Tuesday, 07 September 2021 07:30

Kiswahili - Class 7 End Term 1 Exam 2021 SET 1

Share via Whatsapp

DARASA LA 7, MWISHO WA MUHULA WA 1, 2021
KISWAHILI
JINA....................................................SHULE..........................................

Tumia msamiati ulio mwafaka zaidi ujaze kwenye vihasho 1 hadi 15.

Ni kweli kwamba jinsi tunavyoendelea kukua ndivyo    1   kujifunza mambo mengi aushini.    2  ya hayo ni kazi. Kazi ndiyo    3    wa maisha ya binadamu. Kazi ni kazi, iwe ya   4  au rahisi; usichague. Kwani kazi    5   hutusaidia6 riziki yetu. Tujizoeshe, tupende na    7  kazi mapema. Wajibu    8      nyumbani ni kuwasaidia wazazi katika kazi zote. Ubwete haufai    9     hauwezi kutulisha. Tuchape kazi kwanza    10    tupumzike.

 1. A. tunazidi              B. tunapozidi              C. tunavyozidi            D. tunakozidi
 2. A Mmojawapo        B. Mojawapo              C. Kimojawapo           D. Umojawapo
 3. A. uti wa mgongo   B. uti wa mkono         C. uti wa kichwa         D. uti wa mguu
 4. A. suluhu                B. sulu                        C. zulu                       D. sulubu 
 5. A. ndicho                B. ndiyo                      C. ndilo                      D. ndio
 6. A. kusumbua          B. kuzubua                 C. kuzumbua             D. kusafirisha
 7. A. kuendeleza        B. kuendelesha          C. kuendelea             D.kuendeleshwa 
 8. A yetu                     B. zetu.                       C. letu                       D. wetu
 9. A. na                       B. wala                       C. ingawa                  D. lakini
 10. A. Ndiyo                  B. ndio                        C.ndipo                     D. ndiko

Je    11    wajua kuwa ni haki ya kila mtoto kupata elimu? Ni kwa kutambua jambo hili    12    serikali ya Kenya ilitangaza kuwa itatoa elimu bila malipo kwa watoto wote ili kila    13    apate nafasi ya kujipatia elimu ya msingi. Hali kadhalika watoto wa    14   wa kwenda shule hawapaswi kuajiriwa mahali    15   .

 1. A.,                   B.?                    C. !                 D..
 2. A. ambako      B. ambao          C. ambaye      D. ambapo
 3. A. moja           B. mmoja          C. mamoja      D. mojawapo 
 4. A. rika             B. wakati           C. umri            D. muda 
 5. A. pote            B. kokote          C. popote        D. kote

Kutoka swali la 16 mpaka 30. jibu kulingana na maagizo.

