Tuesday, 01 August 2023 08:21

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 2 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu swali la 1 hadi la 5

(Ni asubuhi baada ya gwaride. Kasim anabisha mlango wa ofisi ya Mwalimu Mkuu. Mwalimu anamkaribisha ndani.)

                                         GRADE5KISWAHILISET22023Q1

Kasim                        : (Akiinama kwa heshima.) Shikamoo mwalimu?

Mwalimu mkuu          : Marahaba Kasim. Umeamkaje? Natumai kila kitu ni salama. Si kawaida yako kunitembelea ofisini asubuhi.

Kasim                        : Nimeamka vyema mwalimu. Nashukuru. Hakika niliamka alfajiri. Mzazi wangu aliniamsha ili anikabidhi barua hii.                                                      (Anamkabidhi mwalimu bahasha.)

Mwalimu mkuu          : Aha! Nilijua lazima una sababu ya kuja ofisini mwangu asubuhi. Barua ina ujumbe gani?

Kasim                        : Sina habari. Nimepewa tu. Labda ni mwaliko au jambo fulani. Mwalimu, ulitufunza kuwa si vyema kusoma barua za watu                                          wengine.

Mwalimu mkuu          : (Akimpongeza.) Hongera Kasim. Wewe ni mtoto mwema. Ni vizuri kutosoma barua ambazo si zako.

Kasim                        : (Akinyenyekea.) Shukran mwalimu. Mzazi wangu pia hunihimiza niwe na uaminifu kwa kuwa, heshima si utumwa.

Mwalimu mkuu          : Nashukuru kwa maneno yako. Sasa unaweza kujiunga na wengine darasani. Endelea kutia bidii za mchwa masomoni.                                            Nitakupatia majibu ya barua alasiri.

Kasim                        : Asante mwalimu. Kwaheri. Tutaonana wakati huo wa alasiri.

Mwalimu mkuu          : Kwaheri ya kuonana.

 1. Je, Kasim alienda katika ofisi ya mwalimu wakati gani?
  1. Jioni
  2. Alasiri
  3. Adhuhuri
  4. Asubuhi
 2. Kitendo cha Kasim kutoisoma barua aliyopewa na mama yake kinaonyesha maadili gani?
  1. Utiifu
  2. Uaminifu
  3. Upendo
  4. Ushirikiano
 3. Kasim na Mwalimu Mkuu walikamilisha mazungumzo yao kwa
  1. Kusalimiana
  2. Kuamkuana
  3. Kuagana
  4. Kufarijiana
 4. Nini maana ya neno hunihimiza?
  1. Hunishauri
  2. Hunionya
  3. Huniambia
  4. Hunitia moyo
 5. Ni Methali gani imetumiwa katika mazungumzo haya?
  1. Heshima si utumwa
  2. Bidii za mchwa
  3. Kwaheri ya kuonana
  4. Hongera

Swali la 6 hadi la 9

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

                                     GRADE5KISWAHILISET22023Q6

Jamii inaweza kukabiliana na tatizo la umaskini ikiwa itajitahidi. Kila raia anafaa kutia bidii katika shughuli anazofanya ili kujipatia riziki. Kazi hizo zinaweza kuwa za kiufundi au za ofisini. Tukumbuke kuwa kazi ni kazi.

Mazingira bora ya kufanyia kazi ni muhimu kwa kila mwananchi. Kuwepo kwa amani na utulivu kutawawezesha raia kubuni nafasi za kazi. Wataweza kujiajiri na kuwaajiri wengine.

Hatua ya kuwaelimisha raia kuhusu kazi za kiufundi ni muhimu kwani itapunguza umaskini. Kazi hizo za kiufundi ni kama vile, usonara, ususi, useremala, na upishi. Wananchi wakipata maarifa haya wataweza kujitegemea na kutegemewa na jamii.

Ni muhimu kutambua kuwa afya bora ina manufaa kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Ukiwa na afya njema utafanya kazi kikamilifu. Hivyo basi umaskini utapunguzwa.

