Displaying items by tag: kiswahili

MASWALI

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA 
Jibu maswali kwa kutamka

 1. Taja vifaa viwili vya shambani.
 2. Bendera yetu ina rangi ngapi? 
 3. Wanafunzi huketi kwenye nini darasani? 
 4. Mwezi wa kumi wa mwaka ni? 
 5. Mtu anayevua samaki anaitwaje?

Kusoma kwa sauti 
Fipi na Feva ni marafiki. Fipi anakula papai na Feva anakula fenesi. kando ya Fipi na Feva kuna paka na panya. Fipi na Feva wanaulizana kama paka na panya wanafanana. Fipi anasema ndiyo, paka na panya wanafanana. Wote ni wanyama wadogo. Feva naye anasema hapana paka na panya hawafanani. Paka ni mkubwa kuliko panya.

SARUFI
Kamilisha kwa '-ake' na '-ao'

 1. Mataifa 
 2. Mwalimu 
 3. Nyimbo 
 4. Tunda 
 5. Mashati

Kanusha 

 1. Alipika 
 2. Wanasoma 
 3. Watavuna
 4. Alikula
 5. Kilioshwa 

Jibu maamkizi 

 1. Habari? 
 2. Hujambo? 
 3. Shikamoo? 
 4. Umeshindaje? 
 5. __nipe penseli. (Wewe, Tafadhali) 

Andika kinyume

 1. Kimbia
 2. Panda 
 3. Lala 
 4. Mrefu
 5. Nyeusi

 

 

Jaza pengo ukitumia 'haraka' au 'polepole'

 1. Amina anakula__ndio maana amechelewa. 
 2. __haina baraka.
 3. Kinyonga anatembea. 
 4. Mgonjwa alitibiwa___akapona.
 5. ___ndio mwendo

Andika tarakimu kwa maneno 

 1. Vikapu 6 __
 2. 44__
 3. Mwanafunzi 1__
 4. Mayai 10__
 5. 83__

VELONA
Huyu ni Velona. Velona ni mtoto. Velona haendi shuleni. Alitoroka nyumbani kwao ili asiende shuleni. Ameajiriwa kazi ya kubeba bidhaa sokoni. Verona halipwi pesa kama mshahara. Yeye hupewa ndizi, maembe, karoti na parachichi kama malipo kwa kazi yake. Velona hulala kwenye vibanda vya mboga sokoni. Bwana Chifu ni jirani yetu. Nitamweleza Bwana Chifu kuhusu Velona.

 1. Velona alitoroka nyumbani kwa nini?
 2. Velona hulala wapi?
 3. Velona hulipwa nini akibeba mizigo? 
 4. _____ni jirani yetu.
 5. Je ni vizuri kuwaajiri watoto?

KUANDIKA
Andika aya moja juu ya; 
"FAMILIA YANGU" 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SARUFI

 1. yake/yao
 2. wake/wao
 3. zake/zao
 4. lake/lao
 5. yake/yao
 6. hakupika
 7. hawakusoma
 8. hawatavuna
 9. hakukula
 10. halikuoshwa
 1. mzuri
 2. sijambo
 3. marahaba
 4. nimeshinda vyema/salama
 5. Tafadhali
 6. tembea
 7. shuka
 8. amka
 9. mfupi
 10. nyeupe
 1. polepole
 2. haraka
 3. polepole
 4. haraka
 5. polepole
 6. sita
 7. arubaini na nne
 8. mmoja
 9. kumi
 10. themanini na tatu
 1. ili asiende shuleni
 2. kwenye vibanda vya mboga sokoni
 3. ndizi, maembe, karoti na parachichi
 4. Bwana Chifu
 5. La/hapana

 Questions for Kiswahili - CBC PP2 End Term 2 Exams 2022 with Answers

 1. Andika kwa herufi ndogo
  T .......... B ..........
  G .......... H ..........
  A .......... R..........
  D .......... E..........
 2. Jaza silabi
  a..........i..........u
  ba..........bi..........bu
  ha he .......... ho..........
 3. Unganisha silabi.
  mo + to = ..........
  so + ko = ..........
  jo + to = ..........
  no + no = ..........
 4. Andika kwa herufi kubwa.
  pete ........................................
  saa ........................................
  tano........................................
  saba........................................
  hema........................................
 5. Jaza vokali 'a'
  b..........ta
  m..........ma
  b..........ba
  k..........ka
  m..........ji
 6. Linganisha
  linga

