Monday, 06 September 2021 07:27

Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 1

Share via Whatsapp

COMPETENCY BASED CURICULUM
GREDI YA 5, MWISHO WA MUHULA WA 1
SHUGHULI ZA KISWAHILI 
JINA....................................................SHULE............................................

SEHEMU 1
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
Mwalimu amsomee mwanafunzi kifungu hiki kisha amwulize mawasli yafuatayo

Paka yuko jikoni. Amebeba panya mdomoni. Panya huyo ni mweusi. Paka anajificha mvunguni mwa meza. mama anamwona paka.

  1. Paka yuko wapi?
    (mwananfunzi ajibu)
  2. Paka amebeba nini mdomoni?
    (mwananfunzi ajibu)
  3. Panya huyo ni wa rangi gani?
    (mwananfunzi ajibu)
  4. Paka anajificha wapi?
    (mwananfunzi ajibu)
  5. Nani anamwona paka?
    (mwananfunzi ajibu)

SEHEMU 2
KUSOMA KWA SAUTI
Mwanafunzi asome kifungu hiki kwa sauti

Ilikuwa siku ya Ijumaa tulipokuwa sebuleni tukitazama runinga. Baba alianza kutusimulia jinsi ambavyo mwalimu wao alikuwa akiwaeleza kuhusu umuhimu wa miti. Hata ingawa alikuwa shuleni miaka sitini iliyopita, alikuwa anayakumbuka vizuri.

Alianza kwa kusema kuwa mwalimu wao alisema kuwa miti huwa maskani ya wanyama mbalimbali sanasana nyuni ambao hutengeneza viota vyao na kutagia mayai humo. Aliendelea kutuambia kuwa wanyama wengine wanaotegemea miti kama makazi ni wanyamapori vile samba , chui, pundamilia na wengine.

SEHEMU 3:
UFAHAMU
Mwalimu asome kifungu hiki na kujibu maswali

  1. NDOTO YA AMINA
    Babu alimnunuluia Amina godoro na foronya. Usiku alipolala, aliota ndoto. Aliota kuwa alikuwa msichana mkubwa. Alikuwa akifanya kazi ya ualimu. Baada ya miaka miwili aliacha ualimu akawa mkulima. Aliuza mazao akapata shilingi laki tatu. Alipokuwa akipeleka pesa zake benkini, aliamka kutoka usingizini.

    1. Nani alimnunulia Amina godoro?
    2. Aliota ndoto wakati gani?
    3. Mara ya kwanza alikuwa akifanya kazi gani?
    4. Baada ya miaka miwili alianza kufanya kazi gani?
    5. Alikuwa akipeleka pesa zake wapi?

  2. MWALIMU BIDII
    Mwalimu Bidii ni mwalimu wa Kiswahili. Anafundisha katika shule ya msingi ya Hekima. Kila siku yeye hutukumbusha kuwa tuwe watoto safi. Kuna siku alituletea ndizi. Tulifurahia mno. Alituahidi kuwa atatupeleka jijini Mombasa.
    1. Mwalimu Bidii hufundisha somo gani?
    2. Mwalimu Bidii hufundisha katika shule gani?
    3. Mwalimu Bidii huwahimiza wanafunzi kuwa watoto__________________
    4. Mwalimu aliwaletea nini?
    5. Mwalimu aliwaahidi kuwa atawapeleka wapi?

SEHEMU 4: SARUFI

  1. Tunga sentensi ukitumia maneno haya
    1. Jiwe 
    2. Embe
    3. Mwiko
    4. Soko
    5. Fimbo
  2. Andika sentensi kwa wingi
    1. Kiatu chake kimeraruka

      _______________________________________________________________
    2. Mtoto yule anakula tunda

      _______________________________________________________________
    3. Goti lake limeumia.

      _______________________________________________________________
    4. Kioo hiki kilivunjika jana.

      _______________________________________________________________
    5. Meza hii ni ya mwanafunzi.

      _______________________________________________________________
  3. Andika akisami kwa maneno
    1. 1/6
    2. 1/4
    3. 1/2
    4. 1/3
    5. 1/5
  4. Geuza maneno yafuatayo katika hali ya ukubwa
    1. Mto
    2. Mtu
    3. Mke
    4. Mti
    5. Mji

INSHA
Andika insha kuhusu
NYUMBANI KWETU

 

MAAKIZO

SEHEMU 1
Mwanafunzi anafai kujibu kulingana na swali aliloulizwa

SEHEMU 2
Mwanafunzi anafai kusoma kwa sauti kifungo chote

SEHEMU 3

  1. NDOTO YA AMINA
    1. Babu
    2. Usiku alipolala
    3. Ualimu
    4. ukulima
    5. benkini

  2. MWALIMU BIDII
    1. Kiswahili
    2. Shule ya msingi ya Hekima
    3. watoto safi
    4. Ndizi
    5. (jijini) Mombasa

SEHEMU 4: SARUFI

  1. Kutunga sentensi:
    Mwanafunzi anafai kutunga sentensi kulingana na maana sahihi ya maneno aliyopewa
  2. Wingi
    1. Viatu vyao vimeraruka
    2. Watoto wale wanakula matunda
    3. Magoti yao yameumia
    4. Vioo hivi vilivunjika jana
    5. Meza hizi ni za wanafunzi
  3. Akisami
    1. Sudusi
    2. robo
    3. nusu
    4. thuluthi
    5. humusi
  4. Ukubwa   
    1. Jito
    2. jitu
    3. jike
    4. jiti
    5. jiji
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Activities - Grade 5 End Term 1 Exam 2021 SET 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students