Friday, 28 October 2022 11:59

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 November 2022 Exams Set 1

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU 3: Ufahamu
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali
Siku takapoamka, ujipate na maskini,
Usije ndugu kumaka, ukakosa tumaini,
Jua kuna kuikuka, aka unajithamini.
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi
Mosi ukienda shuleni, masomo makinikia,
Elimu kuithamini, hadi kuimalizia,
Utapata tumaini, uje kujitegemea,
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi.
Kazi itakapokuja, pesa uanze kuigiza,
Jua kesho inakuja, sifanye kwangamiza,
Usije ukazifuja, maisha kuangamiza,
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi.
Pesa zinapokwezesha, kununua yako mali,
Ni muhimu kuboresha, kwa hali pia kwa mali,
Hekima kuzalisha, kimoja kiwe kiwili,
Ufukara haudumu, unahitaji bidii.
Chunga gharama nyumbani, vifaa napotumia,
Si mojawapo bafuni, si umeme kuonea,
Lishe kibaki mezani, yafaa kuhifadhia,
Ufukara haudumu, unahitaji juhudi.

  1. Taja vina vya kati vya ubeti wa pili;
    1. -a
    2. -ni
    3. -na
    4. -ka
  2. Shairi hili lina beti ngapi?
    1. Nne
    2. Tano
    3. Nane
    4. Kumi na sita
  3. Taja kibwagizo cha shairi bili. 
    1. mosi ukienda shuleni masomo makinikia
    2. siku yanapoamka ujipate maskini 
    3. Ufukara haudumu unahitaji juhudi
    4. chunga gharama, nyumbani vifaa napotumia
  4. Ubeti wa kwanza una mizani ngapi?
    1. 16
    2. 64 
    3. 8
    4. 17
  5. Shairi hili ni la aina gani?
    1. Tathnia 
    2. Tathlitha
    3. Tasdisa
    4. Tarbia
  6. Ubeti wa tatu unatuhimiza kuwa; 
    1. tumia pesa au mali vizuri 
    2. tuwe na hekima 
    3. tufanye bidii 
    4. tuthamini elimu
  7. Neno 'gharama' lina silabi ngapi? 
    1. Saba
    2. Tano 
    3. Tatu
    4. Nane
  8. Mtu anayetunga shairi huitwa; 
    1. Manju
    2. Sogora 
    3. Malenga
    4. Mghani
  9. Kulingana na shairi hili kumaliza ufukara tunafaa kufanya nini? 
    1. Kuamka mapema 
    2. Kufanya bidii 
    3. Kununua mali 
    4. Kula lishe bora
  10. Kibwagizo cha shairi hili kina mizani ngapi A. 
    1. 16
    2. 8
    3. 64
    4. 32

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali yafuatayo
Nyani na binamu walikuwa marafiki wa kufa kuzikana. Waliishi pamoja wakisaidiana kazi za bani. Wote walikuwa na ngozi laini na nyororo. Siku moja nyani na binamu walitayarisha maharagwe kuvaweka kwenye sufuria. Waliwasha jiko la seredani na kuweka sufuria ya maharagwe juu ya yake.
Kama ilivyokuwa kawaida yao, nyani na binamu walienda kuoga mtoni, nyani alijisugua kichwa na mwili wote. Binamu pia alifanya vivyo hivyo huku maharagwe yakiendelea kuiva.
Hatimaye nyani na binamu yake walienda nyumbani. Walijipakulia maharagwe yaliyoiva. Kila mmin akapata kiwango sawa na mwengine. Nyani alikula sehemu vake, naye binamu ale sehemu yake hin ani hushiba. Nyani alitamani kujiongeza mlo. Hivyo basi alitafuta nama va kuiongezea chakula

