Wednesday, 01 March 2023 13:15

Kusikiliza na kuzungumza Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 Set 2

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

Mwalimu amsalimie mwanafunzi. Hujambo?

(Mwanafunzi ajibu)

Mwalimu amtayarishe mwanafunzi kumalizia methali

 1. Polepole _____________________________________________
 2. Mtaka cha mvunguni ____________________________________
 3. Baada ya dhiki _________________________________________
 4. Kikulacho ki ___________________________________________
 5. Maji yakimwagika _______________________________________
 6. Mtoto akililia wembe _____________________________________
 7. Ujana ni moshi _________________________________________

KUSOMA

Soma kifungu kifuatacho kwa sauti huku ukizingatia matamshi bora

Mmea ni kitu chochote kilichomea chenye majani. Mimea huota kutoka kwenye mbegu. Mimi hukusanya mbegu za matunda kama maparachichi na maembe na kuzianika ili zikauke. Zikishakauka, mimi hutafuta mikebe na kuijaza udongo kisha nikapanda mbegu zile. Huwa ninahakikisha nimeficha mikebe hiyo mahali ambapo haiwezi kufikiwa na mifugo. Kila asubuhi, mimi huzinyunyizia mbegu zangu maji hadi siku ile zitaota. Zikishaota, huwa ninazitoa kwenye mikebe na kuzipanda katika shamba letu. Huko pia, mimi huinyunyizia maji mimea yangu michanga. Magugu yakimea kwenye shamba la mimea yangu, mimi huyang'oa kwa mikono. Mimea ikishakauka, mimi hupalilia. Nyanya yangu alinifundisha kufanya haya nilipokuwa mtoto mdogo sana.

MARKING SCHEME

 1. ndio mwendo
 2. sharti ainame
 3. faraja
 4. nguoni mwako
 5. hayazoleki
 6. mpe
 7. ukienda haurudi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kusikiliza na kuzungumza Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students