 1. Kulingana na aya ya kwanza, jamii inaweza kukabiliana na tatizo la umaskini ikiwa _____
  1. itafanya bidii
  2. itakuwa na heshima
  3. itakuwa na utiifu
  4.  itakuwa na uzembe
 2. Kati ya kazi hizi za kiufundi ni gani inahusu utengenezaji wa fanicha
  1. Usonara
  2. Ususi
  3. Useremala.
  4. Upishi
 3. Kulingana na kifungu ni gani kati ya hizi si njia ya kukabiliana na umaskini?
  1. Kujitahidi
  2. Kuondoa amani na utulivu
  3. Mazingira bora ya kufanyia kazi
  4. Kuelimisha raia kuhusu kazi za kiufundi
 4. Ujumbe wa kifungu hiki ni gani?
  1. Kukabiliana na umaskini
  2. Kujitahidi
  3. Afya njema
  4. Kujiajiri na kuajiriwa

Swali la 10 hadi la 12

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

Sungura aliwaalika wanyama wengi kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake. Alimtafuta Kobe ili ampikie. Aliagiza keki kubwa ya karoti. Siku ilipowadia Kobe alirauka kwa Sungura.

"Naomba uwatayarishie wageni wangu nyama, pilau na supu." Alisema Sungura. "Sawa. Je, viungo vyote unavyo?" Aliuliza Kobe. "Ninavyo. Nina mdalasini, iliki, kitunguu maji na kitunguu saumu.' Akajibu Sungura. "Hivyo havitoshi. Bado tutahitaji chumvi, pilipili hoho na nyanya." Alisema Kobe. "Kwa nini viungo hivyo vyote?" Aliuliza Sungura."Nataka kutayarisha supu nzito. Wageni wanywe supu na kula shibe yao." Alisema Kobe. Sungura alimpa Kobe viungo vyote alivyohitaji. Kobe alitayarisha mlo ulionukia. Wanyama walipowasili waliona nyungu kubwa iliyokuwa ikitokota nje ya jiko. Fisi alikuwa miongoni mwa wanyama hawa.

Fisi alinyemelea nyungu wakati wanyama walikuwa wakimwimbia Sungura. " Leo ni siku yangu. Nitakula na kunywa kuliko siku zote." Fisi alijisemea.

Aliepua nyungu na kuanza kunywa supu tamu. Supu yenyewe ilikuwa moto. Hata hivyo, Fisi aliinywa yote huku jasho likimtoka. Hakuwajali wengine. Fisi alipomaliza kunywa supu alijaribu kutembea akashindwa. Alipumua kwa shida. Mara akamwona Kobe akiwa amebeba sinia kubwa la pilau na bakuli la nyama.Fisi alijuta kwanini hangeweza kula chakula hicho.

"Naomba msamaha kwa kunywa supu yote." Fisi alilia. Wanyama walimsamehe na kumpa onyo kali. Fisi aliahidi kuwa hangerudia kosa hilo.

 1. Kwa nini Sungura alimtafuta Kobe?
  1. Awakaribishe wageni
  2. Amwonyeshe kupika
  3. Atafute chakula
  4. Ili afanye shughuli ya upishi
 2. Tabia ya fisi kunywa supu yote bila kuwajali wengine inadhihirisha kuwa fisi ana
  1. ukarimu
  2. ulafi
  3. upendo
  4. njaa
 3. Jina lingine la chakula ni mlo. Je, jina lingine la sherehe ni :
  1. Sikukuu
  2. Karamu
  3. Furaha
  4. Siku ya kuzaliwa

Swali la 13 hadi la 15

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.

                                GRADE5KISWAHILISET22023Q13

Baraka ni mvulana anayependa kula lishe bora. Ana menyu ambayo humhakikishia amepata virutubisho muhimu katika mwili wake. Akimaliza kula huwa anakunywa maji bilauri moja. Anajua umuhimu wa lishe bora ni kumfanya awe na afya bora. Yeye huwa haugui ovyoovyo. Ifuatayo ndiyo ratiba yake.