MARKING SCHEME

 1. t             b
  g             h
  a             r
  d             e
 2. a,e,i,o,u
  ba,be,bi,bo,bu
  ha,he,hi,ho,hu
 3. moto
  soko
  joto
  nono
 4. PETE
  SAA
  TANO
  SABA
  HEMA
 5. bata
  mama
  baba
  kaka
  maji
 6.                                
  linga 2

MASWALI

 1. Imla(herufi ndogo)
  1
 2. Andika herufi h-o
 3. Linganisha
  2
 4. Paka rangi
  3.png
 5. Andika herufi hizi
  4

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. Sahihisha 
 2. Sahihisha
 3.   
  5
 4. Sahihisha
 5. Sahihisha

MASWALI

 1. ZOEZI 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
  Jibu maswali haya utakayoulizwa na mwalimu wako. (Alama 5)
  1. Taja vifaa viwili vya darasani.
  2. Jibu salamu: Shikamoo?
  3. Taja sehemu mbili za mwili.
  4. Tambua vifaa vitatu ya usafi.
  5. Neno "babu' lina herufi ngapi?
 2. ZOEZI LA 2: KUSOMA KWA SAUTI
  Soma kifungu hiki kwa sauti.
  Mimi ni Abdi. Rafiki yangu anaitwa Musa. Siku ya Jumamosi, sisi hucheza pamoja. Leo tunacheza mchezo na Kibe. Musa kufumba macho yake asinione. Mimi ninakimbia ili nijifiche. Nimejificha nyuma ya kiti. Nimejifunika kichwa kwa kitambaa. Musa hajaniona.
 3. ZOEZI LA 3: SARUFI
  Andika majina ya picha zifuatazo. (Alama 3)
  1
 4. Andika nambari kwa maneno. (Alama 4)
  1. 6
  2. 3
  3. 4
  4. 1
 5. Jibu maamkuzi yafuatayo. (Alama 5)
  1. Shikamoo?
  2. U hali gani?
  3. Habari?
  4. Hujambo?
  5. Umeshindaje?
 6. Andika majina ya siku tatu za wiki. (Alama 3)
 7. Unganisha silabi ili kuunda maneno sahihi. (Alama 5)
  1. Ta + no
  2. Ma + ka + o
  3. Ku + la =
  4. Li + pa =
  5. Che + za=
 8. ZOEZI LA 4: UFAHAMU
  Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali. (Alama 5) Siku moja, Mumo alikuwa akitoka shuleni. Alikuwa na rafiki yake, Tausi. Tausi alidungwa na mwiba. Hakuweza kutembea vizuri. Mumo alimshika mkono. Walitembea polepole hadi nyumbani kwa Tausi. Wazazi wa Tausi walimshukuru sana Mumo. Tausi alipelekwa hospitalini. Mwiba ulitolewa. Tausi alipona.
  1. Mumo alikuwa akitoka wapi?
  2. _____alidungwa na mwiba akaumia.
  3. Kwa nini Tausi hakuweza kutembea vizuri?
  4. Wazazi wa Tausi walimpeleka wapi?
  5. Wazazi wa Tausi walimfanyia nini Mumo?
 9. ZOEZI LA 5: KUANDIKA
  Andika sentensi kumi juu ya:
  MWALIMU WANGU

