Friday, 10 March 2023 11:45

Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 End Term 1 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswall 1-5.

(Chura na Jongoo wamekutana karibu na mto)
Chura: Hujambo rafiki yangu Jongoo? Sijakuona tangu tulipouanza mwaka huu. Kwema?
Jongoo: Sijambo kaka. Hali yangu shwari tena kwema kweli kweli. Mwaka huu nimeamua kutulia. Sipendi kutembeatembea ili ngozi yangu isichomwe na jua.
Chura: Oh! Umenikumbusha. Nilitaka unipe siri ya kuwa na ngozi laini, nyororo na inayomeremeta kama kioo.
Jongoo: (Akicheka kwa dhihaka) Ni rahisi sana bwana. Nyanya yangu alinieleza siri hii. Kwanza chukua mafuta ya uto, yachemshe kabisa kisha uruke ndani na ukae humo kwa muda.
Chura:(Akionyesha umakinifu zaidi) Eh! Kisha baadaye nifanyeje?
Jongoo: Hamna jingine. Tayari utakuwa na ngozi kama yangu.
Chura: (Huku akirukaruka na kuondoka) Asante sana rafiki yangu. Hebu nikajaribu mtindo huu mpya.
Jongoo: (Akiangukia kwa kicheko) Haya bwana. Kila la heri.

  1. Ni kwa nini Chura alitaka kujua ikiwa kwa Jongoo kulikuwa kwema?
    1. Walipendana kama chanda na pete.
    2. Hawakuwa wameonana kwa muda mrefu.
    3. Alitaka aibiwe siri ya ngozi nyororo.
    4. Walikuwa wamekutana ghafla bin vuu.
  2. Je, Jongoo alitoa sababu gani iliyomfanya asipende kutembeatembea?
    1.  Hali ya anga haikuwa shwari.
    2. Aliogopa hali ilivyokuwa baridi.
    3. Mara nyingi alikuwa mchovu.
    4. Aliogopa kuchomwa na jua.
  3. Ni nini ambacho Chura alikuwa amesahau akakumbushwa?
    1. Siri ya ngozi laini, nyororo na inayomeremeta.
    2. Jinsi ya kuchemsha mafuta ya uto.
    3. Jinsi ya kuwa na ngozi iliyoparara.
    4. Namna ya kuwa na mtindo mpya wa kuvutia.
  4. Kulingana na Jongoo, ni nani aliyemfunza kuwa na ngozi nyororo?
    1. Wazazi wake
    2. Nyanya yake
    3. Rafiki zake
    4. Mama yake
  5. Unadhani Jongoo alikuwa rafiki wa aina gani?
    1. Wa dhati.
    2. Mwaminifu.
    3. Mnafiki.
    4. Wa chanda na pete. 

Soma kifungu kifuatacho kisha uilbu maswali 6 hadi 8.
Shule yetu inaitwa shule ya msingi ya Mambosasa. Ina madarasa makubwa. Kutokana na ukubwa wake na idadi ya wanafunzi, kila darasa lina walimu wawili waangalizi. Walimu wetu ni mahiri sana katika ufunzaji. Ninasema hivi kwa sababu Mambosasa imeongoza na kushika usukani kwa miaka mitatu sasa. Kuna mabustani ya maua shuleni humu. Katika mabustani haya mmepandwa maua kama vile mawaridi na milangilangi. Katika maktaba yetu kuna vitabu vingi. Wanafunzi wengi huvisoma vile vya hadithi. Ua umejengwa kuizunguka shule letu. Ua huu hutuhakikishia usalama wetu. Uta wenyewe unavutia kwani ulijengwa kwa mawe na ustadi wa hali ya juu.

  1. Kila darasa shuleni Mambosasa lina walimu wawili waangalizi kwa sababu
    1. madarasa ni mengi.
    2. wanafunzi ni wengi.
    3. shule yenyewe ni kubwa.
    4. matokeo yake huwa mazuri.
  2. Kinachoonyesha kuwa walimu wa Mambosasa ni mahiri ni
    1. ukubwa wa madarasa shuleni humo.
    2. kuwapo kwa walimu wawili katika kila darasa.
    3. bidii za wanafunzi.
    4. matokeo bora katika mitihani.
  3. Badala ya kutumia neno mahiri, mwandishi angetumia neno
    1. wazembe.
    2. stadi.
    3. wazuri.
    4. wavivu.
  4. Kulingana na taarifa hii, wanafunzi huenda maktabani
    1. ili wakasome.
    2. kutazama video.
    3. ili wakafanye mikutano.
    4. kutamba hadithi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Ajira ya watoto ni kazi ambazo zinawatumikisha na kuwaathiri watoto kati ya miaka mitano hadi kumi na saba. Kwa namna fulani wao huathirika kiakili, kimwili, kimakazi na kimaadili. Pia ajira hizi ni kizuizi cha watoto hawa kupata elimu. Mateso yanayowapata watoto katika ulimwengu wa ajira ya watoto duniani ni mengi. Ajira hizi huweza kuwa za nyumbani kwa watu wengine, mashambani au viwandani. Kazi wanazozifanya watoto hawa ni pamoja na kulisha mifugo, kuchimba mawe, kufyatua matofali, kuchonga mawe, ujenzi wa barabara, kuvuta au kusukuma mikokoteni na za ndani ya nyumba. Zote hizi ni kinyume na haki za binadamu kwa jumla.

