Monday, 17 October 2022 11:33

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 KPSEA End Term 3 Exam 2022 Set 1 Featured

Share via Whatsapp

Maswali

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Mchezaji wa kabumbu amekutana na mkufunzi wake. Wanajadiliana kuhusu hali ya mchezaji.)
Kocha :          Vipi kaka? Habari za asubuhi? Waonekana kuchechemea. Kulikoni? (akionyesha mshangao mkuu)
Mchezaji:       Habari nzuri ila si sana. Ni kweli, nachechemea kutokana na maumivu ya goti langu la kushoto. Nadhani unakumbuka kilichotokea katika uwanja wa Mwagajasho tulipocheza dhidi ya timu ya Majimoto.
Kocha :           Naam, nakumbuka ulichezewa visivyo ikakubidi kuuaga mchezo. Nilidhani ulipata nafuu. Je, umepokea matibabu yoyote hadi sasa?(alimgusa na kumpapasa gotini)
Mchezaji:        Naam, bata sasa nimetoka kupokea huduma pale hospitalini Dawatamu. Daktari Siha amenishauri kuufanyisha mazoezi mguu huu ili goti lipone upesi. (akiukunja na kuunyosha mguu wake wa kushoto)
Kocha :           Nakutakia afueni ya haraka bwana Kadenge. Kumbuka kuwa tutakuwa na mechi kali dhidi ya timu ya Wazee Hukumbuka wiki ijayo. Mchezaji:         Aa! Nitakuwa nimepona kocha. Asante sana kwa kunikumbusha.
Kocha :           Hewallah bwanamogo. Tutaonana wakati mwingine majaliwa

  1. Hali ya mchezaji ilikuwa shwari ila
    1. viungo vyake.
    2. miguu yake 
    3. magoti yake. 
    4. goti lake
  2. Je, ni nini kinatueleza kuwa mkufunzi  alimjali mchezaji wake?
    1. Alimkumbusha mchezaji kuhusu mechi iliyokaribia.
    2. Alimshughulikia mchezaji wake vilivyo kimatibabu.
    3. Alitaka kufahamu sababu ya mchezaji kuchechemea.
    4. Alimsaidia mchezaji kunufanyisha mgw mazoezi.
  3. Kulingana na bwana Siba, mazoezi ya Kadenge ni nani?
    1. Yule mchezaji aliyeumia wakati wa mechi.
    2. Mkufunzi wa mchezaji yule.
    3. Mwuguzi katika hospitali ya Dawatamu.
    4. Daktari katika hospitali ya Dawatamu.
  4. Je, kocha alipokutana na mchezaji huyo alikuwa ametoka wapi?
    1. Hospitalini Dawatamu. 
    2. Hatujaelezwa. 
    3. Kwa daktari. '
    4. Uwanjani.
  5. Kulingana na mazungumzo haya, mara kwa mara yalikuwa na umuhimu gani?
    1. Yangemwongeza mchezaji nguvu 
    2.  Ili mchezaji awe imara. 
    3. Yangeiponya miguu ya mchezaji .
    4. Yangeharakisha kupona kwa goti la  mchezaji.

Soma kifungu kifuatacho kisha wilbu maswali 6 hadi 8.
           Katika enzi za kale, watu hawakuwa wakivaa nguo zozote. Wacheshi husema kuwa walivalia suti ya Mungu! Miaka ilivyozidi kubingirika, watu wakaona umuhimu wa kujisitiri . Hapo, wakaanza kujifunika kwa ngozi za wanyama. Baadaye, walianza kutumia mablanketi na mashuka.
            Leo hii tunapozungumza, kuna aina nyingi sana za mavazi kiasi kuwa ni vigumu kuchagua ya kununua. Kama ilivyo kawaida, watu hutofautiana katika chaguzi za aina na rangi za mavazi. Yapo mavazi ambayo ni ya wanaume pekee. Vilevile, kunayo yale ambayo ni ya wanawake tu. Baadhi ya haya ya kike ni kanchiri au sidiria, marinda, sketi, blauzi na mengineyo. Watoto nao hawajaachwa nyuma Yapo mavazi ambayo ni ya watoto tu. Je, wafahamu kuwa kuna mavazi yanayoweza kuvaliwa na wanawake na pia wanaume?