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.      
  1. kitabu, kalamu, ubao,(jibu lingine lolote sahihi)
  2. marahaba
  3. mkono, mguu, kichwa, (jibu lingine lolote sahihi)
  4. sabuni, mswaki,(jibu lingine lolote sahihi)
  5. nne
 2.      
 3.    
  1. dawati
  2. kifutio
  3. kiti (jibu lingine lolote sahihi)
 4.    
  1. sita
  2. tatu
  3. saba
  4. moja
 5.    
  1. marahaba
  2. hali njema
  3. mzuri
  4. sijambo
  5. nimeshinda vyema (jibu lingine lolote sahihi)
 6.    
  1. jumatatu
  2. jumanne
  3. jumatano (jibu lingine lolote sahihi)
 7.      
  1. tano
  2. makao
  3. kula
  4. lipa
  5. cheza
 8.    
  1. shuleni
  2. Tausi
  3. Alidungwa na mwiba
  4. nyumbani
  5. walimshukuru

ASSESSMENT RUBRIC

Learning Areas  Score  Exceeds Expectations  Meets expectations  Approaches Expectations  Below Expectations
Kiswahili          

QUESTIONS

Kiswahili

ZOEZI LA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

 1. Jibu maswali mwalimu atakayokuuliza kwa kutamka. (Alama 5)
  1. Tambua vokali zote. 
  2. Wingi wa neno 'mkoba' ni nini? 
  3. Unda neno ukitumia silabi 'cha'.
  4. Taja haki mbili za watoto. e) Chombo cha usafiri kinachopitia kwenye reli ni gani?

ZOEZI LA 2: KUSOMA KWA SAUTI

 1. Soma kifungu hiki kwa sauti. (Alama 10
  Chakula cha nyumbani ni kitamu kuliko cha barabarani. Chakula cha nyumbani huhifadhiwa vizuri. Kila adhuhuri, mama huchemsha maji ya kunywa ya nyumbani. Yeye huyachuja vizuri. Chupa yetu ya chai daima hung'ara kama dhahabu. Mama hapendi tununue chakula cha barabarani. Yeye hutupikia chipsi na chapati. Tunampenda mama.

ZOEZI LA 3: SARUFI

 1. Panga herufi hizi vizuri ili kuunda salamu. (Alama 3)
  1. qamraabh - ....................................
  2. Jewambaa - ....................................
  3. ahirba - ....................................
 2. Jaza pengo kwa kutumia a, e, i, o, u. (Alama 3)
  1. b_ st__n_
  2. ch_ _
  3. m_kt_b_
 3. Tumia vyenu' 'wenu' ai 'zenu' kukamilisha sentensi. (Alama 5)
  1. Wanafunzi ................................... wanaimba vizuri.
  2. Bendera ................................... zinapendeza. 
  3. Vifutio ...................................vimeanguka sakafuni. 
  4. Walimu ...................................wameingia darasani. 
  5. Nyuso ................................... zinameremeta.
 4. Andika majina ya vyombo hivi vya usafiri. (Alama 5
  6 q
 5. Unda maneno yenye silabi au herufi zifuatazo. (Alama 4)
  1. ny - ..................................
  2. me  - ..................................
  3. da  - ..................................
  4. ng  - ..................................
  5. pi  - ..................................

ZOEZI LA 4: UFAHAMU

 1. Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali yafuatayo. (Alama 5)

Tulifunga shule baada ya kumaliza masomo ya muhuld mwezi wa Aprili. Wazazi wangu walinipeleka kwa ami yangu. Ami yangu anaishi mtaa wa Dhahabu. Mtaa wa Dhahabu uko mbali na mjini. Tulienda a kuabiri matatu kuelekea kwa ami.

Njiani niliona pikipiki, baiskeli magari madogo madogo na hata malori.

Hatimaye, tulifika katika kituo cha matatu cha Dhahabu. Ami yangu alikuwa Tayari kunipokea. Alifurahi sana kutuona Tulienda nyumbani kwake kwa tuktuk. Alikuwa ametuandalia chakula kitamu. Nampenda sana ami yangu.

 1. Ami aliishi wapi?
 2. Ilikuwa likizo ya mwezi gani?
 3. Njiani niliona magari, malori, pikipiki na 
 4. Mtaa wa Dhahabu uko mbali na
 5. Ami aliwapeleka nyumbani kwake kwa kutumia nini?

