Wednesday, 29 June 2022 09:53

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 2 Opener Exams 2022 Set 1

Share via Whatsapp

Maswali

Soma vifungu vifuatavyo, Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne.
Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa.

Msimu wa mvua ya masika   1  , wakulima huwa tayari   2  makonde yao kwa upanzi. Siku chache baada ya mvua   3  kuanza, mbegu huanza   4   na kunawiri.     5     kunyeshakwa mvua    6     huja na madhara yake pia, Maji yaliyotuama huwawezesha mbu kuzaana kwa wingi. Halikadhalika, maji haya husomba taka kutoha kila mahali. Matokeo ya hali hii huwa na mlipuko wa maradhi kama   7   . Mvua ambayo kwa kawaida    8   baraka huleta baa chungu nzima, Janga la njaa huwa    9  macho.

1 A. yanapowadia B. inapowadia C. unupowadia D. inayowadia
2 A. wameiandaa B. wameziandaa C. wameuandaa D. wameyaandaa
3 A. yenjowe B. wenyewe C. zenyewe D. muenyewe
4 A. kustawi B. kuchipuka C. kukomaa D. kupogoa
5 A. Ila B. Ingawa C. Angalau D. Lakini
6 A kiholela B. kiyoloya C. kidindia D. kwa haraka
7 A. waba,kichocho
na malaria
B. malale,kichocho
na mkamba
C. homa,kichocho
na surua
D. malaria, kisonono
na kipindupindu
8 A. imekuwa B. ilikuwa C. inakuwa D. Ingekuwa
9 A. imewaangazia B. limewakodolea C. imewakodolea D. inawaangalia

 

Mwanadamu anapaswa kuwana   10    maishani;aelewe    11     utotoni ni mambo yapi hasa angependa kutimiza kabla ya kula chumvi. Akishayajua haya, basi hana budi kuanza kujiweka    12     kuyafikia haya. Bidii pia ni muhimu sana maishani. Wahenga walituasa kuwa     13     . Tusikae   14      na kuyangoja maisha kujipitia   15    mkondo wa maji.

10 A. ndweo B. matayo C. malengo D. upweke
11 A. tangu B. hadi C. mpaka  D. kabla
12 A. stadi za B. mikakati ya C. ujuzi ya D. mwelekeo ya
13 A. penye nia
pana njia
B. ushikwapo
shikamana
C. dhamira ni
dira
D. ajizi ni nyumba
ya njaa
14  A. ugeta B. kitwea C. ange D. tutwe
15 A. mithili wa B. Mfano ya C. mithili ya D. mathalani wa


Kuanzia swali la 16 hadi 30, jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.

