Thursday, 01 September 2022 08:54

Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 2 End Term 2 Exams 2022 SET 1

Share via Whatsapp

MASWALI

SEHEMU YA 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA

  1. Familia yako ina watu wangapi?
  2. Unao ndugu wangapi? 
  3. Ni nani huwapikia katika familia yenu?
  4. Wewe na familia yako mnaishi wapi?
  5. Nyinyi husaidiana vipi katika familia yako?

SEHEMU YA 2: KUSOMA
Zoezi la 1: Kusoma kwa sauti.
Wiki iliyopita, nilihudhuria sherehe ya harusi. Ilikuwa ni wikendi njema. Joto lilikuwa la kadiri. Watu wengi walikuwa shereheni. Nilisimama na kuwatazama.
Alama 10

Zoezi la 2: Kusoma kwa Ufahamu.
Soma hadithi na ujibu maswali yafuatayo.
Jumamosi iliyopita, shangazi yangu alitutembelea. Hakuwa ametutembelea kwa muda wa wiki mbili. Aliniletea peremende na biskuti. Baba na mama walifurahi mno kumwona. Hata hivyo, nilikuwa na furahi kuliko wao. Siku iliyofuata, Jumapili, mimi na shangazi tulienda kanisani ambapo tuliimba na kumchezea Mungu. Ilikuwa ni siku njema.

  1. Shangazi wa mwandishi aliwatembelea siku ya.
  2. Shangazi wa mwandishi alimletea mwandishi
  3. Mwandishi alienda kanisani pamoja na
  4. Kina mwandishi walienda kanisani siku ya
  5. Walipokuwa kanisani, waliimba na kumchezea.

SEHEMU YA 3: SARUFI
Andika sentensi hizi katika wakati uliopo.

  1. Nilichora kibonzo ubaoni.
  2. Tutaandika barua.
  3. Nitamsaidia rafiki yangu.
  4. Tuliongea kwa sauti.

Tumia maneno uliyopewa kujazia vihashe. (vizuri , vibaya)

  1. Viazi___vilitupwa jaani.
  2. Aliongea___kwa heshima.
  3. Wananchi walimchapa___mwizi yule.

Chagua jibu bora zaidi kutoka mabanoni.

  1. Kidole___ni cha mtoto. (huyu, hiki, ile)
  2. Mama___ni mpole. (wao, yangu, lake)
  3. Shule___imepakwa rangi. (hii, lao, changu)

SEHEMU YA 4: KUANDIKA
"Ziandike upya sentensi hizi kwa hati nadhifu.

  1. Jana nilienda kwa nyanya.
  2. Nilipofika nilimkuta akiota jua.
  3. Alinipikia uji wa wimbi.
  4. Niliufurahia uji huo.
  5. Nilimshukuru sana nyanya yangu.


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

(Sahihisha 1-10)

  1. Jumamosi
  2. peremende na biskuti
  3. shangazi
  4. Jumapili
  5. Mungu
  6. Nachora kibonzo kibaoni
  7. Tunaandika barua
  8. Namsaidia rafiki yangu
  9. Tunaongea kwa saut
  10. vibaya
  11. vizuri
  12. vibaya
  13. hiki
  14. yangu
  15. hii

(Sahihisha 26-28)

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 2 End Term 2 Exams 2022 SET 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.