Tuesday, 04 July 2023 11:58

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Opener Exams Term 2 2023 Set 2

Share via Whatsapp

Kusikiliza na kuzungumza

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali.

G6SwaT2OS32023Q1

Juma :         Shikamoo mwalimu?
Bw. Bakari: Marahaba Juma. (Akimwashiria akae) Karibu uketi.
Juma :         (Akiketi) Asante sana mwalimu.
Bw. Bakari: Darasani unaendeleaje na masomo?
Juma :         Mwalimu, ninaendelea vizuri. Ninajikaza kwani mvumilivu hula mbivu.
Bw. Bakari: (Akitikisa kichwa) vizuri sana Juma. Nina furaha sana kusikia kuwa unafanya bidii za mchwa. Je, kuna somo                                          linalokutatiza?
Juma :        Naam mwalimu! Somo la Kiswahili linanipatia changamoto nyingi. Ninajaribu juu chini kujikaza ili nilielewe vizuri.
Bw. Bakari: Bidii ni muhimu sana kama ulivyosema. Vilevile unafaa kufanya mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza Kiswahili. Ukifanya                      hivi utazidi kukipenda Kiswahili.
Juma :        (Akitikisa kichwa kukubaliana naye) Siku hizi huwa nasikiliza vipindi vya Kiswahili kwenye redio na kutazama habari katika                       Kiswahili. Baadaye huwaelezea wenzangu niliyosikia.
Bw. Bakari: Vizuri sana. Hiyo ni hatua ya kutia moyo. Zaidi ya hayo hakikisha unauliza maswali darasani mahali ambapo hujaelewa.
Juma :         Huwa naogopa kuchekwa na wenzangu kwani wanakielewa Kiswahili kuniliko mimi.
Bw. Bakari: (Akimkata kauli) Kuogopa? Kumbuka kuuliza si ujinga.
Juma :         (Akiwazia maneno hayo) Nimekuelewa mwalimu. Kutoka leo nitaanza kuuliza maswali.
Bw. Bakari: Vilevile uwe ukisoma vitabu vya Kiswahili ili ukuze ubunifu wako hasa katika kuandika.
Juma :         Nitafanya hivyo kwa sababu nataka kuwa mwandishi bora darasani.
Bw. Bakari: Aidha kumbuka kushirikiana na wenzako masomoni kwani mkono mmoja haulei mwana.
Juma :         Ndio mwalimu. Nitaufuata ushauri huo. Ninaelewa kuwa umoja ni nguvu...
Bw. Bakari:(Akimchachawiza) Nao utengano ni udhaifu. Ninaona sasa umepata mwamko mpya. Hakikisha umefanya yale                                        tuliyozungumzia. Sasa enda darasani ukaendelee na masomo yako.
Juma :        (Akiondoka) Asante mwalimu. Mungu akujalie mema.

  1. Mwanafunzi alimwamkua mwalimu wake Shikamoo kuonyesha maadili gani?
    1. Bidii
    2. Heshima
    3. Huruma
    4. Uoga
  2. Juma anapata changamoto katika somo gani?
    1. Hesabu
    2. Kiswahili
    3. Kiingereza
    4. Sayansi
  3. Ili kukuza stadi ya kusikiliza na kuzungumza Juma anafanya nini?
    1. Kusikiliza na kutazana vipindi kisha kuwaelezea wenzake.
    2. Kusoma vitabu vya Kiswahili.
    3. Kuandika insha nyingi.
    4. Kushirikiana na wenzake.
  4. Je, ungeyasikiliza mazungumzo ya mwalimu na mwanafunzi, ungejifunza nini?
    1. Kuongea na mwalimu humfanya mwanafunzi asifiwe.
    2. Si vizuri kuuliza maswali sana darasani.
    3. Ni vizuri kutafuta ushauri-nasaha kutoka kwa wakubwa wako.
    4. Somo la Kiswahili ni gumu sana.
  5. Methali 'mkono mmoja haulei mwana' inatufunza kuwa na:
    1. Bidii
    2. Ushirikiano
    3. Upole
    4. Utengano

Swali la 6 hadi la 8

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali. Songambele

G6SwaT2OS32023Q2

Kijiji cha Songambele kina wakazi wengi sana. Wakazi hawa walifurahia utulivu kwa muda mrefu. Hata hivyo, likizo iliyopita wanakijiji walilalamikia mienendo mibaya ya baadhi ya vijana. Kuna vijana ambao walivalia mavazi yasiyofaa. Kuna wale ambao walianza kukataa kwenda shuleni. Wengine hawakutii watu wazima. Walisahau kuwa heshima si utumwa.

