Monday, 03 July 2023 12:07

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 2 Exam 2023 Set 3

Share via Whatsapp

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G5SwaMT2S32023Q1

Wanyama wa porini ni rasilimali tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Wanyama hao wana umuhimu mkubwa katika taifa lolote. Umewahi kuwaona nyumbu wakivuka kutoka Kenya na kuingia Tanzania au kutoka Tanzania kuingia Kenya? Hali hiyo hutoa utulivu mkubwa katika moyo. Kuwaona simba wakiwawinda na kuwala wanyama wengine husababisha furaha kubwa. Hili lina maana kuwa kule kuwatazama wanyama wa porini huleta utulivu. Faida nyingine ya wanyamapori ni kule kuwavutia watalii. Watalii wanaotoka nchini na katika mataifa ya nje humiminika nchini ili kujionea wanyama hao.

Manufaa makubwa ambayo sisi hupata kutokana na watalii ni pesa za kigeni. Watalii wanapotuletea pesa za kigeni, serikali yetu huweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Ni kutokana na pesa hizo ndipo tunapoweza kujenga barabara, shule, hospitali na kadhalika. Wakenya wengi wameajiriwa kufanya kazi zinazohusiana na wanyamapori. Hao ni kama vile madereva, walinzi, wanaowatembeza watalii na wanaofanya kazi katika hoteli za watalii hao.Wafanyakazi hao hufanya kazi kwa bidii ili kufaulu katika maisha yao.Wafanyakazi hao hupata pesa za kusaidia familia zao ili waishi maisha mazuri. Tatizo hutokea wakati tamaa inapofanya tuwinde na kuwaua wanyama hao. Majangili huwawinda wanyamapori wakiwa na lengo la kupata vipusa, pembe za ndovu na ngozi za wanyama hao. Uovu huo unafaa kukomeshwa haraka mno. Ni vyema kuelewa kuwa kuwaangamiza wanyamapori ni kuiletea nchi yetu hasara. Kila mkenya ajitolee kuwatunza wanyamapori.

 1. Pesa za kigeni ambazo huletwa na watalii hutumiwa na;
  1. watalii
  2. shule
  3. wakenya
  4. serikali
 2. Ni kweli kwamba tusipokuwa na wanyamapori;
  1. watalii wataongezeka nchini.
  2. majangili watatajirika.
  3. kiwango cha maendeleo kitarudi chini.
  4. watu wengi wataajiriwa.
 3. Ufuatao ni umuhimu wa wanyamapori isipokuwa;
  1. hutuliza moyo
  2. huwaletea majangili faida
  3. huvutia watalii
  4. huwapa watu ajira
 4. Kifungu kinaeleza kuwa wanaowinda wanyamapori huongozwa na nini?
  1. umaskini
  2. njaa
  3. tamaa
  4. kutojua
 5. Wafanyakazi hao hufanya kazi kwa bidii ili kufaulu katika maisha yao. Maneno haya yanaweza kuelezwa kwa methali gani?
  1. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.
  2. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
  3. Mtoto wa nyoka ni nyoka.
  4. Mtaka yote hukosa yote.
 6. Tambua maana ya 'majangili' kulingana na kifungu.
  1. Wezi wa wanyamapori
  2. Wawindaji haramu
  3. Askari wa wanyamapori
  4. Watalii katika mbuga
 7. Chagua kichwa kinachofaa kwa makala haya.
  1. umuhimu wa watalii
  2. faida na hasara za wanyamapori
  3. umuhimu wa wanyamapori
  4. kuwinda, wanyamapori

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali yanayofuata.

G5SwaMT2S32023Q2

Kutoka kwa: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
Kwenda kwa: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


MADA: MWALIKO WA KUPATA MAFUNZO

Kwa Bwana/Bi,

Jina langu ni Mapato Mapesa. Mimi ndimi katibu wa chama cha Akiba Haiozi. Chama cha Akiba Haiozi ni chama cha wafanyabiashara wa biashara ndogondogo katika mji wa Mumias. Sisi hujihusisha na biashara za rejareja, uchuuzi na shughuli za juakali. Tumekuwa tukiweka akiba kidogo katika benki yenu ya Wekeza. Kwa sasa, tuna akiba ya kima cha shilingi milioni moja. Tuna hamu ya kuwekeza katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujipa faida zaidi. Hata hivyo, hatuna ujuzi wa kutosha kuhusu uwekezaji. Kwa kuwa kuuliza si ujinga, tumeamua kutoa ombi ili mtutumie afisa au maafisa ambao watatueleza mengi kuhusu uwekezaji. Vilevile, tugependa kujua iwapo tunaweza tukapewa mkopo. Tatizo jingine ni kwamba hatujui aina za mikopo mnayotoa na riba inayohusiana na kila aina ya mkopo.

Tuna matumaini makubwa kuwa mtalikubali ombi letu na kukifaa chama hiki. Tunatoa ahadi ya kuendelea kushirikiana na benki yenu pamoja na maafisa wenu. Isitoshe, tutazidi kuweka akiba katika banki iyo hiyo nyakati zote. Iwapo ombi letu litakubalika, tafadhali tupeni ujumbe na wakati mnaopatikana ili tujiendae. Tunawapa shukrani za awali kutoka katika vilindi vya mioyo yetu. Kwaherini.