 1. Sentensi;
  Nilipigiwa mpira ina maana zifuatazo isipokuwa________
  1. mpira ulipigwa ukielekezwa kwangu
  2. nilisaidiwa kupiga mpira
  3. nilipigwa kwa sababu ya mpira
  4. mpira ulitumiwa kunipiga
 2. Umbo hili ni
  kisst7et121s1q17
  1. mstatili
  2. mche
  3. duara dufu
  4. pia
 3. Neno "maji” liko katika ngeli gani?
  1. I-I
  2. YA-YA
  3. I-ZI
  4. LI-YA
 4. Kamilisha methali:
  Mchumia juani
  1. hulia kivulini
  2. hali wali mkavu
  3. huumiza mkonowe
  4. marejeo ni ngamani
 5. Chagua umoja wa sentensi hii:
  Watajiwakilisha wao wenyewe
  1. Nitajiwakilisha sisi wenyewe
  2. Atajwakilisha wewe mwenyewe
  3. Nitajiwakilisha mimi mwenyewe
  4. Atajiwakilisha yeye mwenyewe
 6. Petro alitia masomoni na akuibuka mwanafunzi_____zaidi.
  1. chumvi, mzuri
  2. bidii, upya
  3. fora, bora
  4. kauri, kauli
 7. Msichana alitumia__kulia vibanzi.
  1. umma
  2. uma
  3. kijiko
  4. mwiko
 8. Ni sentensi ipi iliyoakifishwa vizuri?
  1. Nilinunua sukari, chumvi, mayai, biskuti
  2. Baba wa Wambui ni karimu
  3. Lo! Ameshindwa kufunga bao! 
  4. Mji wa Mombasa unapendeza
 9. Ni vazi gani lisilovaliwa na wanaume?
  1. Chupi
  2. Kizibao
  3. Fulana
  4. Kanchiri
 10. Andika kwa wingi
  Mama yake alipoteza ufunguo.
  1. Mama zao walipoteza funguo
  2. Wamama wao walipoteza fungu
  3. Kina mama zao walipoteza funguo
  4. Mama zetu walipoteza funguo
 11. Chagua kiunganishi katika sentensi hii.
  Nilifika sokoni ijapokuwa nilichelewa.
  1. sokoni
  2. nilifika
  3. ijapokuwa
  4. nilichelewa
 12. Tambua kimilikishi katika sentensi ifuatayo:
  Tulimkuta mlevi akiwa amelala nyumbani kwake.
  1. mlevi
  2. kwake
  3. nyumbani
  4. amelala
 13. Mnyama wa porini anayefanana na ng'ombe ni
  1. swara
  2. twiga
  3. pundamilia
  4. mbogo
 14. Kalamu yangu ______jana.
  1. iliibiwa
  2. iliiba
  3. iliibwa
  4. uliibwa
 15. Kifaa cha ufundi kinachotumiwa kukerezea mbao ni
  1. msumeno
  2. patasi
  3. nyundo
  4. timazi

Soma kisa kifuatacho kisha ujibu swali 31 hadi 40.

Siku ya kurudi shuleni iliwadia wazazi wa Pendo waliandamana naye kurudi shuleni. Ulikuwa mwisho wa mwezi na magari ya abiria yalijaa pomoni. Hata hivyo, walifika shuleni salama salimini. Pendo alikuwa amejawa na soni usoni. Hakutaka kumwona yeyote pale shule hasa wanafunzi. Hata hivyo alijikaza kwani alimaizi kuwa lisilobudi hutendwa.

Walimu walimweleza mzazi wa Pendo vile mwanao alivyopotoka zaidi ya kuwa na vipawa adimu. Waliwaeleza pia kuhusu Maria. "Huyu mtoto wa kitajiri ndiye anayempotosha Pendo. Ni lazima aachane naye kabisa ili afaulu katika maisha ya baada "Mwalimu mkuu alisema.

Babake Pendo aliposikia jina Maria likitajwa alianza kutafakari. "Mbona jina hili si geni kwangu?" Alijisaili moyoni. Jina lilo lilifanana na mtoto wa mwajiri wake hata ingawa majina hufanana. Hakuona uwezekano wa mtoto wa mwajiri wake kuwa ndiye aliyemharibu mwanawe. Vilevile, hakuona kama kuna uwezekano kuwa mtoto wa tajiri ungesomea hapo.

Musa, babake Pendo, hakujua alikosomea mtoto wa mwajiri wake. Hata hivyo, fikra na jina hilo zilimtatiza kwa muda baba mtu. Baada ya anuda m pi kupita, Musa alimuuliza mwalimu jinsi ya
LON kumsaidia Pendo. Mwalimu mkuu alieleza kwan ha jandbo Jílo lingesuluhishwa vizuri kwa kuwahusisha wazazi wa Maria

Mwalimu alielezea kwamba wazazi wa Maria walikuwa mabwanyenye katika mitaa ya kifahari. Dhahiri shahiri kuwa haingekosa kuwa yule alikuwa mwajiri wake. Hakutaka mwalimu ajue hivyo licha ya kuwa hisia zake zilidhihisha mengi.

Mwishowe waliagana kwamba Pendo alipaswa kusauriwa na mwalimu na angeripoti katika ofisi ya mwalimu kila alasiri. Pia alipaswa kuadhibiwa kwa kosa lake la kutoroka na ashauriwe barabara na mwalimu kabla ya kwenda kulala.