          Asubuhi        Adhuhuri         Jioni
 Glasi moja ya maziwa  Pilau  Ugali wa wimbi 
 Viazi vikuu  Mchuzi wa kuku   Maharagwe
 Mboga za kiasili  Sukumawiki  Mboga za kiasili
 Tunda  Tunda  Tunda

 

 1. Chakula ambacho Baraka hula siku inapoanza ni gani?
  1. Chamcha
  2.  Virutubisho
  3. Kiamshakinywa
  4. Chajio
 2. Baraka hula _____ katika kila mlo?
  1. Mboga
  2. Matunda
  3. Wali
  4. Ugali
 3. Kwa nini Baraka hula lishe bora?
  1. Ili aepuke magonjwa
  2. Kwa sababu ana ratiba
  3. Ili apewe zawadi
  4. Ili asiwe na afya bora

Soma kifungu kifuatacho. Kina nafasi 16 hadi 20. Umepewa majibu manne hapo. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Nilienda shambani nikaona__16_ya siafu. Walikuwa wametengeneza mstari __17__. Wakati huo nilikuwa nimebeba redio __18__ mkononi. Niliwaondokea wadudu ___19__ nikaenda kukaa __20___ mchungwa kwenye kivuli kuisikiliza redio

 
 16  halailki  safu   mlolongo   kikosi 
 17  ndefu  refu   kirefu   mrefu 
 18  yangu  wangu   changu   langu 
 19  huyo  hayo   hao   hizo 
 20  ndani ya   chini ya   juu ya   katikati ya

 

Kutoka swali la 21 hadi la 30, chagua jibu sahihi.

 1. Chagua nomino ambayo si dhahania:
  1. Furaha
  2. Uzi
  3. Hekima
  4. Ukarimu
 2. Andika sentensi ifuatayo katika hali ya wingi:
  Unyoya wa kuku yule ni mweupe.
  1. Manyoya ya kuku wale ni meupe
  2. Nyoya za kuku wale ni nyeupe
  3. Unyoya wa kuku wale ni mweupe
  4. Manyoya ya kuku yule ni meupe
 3. Chagua sentensi yenye nomino iliyo katika ngeli ya I-ZI:
  1. Ng'ombe wetu alipelekwa malishoni.
  2. Wimbo ulioimbwa uliwavutia wengi.
  3. Nguo iliyofuliwa ilikauka haraka.
  4. Wino ulimwagika sakafuni jana.
 4. Jaza pengo kwa jibu sahihi. Kusoma _____ kunapendeza.
  1. yake
  2. chake
  3. kwake
  4. lake
 5. Jaza pengo katika sentensi hii.
  Mangi alimwita Otieno naye Otieno akamwita Mangi.
  Hivyo wote _____
  1. waliitika
  2. waliitana
  3. waliitiana
  4. waliitwa
 6. Kinyume cha kitenzi anika ni
  1. osha
  2. fu
  3. vua
  4. anua
 7. Sentensi hii iko katika wakati au hali gani?
  Wanafunzi huenda uwanjani kucheza soka.
  1. Hali timilifu
  2. Hali ya mazoea
  3. Wakati ujao
  4. Wakati uliopita
 8. Kanusha sentensi hii: Yeye ataandika ubaoni.
  1. Wao hawataandika ubaoni
  2. Yeye hakuandika ubaoni
  3. Yeye haandiki ubaoni
  4. Yeye hataandika ubaoni
 9. Kati ya Maneno haya ni lipi litakuwa la mwisho katika kamusi?
  1. Pona
  2. Dawa
  3. Kodi
  4. Tibu
 10. Chagua kiambishi kinachofaa kujaza pengo katika sentensi hii.
  Nyinyi _____ tafanikiwa maishani
  1. wa
  2. m
  3. a
  4. ni

INSHA

Andika insha kuhusu mada ifuatayo:

MWALIMU WANGU WA KISWAHILI

MARKING SCHEME

 1. D
 2. B
 3. C
 4. D
 5. A
 6. A
 7. C
 8. B
 9. A
 10. D
 11. B
 12. B
 13. C
 14. B
 15. A
 16. B
 17. D
 18. A
 19. C
 20. B
 21. B
 22. A
 23. C
 24. C
 25. B
 26. D
 27. B
 28. D
 29. D
 30. B

 

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End Term 2 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students