Tuesday, 22 March 2022 09:03

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2022

Share via Whatsapp

Maswali

Chagua jibu sahihi ujazie nafasi wazi

Baada ya siku    1      kupita, wakaona kisiwa      2      mbali, wakakusudia kwenda     3      . Walipokaribia , wakaona    4        moja zuri lakini hakukuwa na     5       yoyote ya watu,wanyama    6       ndege. Miti na majani yalikuwa kama yamelala.   7        nanga, wakashuka kisiwani na wakaingia      8     . Kila     9       , waliona watu wamelala bila     10       yoyote;walistaajabu mno. Wakapanda juu ya      11      jumba , wakaingia      12      chumba , wakaona mambo ni     13      tu. Wakaja hata    14        chumba cha yule mlezi     15       wakazidi kustaajabu.

  A B C D
1
2
3
4
5
6
7
8
9
10
11
12
13
14
15
mingi 
na
kuitazama
jumba
dalali
au
wakatua
jumba
walipopita
ufahamu
kile
na
ile ile
katika
nayo
nyingi
ya  
kutazama
chumba
dalili
 ila
wakatoa
 jumbani
waliopita
kufahamu
 ule
wa
yale yale
kwa
naye
mengi
kwa
kukitazama
nyumba
dhalili
wala
wakaweka
kwa jumba
walipita
fahamu
Ile
cha
hiyo hiyo
na
nao
wengi
kuwa
Kupatazama
vyumba
adili
na
wakatia
katika jumbani
waliyepita 
hamu
lile
kwa
yaya haya
wa
nacho

Chagua jibu sahihi kutoka swali la 16-30

  1. Ni ipi sio maana ya kitawe shinda
    1. faulu
    2. kukaa kutwa
    3. isiyojaa
    4. tabu
  2. Magurudumu nikwa motokaa ilhali ________ ni kwa kitanda.
    1. matendeguu
    2. miguu
    3. matendegu
    4. maguu
  3. Kule mahakamani ,shahidi alitakikana atoe __________
    1. shada
    2. shahada
    3. ushuhuda
    4. ushahidi
  4.  Mtoto ___________ alianguka vibaya sana.
    1. mwenye
    2. yeye
    3. mwenyewe
    4. enyewe
  5. Andika ukubwa wa
    Mtoto wa ngo’mbe anaitwa ndama.
    1. Jitoto la ngo’mbe linaitwa dama
    2. Toto la gombe linaitwa dama.
    3. Jitoto la gombe linaitwa ndama.
    4. Toto la ngo’mbe anaitwa ndama.
  6. Nyoka ______ ana meno ______
    1. yule , ndefu
    2. ile , marefu
    3. yule , marefu
    4. ule , refu
  7. Nini maana ya ‘Tulipeana’
    1. alinipea nami nikampea
    2. tulimpa akachukua
    3. nilimpa naye akanipea
    4. tuliwapa nao wakatupa
  8. Chagua sentensi sahihi
    1. Mtoto ambaye aliyefaulu amezawadiwa.
    2. Mtoto ambao alifaulu amezawadiwa.
    3. Mtoto aliyefaulu ametuzwa zawadi.
    4. Mtoto ambaye aliyefaulu amepewa zawadi.
  9. Watu wanapofiwa huwa wanaambiwa?
    1. alamsiki - binuru
    2. mpo - tupo
    3. poleni - asante
    4. makiwa - tunayo
  10. Kamilisha kwa usahihi
    Msimwache mgonjwa _______
    1. akufe
    2. afe
    3. aafe
    4. akakufe
  11. Mwindaji haramu wa wanyama pori huitwa _______
    1. jasusi
    2. jambazi
    3. jangili
    4. msasi
  12. Kama juzi ilikuwa ijumaa tarehe sita, mtondo itakuwa siku gani na tarehe ngapi?
    1. Jumatano tarehe kumi na moja
    2. Jumapili tarehe nane
    3. Ijumaa tarehe kumi na tatu
    4. Jumatano tarehe kumi
  13. Tumia –a unganifu kwa usahihi
    Pua _______ mtoto inauma
    1. la
    2. wa
    3. ya
    4. za
  14. Chagua sentensi iliyo katika wakati timilifu.
    1. aende shuleni
    2. hajaenda shuleni
    3. ataenda shuleni
    4. huenda shuleni
  15. Jaliza mwanya
    Mahali hapa ______ uchafu mwingi.
    1. nayo ina
    2. nako kuna
    3. napo kuna
    4. napo pana

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31 mpaka 40.