 1. Magari yalijaa pomoni kwa nini?
  1. Ilikuwa siku ya kurudi shuleni
  2. Ilikuwa asubuhi
  3. Ni kawaida ya magari kujaa
  4. Ulikuwa mwisho wa mwezi
 2. Pendo alirudi shuleni
  1. kwa hiari yake
  2. siku ya kufungua shule
  3. kwa furaha mpwitompwito
  4. shingo upande
 3. Pendo alikuwa nyumbani kwa sababu
  1. ulikuwa mwisho wa mwezi
  2. ulikuwa wakati alikizo
  3. alitumwa nyumbani kwa utovnidhamu
  4. alitaka kuja shuleni ma mzazi wake
 4. Maisha ya baadaye ni maisha gani?
  1. Maisha ya kisogoni
  2. Maisha ya masomo
  3. Maisha yajayo
  4. Maisha ya furaha
 5. Pendo alisomea shule ya aina gani?
  1. Ya malazi
  2. Ya wavulana na wasichana
  3. Ya wasichana pekee
  4. Yakutwa
 6. Kwa nini Musa hakutaka wazazi wote wahusike kutafuta suluhisho?
  1. Wazazi wa Maria hakujulikana
  2. Walikuwa ndio waajiri wake
  3. Wangetumia wakati mwingi
  4. Wazazi wa Maria walikuwa bwanyenye
 7. Neno bwanyenye lina maana gani?
  1. maskini hohehahe
  2. mti anayeajiri wengine
  3. mtu mkubwa serikalini
  4. Mtu mwenye mali mengi
 8. Pendo alikuwa amefanya kosa gani?
  1. Hatujaambiwa
  2. Kupigana
  3. Kutoroka shuleni
  4. Kupendana ma Maria
 9. Ni jambo gani Pendo alipaswa kutenda?
  1. Kusauriwa kila siku
  2. Kuadhibiwa
  3. Kutumwa nyumbani
  4. Kuachana ma marariki wote
 10. Hisia za Bwana Musa zilidhihirisha nini?
  1. Kwamba mtoto alikuwa na shida
  2. Kwamba alimjua mzazi wa Maria
  3. Kwamba Pendo alikuwa hajafanya kosa
  4. Kwamba mtoto angeadhibiwa

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 bad 50.

Ni wazi kama jua la mtikati kuwa demokrasia katika nchi yetu ya Kenya imekua kwa kiwango kikubwa. Bila shaka hili ni suala la kujivunia kwani inamaanisha kuwa tunaenda na wakati Demokrasia ni mfumo wa kuendesha serikali iliyochaguliwa na watu kwa manufaa ya watu wenyewe. Tangu tulipojinyakulia uhuru yapata miongo mitano iliyopita, nchi yetu imepiga hatua kubwa katika ulingo wa kisiasa.

Rais wa kwanza wa taifa letu tukufu hayati Mzee Jomo Kenyatta aliposhika hatamu za uongozi, alihakikisha kuwa amewaunganish vananchi wote wa taifa hili na kuwapa sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao. Aliasisi falsafa ya Harambee ambao ulikuwa mwito wa kuwahamasisha wananchi kushirikiana na kuchangia maendeleo yao kwa kuvuta pamoja. Mwito huo ulileta ari na mshawasha kwa wananchi wa Kenya na kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi yao.

Aliposafiri kwa njia ya marahaba ninalo mwaka wa elfu moja mia tisa sabini na nane, hayati rais Daniel Toroitich Arap Moi alishikilia uplíuo huo na kuanzisha mwito wa Nyayo ambao ilimaanisha ya kuwa angefuata nyayo za mladgulizi wake na kuhimiza Wakenya kuishi kwa amani, upendo na umoja.

Hayati Rais Moi alikaa kwenye kiti cha enzi kwa miaka shirini na minne. Ijapokuwa hakuna kapa isiyokosa usubi, alifanya mengi ya kujivunia pia. Hatimaye Rais Mwai Kibaki ambapo Kenya ilijipatia Katiba mpya ambayo hadi sasa imebadilisha sura ya uongozi katika nchi yetu. Kuna mabadiliko mengi ambayo yamejidhihirisha waziwazi hususan katika ulingo wa kisiasa, siyo jinsi mambo yalivyokuwa katika miaka ya awali.

