Friday, 01 September 2023 08:53

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 3 2023 Set 1

Share via Whatsapp

Soma makala yafuatayo halafu ujibu maswali yanayofuata.

G5SwaT3OS12023Q1

Katika msitu wa Eshikalame, Njiwa alijulikana sana kwa sauti yake ya kupendeza. Karibu kila mnyama na kiumbe katika msitu huo alimfahamu kwa ushauri wake aliowatolea. Kila wakati wa jua kuaga miti, ungewapata ndege wakiwa wamejaa kwenye mti ili kufurahia utamu wa nyimbo na ushauri wa njiwa. Wanyama mbalimbali pia walisimama chini ya mti huo. Siku moja, palitokea vita katika msitu huo. Wanyama na ndege walipigana bila kujali. Walipokuwa katika hali hiyo ya vita, Njiwa aliwakariria shairi lililofanya kuacha kupigana. Alianza hivi:

Na wenzangu sikiliza, vita ni kitu kibaya,
Wengi wetu angamiza, kuua bila ya haya,

Kwa makini kichunguza, hapakuwa na ubaya,
Sote tuweni pamoja, tuwe na amani tena.

Makosa yakitokea, usamehe tafadhali,
Vyema wewe kutulia, hasira naziwe mbali,
Jamani nakuambia, yote haya ni ukweli,
Sote tuweni pamoja, tuwe na amani tena.

 1. Kulingana na makala haya, Njiwa;
  1. alijua karibu kila mnyama na kiumbe.
  2. alijulikana na kila mnyama na kiumbe.
  3. alijulikana na wanyama na viumbe wengi.
  4. alikuwa akitolewa ushauri.
 2. Maneno 'wakati wa jua kuaga miti' yana maana gani jinsi yalivyotumika katika kifungu? 
  1. wakati wa jioni
  2. wakati wa mchana
  3. wakati wa adhuhuri
  4. wakati wa asubuhi
 3. Kibwagizo cha shairi lililokaririwa na Njiwa kina mizani mingapi?
  1. 15
  2. 4
  3. 2
  4. 16
 4. Tambua vina vya kati vya ubeti wa kwanza.
  1. ya
  2. za
  3. ja
  4. ya
 5. Ushauri wa Njiwa katika shairi unaweza ukarejelewa kwa methali gani?
  1. Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. 
  2. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu.
  3. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
  4. Siku za mwizi ni arubaini.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yafuatayo.

G5SwaT3OS12023Q2

Hezekia Omulama, kijana aliyekuwa katika gredi ya tatu, alipewa shilingi mia mbili na shangazi yake mwezi wa Disemba. Wakati huo, Hezekia alikuwa mfupi kama nyundo. Baada ya kumshukuru shangazi yake, alitumia pesa hizo kununua sungura mmoja mdogo. Baada ya miezi sita, sungura huyo alizaa vitungule waliopendeza sana. Watoto hao wa sungura waliendelea kulishwa majani mbalimbali ambayo Hezekia na dada yake walichuma shambani. Alifuata ushauri wa wazazi wake kuhusu ufugaji wa sungura hadi alipokuwa na sungura wengi. Alianza kuuza sungura wachache ili apate pesa alizojiwekea katika benki. Baba yake alikuwa amemfungulia akaunti ya watoto.

Hezekia alizungumza na mama yake ili ampe nafasi ya shamba dogo hapo nyumbani pao. Alianza kupanda mboga na matunda. Wakati ambao hakuenda shuleni, yeye na marafiki zake walipalilia mboga na matundo ili kuondoa magugu. Walipomaliza kazi hiyo, Hezekia aliwapa marafiki zake matunda kadhaa kama shukrani. Pia, aliwapa mboga kidogo ili wapeleke nyumbani kwao. Hezekia ana mpango wa kuwa mwanabiashara mkubwa baada ya kumaliza masomo yake. 6.

 1. Hezekia alipewa pesa na nani?
  1. dada wa mama yake
  2. dada wa baba yake
  3. mfanyakazi wa nyumbani
  4. dada yake
 2. Kauli 'mfupi kama nyundo' ni mfano wa;
  1. nahau
  2. tashbihi ya tabia
  3. tashbihi ya umbo
  4. kitanzandimi
 3. Ni kweli kuwa sungura wa Hezekia alizaa Hezekia akiwa katika;
  1. Gredi ya tatu
  2. Gredi ya nne
  3. Gredi ya tano
  4. Gredi ya sita
 4. Kifungu kinaeleza kuwa Hezekia alikuwa na tabia gani;
  A. mtiifu, mwenye bidii
  B. mjanja, mwaminifu
  C. mwenye bidii, mwongo
  D. mpole, anayependa kucheza
 5. Hezekia ana mpango wa kuwa mfanyabiashara katika;
  1. gredi ya saba.
  2. maisha yake yaliyopita.
  3. maisha ya sasa
  4. maisha yake yajaayo.

Soma ufahamu unaofuata kisha ujibu maswali.

G5SwaT3OS12023Q3

Kuna aina nyingi za simu. Simu ambayo hutumika sana ni simu ya mkononi. Simu ya mkononi huitwa rununu, rukono, simutamba au selula. Watu wengi sana hutumia simu siku hizi. Hii ni tofauti na kitambo ambapo watu waliotumia simu walikuwa wachache. Kazi kubwa ya simu ya mkononi ni mawasiliano. Mawasiliano ni kupitisha ujumbe kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Faida ya mawasiliano ya kuzungumza kwa simu ni kuwa hata watu wasiojua kusoma na kuandika huweza kuwasiliana.

