Friday, 22 April 2022 11:11

Shughuli za Lugha Homework Activities - CBC Grade 3

Share via Whatsapp

MASWALI

Kusikiliza na kuzungumza
A. Imla
Mwanafunzi asomewe maneno kisha ayaandike kwenye mapengo.
Maneno ya Imla

  1. Bwana 
  2. fyonza
  3. mwanafunzi
  4. kwama
  5. fyatuka
  6. Nyundo
  7. mwewe
  8. kimbilia
  9. ndimu
  10. ukabila
  11. chinja
  12. pwaguzi
  13. vyombo
  14. kuteketea
  15. vifaa

B Soma maneno haya kwa sauti alikwea
bweni                   alikwea                fyeka                    afya
mbegu                 aliomba                vunjika                 njama
mzalendo            kwekwe                pwaya                  daktari
shuka                  mchoro                 hamali

C. Soma sentensi hizi kwa sauti

  1. Kwa nini njiwa wamelala? 
  2. Wewe hukuimba wimbo wa taifa. 
  3. Nyinyi mlisafisha mazingira. 
  4. Walimu walitufunza tabia nzuri. 
  5. Usikae na mtu usiyemjua.
  6. Salama alizaliwa mwezi wa Machi.

D. UFAHAMU
Mzazi au mlezi amsomee mwanafunzi taarifa hii kwa sauti mara mbili kisha amwulize maswali.
Shule zilipofungwa kwa likizo ya Aprill sikukaa tena mjini. Nilifunga safari yangu hadi mashambani kwa shangazi yangu. Shangazi yangu ni mkulima maarufu katika kijiji cha kwao. Nilifika kwa shangazi alasiri. Shangazi na watoto wake walikuwa shambani wakilima. Nilienda hadi shambani na nikaanza kulima. Hata sikubadilisha nguo.
Jioni tulienda nyumbani. Shangazi alipika kilalio. Baada ya kula, sisi sote tulienda kulala. Mimi nililala katika kitanda kimoja na mkoi wangu. Niliomba Mungu sana usiku huo nisikojoe kitandani; sikutaka kuchekwa na wakoi wangu.

Maswali

  1. Shule zilipofungwa mwandishi aliondoka wapi? ...............................................
  2. Shangazi na watoto wake walikuwa wapi? ...............................................
  3. Ni nani aliyepika kilalio?...............................................
  4. Mbona mwandishi aliomba Mungu sana?...............................................
  5. Chakula cha asubuhi huitwa ...............................................

E.
Je, ni vifaa vipi hutumika shambani
1 auygdad

F.

  1. Mwaka una miezi mingapi? ..............................................
  2. Je, ulizaliwa mwezi gani? ..............................................
  3. Kwa kawaida shule hufungwa miezi gani?
    1. ..............................................
    2. ..............................................
    3. ..............................................
  4. Sherehe ya Jamhuri husherehekewa mwezi gani? ..............................................
  5. Mwezi wa tano ni ..............................................

G.
Tazama picha hizi. Ni kazi zipi unazozijua
2 aighduyada

Wewe ungetaka kufanya kazi gani baada ya masomo?
Kwa nini mtu hafai kufanya mambo haya?

  1. Kwenda msituni peke yako! ..............................................
  2. Kuzungumza na watu usiowajua  ..............................................
  3. Kucheza karibu na shimo?  ..............................................
  4. Kunywa chochote kilicho kwenye chupa ..............................................

H.
Mazingira ni vitu vinavyotuzunguka kama vile:
3 augduyad

  1. Mazingira machafu huleta wadudu na wanyama kama vile
    1. 4 sajygduyada
      ..............................................
    2. 5 sgyhyushuysdf
      ..............................................
  2. Ni muhimu kufungua madirisha wakati wa mchana ili ..............................................
  3. Vitendo viwili vya kusafisha mazingira
    1. ..............................................
    2. ..............................................

I.
Taja majina ya bidhaa hizi;
6 auygduygad

  1. Mtu anayeuza dukani huitwa ..............................................
  2. Pesa za karatasi zinaitwa..............................................
  3. Mtu akikopesha bidhaa bila kulipa huwa amefanya nini? ..............................................
  4. Uzito wa sukari hupimwa kwa kutumia ..............................................

J.