ZOEZI LA 5: KUANDIKA

 1. Andika sentensi kumi kuhusu. (Alama 10)

DARASA LETU

MWONGOZO WA KUSAHISHA

 1.                        
  1. a,e,i,o,u
  2. mikoba
  3. chama, chanjo (neno lolote sahihi)
  4.              
   • Haki ya kuishi
   • Haki ya kuendelezwa
   • Haki ya kulindwa
   • Haki ya kushiriki
   • Haki ya kutobaguliwa
  5. treni
 2. Anaposoma kifungu, mwanafunzi anapaswa kupangiwa daraja kulingana na;
  • Kasi ya kusoma
  • Utamshi wa maneno katika kifungu
  • Usahihi
 3.                
  1. marahaba
  2. waambaje
  3. habari
 4.               
  1. bustani
  2. muktaba
  3. chai, choo, chuo (jibu lingine lolote husika)
 5.                    
  1. wenu
  2. zenu
  3. vyenu
  4. wenu
  5. zenu
 6.                
  1. lori
  2. ndege
  3. meli
  4. tuktuk
  5. treni
 7. Pea alama jibu lolote husika
  1. nyayo, nyaya, nyama
  2. mende, meno, meza
  3. dada, dakika, damu
  4. ngombe, ngamia
  5. pika, picha, pindua
 8.       
  1. mtaa was Dhahabu
  2. Aprili
  3. baiskeli
  4. mjini
  5. tuktuk

MASWALI

SEHEMU YA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

 1. Familia yako ina watu wangapi?
 2. Unao ndugu wangapi? 
 3. Ni nani huwapikia katika familia yenu?
 4. Wewe na familia yako mnaishi wapi?
 5. Nyinyi husaidiana vipi katika familia yako?

SEHEMU YA 2: KUSOMA
Zoezi la 1: Kusoma kwa sauti.
Wiki iliyopita, nilihudhuria sherehe ya harusi. Ilikuwa ni wikendi njema. Joto lilikuwa la kadiri. Watu wengi walikuwa shereheni. Nilisimama na kuwatazama.
Alama 10

Zoezi la 2: Kusoma kwa Ufahamu.
Soma hadithi na ujibu maswali yafuatayo.
Jumamosi iliyopita, shangazi yangu alitutembelea. Hakuwa ametutembelea kwa muda wa wiki mbili. Aliniletea peremende na biskuti. Baba na mama walifurahi mno kumwona. Hata hivyo, nilikuwa na furahi kuliko wao. Siku iliyofuata, Jumapili, mimi na shangazi tulienda kanisani ambapo tuliimba na kumchezea Mungu. Ilikuwa ni siku njema.

 1. Shangazi wa mwandishi aliwatembelea siku ya.
 2. Shangazi wa mwandishi alimletea mwandishi
 3. Mwandishi alienda kanisani pamoja na
 4. Kina mwandishi walienda kanisani siku ya
 5. Walipokuwa kanisani, waliimba na kumchezea.

SEHEMU YA 3: SARUFI
Andika sentensi hizi katika wakati uliopo.

 1. Nilichora kibonzo ubaoni.
 2. Tutaandika barua.
 3. Nitamsaidia rafiki yangu.
 4. Tuliongea kwa sauti.

Tumia maneno uliyopewa kujazia vihashe. (vizuri , vibaya)

 1. Viazi___vilitupwa jaani.
 2. Aliongea___kwa heshima.
 3. Wananchi walimchapa___mwizi yule.

Chagua jibu bora zaidi kutoka mabanoni.

 1. Kidole___ni cha mtoto. (huyu, hiki, ile)
 2. Mama___ni mpole. (wao, yangu, lake)
 3. Shule___imepakwa rangi. (hii, lao, changu)

SEHEMU YA 4: KUANDIKA
"Ziandike upya sentensi hizi kwa hati nadhifu.

 1. Jana nilienda kwa nyanya.
 2. Nilipofika nilimkuta akiota jua.
 3. Alinipikia uji wa wimbi.
 4. Niliufurahia uji huo.
 5. Nilimshukuru sana nyanya yangu.