  1. Kulingana na taarifa, 
    1. zamani watu walivalia mavazi ya bei rahisi.
    2. hakukuwa na nguo zozote kitambo.
    3. kitambo, watu walikuwa na tatizo la kuchagua nguo za kununua.
    4. watu walijisitiri kwa majani mapana
  2. Ni jibu gani laonyesha hatua alizopitia  binadamu hadi kuufunika mwili wake?
    1. Mablanketi na mashuka, mavazi, ngozi  za wanyama. 
    2. Mavazi, mablanketi na mashuka, ngozi za wanyama.
    3. Ngozi za wanyama, mablanketi na mashuka, mavazi.
    4. Mablanketi na mashuka, mavazi, ngozi za wanyama.
  3. Kulingana na ufahamu huu, watu wa sasa tatizo gani kuhusiana na nguo?
    1. Nguo zilizopo hazimtoshelezi kila mmoja.
    2. Wingi wa aina za mavazi hufanya kuchagua kuwe kungumu. 
    3. Mavazi mengi ya kisasa ni ya wanawake na wanaume.
    4. Kunayo mavazi ya wanaume, wanawake na watoto.
  4. Baadhi ya mavazi ya wanawake katika kifungu ni ana
    1. marinda, sidiria na blauzi. 
    2. sketi, chupi na kanchiri.
    3. suruali, marinda na sidiria.
    4. kanchiri, tai na sketi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
         "Wageni wetu waheshimiwa, wazazi, walimu, wakufunzi wa michezo, wachezaji na wanafunzi wenzangu, habari za wakati huu? Hakika, bila kubahatisha maneno, leo ni siku muhimu sana katika tukio ya humu shuleni ya mwaka huu. Naam, ni siku ya kutiwa katika rekodi ya kumbukumbu ili isisahaulike na yeyote. Kama tujuavyo sote, michezo ni njia mojawapo ya kuonyesha uwezo na talanta alizotujalia Mwenyezi Mungu. Naomba nigusie faida kadhaa za michezo. Michezo huipa miili yetu na kutufanya tuwe na afya bora. Kupitia michezo, uwezo wetu wa kushiriki vyema katika timu huonekana. Viungo vyetu hufanya kazi vizuri, uhusiano wetu na wenzetu hujengeka na mawasiliano miongoni mwetu huwa bora. Kujihusisha na michezo baada ya kazi za darasani na nyumbani hupumzisha akili. Tunapojiandaa kushiriki mchuano wa leo, nawatakia kila la heri. Asanteni kwa kunisikiliza."

  1. Unadhani aliyetoa maelezo haya alikuwa yupi?
    1. Mzazi.
    2. Mwalimu 
    3. Mwanafunzi.
    4. Mchezaji.
  2. Ni gani hapa si umuhimu wa michezo
    1. kulingana na kifungu hiki?
    2. Miili yetu hupata nguvu na kutufanya tuwe na afya bora.
    3. Baadhi ya magonjwa hutuondoka miilini tukishiriki michezo.
    4. Uhusiano baina yetu na wenzetu  huimarika.
  3. Michezo huleta pumziko la akili baada  ya shughuli fulani ngumu.
    1. Kuna uwezakano kuwa siku hiyo ilikuwa ya
    2. kuwatakia wachezaji kila la kheri.
    3. kufungwa rasmi kwa shule.
    4. kuzawidiwa kwa wachezaji bora
    5. michezo shuleni humo.

Soma kifungu kifuatacho kisha vilbu maswali 13 hadi 15.
             Kila Jumamosi, mama huenda katika soko la Marikiti ili kuuza bidhaa zake. Yeye huruza matunda ya aina nyingi kama mapapai, maparachichi, maembe, mananasi, machungwa na makarakara. Vile vile, huuza mboga kama kabeji, mchicha na sukumawiki. Aliacha kuuza nyanya na vitunguu baada ya bidhaa hizo kuwa ghali zaidi katika soko kuu.
            Mimi ndimi mwanambee katika familia yetu, hivyo, mama huniachia majukumu kila aondokapo. Kaka zangu wawili na dada zangu watatu hunisaidia kufanya kazi pale nyumbani.
            Jumamosi iliyopita, mama aliondoka kwenda sokoni kama ilivyokuwa kawaida. Tuliamua kugawana kazi pale nyumbani ili tuzimalize kabla hajarejea kutoka sokoni. Niliwaambia dada zangu wafue, wasafishe nyumba na kupika kishuka. Kaka zangu walitakiwa kufyeka nyasi, kuulengata ua na kuchoma taka. Ghafla, niliskia mlio wa mbuzi wetu. “Ni nani atakayewapeleka mbuzi malishoni?" Nikajiuliza.