 1. Tambus orodha inayoangazia nomino za jumla pekee.
  1. majiy,maziwa, mchanga, unga
  2.  watoto, nyumba, kabati, meza
  3. woga,wiva, furaha, hofu
  4. bumba, kigaro,genge, halaiki
 2. Ni sentensi gani iliyotumia kihusishi kwa kuonyesha sababu ya kutenda jambo?
  1. Nimealikwa shereheni kwa Maria
  2. Alinijbu swali hilo kwa dharau
  3. Halima anapendwa kwa utulivu wake
  4. Baba alikuja mkutanoni kwa baiskeli
 3. Maelezo yapi ni sahihi kuhusu ufundi?
  1. Timazi hutumiwa kupimia usawa wa ukuta
  2. Jiriwa hutumiwa kufungia parafujo
  3. Mizani hutumiwa kupimia urefu
  4. Filifili hutumiwa kushikia ubao unapokatwa
 4. Tegua kitendaili kufuatacho:
  Nimemwona bikizee amejitwika machicha
  1. samaki
  2. mvi
  3. ajuza
  4. mnazi
 5. Nahau ipi ina maana ya kupata tabu?
  1. Kula mwande
  2. Enda nguu
  3. Enda mserego
  4. Kula mwata
 6. Jumla ya silabi katika mshororo wa shairi ni
  1. vina
  2. inkisari
  3. mizani
  4. mazida
 7. Kamilisha kwa kiulizi kifaacho zaidi
  Unataka nikusaidie ______?
  1. aje
  2. pi
  3. je
  4. vije
 8. Tabia ya kuongeza yasiyo ya kweli ili kutilia mkazo katika habari fulani huitwa _____
  1. chuku
  2. tafsida
  3. sitairi 
  4. kejeli
 9. Ainisha maneno yaliyokolezwa wino katika, sentensi ifuatayo,
  Haijulikani mtoto huyo alienda wapi.
  1. Kiashiria, kiwakilishi
  2. Kiwakilishi ,kielezi
  3. Kiwakilishi,kulizi
  4. Kivumishi,kielezi
 10. Ukitaka watu wakupishe njia utawaambia
  1. makiwa
  2. simile
  3. kunradhi
  4. hebu
 11. . Andika wingi wa sentensi ifuatayo
  Fundi mzuri amenikarabatia redio yangu
  1. Fundi wazuri wamenikarabatia redio zangu
  2. Mafundi mazuri yametukarabatia redio zetu
  3. Fundi wazuri wametukarabatia maredio yetu
  4. Mafundi wazuri wametukarabatia redio zetu
 12. Neno mkeka lina sauti ngapi?
  1. Mbili 
  2. Tatu
  3. Tano
  4. Nne
 13. Mtu akipatwa na tatizo huwa sio mwisho wake kwani muda mfupi atalitatua na kuendelea, Jumuisha ujumbe huu kwa methali
  1. Kuteleza sio kuanguka
  2. Baada ya kisa mkasa
  3. Kuunguako ndiko kuteketeako
  4. Kuti kava kuanguka si ajabu
 14. Kati ya ala zifuatazo, ipi niya kupuliza?
  1. Fidla
  2. Zumari
  3. Udi
  4. Marimba
 15. Ungo ni gamba la kaa. Ungo pia ni
  1. Kubaleghe kwa wasichana
  2. vumbi la kitu kilichosagwa,
  3. habar isiyo ya kweli
  4. kifaa cha kupepeta nafaka

Soma kifungu kifuatacho kisha wjibu maswali 31 ~ 40

Bwana Toza alikuwa mkaramfu, hivyo hulka yake ilihusudiwa na mabarubaru wengi. Ila falau wangalijua kuchuja, wangeiga yaliyo mema kama mbinu zake za kuzalisha mali zisikowa na ila na kuyatema yasiyofaa. likuwa si ajabu kuwaona wakembe wengi wakitia mirija kwenye mikebe wakaishidilia tumbaku na kuzivuta 'toza’ zao kama Bwana Toza. Kwa kufanya hivyo waljihisi,eti wamefikia upeo wa kunasibishwa na Bwana Toza aliyetosha! Wakaamini kuwa maadamu toza zilitoka ulaya na wakazi
wa huko wana maendeleo makuu, basi kila aivutaye hatimaye angepata ufanisi. Hii ni imani ya jabu inayowakabili hirimu-kuiga, kikasuku, Mzungu akija na miondoko ya kikwao, humwiga wakidhani huo ustaarabu hasa,

Sku zilivyozidi kupita, Bwana Toza akawaambukiza insi wengi uvutaji wa toza akajiona kama mflame aliyetawala himaya nzima ya wavuta mitemba. Wengine waliianza tabia hii kidogo kidogo lakini baada ya muda wakakolewa nayo wakawa watumwa, Waliokuwa wakiivutia maliwatoni, sasa wakaivuta hadharani, wakatafuta viko hasa ili wainue hadhi zao maadamu wanasibishyve na Bwana Toza, Akawa ambari nao zinduna.