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

(Sahihisha 1-10)

 1. Jumamosi
 2. peremende na biskuti
 3. shangazi
 4. Jumapili
 5. Mungu
 6. Nachora kibonzo kibaoni
 7. Tunaandika barua
 8. Namsaidia rafiki yangu
 9. Tunaongea kwa saut
 10. vibaya
 11. vizuri
 12. vibaya
 13. hiki
 14. yangu
 15. hii

(Sahihisha 26-28)

Maswali

SEHEMU YA KWANZA
KUSIKILIZA NA KUONGEA

 1. Habari?
  (Mwanafunzi anajibu)
 2. Hujambo?
  (Mwanafunzi anajibu)

SEHEMU YA PILI
KUSOMA

 1. Soma silabi hizi
  b    t    k    w      z     p     d
 2. Soma neno fupi
  paa     saa      taa    uko       kitu    tai

SEHEMU YA TATU
KISWAHILI LUGHA

 1. Rembesha silabi hizi kwa rangi upendayo.
  03Kispp2et122q1
 2. Linganisha maneno haya.
  Paka       dada
  hapa        paka
  zaza        lala
  lala          zaza
  dada        hapa
 3. Unganisha kisha usome.
  03Kispp2et122q3 Copy
 4. Andika jina la picha hizi
  03Kispp2et122q4

Majibu

SEHEMU YA KWANZA

Mwanafunzi anapswa kujibu maswali vizuri

SEHEMU YA PILI

Mwanafunzi anapaswa kusoma maneno na silabi yaliyoandikwa

SEHEMU YA TATU

 1. Mwanafunzi anapaswa kupaka rangi silabi alizopewa. Rangi yoyote inakubalika
 2.    
  03Kispp2et122qa2      
 3.      
  03Kispp2et122q3 cc 1    
 4. Kitabu, yai

MASWALI

 1. Linganisha silabi. (Alama 5)
  1
 2. Andika majina ya picha. (Alarma 5)
  2
 3. Chora kitabu. (Alama 5)
 4. Andika maneno haya tena
  saa
  tatu
  uji
  moja
  mto
 5. Paka umbo hili rangi. (Alama 5)
  3

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1. ba   ba
  be   be
  bi    bi
  bo   bo
  bu   bu
  da   da
 2. kiti
  meza
  jua
  mguu
  mti
Tagged under

QUESTIONS

 1. Soma kwa sauti (Alama 10)
  Mimi ni kijana mdogo. Niko gredi ya kwanza. Mwalimu wangu ni-Bi Pendo. Baba na mama wanapenda mwalimu wangu. Kila siku mimi hucheza mpira.
 2. KUONGEA NA KUSIKILIZA
  Tazama picha kisha mwalimu atauliza maswall
  1. Kuku anafanya nini?
   1
  2. Mtoto anafanya nini?
   2
  3. Mti umefanya nini?
   3
  4. Uji umefanyaje?
   4
  5. Baba anafanya nini?
   5
 3. Soma hadithi kisha jibu maswali
  Hapo zamani za kale, paliishi paka na panya. Wanyama hawa waliishi pamoja. Walikuwa na ashamba kubwa karibu na msitu. Wanyama hawa walikuwa na watoto. Siku moja paka aliona njaa akala watoto wa panya. Panya alikasirika na kupotelea msituni na paka akaachwa nyumbani.
  1. Taja wanyama katika hadithi
  2. Wanyama hawa walikuwa na_____kubwa.
  3. Shamba la wanyama lilikuwa karibu na_____
  4. Nani alikula watoto?
  5. Nani alikasirika?
  6. Panya alikasirika akapotelea wapi?
  7. Nani aliachwa nyumbani
  8. Paka hula nini?
  9. Chora Paka
 4. Matumizi ya lugha
  Sarufi
  Andika majina a picha
  6
  7
 5. Andika wingi wa majina haya
  1. Kikombe
  2. Mti
  3. Kiti
  4. Mtoto
  5. Mguu
 6. Andika kinyume cha maneno
  1. Keti
  2. Lala
  3. Lia
  4. Panda
  5. Anika
 7. Andika maneno vizuri
  1. tiki
  2. pachu
  3. choma
 8. Andika maneno haya kwa herufi kubwa
  1. Kitabu
  2. Kalamu
  3. Mwavuli
 9. Andika maneno utakayosomewa na mwalimu

