Thursday, 09 March 2023 12:12

Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 3 Opener Exams Term 1 2023 Set 3

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA (Alama 5)

Nitakusomea hadithi kisha nitakuuliza maswali. Sikiliza kwa makini.

rabbit

Sungura mjanja alimtembelea kaka yake ambaye aliishi mjini. Alipofika kwake, aliviona vyumba vingi. Alijisemea, "Kila siku nitakuwa nikilala katika chumba tofauti nihisi jinsi kilivyo." Sungura alipikiwa wali. Aliishi na kaka yake kwa muda wa mwezi mmoja.

 1. Sungura alimtembelea nani?
  (Mwanafunzi ajibu)
 2. Kaka yake sungura aliishi wapi?
  (Mwanafunzi ajibu)
 3. Nani aliviona vyumba vingi?
  (Mwanafunzi ajibu)
 4. Sungura alipikiwa nini?
  (Mwanafunzi ajibu)
 5. Aliishi na kaka yake kwa muda wa miezi mingapi?
  (Mwanafunzi ajibu)

KUSOMA KWA SAUTI (Alama 10)
Soma hadithi hii kwa sauti
Familia ya Bahati ishi jijini Nakuru. Bahati alikuwa mtoto mzuri sana ambaye alipenda kuwasaidia wazazi wake kufanya kazi. Siku moja badala ya kumaliza kazi ya nyumbani, aliondoka kwenda kucheza. Baada tu ya kufunga mlango, kulitokea mtu mmoja aliyemshika kwa nguvu. Mtu yule alimlazimisha amfungulie mlango. Bahati alikataa na kupiga mayowe. Kwa bahati nzuri babake alikuwa ametoka kazini. Kwa umbali alisikia mayowe na kukimbia. Alimkamata mtu yule na kumpeleka kwenye kituo cha polisi.

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Questions and Answers - Grade 3 Opener Exams Term 1 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.