Thursday, 02 September 2021 08:47

Kiswahili: Lugha - Grade 4 End Term 1 Exam 2021 SET 2

Share via Whatsapp

Maagizo

  • Tathmini hii ina sehemu tatu; kusikiliza na kuzungumza, kusoma na sarufi
  • Jibu maswali yote kulingana na maagizo
  • Tumia lugha ya kiswahili kujibu maswali yote.

SEHEMU YA KWANZA
KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA       (Alama 15)

  1.  
    1. Toa majibu ya salamu hizi.  (alama 2)
      1. Alamsiki __________________________
      2. Sabalkheri ________________________
    2.  
      1. Tamka maneno yafuatayo. Lipigie neno mstari ukisikia sauti /kw/   (alama 2)
        kiwi                 kwetu                 karibu                  kwingi
      2. Chagua maneno ambayo ni vitanza ndimi  (alama 3)
        1. dada na kaka
        2. mama na baba
        3. baba na papa
        4. kuku na gugu
        5. chai na mandazi
        6. pata na bata
        7. kiatu na soksi
          Andika hivyo vitanzandimi hapa chini
          1. ________________________________
          2. _________________________________
          3. _________________________________
    3. Tegua vitendawili      (alama 3)
      1. Huku ng'o na kule ng'o _______________________________
      2. Jicho la Mungu linachoma ____________________________
      3. Sijui aendako wala atokako ____________________________
  2. Soma sentensi hizi. Tumia maneno ya heshima badala ya yale yaliyopigiwa mstari.   (alama 5)
    1. Kukojoa kando ya barabara ni hatia.
    2. Nikifika nyumbani nitaenda kunya chooni.
    3. Mama mwenye mimba amezaa.
    4. Alipoketi kwenye vumbi alichafua matako.
    5. Ndugu yake alikuwa anahara sana.

SEHEMU YA PILI
KUSOMA         (alama 10)

Soma habari hii kisha ujibu maswali yafuatayo.

Hapo zamani za kale wanyama wote ambao hula nyasi na majani waliiishi pamoja. Waalishi katika msitu na walikuwa na afya njema.

Wanyama hawa walianza kuzaana na kuwa wengi. Miti nayo ikaanza kuwa michache na mvua kupungua . Wanyama walikosa chakula na hawakujua wafanye nini.

Ndovu alisema wapande miti kwa sababu miti italeta mvua, mvua nayo italeta majani mengi na nyasi. Wanyama walikubaliana kupanda miti kumi mwezi wa Januari. Walichota maji na kunyunyizia miti kwa sababu ya kiangazi. Walipanda miti mitano Februari.

Mvua ilinyesha Machi na wanyama wakapanda miti ishirini. Mwezi wa Aprili, wakapanda miti ishirini na mmoja. Mei na Juni miti kumi na sita. Julai miti mitano, Agosti na Septemba hawakupanda miti yoyote. Oktoba na Novemba wakapanda ishirini na Desemba miti miwili. Mwaka huo wakapanda miti tisini na tisa. Waliendelea hivyo kila mwaka miti ikaongezeka, nyasi na majani vivyo hivyo. Mvua pia ikaendela kunyesha.

Maswali

  1. Wanyama walikuwa wanakula __________________ na __________________
  2. Je, wanyama waliishi wapi? ________________________
  3. Ndovu pia huitwa _________________________
  4. Taja idadi ya miti iliyopandwa mwezi wa nne wa mwaka ________________________
  5. Mwaka huo walipanda miti tisini na tisa. Andika kwa idadi ___________________.
  6. Taja faida moja ya kupanda miti kulingana na kifungu ulichosoma 
    _______________________________________________
  7. Ni miezi gani ambayo wanyama hakupanda miti?
    1. _______________________
    2. _______________________
  8. Ukosefu wa mvua huleta ___________________________
    (masika, kipupwe, ukame, miti)

SEHEMU YA TATU
SARUFI

  1.  
    1. Pigia mstari nomino katika sentensi.    (alama 5)
      1. Wanafunzi wanapanda miti.
      2. Daktari alimtibu mgonjwa.
      3. Rais alihimiza tuwe na upendo
      4. James ni mwalimu bora wa Kiswahili.
      5. Kiatu changu ni kizuri.
    2. Pigia mstari vivumishi katika sentensi   (alama 3)
      1. Halima amevaa nguo nyeupe.
      2. Chumba cha mama ni safi.
      3. Vipepeo wale ni maridadi.
    3. Jaza nafasi kwa kutumia wingi wa nomino kwenya mabano   (alama 3)
      1. Wanafunzi wameokota ____________________ (jiwe) uwanjani.
      2. Hadithi za _______________________ (jitu) zinatisha.
      3. Sebule imepambwa kwa ______________ (ua)  ya kupendeza.
    4. Geuza sentensi hizi ziwe katika umoja (alama 2)
      1. Walimu walifundisha vizuri
        ________________________________________
      2. Vipepeo wameruka kuelekea mashariki
        ________________________________________
    5. Jaza nafasi kwa kutumia "u" au "i"   (alama 2)
      1. Mkebe _____tachomwa
      2. Mipera _____napaliliwa

MARKING SCHEME

  1.  
    1.  
      1. Binuru
      2. Aheri
    2.  
      1. kwetu, kwingi
      2.  
        1. baba na papa
        2. kuku na gugu
        3. pata na bata
    3.  
      1. Giza
      2. Jua
      3. upepo
  2.  
    1. Kwenda haja ndogo
    2. Kwenda haja kubwa
    3. Mja mzito
    4. Makalio
    5. Anaendesha

KUSOMA

  1. Nyasi na majani
  2. Msitu
  3. Tembo
  4. Ishirini na mmoja
  5. 99
  6. Miti inaleta mvua ambayo inaleta majani na nyasi
  7. Agosti na Septemba
  8. ukame

SARUFI

  1.  
    1. Wanafunzi wanapanda miti
    2. Daktari alimtibu mgonjwa.
    3. Rais alihimiza tuwe na upendo
    4. James ni mwalimu bora wa Kiswahili.
    5. Kiatu changu ni kizuri.
  2.  
    1. Halima amevaa nguo nyeupe.
    2. Chumba cha mama ni safi.
    3. Vipepeo wale ni maridadi.
  3.  
    1. mawe
    2. majitu
    3. maua
  4.  
    1. mwalimu alifundisha vizuri
    2. Kipepeo ameruka kuelekea mashariki
  5.  
    1.  Mkebe utachomwa
    2. Mipera inapaliliwa
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili: Lugha - Grade 4 End Term 1 Exam 2021 SET 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.