Wednesday, 13 April 2022 06:30

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End of Term 1 Exams 2022 Set 1

Share via Whatsapp

QUESTIONS

Soma vifungu vifitatavyo vina nufasi 1 mpaku 15. Kwa kila nafasi umepewa majihu munne hapo. Juze pengo kwa kuchagua jawabu lifualo zaidi.
Umuhimu wa teknolojia ya kisasa _1_  maisha ya binadamu _2_  kupuuzwa _3_, _ 4__ sekta zilizonufaika pakubwa_5_ na uvumbuzi huu ni ile ya mawasiliano. Ilapo zamani mawasiliano _6_ katika matumizi ya mbinu kama vile_7_ upigaji wa magoma, kuwasha moto _8_ moshi angani _9_ kuwatuma wajumbe mbalimbali.

  1.                      
    1. ya
    2. wa
    3. katika
    4. kwa
  2.                  
    1. hauwezi
    2. huwezi
    3. haiwezi
    4. hayawezi
  3.                    
    1. kabisa
    2. tena
    3. vile
    4. kamwe
  4.                
    1. Baadhi ya
    2. kati ya
    3. miongoni ya
    4. mithili ya
  5.                    
    1. kutokana na
    2. kilingana na
    3. mintaarafu ya
    4. zaidi ya
  6.                  
    1. yalikuwa
      yamejikita 
    2. yangekuwa
      yalijikita
    3. yamekuwa
      yakajikita
    4. yanakuwa
      yamejikita
  7.                      
    1. ;
    2. _
    3. :
    4. ---
  8.                
    1. uliovusha
    2. iliyovusha
    3. uliyofusha
    4. uliofusha
  9.                
    1. japo
    2. halikadhalika
    3. angaa
    4. wala

Shama _10_ wazo la kujiunga na chuo cha kiufundi kuwa _11_ kujiendeleza maishani. Hata hivyo, aliolewa dhahiri shahiri kuwa _13_ usingepatikana vivi hivi tu bali bidii na uwajibikaji _15_ ulihitajika.

  1.                       
    1. aliiona
    2. aliuona
    3. alijiona
    4. aliliona
  2.                        
    1. nzuri
    2. njema
    3. lema
    4. zuri
  3.                        
    1. lingempa
    2. linampa
    3. litampa
    4. limempa
  4.                     
    1. jogoo la shamba haliwiki mjini
    2. mtaka cha mvunguni sharti ainame
    3. mchuma janga hula na wa kwao
    4. juhudi si pato
  5.                  
    1. wake
    2. wako
    3. wenu
    4. wao
  6.                
    1. wenye
    2. hiyo
    3. wenyewe
    4. ambao

Kuanzia nambari 16 mpaka 30. jibu kila swali kulinganu na maagizo uliyopewa. 

