Friday, 24 March 2023 13:33

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 1 MidTerm Exams Term 1 2023 Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (Alama 5)
Sikiliza kifungu hiki kwa makini kisha ujibu maswali nitakayokuuliza

Kila siku kuna usafiri. Na watu husafiri wakitumia vyombo vya usafiri tofauti tofauti. Kuna wale huendesha magari madogo. Wanafunzi huenda shuleni kwa mabasi. Wafanyakazi hutumia matatu. Wengine hutumia baiskeli na pikipiki. Gari la moshi hubeba mizigo mizito. Mtu pia anaweza kusafiri angani kwa kutumia ndege.

 1. Taja vyombo vitano vya usafiri vilivyotajwa kwenye hadithi.
  (Mwanafunzi ajibu)

KUSOMA KWA SAUTI (alama 10)
Soma hadithi hii kwa sauti.

Shule ni mahali wanafunzi huenda kupata maarifa. Shule yetu inaitwa Bidii. Kuna vifaa tofauti kama vile kalamu, madaftari, chati na bendera. Shule ya Bidii ina sehemu tofauti tofauti kama vile gwaride. uwanja, majlisi, maktaba na vyoo. Madarasa ya shule yetu ni makubwa na safi.

UFAHAMU, SARUFI na KUANDIKA

UFAHAMU (Alama 10)
Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata (alama 5)

Paulo na Pendo ni wanafunzi. Wanasomea katika shule ya Hekima. Paulo na Pendo wako katika gredi ya kwanza. Paulo ni mvulana. Pendo ni msichana. Wote wana umri wa miaka sita. Wao ni wanafunzi wazuri?

 1. Mwanafunzi yupi ni mvulana? (alama 1)
 2. Wanafunzi hao wanasomea katika shule gani? (alama 1)
 3. Taja gredi ambayo wanafunzi hao wanasomea (alama 1)
 4. Pendo na Paulo wana miaka mingapi? (alama 1)
 5. Mwanafunzi yupi ni msichana (alama 1)

Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo.

Mbwa na paka ni wanyama wa nyumbani. Paka anapenda kunywa maziwa na kushika panya. Mbwa anapenda kula mifupa. Paka ana miguu minne. Mbwa pia ana miguu minne. Mbwa hufukuza wezi nyumbani. Paka na mbwa wana faida kubwa nyumbani.

 1. ......................................na....................................ni wanyama wa nyumbani. (alama 2)
 2. Paka anapenda kunywa.................................(alama 1)
 3. Mbwa anapenda kula................................(alama 1)
 4. Paka ana miguu mingapi?................................(alama 1)

2. SARUFI (alama 15)

 1. Chora vifaa vifuatavyo vya darasani (alama 5)
  1. Kalamu
  2. Kitabu
  3. Saa
  4. Kifutio
  5. Meza
 2. Linganisha maamkuzi na majibu  (Alama 4)
  1. Habari
  2. Shikamoo
  3. Hamjambo?
  4. Hujambo?
   (Hatujambo, Sjambo , Njema, Marahaba)
 3. Unda maneno ukitumia silabi zifuataza (Alama 3)
  1. b
  2. ch
  3. k
 4. Andika maneno kwa herufi kubwa.. (Alama 3)
  1. kiatu
  2. paka
  3. yai

KUANDIKA (Alama 10)
Andika maneno kumi utakayosomewa na mwalimu waka

 

 1. ........................................
 2. ........................................
 3. ........................................
 4. ........................................
 5. ........................................
 6. ........................................
 7. ........................................
 8. ........................................
 9. ........................................
 10. ........................................
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 1 MidTerm Exams Term 1 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.