Tuesday, 07 March 2023 13:57

Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 Set 5

Share via Whatsapp

Soma kifungu hiki kisha ujibu swali la 1-5.   

G5SwaT1SE23P1
Mzee Siri ni seremala shupavu sana. Katika karakana yake hutengeneza meza, makochi, vitanda na vifaa vingine. Yeye hupenda kuvaa bwelasuti afanyapo kazi ili nguo zake zisichafuke. Pia huvaa chepeo kujikinga dhidi ya ukali wa jua. Nyumba yake imejengwa kusini mwa shule ya Bora. "Nyumba hiyo ina vyumba sita.

Kila jioni yeye pamoja na familia yake; yeye, mkewe na wanawe wawili huketi sebuleni kupata chajio. Chakula hicho huwa kitamu kama asali. Watoto huwasubiri wazazi wao wanawe kisha wao hufuata. Kila mtu hula kwa heshima. Baada ya mlo wao hunawa mikono na kuviondoa vyombo mezani. Baada ya kula, watoto humsaidia mama yao kuviosha vyombo kisha wanaenda vyumbani mwao kulala fofofo!

Maswali

 1. Karakana ya mzee Siri hutengeneza vitu vifuatavyo isipokuwa
  1. meza
  2. ndoo
  3. makochi
  4. vitanda.
 2. Ili kujikinga na miale ya jua, Bw. Siri huvaa vazi gani kichwani?
  1. Chepeo
  2. Bwelasuti
  3. Chupi
  4. Kabuti.
 3. Nyumba ya Bw.Siri ina vyumba vingapi?
  1. 5
  2. 6
  3. 4
 4. 'Chakula kitamu kama asali' ni mfano
  1. methali
  2. tashbihi
  3. nahau
  4. kitendawili.
 5. Familia ya Bw. Siri ina ya watu wangapi?
  1. 2
  2. 3
  3. 5
  4. 4

Soma shairi hili kisha ujibu swali la 6-10.

Nakushukuru mzazi, haja kunitimizia,
Vyakula nayo mavazi, yote waniangalia,
Japoni huna hata kazi, bado wanifikiria,
Pongezi mzazi wangu, kazi nzuri waifanya.

Shuleni kanipeleka, sare yote ukanipa, 
Ukabaki na mkeka, vitu vyote ukanipa,
Huku mimi nikicheka, kipenzi watapatapa,
Pongezi mzazi wangu, kazi nzuri waifanya.

 1. Shairi hili lina beti ngapi?
  1. Mbili
  2. Nne
  3. Nane
  4. Tano.
 2. Kila ubeti una mishororo mingapi?
  1. Mitatu
  2. Miwili
  3. Minne
  4. Minane.
 3. Mshairi anampongeza nani?
  1. Nyanya yake
  2. Rafiki yake
  3. Mzazi wake
  4. Mwalimu wake.
 4. Kisawe cha neno pongezi ni kipi?
  1. Pole
  2. Hongera
  3. Tafadhali
  4. Karibu.
 5. Mshororo wa mwisho una silabi ngapi?
  1. 2
  2. 4
  3. 16
  4. 8

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali 11-15   

Mfalme wa wanyama, Simba, alikuwa akiwatesa sana wanyamapori. Baadhi ya wanyama kama vile Sungura, Fisi, Ndovu na Mwewe waliamua kumfunza adabu. Ijumaa moja, walikusanyika nje ya nyumba yake kwa hasira. Walikuwa wameapa kuikomesha tabia yake ya kuwatesa wanyama wanyonge.

Sungura alienda kuubisha mlango wa pango la Simba. Simba alinguruma kwa mshtuko wa sauti kubwa ya kuogofya. Wanyama wote walitimua mbio kama Swara isipokuwa Fisi. Walishangaa ikiwa siku hiyo ingewaishia vyema. Walipouona ujasiri wa Fisi,walirudi na kuungana naye. Wal'zungumza kwa sauti ndogo kisha wakaelewana kufanya maongezi kwa amani bila kuzua fujo. Hatimaye walielewana na Simba akaahidi kutokula chakula cha wenzake tena ila angekuwa anaenda kuwinda chakula chake mwenyewe.