  1. Kiambishi ki-kimctumika vipi katika sentensi ifuatayo.
    Wanafunzi wale walikuwa wakizingatia nidhamu.
    1. Kuonyesha masharti. 
    2. Kuonyesha hali ya kuendelca.
    3. Kuonyesha jinsi ya kutenda.
    4. Kuonyesha vitendo vinavyofanyika pamoja.
  2. Kutokana na kitenzi vumilia tunapata sifa gani?
    1. Uvumilivu 
    2. Kuvumilia
    3. Vuma
    4. Vumilivu
  3. Andika wingi wa sentensi ifuatayo.
    Sonara alinifulia mkufu huu.
    1. Sonara walitufulia mikufu hii. 
    2. Masonara walinifulia mikufu hii.
    3. Sonura walitufulia mikufu hizi.
    4. Masonara walitufulia mikufu hii.
  4. Ipi ni sauti ghuna?
    1. b
    2. th
    3. sh 
    4. f
  5. Chagua ukanushaji wa sentensi ifuatayo.
    Bakari ameuchukua mkoba wake.
    1. Bakari hakuuchukua mkoba wake.
    2. Bakari hajauchukua mkoba wake.
    3. Bakari hauchukui mkoba wake.
    4. Bakari hatauchukua mkoba wake.
  6. ....................................ni mtu ambaye huwabobca watu mizigo kwa malipo.
    1. Dalali
    2. Megazega
    3. Mjumu
    4. Hannali
  7. Ainisha maneno yaliyoangaziwa katika sentensi ifuatayo.
    Nyumba yenu imejengwa vizuri lakini ile si thabiti.
    1. kivumishi kivumishi, kielczi
    2. kiwakilishi, kiunganishi, kiashiria
    3. kivumishi kiunganishi, kiwakilishi
    4. kielczi, kiunganishi. kiwakilishi
  8. Mtu unapotaka kupishwa njia husemaje?
    1. Simile
    2. Ashakum
    3. Samahani
    4. Hebu
  9. Akisami 5/7 kwa maneno ni
    1. subui tano
    2. humusi saba
    3. thumni tano
    4. saba kwa tano
  10. Chagua jozi ambayo hailingani.
    1. simba, shibli
    2. nzige, kimatu
    3. papa, kincngwe
    4. sungura, kinyempre
  11. Andika kauli ya kutendewa ya sentensi ifuatayo.
    Fundi alimshonea Shama kiatu kibandani.
    1. Kiatu cha Shama kilishonwa na fundi kibandani.
    2. Shama alishonewa kiatu kibandani na fundi.
    3. Kiatu kilishonewa kibandani kwa Shama na fundi.
    4. Fundi alimshoneshea Shama kiatu kibandani.
  12. Tegua kitendawili kifuatacho;
    Hausimiki hausimami.
    1. Moto 
    2. Mkoba 
    3. Moshi
    4. Mkulu
  13. Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
    1. Kibe ni kijana mpole: Yeye ni mwerevu darasani
    2. "Uwanja huu," akasema mwalimu una nyasi ndefu.
    3. Wakazi wengi wa mtaa huu ni wafanyabiashara
    4. Selina (yule wa runingani) ana sifa kochokocho.
  14. Kanda ni utepe wa kunasia sauti au picha.
    Kanda pia ni
    1. mfuko wa ngozi wa kuhifadhia vitu.
    2. namna ya chombo cha usafiri baharini.
    3. mtu mwenye tabia ya udanganyifu.
    4. kuivisha vitu kama mikate kwenye joko.
  15. Andika methali yenye maana sawa na hii
    Kikulacho ki nguoni mwako.
    1. ibilisi wa mtu ni mtu.
    2. Mla nawe hafinawe ila nizaliwa nawe.
    3. Zimwi likujualo halikuli likakumaliza.
    4. Dawa ya moto ni moto.