Azima ya kufikia kilele huwafanya wakwasi kutafuta sia. Bwana Toza akang'amua kuwa sasa ana wafuasi tosha. Kwa hivyo akaona kuwa lau angekiwania kiti cha ubunge cha eneo la kwao, angejinyakulia kiti hicho bila shida. Uchaguzi ulipotangazwa, akajitwika mzigo wa hugaragazana na wawaniaji wengine. Akawakusanya wafuasi wake wa tozani, Kwa moyo na robo moja, wakashauriana, kuhusu jnsi ya kuwakabili wapinzani wao.

Ukawa ndio mwanzo mkoko ualike maua. Alama ya chama chao ikawa kiko. Basi katika mikutano ya kampeni wakaviwasha viko vyao na huku vyafuka moshi wangeviinua na kupasua hewa kukinadi chama chao.

Mara kwa mara Bwana Toza alizoea kuamka bukrata ila mara nyingj alijihisi kuwa amechoka tiki na kuregea parafujo za mwili,kutokana na mavune ya kampeni na mtindi aliopiga kila uchao.

Siku moja karibu na mwisho wa majira ya kampeni, Bwana Toza alifika kuwahutubia wafuasi wake waliokuwa wameongezeka kupita kiasi. Alikuwa bado hajapata nafuu. Hata hivyo alijikakarmua kwa shida, huku akikohoakohoa. Huku mkono watetema alisema, ‘kikoo!” Halaiki ikajibu kwa mwangwi ‘ikooo~o! ‘Mara ya pili akajaribu kusema, ‘kik-oho—ho-kho--kho—”

Badala ya kiko kikawa kikohozi kisichopoa. Hakuendelea. Akaanguka kifudifudi. Wafuasi wake wakamkimbilia na kugundua kuwa alikuwa amepaliwa na pumzi, Wakajaribu maarifa yote ya huduma ya kwanza, walimvuvia, wakampepesa, wakambinyabinya kifua lakini wapi! Jitihada za ‘kuinusuru aushi ya Bwan Toza kitambo kile, Mambo yote yakafikia hatima ya ghafla.

Upasusi ulipofanywa ulionyesha kuwa Bwana Toza alimalizwa na toza. Pafu lilikuwa jeusi kama kaa lilininginiwa na masizi meng ajabu. Ripoti hi iliposomwa mbele ya wafuasi wake, wakaduwaa macho pima, Mitemba ikaanza kuwadondoka kutoka midomoni mmoja mmoja.

 1. Chagua kaulisahihi kulingana na aya ya kwanza:
  1. Sifa za Bwana Toza ziliwavutia vjana wote
  2. Bwana Toza likuwa mtu wa furaha
  3. Bwana Toza alijipatia mali kw njia haramu
  4. Mambo yote ya Bwana Toza yalifaa
 2. Wakembe walitia mirija kwenye mikebe
  1. ili wapate viko vya kuvutia tumbaku
  2. kwa maelekezo ya Bwana Toza
  3. kwa kuogopa kushike vikoa halisi
  4. ili wajiinganishe na Bwana Toza
 3. Kosa kubwa la vijana kulingana na makala
  1. kupuuza ustaarabu wao na kuiga hata yasiyofaa
  2. kuiga ustaarabu wakigeni pamoja na wa kwao
  3. kuvutiwa na maendeleo ya nchi za ulaya
  4. kuvuta viko vilivyotengenezewa ulaya,
 4. Wengine walianzia tabia hii kidogo kidogo lakini baada ya muda wakakolewa nayo wakawa watumwa’ Ni methali gani inayoambatana na kauli hii?
  1. Anayeonja asali huchonga mzinga.
  2. Abadi abadi kamba hukata jiwe.
  3. Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma.
  4. Mwanzo wa ngoma ni lele
 5. Kilichomifanya Bwana Toza kujitosa katika ulingo wa siasa ni
  1. kujitafutia sifa zaidi
  2. kujitafutia kipato zaidi
  3. kupata wafuasi zaidi
  4. kusumbuliwa na pesa
 6. Alama ya chama cha Bwana Toza ilikuwa
  1. sigara
  2. mtemba
  3. mrija
  4. vidole
 7. Uchovu wa Bwana Toza ulichangiwa na
  1. ugonjwa na kampeni
  2. uzee na ulevi
  3. uchovu na ulevi
  4. uchovu na kuamka mapema
 8. Moana ya‘kuanguka kifudifudi' ni
  1. kuangukia mgongo
  2. kuanguka bila hiari
  3. kuanguka kwa kishindo
  4. kuangukia tumbo
 9. Wafuasi watipojuzwakuhusu chanzo cha mauti ya Bwana Toza
  1. walipigwa na butwaa
  2. walichanganyiki wa sana
  3. waliogopa sana
  4. walipiga kamsa
 10. Kichwa mwafaka kwa makala haya ni
  1. Madhara ya ulevi
  2. Kifo cha mtu wa watu
  3. Madhara ya tumbaku
  4. Mbio za sakafuni huishia ukingoni