Naikumbuka siku hiyo vizuri. Niliamka alfajiri mbichi tayari kuanza safari kutoka kijijini mwetu hadi mji mkuu. Hii ndiyo iliyokuwa mara yangu ya kwanza kuuzuru mji huu. Moyoni nilikuwa na bashasha isiyokuwa ya kawaida kwa sababu siku hiyo ningeuona mji ambao sifa zake nilikuwa nikizisikia tu kutoka kwa wenzangu waliobahatika kuutembelea. Hamu ya kuona majengo marefu, barabara zilizosakifiwa, magari mengi, watu wa asili mbalimbali na mabustani ya starehe ilinigubika ikawa sijifai kwa matumaini.

Nilitembea hatua chache hadi kituo cha mabasi, nikapata daladala moja iliyotoza nauli nafuu, nikaiabiria mpaka mji uliokuwa pua na mdomo kutoka kitongojini mwetu. Hapo nilitumainia kupata matwana ya kusafiria hadi mji mkuu. Kwenye stesheni kulikuwa na msongarnano wa matwana na harakati za utingo waliokuwa waking’ang‘ania abiria. Nikaingia katika matwana moja iliyoitwa Upepo. Nilikuwa abiria wa kumi na wawili kuingia. Baada ya dakika tano hivi, gari lilijaa abiria,wote kumi na wanne. Tukang’oa nanga. Mandhari ya kupendeza yalijikunjua mbele yangu. Upepo mwanana kupitia dirishani,mpito wa kasi wa miti, mazigazi ....vyote vilishirikiana kunipumbaza kiasi cha kunisahaulisha kufunga mkanda wa usalama.

Baada ya robo saa utingo alidai nauli. Nikapeleka mkono kwa tahadhari kwenye kibindo changu ambamo nilikuwa nimezifutika hela za usafiri na masurufu. Nikatoa noti ya shilingi mia mbili na kumkabidhi utingo huku nikitarajia baki. Utingo alinikazia macho, akanyoosha mkono na kusema, “Mia mzaidi!“ Nikarudi tena kwenye kibindo, nikatoa noti mbili za shilingi hamsini na kumpa. Safari ikaendelea.

Tulipofika mji mdogo wa Pilia, matwana ilisimama. Utingo aliinama chini ya viti, akatoa vibao na kuviweka baina ya viti vya kawaida. Kisha akaanza kutangaza. “Wa Jiji na mia; mia hamsini”. Abiria walioonekana kuwa wachovu kwa kungojea na kupigwa na mzizimo wa kipupwe walipigana vikumbo kuingia huku utingo akiwaelekeza kwenye vile vibao. Viti vilivyotengenezewa abiria watatu vikaishia kubeba abiria watano. Matwana nayo ikawa haina budi kustahimili uzito wa abiria ishirini na watatu. Tukawa tunabanana kweli kweli. Utingo naye alining’inia mlangoni huku shati lake likipeperushwa na upepo. Nilipojaribu kulalamikia hali hii nilinyamazishwa hata na abiria wenzangu.

Gari Iikaanza mwendo tena huku likiendeshwa kwa kasi ya umeme. Abiria waliokuwa wakizungumza sasa walinyamaza kila mmoja roho i mkononi. Kimya cha kaburi kikatawala hadi pale utingo alipomwambia dereva. “Weka ngoma.“ Muziki ukahanikiza hewani kwa fujo. Baadhi ya abiria wakaanza kuyumbisha vichwa kwa kufuata mdundo wa muziki ambao ulitishia kuvipasua viwambo vya masikio yangu.

Njiani tulikutana na walinda usalama ambao walitusimamisha. Utingo alishuka na kwenda chemba na mmojawapo wa hao maafisa kisha akarudi huku kipaji chake kimenawiri kwa tabasamu. Akasema, “Nimempaka mafuta viganjani.” Baadhi ya abiria walitikisa vichwa, wengine wakacheka kama kwamba wameona kinyago. Mimi nilibaki kuduwaa tu. Gari liliongeza mwendo na baada ya muda mfupi tukafika kwenye mji mmoja ambao ulikuwa na majengo makubwa makubwa. Nikadhani tumefika mji mkuu. Nilipomuuliza abiria jirani aliniambia kuwa huu ulikuwa tu mji mkuu wa Jimbo la Buraha. Tukazidi kuyakunja rnasafa ya safari hii kwa kasi ya kuogofya huku dereva akitafuna majani aliyokuwa akiyatoa mfukoni mwa shati lake. Kadiri alivyoyatafima ndivyo alivyozidisha kasi. Nikahisi kama gari linapaa juu angani. Nikataka kumwambia dereva jambo, lakini nikajiambia, “Ikiwa wengine wamenyamaza sembuse mimi?“

