Tuesday, 06 September 2022 07:24

Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 2 Exams 2022 SET 1

Share via Whatsapp

MASWALI

KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA 
Jibu maswali kwa kutamka

  1. Taja vifaa viwili vya shambani.
  2. Bendera yetu ina rangi ngapi? 
  3. Wanafunzi huketi kwenye nini darasani? 
  4. Mwezi wa kumi wa mwaka ni? 
  5. Mtu anayevua samaki anaitwaje?

Kusoma kwa sauti 
Fipi na Feva ni marafiki. Fipi anakula papai na Feva anakula fenesi. kando ya Fipi na Feva kuna paka na panya. Fipi na Feva wanaulizana kama paka na panya wanafanana. Fipi anasema ndiyo, paka na panya wanafanana. Wote ni wanyama wadogo. Feva naye anasema hapana paka na panya hawafanani. Paka ni mkubwa kuliko panya.

SARUFI
Kamilisha kwa '-ake' na '-ao'

  1. Mataifa 
  2. Mwalimu 
  3. Nyimbo 
  4. Tunda 
  5. Mashati

Kanusha 

  1. Alipika 
  2. Wanasoma 
  3. Watavuna
  4. Alikula
  5. Kilioshwa 

Jibu maamkizi 

  1. Habari? 
  2. Hujambo? 
  3. Shikamoo? 
  4. Umeshindaje? 
  5. __nipe penseli. (Wewe, Tafadhali) 

Andika kinyume

  1. Kimbia
  2. Panda 
  3. Lala 
  4. Mrefu
  5. Nyeusi

 

 

Jaza pengo ukitumia 'haraka' au 'polepole'

  1. Amina anakula__ndio maana amechelewa. 
  2. __haina baraka.
  3. Kinyonga anatembea. 
  4. Mgonjwa alitibiwa___akapona.
  5. ___ndio mwendo

Andika tarakimu kwa maneno 

  1. Vikapu 6 __
  2. 44__
  3. Mwanafunzi 1__
  4. Mayai 10__
  5. 83__

VELONA
Huyu ni Velona. Velona ni mtoto. Velona haendi shuleni. Alitoroka nyumbani kwao ili asiende shuleni. Ameajiriwa kazi ya kubeba bidhaa sokoni. Verona halipwi pesa kama mshahara. Yeye hupewa ndizi, maembe, karoti na parachichi kama malipo kwa kazi yake. Velona hulala kwenye vibanda vya mboga sokoni. Bwana Chifu ni jirani yetu. Nitamweleza Bwana Chifu kuhusu Velona.

  1. Velona alitoroka nyumbani kwa nini?
  2. Velona hulala wapi?
  3. Velona hulipwa nini akibeba mizigo? 
  4. _____ni jirani yetu.
  5. Je ni vizuri kuwaajiri watoto?

KUANDIKA
Andika aya moja juu ya; 
"FAMILIA YANGU" 



MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

SARUFI

  1. yake/yao
  2. wake/wao
  3. zake/zao
  4. lake/lao
  5. yake/yao
  6. hakupika
  7. hawakusoma
  8. hawatavuna
  9. hakukula
  10. halikuoshwa
  1. mzuri
  2. sijambo
  3. marahaba
  4. nimeshinda vyema/salama
  5. Tafadhali
  6. tembea
  7. shuka
  8. amka
  9. mfupi
  10. nyeupe
  1. polepole
  2. haraka
  3. polepole
  4. haraka
  5. polepole
  6. sita
  7. arubaini na nne
  8. mmoja
  9. kumi
  10. themanini na tatu
  1. ili asiende shuleni
  2. kwenye vibanda vya mboga sokoni
  3. ndizi, maembe, karoti na parachichi
  4. Bwana Chifu
  5. La/hapana
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - CBC Grade 3 End Term 2 Exams 2022 SET 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students


.