Kwa mujibu wa katiba ya sasa, wakati wa uchaguzi mpiga kura atahitajika kuwachagua viongozi zaidi ya watano. Atahitajika kumchagua rais, gavana wa jimbo lake, seneta, mbunge, mwakilishi wa wanawake bungeni na mwakilishi wa baraza la jimbo. Kwa ujumla, inatazamiwa kuwa katiba hii itaibua viwango vya hali ya juu vya uwajibikaji miongoni mwa wanasiasa na wale wote walio katika nafasi za uongozi.

 1. Kidemokrasia, viongozi wa serikali hupigiwa kura na kuchaguliwa na______ wa nchi husika.
  1. wabunge
  2. watu
  3. wazalendo
  4. raia
 2. Kiongozi mkuu kabisa wa nchi ambayo ni jamhuri na huchaguliwa kidemokrasia ni
  1. Gavana
  2. Waziri mkuu
  3. Rais
  4. Mfalme
 3. Ni kauli ipi si sahihi kwa mujibu wa kifungu?
  1. Kenya imekuwa nchi huru kwa zaidi ya miaka hamsini
  2. Kenya ilijinyakulia uhuru wake mwaka wa hamsini
  3. Rais wa kwanza na wa pili kwa sasa hivi ni hayati
  4. Kenya tuliadilisha katiba waskati wa Rais Mwai Kibaki
 4. Katika aya ya pili, mwandishi hatudokezei kuwa
  1. Hayati Mzee Jomo Kenyata aliwapa wananchi wa Kenya sababu tosha ya kuionea fahari nchi yao
  2. Hayati Daniel Toroitich Arap Moi aliaga mwa wa elfu moja mia tisa sabini na nane
  3. Rais Moi alianzisha kauli mbiu ya kufuata nyayo za Mzee Kenyatta
  4. Mwito wa Harambee ulianzishwa
 5.  Msemo ".... Aliposafiri njia ya marahaba ...." haumaanishi?
  1. alipoaga 
  2. aliposafiri jongomeo
  3. alipofariki
  4. alipoenda na kucheza ngoma
 6. Kulingana ma kifungu
  1. Hayati rais Moi aliongoza nchi ya Kenya kwa zaidi ya miongo miwili
  2. Kauli mbiu ya Harambee ilihimiza Wakenya kutoishi kwa amani, upendona umoja
  3. Rais Kibaki alibadilisha sura ya uongozi
  4. Katiba mpya imeibua maswala mengi mazito
 7. Methali nyingine yenye maana sawa na "Hakuna kapa isiyokosa usubi" ni
  1. hakuna kovu la masimango
  2. hakuna masika yasiyokuwa na mbu
  3. kila shetani na mbuyu wake
  4. haba na haba hujaza kibaba
 8. Nchi ya Kenya ilipatia uhuru mwaka wa
  1. 1973
  2. 1964
  3. 1963
  4. 1978
 9. Katika aya ya mwisho tunadokezewa ya kwamba
  1. mpiga kura atapiga kura kuwachagua viongozi watano
  2. katiba mpya itaibua viwango vya ajabu
  3. bunge litakuwa na wawakilishi wa wanawake
  4. rais, makamu wake, spika na seneta ni baadhi ya viongozi wa serikali ambao watachaguliwa wakati wa uchaguzi
 10. Neno miongoni mwa limepigwa mstari katika ufamu liko katika kitengo kipi cha sarufi?
  1. Kihisishi
  2. Kihusishi
  3. Kiunganisho
  4. Kivumishi

MAAKIZO

 1. C
 2. B
 3. A
 4. D
 5. B
 6. C
 7. A
 8. D
 9. B
 10. C
 11. A
 12. D
 13. B
 14. C
 15. C
 16. D
 17. D
 18. B
 19. A
 20. D
 21. C
 22. B
 23. C
 24. D
 25. A
 26. C
 27. B
 28. D
 29. C
 30. A
 31. D
 32. D
 33. C
 34. C
 35. A
 36. B
 37. D
 38. C
 39. A
 40. B
 41. D
 42. C
 43. B
 44. B
 45. D
 46. A
 47. B
 48. C
 49. C
 50. B

Download Kiswahili - Class 7 End Term 1 Exam 2021 SET 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students