Baada ya kitambo kidogo mvua ilianza kunyesha. Kukawa na ukungu na utelezi barabarani. Abiria mmoja alimsihi dereva kupunguza mwendo. Hayo hayakumgusa dereva mshipa. Aliongeza kasi kana kwamba hajasikia lolote. Gari Iilifika kwenye kuruba,dereva akawa haoni vizuri. Ghafla nikasikia, “Kirrr..!“ Kisha_“Mungu wangu!" Halafu, ‘ngu!'Kiza cha kaniki kikatanda.

Maswali:

  1. Kulingana na kifungu;
    1. Wenzake msimulizi waliwahi kupata fursa ya kuishi katika Mji Mkuu.
    2. Barabara za Mji Mkuu hazina mashimo.
    3. Mji Mkuu una majumba mengi marefu.
    4. Msimulizi ana mwao na hali ilivyo katika Mji Mkuu.
  2. Chagua jibu sahihi kuhusu vituo vya magari kwa mujibu wa aya ya pili:
    1. Wasafiri wengi kushindania nafasi
    2. Magari mengi kushindania wasafiri
    3. Misongamano mingi ya kungangania wasafari
    4. Shughuli nyingi za kungangania nafasi.
  3. Mazingira ya kuvutia yalimwathiri Msimulizi kwani:
    1. Aliduwaa na kujisahau.
    2. Alifurahia upepo na kujisahau.
    3. Alizubaa na kupuuza sheria za usafiri.
    4. Alipumbaa na kupinga sheria za usafiri.
  4. Msimulizi alikuwa amehifadhi pesa katika:
    1. Mfuko mdogo ndani ya suruali.
    2. Mfuko mdogo mbele ya suruali.
    3. Mfuko wa nguo iliyoshonwa kiunoni.
    4. Mkunjo wa nguo uliofingwa kiunoni.
  5. Katika mji wa Pitia abiria walipigana vikumbo kuingia garini kwa sababu:
    1. Kulikuwa na uhaba wa magari.
    2. Kulikuwa na uhaba wa viti.
    3. Walikuwa wamechoka kungojea matwana
    4. Walikuwa wamepigwa na baridi na mvua.
  6. Kulingana na kifungu ajali barabarani husababishwa na:
    1. ukosefu wa magari, kubeba abiria wengi.
    2. kiburi cha madereva. kutozingatia maelekezo barabarani.
    3. ukosefu wa mikanda ya usalarna, madereva kutowajibika.
    4. muziki wa kupasua viwambo madereva kutoona vizuri.
  7. Msimulizi ni mkakamavu kwa vile:
    1. Alishutumu hali ya gari kubeba abiria kuliko kiasi.
    2. Alishutumu hali ya shati na utingo kuning‘inia nje.
    3. Alinyarnaza alipoona dereva akikaribia kuruba kwa kasi.
    4. Alinyamaza alipoona utingo akienda chemba na afisa.
  8. Chagua jibu lisilo sahihi kulingana na kifungu:
    1. Abiria wengine waliufurahia muziki garini.
    2. Ufisadi unaweza kusababisha ajali barabarani.
    3. Abiria wanaweza kuzuia ajali barabarani.
    4. Kuruba ndiyo iliyosababisha ajali garini.
  9. Ni mfuatano upi wa matukio ufaao kwa mujibu wa kifungu?
    1. Kucheza muziki, kukutana na polisi, kufikia kuruba, mvua kunyesha, kupata ajali
    2. Kukutana na polisi, kuhonga, kucheza muziki, kufikia kuruba, kupata ajali
    3. Kucheza muziki, kukutana na polisi, kuhonga, kufikia kuruba, kupata ajali.
    4. Kukutana na polisi, gari kupaa juu, mvua kunyesha, kufikia kuruba, kupata ajali.
  10. 'Kiza cha kaniki kilitanda’ kulingana na kifungu ina maana:
    1. Msimulizi akapoteza fahamu.
    2. Msimuiizi akapoteza uwezo wa kuona.
    3. Kukawa na weusi mkubwa.
    4. Kukawa na giza totoro.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41 mpaka 50.

