Friday, 14 April 2023 07:32

Shughuli za Kiswahili Kusikiliza, Kuzungumza na Kusoma kwa Sauti Questions and Answers - CBC Grade 2 End Term 1 Exams 2023 SET 2

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (Alama 5)

Sikiliza hadithi nitakayokusomea kwa makini kisha ujibu maswali nitakayokuuliza.

Ilikuwa siku ya Jumanne. Tulifika shuleni mapema. Tulipanga madawati vizuri. Tuliokota taka uwanjani. Tulinyunyizia maua maji. Kengele ilipigwa.

  1. Ilikuwa siku gani?
    (Mwanafunzi ajibu)
  2. Tulifika shuleni wakati gani?
    (Mwanafunzi ajibu)
  3. Tulipanga nini vizuri?
    (Mwanafunzi ajibu)
  4. Tuliokota nini uwanjani?
    (Mwanafunzi ajibu)
  5. Ni nini ilipigwa?
    (Mwanafunzi ajibu)

KUSOMA KWA SAUTI

Soma kifungu hiki kwa sauti.
Grade2kswtgtrqn3

Abdi ni mvulana mtiifu. Alipenda sana wanyama. Baba yake alijua kile ambacho Abdi alipenda. Alimwambia kuwa wataenda kuwaona wanyama. Abdi alijiandaa kwa furaha. Baadaye walianza safari kuelekea mbuga ya wanyama. Waliona sungura, kinyonga, chura na kaa. Waliangalia upande mwingine na kuona simba, tembo, punda milia, twiga na tumbiri. Waliona wanyama wengi sana. Abdi alimshukuru sana baba yake kwa kumpeleka kuwaona wanyama mbugani. Abdi alisema kuwa hatawahi kuisahau siku hiyo.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Kusikiliza, Kuzungumza na Kusoma kwa Sauti Questions and Answers - CBC Grade 2 End Term 1 Exams 2023 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.