Bi.Mwema ni mmoja wa wanakijiji hiki. Alikuwa na shirika lake kwa jina, Boresha Vijana. Kupitia kwa shirika hili, alitumia redio kuwaelimisha vijana kuhusu mienendo mizuri. Aliandaa siku ya michezo kijijini. Vikundi mbalimbali vilishiriki. Baada ya michezo hii, washindi walituzwa. Bi.Mwema alitumia nafasi hii kuwashauri.

Bidii ya Bi.Mwema ilifaulu. Vijana waliokuwa wamepotoka walibadilika. Wanakijiji walifurahi. Walitambua juhudi za Bi.Mwema. Waliandaa sherehe kubwa. Walimtuza Bi.Mwema kwa juhudi zake. Hakika, mcheza kwao hutuzwa.

  1. Wakazi wa kijiji cha Songambele walifurahia _______________________________ kwa muda mrefu.
    1. maandamano
    2. amani
    3. vijana
    4. shida
  2. Kulingana na aya ya kwanza baadhi ya vijana walikosa maadili gani?
    1. Utiifu
    2. Umoja
    3. Bidii
    4. Ukarimu
  3. Maana ya neno andaa kama ilivyotumika katika kifungu hiki ni:
    1. Tayarisha
    2. Safari
    3. Zuru
    4. Maliza

Swali la 9 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

SHULE YA TAMARA, S.L.P 130,
BUSARA.
05-05-2023

Kwa muhibu Pendo,
Pokea salamu nyingi kutoka kwangu. Hujambo? Natumai huna neno. Mimi ni mzima. Ninaendelea vizuri na masomo yangu. Musimu huu wa masika huku kwetu kuna mvua nyingi sana. Wazazi na walimu wanahakikisha kuwa tumejikinga vilivyo na mvua na mbu ambao wameongezeka. Kwa kufanya hivi hatutapata magonjwa kama vile Mafua, Nimonia na Malaria. Nakushauri pia uwe mwangalifu.

Madhumuni ya kukuandikia barua hii ni kukupa mawaidha kuhusu faida za mahusiano mema na wenzako shuleni. Kuanzia ukiwa na uhusiano mzuri na wenzako, utaweza kushirikiana nao. Umoja huu utakufaa masomoni na maishani. Utaweza kujifunza mengi kutoka kwa wenzako. Vilevile ukiwa na matatizo watakusaidia. Kumbuka kuwa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.

Kuongezea mahusiano mema huleta heshima. Wahenga walisema kuwa heshima si utumwa. Ukimheshimu mwenzako atakupenda na kukukubali jinsi ulivyo. Heshima kwa wengine huondoa uadui ambao huleta utengano shuleni. Wanafunzi hushirikiana na kufanya vyema masomoni. Kusema kweli mahusiano mema ni uti wa mgongo wa elimu.

Licha ya hayo amani huletwa na mahusiano mema. Mwanafunzi akitangamana na wengine huweza kuwaelewa nao kumwelewa. Shuleni kuna wanafunzi wenye hali mbalimbali. Utangamano mzuri wa wanafunzi hukuza amani. Amani huwawezesha kusoma vyema bila usumbufu wowote. Huweza kujifunza mengi na kuwa mwerevu zaidi.

Ninatumai nimekuongezea maarifa sahibu yangu. Hakikisha unahusiana vyema na wenzako ili uishi maisha mema. Kwaheri!

Wako wa moyoni,
Amara Mwara

  1. Kifungu ulichokisoma ni cha aina gani?
    1. Masimulizi
    2. Barua ya kirafiki
    3. Barua rasmi
    4. Wasifu
  2. Mwandishi aliandika barua hii katika msimu gani?
    A. Wa jua kali
    B. Wa baridi kali
    C. Wa mvua nyingi
    D. Wa mvua ndogo ndogo.
  3. Mwandishi wa barua hii ni nani?
    1. Tamara
    2. Amara
    3. Mwalimu
    4. Mzazi
  4. Gani si manufaa ya mahusiano mema kulingana na kifungu?
    1. Heshima
    2. Umoja
    3. Amani
    4. Fujo

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

G6SwaT2OS32023Q3

Siku moja tulizuru hospitali na kumuuliza daktari kiungo kilicho muhimu kuliko vingine. Daktari alitueleza kuwa mwili wa binadamu una viungo mbalimbali vinavyotekeleza kazi tofautitofauti. Viungo vinavyomeng'enya au kusaga chakula ni tumbo kongosho, uchengelele, utumbo mpana, nyongo, kibofu cha nyongo, kibole na wengu. Ubongo na uti wa mgongo huwezesha mwili kujifahamu. Moyo nao huzungusha damu mwilini. Hatimaye zoloto na pafu hutumika katika mfumo wa hewa. Ni vigumu kusema ni kiungo kipi kilicho muhimu kuliko vingine. Tunafaa kutunza viungo hivi. Tunafaa kufanya kazi kwa kuchangizana kama viungo vya mwili.