MARKING SCHEME

 1.    
  1. anatembea
  2. analia
  3. umeanguka/umevunjika
  4. umemwagika
  5. ameketi
 2.      
  1.      
   • paka
   • panya
  2. shamba
  3. msitu
  4. paka
  5. panya
  6. msituni
  7. paka
  8. panya
 3.      
  1. kiti
  2. meza
  3. chupa
  4. kijiko
  5. jicho
  6. ua
 4.    
  1. vikombe
  2. miti
  3. viti
  4. watoto
  5. miguu
 5.      
  1. simama
  2. amka
  3. cheka
  4. shuka
  5. anua
 6.    
  1. kiti
  2. chupa
  3. macho
 7.      
  1. KITABU
  2. KALAMU
  3. MWAVULI
Tagged under

Maswali

 1. UFAHAMU 
  Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswallyerfuatayo:

  Karimi ni msichana nadhifu. Yeye husoma katika gredi ya kwanza shuleni leleji. Mwalimu wake wa darasa ni Bi Khadija. Kiranja wa darasa ni mvulana. Jina lake ni Adhoch.
  1. Karimi ni msichana wa aina gani?
  2. Ako katika gredi gani?
  3. Shule yake inaitwaje?
  4. Mwaiimu wake wa darasa anaitwaje?
  5. Kiranja woo anaitwaje?

 2. SARUFI (Mama 20)
  1. Andika majina ya vyakula hivi (Mama 5)
   03Kisg1et1q2.1a
  2. chagua jibu sahihi. (Mama 5)
   1. Ndizi ___________ zimeharibika. (zetu, langu)
   2. Mihogo ___________ imepikwa. (letu, yetu)
   3. Embe ___________  limeiva. (Iangu, zangu)
   4. Muwa ___________  ni mtamu. (zetu, wangu)
   5. Viazi ___________  ni vikubwa. (chetu vyetu)
  3. Tumia haya maneno kujaza pengo
   (nawa mikono, futa kamasi, kata kucha)
   1. Mtoto ali ___________ kwenye pua lake.
   2. Baada ya kutoka msalani ali ___________
   3. Mwanafunzi ali___________  zake ndefu za vidole
  4. Jaza pengo kwa kutumia maneno haya
   (pole, tafadhali, kwaheri)
   1. Ukimkosea mtu utamwambia ___________
   2. Ukimuaga mtu unasema ___________  ya kuonana.
   3. ___________  nisaidie kalamu yako.
  5. Andika majina ya nambari hizi kwa maneno
   1. 10 ___________ 
   2. 8   ___________ 
   3. 6   ___________ 
   4. 7   ___________

 3. KUANDIKA.
  Unda maneno kumi kutoka kwenye jedwali
  kwa mfano: a na bi sha - anabisha
  nya  bu bi na mba za
  mu ba sha a ha sa

  1. ___________________________
  2. ___________________________
  3. ___________________________
  4. ___________________________
  5. ___________________________
  6. ___________________________
  7. ___________________________
  8. ___________________________
  9. ___________________________
  10. ___________________________

Majibu

 1.               
  1. nadhifu
  2. gredi ya kwanza
  3. Leleji
  4. Bi Khadija
  5. Adhoch
 2.          
  1.        
   1. mhindi/ mahindi
   2. sukuma
   3. kitunguu
   4. nyanya
   5. maharagwe/maharage
  2.       
   1. zetu
   2. yetu
   3. langu
   4. wangu
   5. vyetu
  3.            
   1. futa kamasi
   2. nawa mikono
   3. kata kucha
  4.              
   1. pole
   2. kwaheri
   3. tafadhali
  5.          
   1. kumi
   2. nane
   3. sita
   4. saba
 3. Sahihisha maneno yoyote kumi ambayo yametengenezwa kulingana na maagizo
  mfano: babu, hamu, sanaa, hasa, baa, bisha, nasa, sana, zamu, zaba, shamba, ana, amba, anabisha, sambaza, sambaa, saba, na mengineo
Page 1 of 5