Friday, 02 September 2022 07:23

Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 1 End term 2 2022

Share via Whatsapp

MASWALI

 1. ZOEZI 1: KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
  Jibu maswali haya utakayoulizwa na mwalimu wako. (Alama 5)
  1. Taja vifaa viwili vya darasani.
  2. Jibu salamu: Shikamoo?
  3. Taja sehemu mbili za mwili.
  4. Tambua vifaa vitatu ya usafi.
  5. Neno "babu' lina herufi ngapi?
 2. ZOEZI LA 2: KUSOMA KWA SAUTI
  Soma kifungu hiki kwa sauti.
  Mimi ni Abdi. Rafiki yangu anaitwa Musa. Siku ya Jumamosi, sisi hucheza pamoja. Leo tunacheza mchezo na Kibe. Musa kufumba macho yake asinione. Mimi ninakimbia ili nijifiche. Nimejificha nyuma ya kiti. Nimejifunika kichwa kwa kitambaa. Musa hajaniona.
 3. ZOEZI LA 3: SARUFI
  Andika majina ya picha zifuatazo. (Alama 3)
  1
 4. Andika nambari kwa maneno. (Alama 4)
  1. 6
  2. 3
  3. 4
  4. 1
 5. Jibu maamkuzi yafuatayo. (Alama 5)
  1. Shikamoo?
  2. U hali gani?
  3. Habari?
  4. Hujambo?
  5. Umeshindaje?
 6. Andika majina ya siku tatu za wiki. (Alama 3)
 7. Unganisha silabi ili kuunda maneno sahihi. (Alama 5)
  1. Ta + no
  2. Ma + ka + o
  3. Ku + la =
  4. Li + pa =
  5. Che + za=
 8. ZOEZI LA 4: UFAHAMU
  Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali. (Alama 5) Siku moja, Mumo alikuwa akitoka shuleni. Alikuwa na rafiki yake, Tausi. Tausi alidungwa na mwiba. Hakuweza kutembea vizuri. Mumo alimshika mkono. Walitembea polepole hadi nyumbani kwa Tausi. Wazazi wa Tausi walimshukuru sana Mumo. Tausi alipelekwa hospitalini. Mwiba ulitolewa. Tausi alipona.
  1. Mumo alikuwa akitoka wapi?
  2. _____alidungwa na mwiba akaumia.
  3. Kwa nini Tausi hakuweza kutembea vizuri?
  4. Wazazi wa Tausi walimpeleka wapi?
  5. Wazazi wa Tausi walimfanyia nini Mumo?
 9. ZOEZI LA 5: KUANDIKA
  Andika sentensi kumi juu ya:
  MWALIMU WANGU


MWONGOZO WA KUSAHIHISHA

 1.      
  1. kitabu, kalamu, ubao,(jibu lingine lolote sahihi)
  2. marahaba
  3. mkono, mguu, kichwa, (jibu lingine lolote sahihi)
  4. sabuni, mswaki,(jibu lingine lolote sahihi)
  5. nne
 2.      
 3.    
  1. dawati
  2. kifutio
  3. kiti (jibu lingine lolote sahihi)
 4.    
  1. sita
  2. tatu
  3. saba
  4. moja
 5.    
  1. marahaba
  2. hali njema
  3. mzuri
  4. sijambo
  5. nimeshinda vyema (jibu lingine lolote sahihi)
 6.    
  1. jumatatu
  2. jumanne
  3. jumatano (jibu lingine lolote sahihi)
 7.      
  1. tano
  2. makao
  3. kula
  4. lipa
  5. cheza
 8.    
  1. shuleni
  2. Tausi
  3. Alidungwa na mwiba
  4. nyumbani
  5. walimshukuru

Download Kiswahili Questions with Answers - CBC Grade 1 End term 2 2022.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students


.