  1. Neno tulizuru lina maana sawa na
    1. tuliuliza
    2. tulitoka
    3. tuliona
    4. tulitembea
  2. Kifungu hiki kinazungumzia nini?
    1. Utunzaji wa viungo vya mwili.
    2. Viungo vya ndani vya mwili.
    3. Viungo muhimu kuliko vingine
    4. Viungo vya ndani na vya nje vya mwili
  3. Kulingana na kifungu:
    1. Hakuna kiungo kilicho muhimu kuliko kingine.
    2. Moyo ni muhimu kuliko viungo vingine vyote.
    3. Kuna viungo muhimu kuliko vingine.
    4. Mapafu ni muhimu kuliko moyo.

Swali la 16 hadi la 20

Soma kifungu kifuatacho. Kwa kila swali umepewa majibu manne. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Muhula ___16__ tulifunzwa mambo __17__ katika somo __18__ ninalipenda sana Kiswahili. Tulifundishwa vivumishi vya sifa kama vile  __19__ na viwakilishi vya nafsi kama vile __20__.

   A   B   C   D 
 16.   uliopita   iliyopita   zilizopita   kilichopita 
 17.  kingi  wengi   vingi   mengi 
 18.  ambayo   ambazo   ambalo  ambao
 19.  changu  kubwa  hili  watatu
 20.  mimi  huu  kumi  dogo

 

Swali la 21 hadi la 30

Chagua jibu sahihi.

  1. Hii ni picha ya mchezaji. Anacheza mchezo gani?
    G6SwaT2OS32023Q21
    1. Chesi
    2. Kandanda
    3. Tenisi
    4. Jugwe
  2. Hili ni jedwali la maneno. Chagua jibu linaloonyesha vitenzi?
     A   shamba   Mimi   Wangu 
     B  lakini  Lo!   Polepole 
     C  lala  Soma   palilia
     D  Nyuma ya   Igiza   Pendwa 
  3. Kati ya maneno haya ni gani litakuja mwisho kialfabeti?
    1. Kavu
    2. Kaa
    3. Kaza
    4. Hal
  4. Ni maneno yapi yaliyo katika ngeli moja?
    1. Ukuta, unywele, uzi
    2. Mkeka, sikio, jicho
    3. Nyusi, goti, tumbo 
    4. Pafu, moyo, ini
  5. Chagua jibu ambalo ni wingi wa sentensi:
    Mpera wa mkulima mrefu una ua.
    1. Mpera wa wakulima warefu una maua. 
    2. Mipera ya wakulima warefu ina maua.
    3. Mipera ya mkulima mrefu ina maua. 
    4. Mipera ya wakulima warefu ina nyua.
  6. Chagua maamkuzi au maagano ya wakati wowote
    1. Masalkheri
    2. Sabalkheri
    3. Alamsiki
    4. Salaam aleikum!
  7. Ni maelezo gani yasiyo sahihi kuhusu alama za uakifishi?
    1. Alama ya hisi hutumiwa kuonyesha mshangao.
    2. Alama ya ritifaa hutumiwa katika maneno yenye ving'ong'o
    3. Koloni hutumika kuonyesha hisia mbalimbali.
    4. Alama ya kiulizi hutumika katika sentensi ambayo ni swali.
  8. Chagua sentensi ambayo imetumia kirejeshi 'amba-' vizuri.
    1. Waimbaji ambaye hawakuimba walienda.
    2. Kalamu ambayo imevunjika ni yangu.
    3. Mkeka ambalo umeanguka ni huu.
    4. Meza ambacho imejengwa ni nzuri.
  9. Kamilisha tashbihi hii:
    Mlafi kama ________________________________
    1. Fisi
    2. Chiriku
    3. Kasuku
    4. Nzi
  10. Chagua jibu ambalo ni tofauti na mengine.
    1. Kiangazi
    2. Masika 
    3. Kipupwe 
    4. Mafuriko

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako

Andika insha ya kusisimua kuhusu mada ifuatayo:

MECHI YA KUFURAHISHA

MARKING SCHEME

  1. B
  2. B
  3. B
  4. C
  5. B
  6. B
  7. A
  8. A
  9. B
  10. C
  11. B
  12. D
  13. D
  14. B
  15. A
  16. A
  17. D
  18. C
  19. B
  20. A
  21. B
  22. C
  23. C
  24. A
  25. B
  26. D
  27. C
  28. B
  29. A
  30. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 6 Opener Exams Term 2 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students