Wenu mwaminifu,
G5SwaMT2S32023Q3
Mapato Mapesa (katibu)

 1. Kifungu hiki ni mfano wa;
  1. barua ya kirafiki.
  2. barua rasmi.
  3. baruapepe.
  4. barua ya kiofisi.
 2. Ni kweli kuwa anayeandikiwa barua hii ni wa jinsia gani?
  1. ya kike
  2. ya kiume
  3. haijulinani
  4. katibu
 3. kulingana na kifungu, kwa nini mwandishi na wenzake wana hamu ya kuwekeza katika miradi mbalimbali?
  1. ili wajue mengi kuhusu uwekezaji
  2. ili wapate faida
  3. ili watembelewe na maafisa wa benki
  4. ili waweke akiba
 4. Wanachama wa chama cha Akiba Haiozi wanafahamu kuwa;
  1. Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki. 
  2. Majuto ni mjukuu huja baadaye.
  3. Ngoja ngoja huumiza matumbo. 
  4. Haba na haba hujaza kibaba.

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yanayofuata.

Familia kuteseka, sababu umasikini,
Chakula wanaposaka, ni ukweli hawaoni,
Mavazi yameraruka, kichwa hadi mguuni,
Bidii yahitajika, kuushinda uchochole.

Kuanza kule shuleni, kujikaza ni lazima,
Shambani pia kazini, tukilala tutazama,
Bidii iwe moyoni, kujitolea daima,
Bidii yahitajika, kuushinda uchochole.

 1. Chagua kina cha kati cha ubeti wa kwanza.
  1. na
  2. ma
  3. ni
  4. ka
 2. Mwandishi wa shairi hili angetumia neno gani jingine badala ya neno 'familia'?
  1. ayali
  2. jamii
  3. ndugu
  4. sahibu
 3. Umaskini husababisha nini kutokana na ubeti wa kwanza?
  1. ukosefu wa mavazi na chakula
  2. ukosefu wa elimu na amani
  3. ukosefu wa chakula na elimu
  4. ukosefu wa mavazi na amani
 4. Kibwagizo cha shairi hili kina mizani mingapi?
  1. 10
  2. 2
  3. 14
  4. 16

Chagua jibu lifaalo ili kujazia nafasi zilizoachwa.

Mtu __16__ anayetaka kufaulu __17__ lazima awe mwenye bidii. Bidii ni muhimu sana kwetu. Tunafaa kuwa wenye bidii masomoni, kazini __18__ michezoni. Mtu asiyependa bidii hawezi akafaulu katika __19__ lolote. Je __20__ wewe ni mwenye bidii au unapenda uzembe?

   A   B   C   D 
 16.   yoyote   yeyote   wowote   ambaye 
 17.  kwenye maisha   kwa maisha   katika maisha   katika maishani 
 18.  lakini  au  wala   na 
 19.  kitu  shughuli   mambo   jambo 
 20.  ,  ?  !  :

 

 1. Tambua aina za nomino zilizopigiwa mistari. Mtoto alijawa na furaha alipokunywa maziwa.
  1. pekee, wingi, dhahania
  2. kawaida, wingi, shahania
  3. pekee, dhahania, wingi
  4. kawaida, dhahania, wingi
 2. Chagua neno lenye silabi nne kati ya maneno yafuatayo.
  1. beba
  2. wekea
  3. tembelea
  4. hajaja
 3. Tambua sentensi iliyotumia koma.
  1. Amemaliza chakula.
  2. Wewe ni nani?
  3. Amenunua kitabu, kalamu na kichongeo.
  4. Ala! Wacha kuharibu mazingira.
 4. Ikiwa jana ilikuwa Jumatatu, keshokutwa itakuwa lini?
  1. Alhamisi
  2. Jumatano
  3. Jumanne
  4. Ijumaa
 5. Chagua wingi wa;
  Ubao wenyewe una ufa mkubwa.
  1. Mbao zenyewe zina maufa makubwa.
  2. Mabao yenyewe yana nyufa kubwa. 
  3. Mabao yenyewe yana maufa makubwa.
  4. Mbao zenyewe zina nyufa kubwa. 
 6. Tegua kitendawili.
  Dhahabu yangu ya thamani haisimami.
  1. shamba
  2. mkufu
  3. siafu
  4. maji
 7. Nomino gani isiyopatikana katika ngeli ya I-ZI?
  1. kabati
  2. kalamu
  3. karatasi
  4. kamba
 8. Tambua aina za maneno yaliyopigiwa mistari. Lo! Kumbe wote wamelala ndani ya chandarua.
  1. kiwakilishi, kihusishi
  2. kihisishi, kivumishi
  3. kihusishi, kihisishi
  4. kihisishi, kihusishi
 9. Bwana harusi alivaa ______________________________ shingoni.
  1. koja la maua
  2. shada la maua
  3. mkungu wa maua
  4. kishazi cha maua
 10. Chagua kitenzi kilichonyambuliwa katika kauli ya kutendeka.
  1. pika 
  2. weka
  3. fulika
  4. cheka

INSHA

Andika insha ya masimulizi kuhusu;

SAFARI YA KUFURAHISHA  

MARKING SCHEME

 1. D
 2. C
 3. B
 4. C
 5. B
 6. B
 7. C
 8. C
 9. C
 10. B
 11. D
 12. D
 13. A
 14. A
 15. D
 16. B
 17. C
 18. D
 19. D
 20. A
 21. D
 22. C
 23. C
 24. A
 25. D
 26. B
 27. A
 28. D
 29. A
 30. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 5 Mid Term 2 Exam 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students