  1. Chora ndege umpendaye?

                                                                                        

     

     

     

     

     

     

     

     

  2. Kwa nini unampenda ndege huyo!
    1. ..............................................
    2. ..............................................
    3. ..............................................
  3. Unamtunzaje ndege unayempenda?
    1. ..............................................
    2. ..............................................
    3. ..............................................
  4. Hawa ni ndege gani?
    8 uyauydada
  5. Nyumba ya ndege wa porini ni

A. KUANDIKA
Jaza mapengo kwa maneno yanayofaa zaidi
Juu ya mti _ 1__ (hiyo, hizo, huo) palikuwa na _2__ (kizimba, kiota, kikombe) cha ndege. Ndani palikuwa na mayai _ 3__ (mbili, mawili,pili) ya ndege. Mayai hayo__4_ (ilikuwa, yalikuwa, zilikuwa) ya ndege. Mimi __5__ (hakuyachukua, sikuyachukua,hachukui) mayai yale. Niliyaacha hapo nikaondoka. Nilirudi hapo __6__ (kabla ya, baada ya, badala ya) wiki_._7__ (tatu, mitatu, watatu). Niliwapata _8_ (vifaranga, viyoyo, makinda) kiotani. Nilikimbia hadi nutimbani. Nilimkuta baba ___9____ (zake, yangu, 'langu). Aliniambia hao ni watoto wa ndege. Alisema niachane na ndege __10__ (wandogo, wadogo, ndogo).

B. Andika maneno yanayoanza kwa herufi hizi kwa hati hadhifu

  1. dh ..............................................    ..............................................
  2. th ..............................................    ..............................................
  3. ny ..............................................    ..............................................
  4. ng ..............................................    ..............................................
  5. sh ..............................................    ..............................................

C.Kuandika kuhusu soko
Soko letu linaitwa Marikiti. Watu wengi hupenda kununua __1__ (bidhaa, bidha) huko. Kuna vitu ainati ambavyo __2__ (hupandwa, huuzwa) kwa ___3___ (noti, bei) nafuu sana.__4__ (Wauzaji, Wanunuzi) hutumia __5__ (pesa, vyakula) kununua wanachohitaji. Kuna wale ambao huwaomba wauzaji __6__ (wawaongezee, wawapunguzie) bei. Muuzaji akiuza yeye hupata__7____ (hasara, faida). Ukinunua kitu mara nyingi huwa unapewa -__8_(risiti, karatasi). Mchele au unge hupimwa kwa __9__ (kipino, ratili), lakini maziwa hupimwa kwa ___10___ (pakiti, mafungu)

D. Kuandika kuhusu usalama
Tulikuwa tumesimama ___1__ (katikati ya , ndani ya) kaka na dada. Mzee ___2____ (moja, mmoja) alikuja akatusalimia. Alituomba tumwonyeshe njia um kwenda sokoni. ___3___ (kabla ya, baada ya) kumwonyesha, alitushukuru na ___4___  (aliondoka, ataondoka). "Kwa nini mzee huyo ana macho (mekundu, nyekundu)? kaka akauliza “Labda ni mgonjwa,” nilijibu. Matatu iliwasili. Tuliingia na kuelekea sokoni. Tulifika sokoni haraka. __6__ (Tutanunua, Tulinunua) vitu tulivyotaka. Nilimwona mzee ___7___ (yule, ule) mwenye macho mekundu. Alikuwa ameshikwa na askari. Alishikwa ____8___ (lakini, kwa sababu) aliwauzia watoto bangi. Alikuwa mzee mbaya. Alitaka kuharibu maisha ya ___ 9___  (wazee, watoto). Tulichukua mizigo, tukaenda kwetu nyumbani.

SARUFI
A. Tumia maneno yaliyo kwenye kisanduku kujaza mapengo

Ndani ya Chini ya, Nje ya, kando ya, Juu ya 
  1. Panya yuko ..............................................shimo.8 aygduyada
  2. Mtoto mepanda..............................................ya mti. sarufi 2
  3. Kitabu kimeanguka..............................................ya meza sarufi 3 ahdauihda
  4. Watoto wanacheza..............................................ya nyumba. sarufu 4 auygdauygdyua
  5. Gari limeegeshwa..............................................ya barabara sarufi 5 IUdiuada

B. Tumia alama ya kuuliza swali (?)

  1. Wewe unaenda wapi .............................................
  2. Kwa nini unacheka.............................................
  3. Unapenda somo gani.............................................
  4. Jani lilianguka lini.............................................
  5. Kinyonga anatembea polepole kwa nini.............................................

C.Tumia "polepole" au "haraka"

  1. Mnyama huyu huwa anaenda .............................................leopard auhydguygad
  2. Ni vizuri kufagia sakafu ............................................. ili iwe safi
  3. Kimani alishinda mbio kwa sababu alikimbia.............................................
  4. Mnyama huyu huwa anaenda .............................................chameleon aygduyagda
  5. Kukiwa na baridi nguo hukauka .............................................
  6. Dereva aliendesha gari .............................................likaanguka

D. Andika Kinyume

  1. Lala .............................................
  2. Keti .............................................
  3. Cheka .............................................
  4.  Tabasamu .............................................
  5. Nenda .............................................
  6. Penda .............................................