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40
Mwili wa mwanadamu hawezi kufanya kazi kama inayotarajiwa iwapo hauna afya. Watu wengine hudhani kuwa afya ni jambo la nasibu tu. Hawa huachilia miili yao kufanya kazi kama punda bila kujali maslahi yao. Mtu asiyejali rai yake huchakaa haraka na kuwa dhaifu.
Njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa mwilfuna nguvu na siha inayostahili ni kupitia kwa vyakula. Uzingatiaji wa lishe bora ni muhimu kwa afya ya mwanadamu. Lishe bora huurutubisha mwili na kuacha ukiwa katika hali nzuri. Maandalizi bora ya vyakula ni kuhakikisha kuwa vimeiva kabisa ili kuepuka maumivu ya tumbo na kasoro nyinginezo. Aidha, vyakula visivyoandaliwa vizuri humfedhesha mwenyeji mbele ya wageni wake.
Ulaji wa chakula haumaanishi kula bila breki. La, unamaanisha kula vyakula ambavyo vina manufaa kwa mwili yetu. Baadhi ya watu hula vyakula vyenye wingi wa mafuta, Mafuta mengi hatimaye huleta madhara hasa kwa mtu asiyefanya mazoezi ya viungo vya mwili Ulaji wa mayai kwa wingi pamoja na nyama ya kuchoma huweza kumletea mlaji matatizo ya kiafya. Vyakula hivi na vingine huhitaji kuliwa kwa vipimo.
Mikono haina budi kuwa safi kabla ya kuanza kula kwa wengine, kumwanikaida tu, hawatumii sabuni kamwe. Kukipakia chakula bila kuzingatia usafi huweza kusababisha uele wa waba. Isitoshe, maji yasipochemshwa huweza kusababisha maradhi haya. Ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha kuwa viwango vya usafi vimezingatiwa kila wanapotaka kula
Yapo maradhi mengine ambayo husababishwa na wadudu, Mfano wa haya ni malaria na malale, Ni vyema kuzingatia usafi wa mazingira yetu ili kuyaepuka magonjwa haya. Vitu vinavyovunda navyo visiachwe kuzagaa kila mahali ili kuwaondoa nzi wanaoweza kucheza magonjwa. Aidha, nyasi na vichaka vinufaa kufyekwa bila kusahau kuondoa mikobe na vidimbwi vya maji takat.
Uvutaji wa sigara na ulevi ni baadhi ya tabia ambazo huwaletea waja matatizo ya kiafya. Moshi unaovutwa una madhara mengi sio tu kwa afya ya mvutaji bali pia kwa walio karibu naye. Pombe humdhuru mnywaji kwa namna nyingi; kuna wale ambao hukumbwa na tatizo la ini. Miili ya hawa hushindwa kufanya kazi na hivyo wakaishia kutangulia mbele ya haki.
Mwili vilevile huhitaji mazoezi ya viungo ili kuweza kubaki katika hali nzuri ye afya na utendakazi. Baadiri ya watu hufanya mazoezi ya kukimbia asubuhi na jioni jioni. Wengine hutembea masafa fulani ili kama wanavyosema wenyewe kunyosha miguu. Wengi hununua baiskeli ili watumie nguvu kuziendesha; kusudi darnu ipate kuranda vizuri kote mwilini na viungo kunyooka. Baadhi hujinunulia vifaa vya kufanyia mazoezi nyumbani au kulipa ada ya kutumia sehemu zenye vifaa hivyo.
Rai zetu ni ngao zetu. Bila siha, sisi silolote si chochote. Mtu huwa kama gogo tu. Ni wajibu wetu kuzingatia na kufanya yote tunayoweza ili kuhakikisha kuwa siha zetu hazituponyoki.

  1. Chagua maelezo sahihi kulingana na aya ya kwanza.
    1. Mwili wa mwanadamu haufanyi kazi yoyote bila afya. 
    2. Afya ya mwanadamu ni jambo la nasibu.
    3. Afya huusaidia mwili kuendesha shughuli ipasavyo.
    4. Mwili wa mwanadamu unapochakaa madhara ya afya nzuri hujulikana.
  2. Kwa nini vyakula visipoivishwa vizuri huleta hasara?
    1. Vyakula hivyo hukosa virutubishi.
    2. Vyakula hivi haviwezi kutafunika.
    3. Mwili hushindwa kuondoa vyakula hivi.
    4. Husababisha shida za afya na kuleta aibu.
  3. Ulaji mzuri ni ule wa
    1. kutumia vipimo vidogo vya chakula.
    2. kutumia kipimo kikubwa cha vyakula.
    3. kutumia kipimo kifaacho cha chakula.
    4. kutumia kipimo chochote cha chakula.
  4. Kuhusu vyakula vya mafuta, mwandishi wa makala haya anapendekeza kuwa,
    1. wanaotumia mafuta mengi wafanye mazoezi.
    2. watu wasitumie mafuta katika vyakula.
    3. vyakula vyenye mafuta vitumiwe na watu wenye miili midogo.
    4. viliwe kwa wingi ili kuimarisha afya ipasavyo.
  5. Kwa baadhi, kunawa in kaida tu'kauli hii ina maana gani?
    1. Watu wote hunawa vizuri kabla ya kula.
    2. Wengine hunawa kimazoca tu bila kuwa makini.
    3. Wengine hunawa kwa kulazimishwa tu.
    4. Wao hunawa kwa njia ifaayo wakati wote.
  6. Mdudu anayeambukiza ucle wa malale huitwaje?
    1. Mbungo
    2. Mbu
    3. Parare
    4. Funza
  7. Sigara huwa na madhara yapi?
    1. Kuwaathiri hata walio mbali sana na mvutaji.
    2. Humwathiri mvutaji peke yake.
    3. Huwaathiri wengine badala ya mvutaji.
    4. Humwathiri mvutaji na walio karibu naye.
  8. Watu hununua baiskeli kwa sababu.
    1. kuimarisha afya zao.
    2. kufika kazini haraka.
    3. kuwabebea jamaa zao.
    4. kumaliza nguvu yao.
  9. Kulingana na aya ya mwisho.
    1. mtu asipokuwa na afya hugeuka kuwa gogo.
    2. afya ni silaha ya kujikinga na maadui.
    3. ni vyema kuzingatia njia mbalimbali za kuboresha afya.
    4. ni vizuri watu wanene watembee kuimarisha afya.
  10. Maana ya neno "huurutubisha' jinsi lilivyotumika ni
    1. huunenenpesha
    2. huustawisha
    3. huudhalilisha
    4. huutia mbolea