Tenga alilelewa katika mazingira yaliyojaa neema, furaha na uchangamfu. Wazazi wake Bwana Mtanga na Bi. Zuhura waiikuwa wakwasi wa kutajika katika janibu hizo, si kwa mali tu bali kwa nyoyo zao zilizokuwa tayari kila mara kuwakirimu wanakijiji kwa lolote.

Bwana Mtanga na Bi. Zuhura hawakuiala maskini wakaamka matajiri. Mtanga alianza kazi kama tarishi katika Makavazi ya Umma. lngawa hii ilikuwa kazi ya kijungu jiko . Mtanga hakwenda nguu: alijitahidi kwa vyovyote vile kujinyanyua. Akajisajili kwa kozi mbalimbali za usimamizi wa makavazi na kuhilimu vyeti tofautitofauti vikiwemo stashahada na shahada katika masuala ya usimamizi wa mashirika ya umma. Jitihada zake zikazaa matunda. Akapandishwa cheo mwaka baada ya mwingine hadi akawa msimamizi wa Makavazi ya Umma. Baadaye akaajiriwa na shirika la Msalaba Mwekundu kama Mkrurugenzi wa Huduma za Kijamii.

Bi. Zuhura naye baada ya kuhitimu masomo ya shule ya upili,alisomea taaluma ya ukutubi na baadaye kuajiriwa katika maktaba ya chuo kikuu cha Tungama. Hapa Zuhura alitambua kuwa amepata nafusi adimu ya kutia makali ubongo wake. Akajisajili kwa kozi ya ukutubi na kuhitimu shahada ya daraja la kwanza katika taaluma hii. Wakuu wake kazini wakavutiwa na juhudi zake na kumpandisha cheo akawa Mkutubi Mkuu.

Wakati Bwana Mtanga na Bi. Zuhura walipokuwa wakijiendeleza kitaaluma na kiuchumi,Tenga naye alikuwa anajikalia tu kama uyoga bila mpalilizi. Nyadhifa za wazazi wake zilimpokonya Tenga ushirika wa wazazi wake. Ile michezo yake na wazazi wake kabla ya chajio, yale matembezi ya kila Jumapili yote yakatoweka. Baba na mama wakawa wanarudi nyumbani baada ya saa nne usiku wakiwa wametoka kwenye masomo ya kuupigia msasa ujuzi wao; Jumamosi na Jumapili wana majadiliano na wanafunzi wenzao. Nyakati nyingine wazazi wote wawili walikuwa kwenye safari za kikazi. Nyakati kama hizi Tenga angepelekwa kwa shangazi ambako angekaa na kijakazi wake kwa wiki tatu; anaenda shuleni na kurudi huko huko kwa shangazi.

Wahenga walisema kwamba, akosaye la mama hata la mbwa huamwa. Pengo la malezi lililoachwa na wazazi wa Tenga Iilijazwa na walezi wengine wakiwemo vijakazi , shangazi, marika,walimu,majirani na hata vibonzo. Tenga alijifunza mengi kutokana na walezi hawa. Alifunzwa namna ya kupigana miereka kutumia ujanja kujitoa katika matatizo,kutumia maneno makali,kujihami alipochokozwa na wenzake, pamoja na mitindo mbalimbali ya kujinadhifisha. Mafunzo ambayo Tenga aliyapata hasa kutoka kwa marika yaliutia ila mwenendo na uhusiano wake na walimu. Darasani akawa anaishi kuvuruga masomo kwani kila mara angetenda kituko ili mwalimu na wanafumi waubaini uwepo wake. Vituko hivi vilisababisha kudorora kwa alama zake. Walimu wakajaribu kuurekebisha utundu wake lakini zikawa kama juhudi za mfa-maji. Tabia ya Tenga haikuwa ufa tena bali ukuta ambao ulihitaji kujengwa upya. Mkuu wa Idara ya Ushauri na Uelekezaji shuleni ilibidi ahusishwe. Akamhoji Tenga na kupambaukiwa kuwa vitendo vya Tenga vilikuwa na asili ambayo ilihitaji kuchunguzwa. Akampendekezea mwalimu wa darasa kuwashirikisha wazazi kalika kutafuta mbinu za kumwelekeza Tenga zaidi.

