Thursday, 03 August 2023 08:31

Shughuli za Kiswahili Ufahamu, Sarufi na Kuandika Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 2 Exams 2023 Set 1

Share via Whatsapp
  1. UFAHAMU    (Alama 10)
    1.  Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo.  (Alama 5)
                                                GRADE3kiswahiliET22023Q1
      Talia anapenda kucheza kandanda. Yeye ni kipa wa timu yetu ya shule. Yeye pia hushiriki katika mbio za mita mia moja. Siku ya michezo, Talia alianguka alipokuwa akicheza kandanda. Mguu wake ulifura. Alifanyiwa huduma ya kwanza halafu akapelekwa hospitalini. Daktari alimtibu. Talia alipata nafuu. Alirudi shuleni. Ndoto ya Talia ni kuwa mchezaji wa kandanda akiwa mkubwa.
      1. Talia anapenda kucheza mchezo upi?
        (alama 1)
      2. Talia hushiriki katika mbio zipi?
        (alama 1)
      3. Ni nini kilimtendekea Talia alipokuwa akicheza kandanda?
        (alama 1)
      4. Mguu wa Talia ulipofura alifanyiwa nini?
        (alama 1)
      5. Talia angependa kuwa nini akiwa mkubwa?  
        (alama 1)
    2. Soma hadithi kisha ujibu maswali yafuatayo.     (Alama 5)
      "Nilikuwa na hamu kubwa ya kuona Papa akifunga ndoa. Pweza na Kasa waliamka mapema siku ya Ijumaa. Moja kwa moja wakaelekea sokoni kununua nguo na vyakula mbalimbali. Mimi na Chura tulipata bahati ya kuandamana nao. Mle sokoni kulikuwa na vibanda vingi pamoja na wachuuzi wengi. Kila Pweza na Kasa waliponunua nguo au chakula walipewa risiti. Bidhaa zilipimwa kwenye ratili au mizani. Nilifurahi sana nikiwa pale sokoni.
      1. Nani alikuwa akifunga ndoa? ____   (alama 1)
      2. Ni nani walienda sokoni? ____ na ____  (alama 2)
      3. Walienda sokoni siku ya? ____ (alama 1)
      4. Pweza na Kasa walipewa _____ baada ya kununua bidhaa.  (alama 1)
  2. SARUFI         (alama 15)
    1. Andika majina ya vifaa vinavyotumika kusafisha mazingira   (AlamaGRADE3kiswahiliET22023Q2
    2. Tunga sentensi sahihi ukitumia maneno yafuatayo (alama 2)
      1. Haraka _____
      2. Polepole _____
    3. Andika kinyume cha kitendo    (alama 2)
      1. Analia _____
      2. Anavaa _____
    4. Ambatanisha miezi ya mwaka na shughuli sahihi. (alama 3)
      1. Mei                      Sikukuu ya Madaraka.
      2. Juni                     Sherehe za Krismasi.
      3. Disemba             Sikukuu ya wafanyakazi.
    5. Chagua jibu sahihi   (alama 3)
      1. Viti hivi ni _____ (vyao, chake)
      2. ______ hupika vyakula vitamu. (Bawabu, Mpishi)
      3. Mwigizaji anafanya kazi ya? _____ (ukimbiaji, uigizaji)
    6. Kanusha sentensi zifuatazo (alama 2)
      1. Yeye atachora _____
      2. Dereva atasimamisha lori _____
  3. KUANDIKA
    Andika sentensi tano kuhusu:
    DARASA LETU 

MPANGO WA KUASHIRIA

  1.  
    1.  
      1. kandanda
      2. mbio za mita mia moja
      3. alianguka
      4. alifanyiwa huduma ya kwanza halafu akapelekwa hospitalini
      5. kuwa mchezaji wa kandanda
    2.  
      1. Papa
      2. Pweza na Kasa
      3. Ijumaa
      4. risiti
  2.  
    1.  
      1. ufagio
      2. ndoo
      3. reki
    2.  
      1. Leo nilitembea haraka
      2. Mama alikimbia pole pole.
    3.  
      1. anacheka
      2. anavua
    4.  
      1. Mei   — Sikukuu ya wafanyakazi
      2. Juni  — Sikukuu ya Madaraka
      3. Disemba — Sikukuu ya wafanyakazi
    5.  
      1. vyao
      2. Mpishi
      3. uigizaji
    6.  
      1. Yeye hatachora
      2. Dereva hatasimamisha gari
  3.  
    • darasa letu ni kubwa
    • darasa letu lina mlango moja
    • darasa letu lin madirisha mengi
    • darasa letu limejengwa kwa mawe
    • darasa letu limejaa wanafunzi

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Shughuli za Kiswahili Ufahamu, Sarufi na Kuandika Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 2 Exams 2023 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.