Maswali

  1. Nyani na binadamu walikuwa marfiki wa kufa kuzikana. Hii ina maana gani? 
    1. Wote walikufa 
    2. Walipendana sana 
    3. Walisaidiana 
    4. Walifahamiana
  2. Nyani na binadamu walipika chakula gani? 
    1. Madondo 
    2. Pure 
    3. Ndovi
    4. Wali
  3. Nyani na binadamu walikuwa na mazoea ya kufanya nini? 
    1. Kupika maharagwe 
    2. Kuoga mtoni 
    3. Kuwasha jiko
    4. Kula sima
  4. Nyani na binadamu walitumia jiko la seredani je, jiko hili linatumia nini? 
    1. Kuni
    2. Mafuta 
    3. Makaa
    4. Gesi
  5. Mbona nyani alipanga njama ya kujiongeza chakula? 
    1. Alikuwa mlafi 
    2. Alitaka kuwapelekea wanawe 
    3. Kilikuwa kitamu sana 
    4. Hakushiba
  6. Taja methali moja ambayo inaonyesha ushirikiano kati ya nyani na binadamu? 
    1. ajizi ni nyumba ya njaa 
    2. umoja ni nguvu utengano ni udhaifu 
    3. bidii hulipa 
    4. mwana hutazama kisogo cha ninaye
  7. Nyani na binadamu walipenda kuoga mtoni. Neno mto liko katika ngeli gani? 
    1. PA-KU-MU
    2. U-I 
    3. LI-YA
    4. I - ZI

Jaza nafasi zilizoachwa kwa majibu yanayofaa
Safari_18_ nilikuwa _19_ dhidi ya _20_ kinywani chochote_21_ kuepukana na kutiliwa dawa za kulevya ambazo zingedhuru afya yangu.

  1.    
    1. kilifika
    2. itakapofika
    3. imefika
    4. ilipofika
  2.    
    1. nimeruhusiwa 
    2. nimeonywa
    3. nimepewa
    4. nimekabiliwa
  3.    
    1. kunyweshwa 
    2. kunywewa
    3. kukunywa
    4. kunywa
  4.    
    1. ndani ya njia 
    2. njia
    3. karibu na njia 
    4. njiani
  5. Ni lipi jibu mwafaka kwa maamkizi makiwa?
    1. yamepita
    2. jaala
    3. nawe pia
    4. asante
  6. Ni lipi si pambo la mwili katika kundi lifuatalo?
    1. Aproni 
    2. Mkufu
    3. Herini
    4. kidani
  7. Chagua nomino ya dhahania katika orodha inayofuata.
    1. kiamshakinywa 
    2. maisha
    3. Jumamosi 
    4. tita-la kuni

Andika wingi wa sentensi hii
Chupa yake imevunjika. 

  1. Chupa zao zimevunjika 
    1. Chupa zake zimevunjika 
    2. Vyupa vya vimevunjika 
    3. Machupa yao yamevunjika
  2. Chagua methali yenye maana sawa na Mgaagaa na upwa hali wali mkavu. 
    1. asiyesikia la mkuu huvunjika guu 
    2. mtaka cha mvunguni sharti ainame 
    3. majuto ni mjukuu
    4. heshima si utumwa
  3. Ni neno lipi kati ya maneno haya halina maana sawa na ugonjwa?
    1. Maradhi 
    2. Uele
    3. Uwele
    4. Ukongo
  4. Chagua kundi la maneno ya ngeli ya U-ZI
    1. upishi, ulezi uovu
    2. ukuta, nguo, nywele 
    3. mkoba, miti, mkono 
    4. nyasi, nywele, uta
  5. Ni neno lipi limeambatanishwa vizuri na kinyume chake?
    1. Rafiki - mwandani
    2. Simama - usisimame 
    3. Tabasamu - cheka 
    4. Nuna - tabasamu
  6. Chagua kiunganishi katika sentensi ifuatayo Alinunua koti kubwa lakini halipendezi. 
    1. alinunua 
    2. lakini 
    3. kubwa
    4. halipendezi

INSHA
Andika insha ya kusisimua ukizingatia mada ifuatayo;
CHAKULA NIKIPENDACHO

 

 

 



MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

  1. B
  2. C
  3. D
  4. A
  5. A
  6. A
  7. C
  8. D
  9. B
  10. D
  1. C
  2. C
  3. B
  4. C
  5. D
  6. A
  7. B
  8. D
  9. A
  10. C
  1. B
  2. A
  3. C
  4. D
  5. A
  6. B
  7. D
  8. A
  9. C
  10. D
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 End of Term 3 November 2022 Exams Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students