E. Andika wingi wa sentensi hizi

  1. Mimi niliandika vizuri. .............................................
  2. Wewe nenda sokoni.  .............................................
  3. Yeye atasoma kitabu. .............................................
  4. Choo kitasafishwa. .............................................
  5. Mdudu anauma. .............................................

F. Kanusha sentensi hizi 

  1. Mimi ninasoma vibaya .............................................
  2. Nyinyi mlifanya makosa  .............................................
  3. Yeye atachora nyumba  .............................................
  4. Sisi tulipita mtihani  .............................................
  5. Msichana anaenda ziara .............................................

G. Sahihisha sentensi hizi

  1. sarah anapenda samaki .............................................
  2. dada alizaliwa juni .............................................
  3. sherehe ya leba ni mei .............................................
  4. tutaenda Nakuru agosti .............................................
  5. huu ni mwaka wa tatu .............................................

H. Andika umoja wa sentensi hizi

  1. Vitabu vyao vimepotea .............................................
  2. Watoto wao wanalia .............................................
  3. Hii ni mikoba yao .............................................
  4. Kalamu hizi ni zao .............................................
  5. Madawati yao yamenunuliwa .............................................

I. Tumia "-ake" au "-ao"

  1.  Yai .............................................limevunjika.
  2. Maembe.............................................yameiva yote.
  3. Duka.............................................limefungwa.
  4. Sahani ............................................ zimepangwa kabatini. 
  5. Vyoo ............................................vimeoshwa.

MSAMIATI
Mimea hii, hutupatia mazao gani?
end 1 agduyagda

  1. Mtu anayeipenda nchi yake ni .............................................(Mwananchi, mzalendo)
  2. Mtu anayeijali nchi yake hupenda.............................................(vita, amani)
  3. Sheria za nchi ya Kenya zimeandikwa kwenye .............................................(Kitabu, katiba)
  4. Bendera yetu ina rangi ............................................. (tatu, nne)
  5. Wakazi wa nchi ni .............................................(ruiya, raia)
    Andika majina ya miezi ambayo ina siku thelathini na moja
  6. .............................................
  7. .............................................
  8. .............................................
  9. .............................................
  10. .............................................
    Andika majina ya miezi ambayo ina siku thelathini (30)
  11.  .............................................
  12. .............................................
  13. .............................................
  14. .............................................
  15. Ni mwezi upi umbo huwa na siku ishirini na nane (28) au ishirini na tisa (29)?.............................................

Tambua kazi ya watu hawa
end 2 hgdughdad

Andika vitendo vitatu ambavyo vinaweza kusababisha fujo au ghasia K.m kuchoma mali ya watu

  1. ..........................................................................................
  2. ..........................................................................................
  3. ..........................................................................................

Kwa nini ni muhimu kufanya mambo haya?

  1. Kufyeka nyasi zilizoko karibu na nyumba zetu? ..........................................................................................
  2. Kuchoma takataka ..........................................................................................
  3. Kusafisha vyoo shuleni ..........................................................................................
  4. Chora vifaa viwili ambavyo hutumiwa kusafisha mazingira..........................................................................................

                                                                        

     

     

     

     

     

                                                                       
  5. Mtu anayenunua bidhaa dukani huitwa ..........................................................................................
  6. Pesa anazorudisha mnunuzi baada ya kununua zinaitwa .............................................
  7. Kuuza bidhaa kidogo kidogo ni kuuza kwa .............................................
  8. Kuuza bidhaa kwa wingi ni kuuza kwa .............................................
  9. Pesa ambazo si za karatasi huitwa.............................................(Baki, Sarafu, Rejareja, Muujazi, Jumla) 
  10. ............................................. ni ndege wa nyumbani (bata, kanga)
  11. ............................................. ni ndege mwenye macho makubwa (bundi, punda)
  12. Mtoto wa kuku ni .............................................(kiyoyo, kifaranga)
  13. Mdomo wa ndege huitwa.............................................(meno, kidona)
  14. Njiwa ni ndege.............................................(mkali, mpole) 
  15. Bidha kama mboga na matunda hupimwa kwa.............................................(mafungu, pakiti)

MWONGOZO

D. UFAHAMU 

  1. Mjini 
  2. Mashambani
  3. Shangazi
  4. Ili asikojoe kitandani
  5. Staftanı/Kiasha kinywa

E. Shambani

  1. Jembe
  2. Shoka
  3. Plau
  4. Reka
  5. Upanga

F.