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia 41 mpaku 50
Juma alipiga goti huku machozi yakimdondoka njia nne nne. Mbele yake palikuwa na makaburi mawili. Waliokuwa wamelala mle hawakuwa na habari juu ya kihoro na simanzi ya aliyepiga magoti pule. Iala kwanza lilikuwa kongwe kiasi na lilikuwa limemca vichuka na magugu. La pili likionyesha upya kwani mashadu ya maua yaliyowekwa na wuombolezaji yalikuwa bado mabichi. Babake na mamake Juma walikuwa wamelazwa makaburini humu mtawalia.
Kwa Juma, maisha hayakuwa na maana tena. Alikuwa mwanafunzi wa miaka kumi na miwili na alikuwa katika darasa la saba. Hakuwa amchitimu kujitegemea na kukimu mahitaji yake. Aliokuwa akiwategemea sasa wamemwacha akiwa yatima. Hakuna yeyote ambaye ungelijaza pengo lililo achwu mu wavyelo wake. Zaidi ya haya alisononeka kuwapoteza wazazi wote wawili kwa kipindi cha miaka miwili tu. Ilaya yalikuwa kwake kama dondandugu lisilopona.
Kwa sasa Juma anayakumbuka mengi. Anakumbuka maisha ya babake. Alikuwajibaba zito na lenye sura jamala na siha nzuri. Baba mtu alikuwa na chake na alijiweza kiuchumi. Wengi pale mjini walimheshimu na kumstahi kutokana na uwezo wake huo. Aidha, alitunza familia yake vilivyo. Juma bakumbuki hata siku moja aliyokosu chochote alichohitaji kutoka kwa babake. Alikuwa mwenye bidii kazini mwake pia.
Walakini kama mja asiyckamilika, baba mtu alikuwa na taksiri moja. Aliyapenda maisha ya anusa na kufukuzia wasichana wadogo mlc mjini. Mamake Juma aliyajua fika haya. Alijaribu kuzozana ntuye ili aache tabia hii potovu. Lakini kila alipothubutu, mama mtu alifokewa na kukemewa kuwa anche upuuri wa wanawako. Akafika kufyata ulimi na kumwachia Molu uyaongoze maisha ya mumewe.
Hata hivyo, hakuna marcfu yasiyo na kikomo. Baada ya kuponda raha na vimanda si haba alianza kuugua. Maradhi yake yakawa na msururu. Mara alipata mafua yasiyopona, mara kucndesha mara maradhi ya ngozi. Haya yalimtia wasiwasi. Baada ya kukaguliwa na matabibu kadhaa alipatikana kuwa "ameumwa na mdudu" Hakuyaamini haya. Baba aliyekuwa na bushasha na mcheshi aliingiwa na upweke! na kutotaka kutangamana na yeyote hata jamaa yake.
Waliosema kuwa hakuna msiba usiokuwa na mwenzake hawakutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Maradhi haya yaliifilisi jamaa huku aing ang'aniwa kupata tiba. Wakaenda kwa waganga na waganguri, Waganga nao wakafidi tamu.
Muda si muda, mama naye akaanza kuugua. Baada ya uchunguzi akapatikana na ugonjwa sawa na wa bwanake. Ikawa ni kama mji umcrogwa. Baadaye babaye akaaga dunia na mamaye hakukawia sana. Akasalimu amri na kumfuta mumewe. Juma, kijana mdogo akaachwa na upweke.
Kama kawaida, mja hakosi neno. Wengi walisikika wakisema hili na lile kuhusu vifo hivi. Wengine walionera minong'ono lakini Juma alijua ukweli wa vifo vya wazazi wake