Bwana Mtanga na mkewe Zuhura walipoambiwa kuhusu hali ya Tenga walipigwa nu bumbuazi. Hawakuwa wameyawazia madhara ya kutoshiriki kikamilifu katika malezi ya mtoto wao. Mwalimu aliwaambia ya kwamba nusura Tenga ajiingize na wenzake katika matumizi ya dawa za kulevya Iakini akakataa na kusema kuwa hata babake hakujaribu kutumia kitu chochote. Wazazi waliona haya na kujilaumu. Hata hivyo walishukuru ya kwamba walimu waliyagundua matatizo haya kabla hayajaiangziniiza familia yao.

Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa kifungu.

  1. Bwana Mtanga na Bi. Zuhura:
    1. walimlea Tenga kwa kushauriana, walikuwa mashuhuri;
    2. walimlea Tenga kwa kuchangamkiana, walikuwa maarufu
    3. waliingiliana vyema na majirani, walipenda kusaidia
    4. waliingiliana vyema na walimu, walipenda kutoa.
  2. Utajiri wa wazazi wa Tenga ulitokana na:
    1. uwajibikaji wao katika shughuli zao
    2. kupata vyeo katika madaraja tofautitofauti
    3. kupata shahada na stashahada mbalimbali
    4. uwajibikaji wao katika taaluma zao
  3. Wazo kuu linalojitokeza katika aya ya nne ni kwamba:
    1. Jambo Iolote likifanywa bila ushirikiano huleta madhara
    2. Jambo lolote likifanywa bila kipimo huweza kuleta madhara
    3. Jambo lolole likifanywa bila utulivu huweza kuleta madhara
    4. Jambo lolote likifanywa bila mtazamo huweza kuleta madhara
  4. Kifungu kinaonyesha kuwa ukosefu wa malezi bora husababisha:
    1. kupigana miereka daima ili kupata maslahi
    2. kudhoofika kwa maadili
    3. kuharibu masomo darasani ili kuonekana kote
    4. kuharibika kwa urafiki
  5. "Tabia ya tenga haikuwa ufa bali ukuta abao ulihitaji kujengwa upya" ina maana;
    1. Tabia ya tenga ilikuwa imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kurekebishwa kikamilifu
    2. Tabia ya tenga ilikuwa imeharibika kabisa kiasi cha kuhitaji kushauriwa kikamilifu
    3. tabia ya Tenga ilihitaji kushughulikiwa kikamilifu
    4. tabia ya Tenga ilihitaji kutambuliwa kikamilifu
  6. Kwa mujibu wa kifungu. Idara ya Ushauri ya Uelekezaji inasaidia katika malezi kw
    1. kuwahoji vijana na kuwaita wazazi wao
    2. kutambua matatizo ya vijana na kuonyesha mbinu za kuwashirikisha
    3. kutambua matatizo ya vijana na kuangazia mbinu za kuyasuluhisha
    4. kuwahoji vijana na kuwaambia matatizo yao
  7. Kulingana na aya ya mwisho, wazazi wa Tenga
    1. hawakujua umuhumi wa kukaa karibu na watoto wao
    2. walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu wa walezi wao
    3. walipuuza umuhimu wa ushirika wa karibu na mtoto wao
    4. hawakujua umuhimu wa kukaa karibu na walezi wao
  8. Chagua jibu lipi linaloonyesha sifa za Tenga.
    1. mcheshi, mwenye kupenda wazazi
    2. mwenye mapenzi ya dhati anayelafuta kushirikishwa
    3. mchangamfu mwenye kupenda unadhifu
    4. mwenye msimamo imara, anayetafuta kutambuliwa
  9. Kisawe cha, ‘hakwenda nguu.’ ni:
    1. hakujitia kapuni
    2. hakujitia hamnazo
    3. hakufa moyo
    4. hakufa kikondoo
  10. Maana ya, ‘kujihami' kwa mujibu wa kifungu ni:
    1. kujitetea
    2. kujinasua
    3. kujihadhari
    4. kujizatiti

Majibu

  1. B
  2. C
  3. C
  4. A
  5. B
  6. A
  7. D
  8. B
  9. A
  10. C
  11. D
  12. D
  13. B
  14. A
  15. C
  16. D
  17. C
  18. D
  19. C
  20. B
  21. C
  22. D
  23. C
  24. D
  25. B
  26. C
  27. A
  28. C
  29. B
  30. D
  31. D
  32. B
  33. C
  34. D
  35. A
  36. B
  37. A
  38. D
  39. C
  40. A
  41. C
  42. D
  43. B
  44. B
  45. A
  46. C
  47. C
  48. D
  49. C
  50. A
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 1 2022.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students