Wednesday, 04 May 2022 12:34

Kiswahili Activities Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 1 Exams 2022 SET 2

Share via Whatsapp

MASWALI
SEHEMU 1: KUSIKILIZA NA KUONGEA

Mwalimu amuulize mwanafunzi4maswalLyafuatayo.

 1. Habari yako?
  (Mwanafunzi ajibu)
 2. Taja tunda unalolipenda.
  (Mwanafunzi ajibu)
 3. Tunda hilo linapatikana wapi?
  (Mwanafunzi ajibu)
 4. Kabla ya kula tunda unafaa ufanye nini?
  (Mwanafunzi ajibu)
 5. Tunda hilo huwa tamu likiwa bivu au bichi?
  (Mwanafunzi ajibu)

SEHEMU 2: KUSIMA KWA SAUTI
Soma kifungu hiki kwa sauti

Niliamka asubuhi na mapema. Kulikuwa na utulivu kwa sababu watu wengi hawakuwa wameamka. Hata wazazi wangu bado walikuwa wakilala. Nilienda bafuni nikaoga. Kisha nikaenda jikoni kutayarisha staftahi. Sikutaka nichelewe kufika shuleni. Baada ya kupata staftahi, nilipiga meno mswaki kisha nikavaa sare za shule. Nilitoka mbio hadi shuleni. Siku hiyo ilikuwa siku ya kuzuru mbuga ya wanyama.

SEHEMU 3: UFAHAMU
Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali.

Hapo zamani za kale, kuku na mwewe. Walikuwa marafiki wa chanda na pete. Walikuwa wakiishi pamoja. Kila asubuhi walienda kulima katika shamba lao. Kuku alikuwa na vifaranga watano naye mwewe alikuwa na makinda wawili.
Siku moja kuku alimkanyaga kinda mmoja hadi akaaga dunia. Ingawa ilikuwa ajali, mwewe aliapa kulipiza kisasi. Kuku aliamua kutoroka hadi kwa binadamu. Tangu siku hiyo, mwewe huwashika vifaranga wa kuku kulipizd kisasi.

 1. Kila asubuhi kuku na mwewe walienda wapi?
 2. Kuku alikuwa na vifaranga wangapi?
 3. Mwewe alikuwa na makinda wangapi?
 4. Nani alimkanyaga kinds?
 5. Kuku alitoroka hadi wapi?

SEHEMU 4: SARUFI
Kanusha sentensi.

 1. Enda nyumbani.
 2. Mtoto anakula ndizi.
 3. Baba analima shambani
 4. Kaka amepika chakula
 5. Soma kitabu hiki.

Andika kinyume.

 1. Shuka
 2. Rudi
 3. Keti
 4. Funika
 5. Jenga

Andika tarakimu kwa maneno.

 1. 86
 2. 92
 3. 126
 4. 74
 5. 225

Andika majina ya maumbo haya.
3

Andika maneno kwa wingi

 1. Uzi
 2. Ukuta
 3. Meza
 4. Tunda
 5. Mwanafunzi

SEHEMU 5: KUANDIKA
INSHA

Andika insha juu ya:

DARASA LETUMWONGOZO WA KUSAHIHISHA

Ufahamu

 1. Kwa shamba
 2. Watano
 3. Wawili
 4. Kuku
 5. Kwa binadamu

Sarufi

 1. Usiende nyumbani
 2. Mtoto hali ndizi
 3. Baba halimi shambani
 4. Kaka hajapika chakula
 5. Usisome kitabu hiki
 6. Panda
 7. Enda
 8. Simama
 9. Funua
 10. Bomoa
 11. Themanini na sita
 12. Tisini na mbili
 13. Mia moja, ishirini na sita
 14. Sabini na nne
 15. Mia mbili, ishirini na tano
 16. Pembe tatu
 17. Mstatili
 18. Duara
 19. Duara dufu
 20. Mraba
 21. Nyuzi
 22. Kuta
 23. Meza
 24. Matunda
 25. Wanafunzi
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Activities Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 1 Exams 2022 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.