  1. Kumi na miwili
  2. Chagua katika ya Januari hadi Disemba
  3.                      
    1. Aprili
    2. Agosti
    3. Disemba
  4. Disemba
  5. Mei

G

  1. Ualimu, 
  2. Useremala,
  3. Upishi,
  4. Uashi,
  5. Sarakasi
  6. ajibu kutegemea mwanafunzi
  7. Kuna wanyama
  8. Wanaweza kuwa watu watuya
  9. Unaweza kuanguka ndani
  10. Vitu vingine ni sumu

H. Mazingira

  1. Misitu
  2. Majengo
  3. Mto
  4.                    
    1. Nzi
    2. Pariya
  5. Kuleta hewa safi
  6.                  
    1. Kupangusa
    2. Kufagia
    3. Kuzoa taka

I. Kununua dukani

  1. Unga
  2. Vipuli
  3. Suruali
  4. Peremende
  5. Mafuta ya kujipaka
  6. Rinda
  7. Muuzaji
  8. Noti
  9. Amechukua deni 
  10. Ratili

J

  1. Mchoro
  2.                      
    1. Wana faida
    2. Anapendeza
    3. hufigwa bwa urahisi
  3.                        
    1. Kuwapa matiba
    2. Kuwajengoa Kiben
    3. Kuwapa maji na chakula
    4. Kuwapiga dawa ya kuzuia viroboto
  4. Mwewc, njiwa, tausi
  5. Kiota

KUANDIKA 
A

  1. Huo
  2. Kiota
  3. Mawili
  4. Ya kuwa
  5. Sikuyachukua
  6. Baada ya
  7. Tatu
  8. Makinda
  9. Yangu 
  10. Wadogo

B

  1. Dhambi, Dhihaki
  2. Thamani, thurea
  3. Nyanya, niyayo
  4. Ngano, ngiri
  5. Shati, shamba

C

  1. Bidhaa
  2. Huuzwa
  3. Bei
  4. Vanunuzi
  5. Pesa
  6. Wawapunguzie 
  7. Faida
  8. Risiti\ratili
  9. Pakiti

D

  1. Katikati ya
  2. Mmoja
  3. Baada ya
  4. Aliondoka
  5. Mekundu
  6. Tulinunua
  7. Yule
  8. Kwa sababu bagu Watoto unda

SARUFI
A

  1. Ndani ya
  2. Juu ya
  3. Chini
  4. Nje
  5. Kando

C

  1. Haraka
  2. Polepole
  3. Haraka
  4. Polepole
  5. Polepole
  6. Haraka 

D

  1. Amka
  2. Simama
  3. Lia
  4. Nuna
  5. Rudi
  6. Chukia

E

  1. Sisi tuliandika vizuri
  2. Nyinyi nendeni sokoni
  3. Wao watasoma vitabu
  4. Vyoo vitasafishwa
  5. Wadudu wanauma

F

  1. Mimi sisomi vibaya
  2. Nyinyi hamkufanya makosa
  3. Hatachora nyumba 
  4. Sisi hatukupita mtihani
  5. Msichana haendi ziara

G

  1. Sarah anapenda samaki.
  2. Dada alizaliwa Juni. 
  3. Sherehe ya Leba ni Mei.
  4. Tutaenda Nakuru Agosti:
  5. Huu ni mwaka wa tatu,

H

  1. Kitabu chake kimepotea
  2. Mtotu wake analia
  3. Huu ni mkoba wake
  4. Kalamu hii ni yake 
  5. Dawati lake limenunuliwa

I

  1. lao/lake
  2. yake/yao 
  3. lao/lake 
  4. zao zake 
  5. vyao vyake

MSAMIATI

  1. Mahindi
  2. Ndizi
  3. Mananasi
  4. Maembe
  5. Mzalendo
  6. Amani
  7. Katiba
  8. Nne
  9. Raia 
  10. Disemba 
  11. Januari 
  12. Machi
  13. Mei 
  14. Agosti 
  15. Septemba
  16. April
  17. Juni
  18. Novemba 
  19. Februari 
  20. Daktari 
  21. Mkulima 
  22. Mvuvi 
  23. Mwanajeshi 
  24. Kuiba mali ya watu/Kuharibu mali/Kuvunja vitu
  25. Kuteka nyara watoto 
  26. Kupiga watu 
  27. Kuzuia wadudu na wanyama 
  28. Kuzuia haulu mbaya na wadudu 
  29. Kuzuia harufu mbaya, na magonjwa
  30.                            
    1. Reki
    2. Ufagio
    3. Fyekeo
    4. Talata
  31. Mteja 
  32. Mnunuzi, baki, sazo 
  33. Rejareja 
  34. Jumla 
  35. Sarafu 
  36. Bata 
  37. Bundi
  38. Kufaranga
  39. Kidona 
  40. Mpole
  41. Mafungu
Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Lugha Homework Activities - CBC Grade 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.