Yasoma makala haya kisha ujibu maswali 41 ~ 50

Adinasi walio na kasoro ya macho, miguu, masikio na kadhalika,ambao kwa bahati mbaya tunawaita vipofu, viwete na viziwi, Kwa kukosa majina bora zaidi, wanahitaji macho, miguu, nasikio na hata mikono yetu. Ni mara ngapi watu hao wamekosa watu wa kuwaongoza kuvuka barabarani au hata 'gurufuni? Mara ngapi watu waliolemaa miguu wameachwa tu waozee mahali pamoja bila kupata mtu wa kuwageuza hata waliapo kwa uchovu na maumivu? Ni mara ngapi wamekosa wa kuwapeleka ‘watakapo; wengine hata kunyimwa viti vya magurudumu hata vipatikanapo?

Kijumla, hasa katika Janibu za Afrika, wengi wanaowapata watoto waatilifu hudhani wamechomekwa mizizi au kuapizwa na wazee wao waliowatangulia, Huku wakinaonea wana buheri wa hamsa wa ishirini si ajabu kusikia kuwa mtoto alizaliva miaka kadhaa iliyopita na kufichwa hata mvunguni mwa kitanda katika humba klichofichama. Si ajabu pia kuwaona wata kam hata wakienda vilingeni kupungiwa wanao. Utawaona wakwasi wenye mashamba madal basari, mapana kama uwanja wa ahera wenye matumbo kama viriba na waendeshao magari ya kifahari wakiingia vilingeni mali mengi na mwanawe asipone, hali hii huzidisha tu dhuluma kwa muatilifu kwa kuwa sasa huonekana kama mjalaana.

Watoto waatilifu pia hubaguliwa kimasomo, Sijui aliyefichwa mvunguni atapata elimu lini? Vipi? Wao huchukuliwa eti kasoro waonekanazo nazo zitawakwaza masomoni. Hata serikal ikijaribu kuwatengenezea shule maalum, bado kunao wanaowanyima wango nafasi bila kujua kuwa Maulana humyima huyu hiki na kumpa kile. Kuwanyima fursa ya kuvitambua vipawa vyao ni dhuluma isiyomithilika.

Ajabu ni kuwa, waatilifu wakomaapo, wengi hukaa bila kupata wa kuwaoa au kuoa licha ya juhudi zao za kujimudu kiuchumi na kijamii. Wengi huchelea kubezwa eti wameoa 'wasiojiweza’. Jitihada za wengi kuwaoa watilifu zimevuliwa mbeleko na watu wa familia za

Kuchekwa kukebehiwa na kudharauliwa huwaletea simanzi waatilifu hawa na hujiona kara kizazi kisicho na thamani. Na ni nani aliyechagua au kuamua kuzaliwa katika hali aliyo kwayo? Ni nani aliyesema kuwa tusio na uatilifu ulio dhahiri tumekamilika? Je tukichungua kila mmoja wetu upungufu tulio nao kisha tudhulumive tutateta? Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mini kumbi. Waidha, mdharau biu hubiuka yeye.