 1. Mfalme wa wanyama alikuwa nani?
  1. Fisi
  2. Ndovu
  3. Simba
  4. Mwewe.
 2. Wanyama walimtembelea Simba siku gani?
  1. Alhamisi
  2. Ijumaa
  3. Jumatano
  4. Jumamosi.
 3. Ni mnyama yupi hakuenda kwa Simba?
  1. Tembo
  2. Fisi
  3. Sungura
  4. Swara.
 4. Simba aliwatesaje wanyama wengine
  1. Aliwachapa.
  2. Aliwanyima maji.
  3. Aliwanyang'anya mlo.
  4. Aliwatesa waliokuwa wanyonge.
 5. Kati ya wanyama waliomtembelea Simba, ni yupi aliye tofauti?
  1. Mwewe
  2. Sungura
  3. Fisi
  4. Ndovu.

Soma kifungu hiki kisha ujaze mapengo katika swali 16-20 kwa jibu mwafaka.

Sote ___16___ katika lango la mbuga ya wanyama la Nairobi saa ___17___ kamili. Lilionekana kuwa ___18___ kuliko mlango wa kawaida. Mtu ___19___  alitukaribisha. Tulienda sehemu mbalimbali na kuwaona wanyama ___20___.

   A   B   C   D 
 16.   walifika   tulifika   mlifika   nilifika 
 17.  pili   wawili  miwili  mbili
 18.  kikubwa   mkubwa   kubwa  mikubwa 
 19.  mmoja  moja  kimoja  wamoja
 20.  nyingi  chache  wengi  mingi

 

Kutoka swali la 21 hadi 30, chagua jibu sahihi.

 1. Ni neno lipi litapatikana kwanza katika kamusi?
  1. Beba
  2. Babu
  3. Bata
  4. Benki.
 2. Neno mkono katika ukubwa ni _______________
  1. kono
  2. likono
  3. jikono
  4. mikono.
 3. Ni neno gani linapatikana katika ngeli ya LI-YA?
  1. Jua
  2. Joto
  3. Ua
  4. Giza.
 4. Andika sentensi ifuatayo katika wingi.
  Mti umekatwa.
  1. Miti imekatwa.
  2. Miti zimekatwa.
  3. Miti yamekatwa.
  4. Miti zitakatwa.
 5. Kinyume cha shangazi ni
  1. mbiomba
  2. amu
  3. mjomba
  4. nyanya.
 6. Kamilisha methali hii.
  Mtoto akibebwa hutazama _________________________ cha nina.
  1. kichwa
  2. nywele
  3. uso
  4. kisogo
 7. Ala! Hujapata chakula?
  Neno 'Ala!' ni _____________________
  1. kihusishi
  2. kihisishi
  3. kielezi
  4. kivumishi
 8. Jozi ipi iliyo na visawe?
  1. Papa - baba
  2. Toa - doa
  3. Simu - rununu
  4. mama - baba
 9. Jibu la hujambo ni?
  1. Hatujambo
  2. Njema
  3. Sijambo
  4. Nzuri.
 10. Kamilisha tashbihi ifuatayo.
  Nyeupe kama ________________________
  1. theluji
  2. unga
  3. neti
  4. malaika.

INSHA

KUANDIKA

Andika insha kuhusu: 'NCHI YANGU'MARKING SCHEME

 1. B
 2. A
 3. C
 4. B
 5. D
 6. A
 7. C
 8. C
 9. B
 10. C
 11. C
 12. B
 13. D
 14. D
 15. A
 16. B
 17. D
 18. C
 19. A
 20. C
 21. B
 22. A
 23. B
 24. A
 25. C
 26. D
 27. B
 28. C
 29. C
 30. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Opener Exams Term 1 2023 Set 5.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students