  1. Tumearifiwa kuwa ajira za watoto huweza kuwaathiri watoto
    1. kimaadili, kimakazi na kidini.
    2. kiakili, kimavazi na kidini.
    3. kimakazi, kiakili na kimaadili.
    4. kiakili, kimwili na kiukoo.
  2. Kulingana na kifungu, ajira za watoto haziwezi kuwa
    1. nyumbani kwa wengine.
    2. katika viwanda.
    3. mashambani.
    4. shuleni.
  3. Haki za binadamu hazimkubali mtoto
    1. kuosha vyombo nyumbani kwao.
    2. kuvuta mikokoteni kwa malipo.
    3. kulifagia darasa lao.
    4. kufua sare zake. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswall
Malaria ni ugonjwa hatari unaosambazwa na aina fulani ya mbu. Si mbu wote husambaza malaria. Aliyewahi kuugua malaria hawezi kuyasahau makali yake. Masaibu yake huanza kwa baridi kali. Mhasiriwa hutetemeka sana. Baadaye joto la mwili hupanda na kufuatiwa na homa kali. Baada ya muda, mhasiriwa hutokwa na jasho.
Malaria ikitibiwa kwa dawa za kisasa, mhasiriwa hupata nafuu na hatimaye kupona. Isipotibiwa kwa wakati, husambaa mwilini na huweza hata kusababisha kifo kwa muda wa siku chache. Kwa miaka mingi, malaria imekuwa tishio katika maeneo mengi. Imewahi kuwaua wengi kwa kipindi kifupi huko India, Ugiriki, Roma na katika mataifa ya Afrika Magharibi. Takribani miaka mia tatu iliyopita, dawa ya malaria iitwayo kwinini ilivumbuliwa.

  1. Kulingana na habari, si kweli kusema kuwa
    1. si mbu husambaza malaria
    2. mtu aliyewahi kuugua malaria hasahau makali yake upesi.
    3. dawa za kisasa haziwezi kutibu malaria.
    4. kwinini ni dawa ya malaria.
  2. Ni gani hapa si dalili ya malaria kulingana na kifungu?
    1. Kutapika
    2. Joto jingi
    3. Kutetemeka
    4. Homa kali
  3. Taarifa inasema kwamba mataifa yaliyorekodi vifo vya wengi kwa muda mfupi kutokana na malaria si pamoja na
    1. Roma
    2. Ugiriki
    3. India
    4. Ajentina 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Wiki iliyopita, shule yetu iliandaa sherehe kubwa sana. Sherehe hiyo ilikuwa ya kuwazawidi wanafunzi _16_ waliofanya vizuri_17_ mashindano ya uandishi wa insha. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na gazeti _18_Jichopevu yalijumuisha shule mia moja. Shule yetu ikawa ya __19__na kuzishinda nyingine tisini na___20___

  1.                    
    1. watukutu
    2. wazembe
    3. hodari
    4. wakali
  2.                  
    1. kwa
    2. katikati
    3. katika
    4. kua
  3.                          
    1. wa
    2. la
    3. ya
    4. za
  4.                
    1. kwanza
    2. kuanza
    3. mbili
    4. moja
  5.                      
    1. sita
    2. saba
    3. nane
    4. tisa

Kutoka swali la 21-30, jibu swali kulingana na maasizo uliyopewa.

  1. Teua sentensi iliyo katika kauli ya kutendwa.
    1. Machoine na dada yake waliandikiana barua.
    2. Mwalimu amesaidiwa kubeba vitabu.
    3. Yeye hupenda kulia bila sababu.
    4. Uzi wa Mwanaidi ndio uliokatika. 
  2. Ni majina yapi yaliyo katika ngeli moja?
    1. Uyoga, ua, upishi.
    2. Kijiko, kiongozi, kiwavi.
    3. Chepeo, kiazi, vitu.
    4. Marashi, magonjwa, makosa.
  3. Kisawe cha neno kinyonga ni
    1. kenge.
    2. nyoka.
    3. mjusi.
    4. lumbwi.
  4. Meza ya seremala imevunjika katika wingi ni
    1. Meza za maseremala zimevunjika.
    2. Meza za seremala zimevunjika.
    3. Mameza za maseremala zimevunjika.
    4. Meza za waseremala zimevunjika.
  5. Katika maneno uliyopewa, ni lipi litakuwa la mwisho katika kamusi?
    1. Mshikaki
    2. Mswaki
    3. Msaada
    4. Msaragambo
      1. i
      2. iii
      3. iv
      4. ii
  6. Kanusha sentensi ifuatayo:
    Juma anaimba polepole
    Juma ..................
    1. haimbi polepole.
    2. hataimba polepole.
    3. hakuimba polepole.
    4. hajaimba polepole.
  7. Chagua sentensi iliyo katika nafsi ya tatu.
    1. Mlitutembelea jana kwa sherehe.
    2. Alinunuliwa mwanasesere maridadi.
    3. Nimeamua kufanya bidii masomoni.
    4. Mwalimu aliyekuwa darasani ametoka.
  8. Kidani ni pambo la
    1. kichwani.
    2. miguuni.
    3. kifuani.
    4. mikononi.
  9. Lo! Nyoka mrefu ameingia ndani ya shimo polepole. Kivumishi ni kipi hapa?
    1. Lo!
    2. Mrefu
    3. Ndani ya
    4. Polepole
  10. Chagua ukubwa wa neno mji.
    1. Miji
    2. Majiji
    3. Kijiji
    4. Jiji

MAJIBU

swa

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 End Term 1 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students