Thursday, 03 August 2023 08:29

Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 2 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA        (Alama 5)

 1. Mwalimu atamwamkua mwanafunzi kisha amwambie., "Leo tutajifunza kuhusu usafi wa mazingira. Nitakuuliza maswali nawe utajibu kwa Kiswahili
  1. Ukitaka kufagia utatumia nini? (Alama 1)
   (Mwanafunzi ajibu)
  2. Baada ya kukusanya taka utazipeleka wapi? (Alama 1)
   (Mwanafunzi ajibu)
  3. Taja vitu viwili ambavyo utatumia kuosha nyumba?  (Alama 2)
   (Mwanafunzi ajibu)
  4. Watu hutumia nini kufyeka nyasi ndefu?   (Alama 1)
   (Mwanafunzi ajibu)
 2. KUSOMA KWA SAUTI    (Alama 10)
  Soma hadithi hii kwa sauti
  Simu ya baba ilikiriza mfululizo. Baba aliijibu na kuzungumza. Mwishowe, aliiweka chini na kutabasamu. Shangazi ndiye aliyekuwa akimpigia baba simu. Baba alituambia kuwa shangazi alitaka twende kwake kesho. Alitaka tuone boma lake.
  "Tutaenda na wewe?" Hawa alimuuliza. Hawa alikuwa kifunguamimba. Alikuwa na miaka tisa. Dada yake aliitwa Hawi.
  Alikuwa na miaka saba. "Tutaenda sote kesho asubuhi," Baba alimjibu. Familia hiyo iliamka mapema. Watoto walijitayarisha wenyewe. Mama alipika kiamshakinywa. Baba aliwalisha ng'ombe. Walipomaliza kunywa chai kwa mahamri, baba alifunga nyumba.

MPANGO WA KUASHIRIA

 1.  
  1. kifagio
  2. shimo la taka
  3. sabuni na maji
  4. fyekeo
 2. kusoma kwa sauti

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Kusikiliza na Kuzungumza, Kusoma kwa Sauti Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 2 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.