  1. Familia ya kina mwandishi ina jumla ya watu wangapi?
    1. Saba
    2. Sita. 
    3. Wanane.
    4. Watano.
  2. Ni kwa nini mama wa mwandishi hauzi nyanya na vitunguu?
    1. Bidhaa hizo hazipatikani katika soko kuu.
    2. Bei ya bidhaa hizo imepanda mno katika soko la Marikiti.
    3. Bidhaa hizo zimekuwa ghali mno katika soko kuu.
    4. Nyanya na vitunguu hazipatikani  katika soko la Marikiti.
  3. Chagua orodha ya bidhaa ambazo mama wa mwandishi huuza.
    1. Karoti, mboga na nyanya.
    2. Kabeji, matunda na vitunguu.
    3. Mayai, matunda na mboga.
    4. Kabeji, makarakara na maembe. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa
            Uchaguzi uliokamilika hivi majuzi ulidhihirisha kuwa, kwa sasa, wananchi ni wapenda amani. Wengi walidhani kuwa, baada ya mshindi wa     16    urais kutangazwa, wakenya wangetafuta silaha za kutoana    17    na kuharibiana mali. Kinyume na hivyo, amani    18    kote. Huu ndio moyo wa uzalendo. Tukubali matokeo na tuendelee kufanya kazi ili kuboresha     19    Ni kweli bayana asiyekubali kushindwa     20  .

  16   A. meza ya  B. dawati la    C. kiti cha    D. kabati la  
  17   A. mamlakani  B. roho    C. ofisini   D. mikono
  18   A. imetamalaki  B. imepungua   C. imezorota   D. imepotea
  19   A. uhuru  B. umaskini    C. utawala   D. uchumi
  20   A. ni mshindi  B. si mshindani   C. si mshindaji   D. ni mshindani

Katika swali la 21 - 30, jibu swall kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Ni sentensi gani haijatumia amba kwa usahihi?
    1. Maua ambayo walichuma yananukia.
    2. Wageni ambao walingojewa walifika.
    3. Majina ambao walitajiwa hayakuwa  yao.
    4. Masomo ambayo tulisomeshwa yalitufaa.
  2. Chagua neno lililo katika ngeli tofauti.
    1. Mezani.
    2. Mfukoni.
    3. Sahani.
    4. Chumbani.
  3. Chagua sentensi iliyo katika kauli ya kutendesha..
    1. Tiko na kosa huandikiana barua.
    2. Rama ameufunga mlango.
    3. Mzee Tomoko amepanda miche.
    4. Mvua kubwa ilikatiza safari
  4. Ni mnyama yupi hapa baishi majini?
    1. Samaki.
    2. Kuchakulo.
    3. Mamba
    4. Kiboko
  5. Tumia kiámbishingeli sahihi kukamilishia sentensi ifuatayo:
    Hatuku la uyoga wenye sumu. 
    1. U
    2. ya 
    3. i
    4. zi
  6. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo: Maji yaliyotekwa yamemwagika.
    Maji
    1. zilizotekwa zimemwagika.
    2. yaliyotekwa yamemwagika.
    3. iliyotekwa imemwagika.
    4. waliyoteka yamemwagika.
  7. Kamilisha methali ifuatayo: Kidole kimoja
    1. hujaza kibaba
    2. walaji ni wengi.
    3. huvikwa pete.
    4. hakivunji chawa.
  8. Ni sentensi ipi haijatumia kivumishi kimilikishi kwa usahihi?
    1. Jirani yangu anaitwa Tindi.
    2. Madarasa yao yameoshwa vizuri.
    3. Kina mama yao wana mioyo safi.
    4. Mjomba wetu hapendi kununa.
  9. Chagua majina yaliyo katika ngeli ya A-WA.
    1. Uzi,
    2. Kuta, nyuzi, ufizi.
    3. Nzi, kipepeo, kiroboto.
    4. Utepe, uteo, uchafu.
  10. Chagua sentensi iliyoakifishwa kwa usahihi.
    1. Wanyama wafugwao ni pamoja na: ngo'mbe, mbuzi na kondoo.
    2. Ukienda, ng'ambo uniletec haya: vikoi, saa na mkufu.
    3. Ala, kumbe unajua kuendesha baiskeli.
    4. Mwalimu alisema tulete nini kesho.

Majibu

  1. D
  2. C
  3. D
  4. B
  5. D
  1. B
  2. C
  3. B
  4. A
  5. C
  1. B
  2. D
  3. A
  4. C
  5. D
  1. C
  2. B
  3. A
  4. D
  5. B
  1. C
  2. C
  3. D
  4. B
  5. A
  1. B
  2. D
  3. C
  4. C
  5. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 6 KPSEA End Term 3 Exam 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students