamu wake ni baadhi ya viongozi watakaochaguliwa na raia wakati wa kura. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50.
Suala la vijulanga na watu wazima kutumia mihadarati ni mojawapo ya matatizo yanayowatinga akili na kuwatesa watu anuwai siku hizi. Hapo awali jambo hili lilionekana kama mwiko. Siku hizi laonekana jambo la kawaida katika jamii zetu.

Dawa za kulevya zimekuwa tatizo sugu ambalo linahitaji kushughulikiwa kwa kila njia. Si jambo la mjadala tena na wala hatuwezi kujitia hamnazo kuhusiana na swala hili. Hii ni kwa sababu mihadarati imepenya kila mahali shuleni, vyuoni hata kazini. Watu wengi huanza tabia hii kimchezochezo na mwishowe huwawia vigumu kujikwamua; kumbe ni kweli walivyonena wahenga kuwa mazoea yana tabu!

Mihadarati hii ina athari nyingi. Wanaoathirika zaidi ni wanagenzi. Kadri wanavyoendelea kutumia dawa hizi ndivyo wanavyo kuwa waraibu. Utumiaji wa dawa hizi huwazuzua na kuwasisimua na mwishowe hushadidi katika matumizi yake. Madhara ya dawa hizi ni mengi, mathalani uvutaji wa sigara huchangia pakubwa katika kusababisha ugonjwa wa pumu. Mvutaji sigara huingiza moshi mwilini. Kumbe moshi ule huwa sumu. Moshi ule huharibu mapafu na umio. Vidole vya mvutaji huwa vyeusi. Harufu itokayo mdomoni mwake aidha si ya kupendeza.

Wapendao kupuliza hashishi pia hawajaachwa nyuma. Wao huona vimulimuli na kujihisi wenye nguvu za kulivunja jabali, wengine huonekana wachovu na hivyo kulala kupitia kiasi. Hawazingatii afya, hukosa malengo na hawalengi shabaha katika kazi. Aidha hukosa hamu ya kazi, chakula na hata maendeleo ya binafsi.
Wanafunzi wanapozama katika kuvuta bangi huacha shule kwa kuona elimu ikiwa sumbufu. Watu wazima wavutao bangi hutokwa na utu wakawa kama hayawani na kutenda matendo ya kukirihi kama vile ubakaji wa watoto na wanawake.

Miraa ni aina nyingine ya mihadarati. Utafunaji wake vilevile una madhara. Miraa humfanya mtu kupoteza usingizi na kuzembea. Iwapo matumizi yatakithiri, mtu hukosa uwezo wa kuzaa au kuzalisha.

Ni hatia kujihusisha na mihadarati kwa njia yoyote ile iwe ni utumiaji au uuzaji. Ni jambo la kukata maoni kuona baadhi ya vijana wakitumiwa na maajenti ili kuuza dawa hizi. yeyote yule atakayepatikana akihusika na vitendo vya kusafirisha, kuuza na kutumia dawa za kulevya atatiwa mbaroni, ashtakiwe, ahukumiwe na kufungwa jela kwani huu ni uhalifu.

  1. Suala la matumizi ya mihadarati ni baadhi ya matatizo yanayowatatiza watu ‘anuwai'. Neno anuwai linamaanisha
    1. watu wote
    2. watu wa aina na aina
    3. watu mbalimbali
    4. watu wengi.
  2. Kifungu 'hatuwezi kujitia hamnazo' kina maana ya
    1. hatuwezi kujifanya hatuelewi dawa za kulevya
    2. hatuwezi kuupaza athari za dawa za kulevya
    3. hatuwezi kukubali dawa za kulevya
    4. hatuwezi kukoma kutumia dawa za kulevya.
  3. Dawa ipi ya kulevya hukosesha watu utu?
    1. Hashishi.
    2. Pombe.
    3. Bangi.
    4. Sigara.
  4. Zifuatazo ni athari za dawa za kulevya isipokuwa
    1. kukosa hamu ya maandeleo ya binafsi
    2. kupuuza masomo
    3.  ubakaji wa watoto na wanawake
    4. kuwa na nguvu ya kufanya kazi.
  5. Uraibu humfanya mtu
    1. kupuuza matumizi ya dawa za kulevya
    2. kuzidi kutumia dawa za kulevya
    3. kuhalalisha matumizi ya mihadarati
    4. kuanza kutumia dawa za kulevya.
  6. Kati ya dawa zifuatazo ni ipi imehalalishwa humu nchini?
    1. Miraa
    2. Bangi
    3. Kokeni
    4. Hashishi.
  7. Athari za dawa za kulevya si pamoja na
    1. pumu
    2. kansa
    3. utasa
    4. utapiamlo.
  8. Watu wengi huanza kujiingiza katika dawa za kulevya kwa njia gani?
    1. Kimchezomchezo kwa kujitia hamnazo.
    2. Baada ya kujiunga na vyuo vikum. 
    3. Baada ya kuonyeshwa na wandasi.
    4. Wanapopatwa na shida.
  9. Athari gani anayopata mvutaji bangi?
    1. Hubaka watoto na wanawake.
    2. Huwa hayawani.
    3. Hutelekeza majukumu yao.
    4. Hukamatwa na polisi.
  10. Kichwa kifaacho makala haya ni.
    1. Uraibu wa dawa za kulevya.
    2. Unyama wa watumizi wa mihadarati.
    3. Madhara ya mihadarati.
    4. Matumizi ya dawa za kulevya.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa.

Wewe ni kinara wa wanafunzi shuleni. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wenzako kuhusi umuhimu wa kudumisha usafi shuleni.

..........................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

MWONGOZO

swa

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 4.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students