  1. Juma alipiga goti kwa sababu ya.
    1. makaburi yaliyokuwa yamemea vichaka.
    2. wazazi wale walikuwa makaburini,
    3. huzuni ya kufiwa na wazazi wote.
    4. kuweko kwa makaburi mawili,
  2. Ni kweli kuwa,
    1. mama alitangulia kufariki.
    2. baba alitangulia kufariki.
    3. wazazi walifariki wakati mmoja.
    4. baba na mama walifariki baada ya mwaka.
  3. "Babake Juma aliheshimiwa kwa kuwa,
    1. alikuwa mwenye sura ya kuvutia.
    2. aliturva familia yake vilivyo.
    3. alikuwa tajiri wa kutajika.
    4. alikuwa mwenye bidii kazini.
  4. Neno jingine lenye maana sawa na taksiri
    1. dosari
    2. huzuni
    3. raha 
    4. fujo
  5. Chagua sifa za babake Juma kulingana na kifungu
    1. mpenda raha, asiyejali familia yake.
    2. mwenye mali, anayejali maslahi ya wote.
    3. mwenye sura nzuri, asiyewajibika kazini. 
    4. mpenda anasa, anayelunza aila yake.
  6. Baba Juma alimfokea mkewe kwa kuwa,
    1.  mke alikuwa akifuata uvumi.
    2. mke alikuwa ukimwambia ukweli.
    3. mke alikuwa akimfuatafuata mjini.
    4. mke alitaka ushauri kutoka kwake.
  7. Maana ya kifungu ameumwa na dudu ni
    1. Aliambukizwa maradhi ya UKIMWI,
    2. Aliambukizwa maradhi ya kuendesha.
    3. Alifikiwa na wadudu ambao walimwuma.
    4. Alichokoza wadudu akapata maradhi
  8. Methali "Hakuna msiba usiokuwa na mwenzake inamaanisha,
    1. kumliwaza mgonjwa kulileta huzuni
    2. familia ya mhusika iliambukizwa maradhi ya baba.
    3. kuugua kwa mama kulimletea baba huzuni.
    4. ugonjwa wa mzazi ulifuatwa na matatizo mengine
  9. Maelezo yapi si sahihi kulingana na kifungu?
    1. Juma hakuelewa chanzo cha vifo vya wazazi.
    2. Majirani walijua chanzo cha vifo vya wazazi
    3. Mgonjwa alipotibiwa hakupata nafuu.
    4. Baba alipofariki mama hakuishi muda mrefu.
  10. Funzo la kifungu hiki ni kutva.
    1. Kufuata starehe sana hakuna mwisho mwema.
    2. Mara nyingi UKIMWI huambukizwa wale wanaojitunza vyema.
    3. Kubaki yatima kulimfanya Juma awajali wazazi
    4. Kuambukizwa maradhi huileta familia pamoja.

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Andika insha ya maelezo kuhusu.

MADHARA YA KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................

MARKING SCHEME

swahili marking scheme

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End of Term 1 Exams 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students