Wednesday, 23 March 2022 08:43

Kiswahili Activities Questions and Answers - Grade 4 Opener Exam Term 1 2022

Share via Whatsapp

KISWAHILI ACTIVITIES



Maswali

SEHEMU YA 1:

  1. Kusikiliza na kuzungumza
    Sema umuhimu wa vifa hivi
    OT122kiss1
  2. Taja miezi mitatu ya mwaka,
  3. Eleza umuhimu wa mazingira

SEHEMU YA 2: 

  1. Kusoma
    Halima ni mwanafunzi mzuri. Nyumbani kwao wana duka kubwa sana. Humo dukani wao huuza sukari, mikate, unga na mafuta. Jana kaka alinunua kilo tano za sukari na mikate mitatu. Alimpea muuzaji pesa kisha akaenda.

    Alipofika nyumabni, mama alimuuliza, "mbona hukununua mafuta?" Kaka alisema mafuta yaliuzwa kwa bei ghali sana. Halima alitwambia kuwa duka lao huwapatia faida nyingi sana.

  2. Kusoma ufahamu
    Twiga hupatikana katika maeneo ya kusini mwa Afrika, pamoja na Afrika mashariki-Kenya, Uganda na Tanzania. Ndiye mnyama mrefu zaidi duniani. Urefu wake ni kati ya mita nne nukta tatu na mita tano nukta nane. Uzito wa twiga na kilo mia nane na elfu moja, mia mbili na hamsini. Aliye na uzito wa juu ni wa kiume.

    Twiga ana maisha ya takribani miaka ishirini na mitano. Chakula chake ni nyasi na majani ambayo huyafikia kwa shingo lake ndefu sana. Ulimi wa twiga unafikia urefu wa centimita arobaini na tano.

    Mtoto wa twiga azaliwapo ni mrefu kuliko mwanadamu aliyekomaa. Mtoto huyo anaweza kusimama baada ya dakika kumi. Baada ya saa kumi anaweza kukimbia kando ya wazazi wake.

    twiga ndiye alalaye kwa muda mfupi zaidi, kati ya dakika kumi na saa mbili kwa usiku. Twiga ana uwezo wa kulala huku akisimama. Yeye ni kivutio kwa watalii.

    1. Taarifa hii inahusu mnyama gani? 
    2. Taja eneo moja ambayo twiga hupatikana
    3. Kati ya twiga wa kiume na wa kike, nani ana uzito wa juu?
    4. Ulimi wa twiga unafikia urefu wa centimita ngapi?

      Andika kweli au la
    5. Twiga ana uwezo wa kulala huku akiwa amesimama

SEHEMU YA 3

Sarufi
Jaza "juu ya" au "chini ya"

  1.     
    OT122kissh31
    Paka ako _____________ meza.
  2.    
    OT122kissh32
    Mpira uko _____________ kiti.

  3. OT122kissh33   
    Mtoto amelala _____________ kitanda

    Jaza 'Huyu' au 'Hawa'
  4. _____________ ni wanaume
  5. _____________ walimu wananipenda

SEHEMU YA 4
KUANDIKA
Andika insha juu ya:

MNYAMA NIMPENDAYE



Mwongozo wa Kusahihisha

SEHEMU YA 1

  • Mwanafunzi anapaswa kutaja umuhimu wa kila kifaa kilichoonyeshwa
  • Mwanafunzi anapaswa kutaja miezi yoyote tatu 
  • Mwanafunzi anapswa kutaja umuhimu wa mazingira

SEHEMU YA 2

  1. Kusoma ufahamu- Mwanafunzi anapaswa kusoma hadithi vyema
  2. Kusoma ufahamu
    1. twiga
    2. kusini mwa afrika na afrika mashariki
    3. twiga wa kiume
    4. centimita arobaini na tano
    5. Kweli

SEHEMU YA 3

  1. chini
  2. juu
  3. juu
  4. Hawa
  5. Hawa

SEHEMU YA 4

Mwanafunzi anapaswa kuandika insha juu ya mada aliyopewa.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Activities Questions and Answers - Grade 4 Opener Exam Term 1 2022.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students