Kunao watu ambao husikiliza redio kupitia simu. Watu hao husikiliza taarifa za habari na mambo mengine kupitia redio iliyo kwenye simu. Simu pia hutumika kupiga hesabu kwa kutumia kikokotoo, kupiga picha na kucheza video. Hakika, simu ina umuhimu mkubwa katika maisha. Hata hivyo, simu pia ina madhara yake. Kutumia simu kila wakati kunaleta shida mbalimbali. Kwa mwanafunzi, kutumia simu kila wakati humpotezea mwanafunzi huyo nafasi ya kufanya mambo muhimu. Mambo muhimu kwa mwanafunzi ni kusoma na kufanya kazi za ziada.

 1. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kuwa;
  1. kuna aina za simu zisizojulikana.
  2. watu wote hutumia simu siku hizi. 
  3. watu wachache huwa hawatumii simu. 
  4. kuna aina chache za simu.
 2. Kifungu kinaeleza kuwa kitambo;
  1. hakuna aliyetumia simu.
  2. watu wengi hawakujua simu.
  3. watu wengi hawakuwa na simu.
  4. hakuna aliyejua simu.
 3. Kulingana na aya ya pili, simu huweza kufanya yafuatayo isipokuwa;
  1. kusikiliza taarifa za habari.
  2. kupiga picha.
  3. kupiga hesabu
  4. kufanya mawasiliano
 4. Ufahamu unaeleza kuwa mambo gani ambayo ni muhimu kwa mwanafunzi?
  1. kusoma na kufanya kazi za ziada
  2. kusoma na kucheza na wenzake
  3. chakula bora na kucheza
  4. kucheza na kufanya kazi za ziada
 5. Ufahamu unaeleza kuwa simu;
  1. haina umuhimu wowote. 
  2. ina faida na madhara. 
  3. ina madhara mengi.
  4. haina madhara yoyote.

Chagua jibu linalofaa kati ya majibu uliyopewa ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Fisi alipohisi kuwa chakula ___16___ kilikuwa kikiandaliwa mahali, ___17___ na mate ndo ndo ndo! Alianza kutembea
___18___ ili mtu asimsikie. Alielewa kuwa haraka haraka haina baraka. ___19___ karibu na nyumba hiyo, aliingia na kuchukua chakula kilichokuwa ndani ya chungu. Baada ya kumeza, ndipo alipogundua kuwa alikuwa amemeza jiwe. Alichomeka sana tumboni ___20___. Akaelewa kuwa tamaa ina madhara mengi.

   A   B   C   D 
 16.   vitamu   tamu   kitamu   mtamu 
 17.  alitiririkwa  alidondokwa   aliteremkwa   alimwagikwa 
 18.  kwa upole   polepole   haraka   kwa mbio 
 19.  Alipofika  Alivyofika  Aliyefika  Aliofika
 20.  wake  yake   lake   mwake 


Jibu maswali yafuatayo kulingana na maagizo.

 1. Tambua nomino ya pekee kwenye sentensi ifuatayo.
  Amina alicheza kwa furaha baada ya kusoma na kunywa chai.
  1. chai
  2. Amina
  3. furaha
  4. kusoma
 2. 'Cheza' ni kwa chezewa kama vile pika ni kwa;
  1. pikwa
  2. pikia
  3. pikiwa
  4. pikika
 3. Chagua neno litakalokuwa la pili kwenye kamusi.
  1. chupa
  2. chungu
  3. chumba
  4. chuma
   1. iii
   2. iv
   3. i
   4. ii
 4. Orodha gani iliyo na nomino za dhahania pekee?
  1. huzuni, uchoyo, uchafu
  2. maji, maziwa, sukari
  3. amani, upendo, chuki
  4. umati, kicha, thureya
 5. Sentensi gani iliyoakifishwa kwa njia inayofaa?
  1. Miji ninayoijua ni Nairobi na Mombasa.
  2. Tutaenda sokoni siku ya alhamisi.
  3. Nimenunua unga, sukari, na sabuni.
  4. Darasa letu limeoshwa na wanafunzi
 6. Nomino gani isiyopatikana katika ngeli ya LI-YA?
  1. gari 
  2. darasa
  3. giza
  4. jitu
 7. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari. Amerudi kwa sababu alisahau pesa juu ya meza.
  1. kiunganishi, kihisishi
  2. kiunganishi, kihusishi
  3. kivumishi, kihisishi
  4. kivumishi, kihusishi
 8. Chagua wingi wa;
  Mwashi huyu amechukua saa yangu.
  1. Waashi hawa wamechukua saa zangu.
  2. Waashi hawa wamechukua masaa yetu. 
  3. Waashi hawa wamechukua masaa yangu
  4. Waashi hawa wamechukua saa zetu. 
 9. Sentensi gani iliyo katika wakati uliopita hali ya kuendelea?
  1. Musa alienda sokoni.
  2. Sote tunapangusa viatu vyetu.
  3. Yohana angali anakata kucha zake.
  4. Walikuwa wakisugua meno yao.
 10. Tegua kitendawili.
  Nifunue nikufunike.
  1. kofia
  2. mwavuli
  3. nyumba
  4. kifuniko

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu mada inayofuata.

AJALI BARABARANI

MARKING SCHEME

 1. C
 2. A
 3. D
 4. B
 5. A
 6. B
 7. C
 8. C
 9. A
 10. D
 11. C
 12. C
 13. D
 14. A
 15. B
 16. C
 17. B
 18. B
 19. A
 20. D
 21. B
 22. C
 23. A
 24. C
 25. A
 26. C
 27. B
 28. D
 29. D
 30. B
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 3 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students