 1. Mwandishi anaonekana kutokubaliana na
  1. majina mbalimbali wanayoitwa walemavu
  2. hali ya watu kupata ulemavu mbalimbali
  3. kuwa yapo mambo wasiyoyaweza waatilifu
  4. walemavu wanahitaji msaada wa wazima
 2. Kukosa kumsaidia mlemavu kuvuka njia ni ukosefi wa
  1. uzalendo
  2. huruma
  3. amani
  4. upole
 3. Gurufu kulingana na makala ni
  1. barabara yenye kuruba nyingi
  2. barabara pana za mijini
  3. baraste isiyo na shughuli nyingi
  4. barabara yenye magari mengi
 4. Njia bora zaidi ya kuwaauni wate wenye ulemavuni
  1. kuwapeleka ila mahal wanapotaka
  2. kuwanunulia chochote wanachohijati
  3. kuwaongoza kuvumbua namna ya kijikimu
  4. kuwahurumia kutokana na maumbile yao
 5. Kauli gani SI sahihi kuhusu mitazamo ya ulemavu barani Afrika?
  1. Ulemavu husababishwa na laana ya wazee
  2. Uailifu hutokana na kurogwa na wenye nia mbaya
  3. Uatilifu humalizwa kwa uganga wa kienyeji
  4. Ulemavu ni jambo la kudura tu
 6. Zifuatazo ni ishara za ukwasi zilizoangaziwa kwenye makala haya ila
  1. tumbo kubwa lililoshuka
  2. makonde makubwa
  3. kumiliki magari mengi
  4. magari ya kifahari
 7. Manufaa ya elimu kulingana na mwandishi ni
  1. utambuzi wa vipawa
  2. kutimiza haki za watoto
  3. kujipatia ajira nzuri
  4. kuyatawala mazingira
 8. Watu hawapendi kuwaoa au kuolewa na walemavu kwa
  1. kuogopa majukumu
  2. kuhofia kudharauliwa
  3. kuwaona kama kinyaa
  4. kutowaona kama binadamu
 9. Mtu asiyewesa kusikia huitwa
  1. bubu
  2. toinyo
  3. kibunye
  4. kiduko
 10. Msimamo wa mwandishi katika aya ya mwisho ni kuwa
  1. Mungu pekee ndiye mpaji na mtoaji wa yote tuliyonayo
  2. Kila mmoja wetu ana kasoro za walemavu
  3. Familia ni kikwazo katika ndoa za walemavu
  4. Wanyonge wanapodharauliwa huwa hawana thamani tena

INSHA

Endeleza insha ifuatayo ma kuifanya iwe ya kusisimua

Ilikuwa asubuhi ya kawaida kama nyingine. hakuna aliyetazamia kuwa tungekumbwa na mkasa kama huo

Mwongozo wa kusahihisha

 1. A
 2. D
 3. C
 4. B
 5. C
 6. A
 7. A
 8. D
 9. C
 10. C
 1. A
 2. D
 3. B
 4. A
 5. C
 6. D
 7. B
 8. A
 9. D
 10. C
 1. B
 2. D
 3. B
 4. A
 5. A
 6. C
 7. D
 8. A
 9. D
 10. D
 1. D
 2. B
 3. B
 4. C
 5. A
 6. A
 7. C
 8. D
 9. D
 10. C
 1. A
 2. D
 3. B
 4. C
 5. A
 6. B
 7. D
 8. A
 9. D
 10. C
Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Term 2 Opener Exams 2022 Set 1.


Tap Here to Download for 30/-
Why download?

 • ✔ To read offline at any time.
 • ✔ To Print at your convenience
 • ✔ Share Easily with Friends / Students