Monday, 13 September 2021 08:46

Insha - Class 8 Kiswahili Revision Notes

Share via Whatsapp


Insha za Methali

Hutahiniwa kwa namna tatu
Mwanzo, mada na tamati au kijalizio
Iwapo ni mada,jadili au fafanua ikiwa una uwezo
Iwapo ni tamati, jalizia kwa maneno uliyopewa
Iwapo ni mwanzo, endeleza kisa moja kwa moja
Simulia kisa kinachooana na maudhui

Methali za wema, Usaidizi wa Rafiki na Udugu

  • Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
  • Heri jirani wa karibu kuliko ndugu wa mbali
  • Kwendako mema hurudi mema
  • Wema hauozi
  • Jaza ya ihsani ni ihsani
  • Kumpoa mwenzio sio kutupa
  • Wawili si mmoja
  • Damu ni mzito kuliko maji
  • Damu ni damu si kitarasa
  • Zimwi likujualo halikuli likakwisha

MsamiatI na Mapambo

  • Saidia na kama
  • Maiti na jeneza
  • Kiko na digali
  • Sahani na kawa
  • Kinu na mchi
  • Alinitilia upendo/alinipiga jeki
  • Hali mbaya ya mtu
  • Mchafu kama kilihafu/fungo/kisafu
  • Dovuo mdomoni/mashavuni
  • Ngecha menoni/matongo machoni
  • Hali ya umaskini/unyonge/ugonjwa
  • Si lolote si chochote
  • Masikini hohehahe
  • Si wa koleo si wa mani
  • Kwake hakufuki moshi
  • Si hayati si mamati/si hai si mahututi
  • Hawana be wala te
  • Nikawa gofu la mtu/kifefe/fremu ya mtu
  • Anachungulia kaburi

Miundo ya maumbo

  • Ilikuwa dhahiri shahiri kuwa angeenda jongomeo
  • Nilipiga moyo konde nikampiga jeki Kwa hali na mali
  • Alinitilia upendo kwani akufaaye Kwa dhiki ndiye rafiki
  • Nilikumbuka alivyonipakatana kuniasa
  • Nilikuwa sina be wala te baada ya wazazi kwenda jongomeo
  • Matumaini yangu yalifufuka pindi nilipokutana na _______________
  • Machozi yalimlengalenga na kumbubujika kama maji mferejini

Kupokea methali

  • Waambao waliamba _____________
  • Wahenga hawakutupa ulimi wa kulazia walipoanga ______________
  • Chambilecho wahenga ______________
  • Wahenga hawakutoa ngebe walipokuli ________________
  • Yakini, wema ____________________

Tamati

  • Ndipo iliponiwia bayana kuwa ______________
  • Ndipo walipofutika mtimani kwangu ukweli wa methali _______________
  • Sitalifuta tukio hilo katika kumbukumbu zangu
  • Tanbihi-mwalimu ana uhuru wa kuongeza mengine

Methali za Kutohadaika

Chanzo cha matatizo
Alipovunja ungo/baleghe
Alipovuka kizingiti cha lango la shule, chuo kikuu ___________ maisha yake yaliingia ufa
Alopowachagua marafiki vichwa maji/nyamafu _______________
Alianza kujipalia makaa kama chachandu pweza
Mambo yalianza kumwendea tenge/shote/shoro/mvange/msobe msobe/upogoupogo
Kufilisika – hana be wala te , hana kazi wala bazi/hana hanani, fukara fukarike
Kushikwa – kuhaha na kugwaya, kutweta na kuhema, pumzi juu juu
Alitamani dunia ipasuke na kummeza mzima mzima
Kamasi ilimtonatona puani kama matone ya mvua
Alinaswa/tiwa vituku/pingu/lishwa kalenda
Aibu – shikwa na haya/soni
Iva uso
Vunja uso
Kichwa kifuani kama kondoo
Teseka – alikula mumbi/mavi/kwata
Alifunzwa na ulimwengu usiokuwa na huruma
Kitumbua kiliingia mchanga
Alitekwa bakunja/pubazwa na
Urembo/fedha/sura/jamali

Vipokezi vya methali
Yakini ________________
Taibu __________________
Ama kweli __________________
Chambilecho wahenga ________________________
Wahenga na wahenguzi ______________________
Nakubaliana na wazee wa kale _______________________

Utekaji nyara

Mapambo
Uzuri wa siku/mtu – siku ilikucha vizuri/upepo mwanana
Umande ulimeremeta metumetu kama nyota angani
Ndege walikorokocha na kughani lahani nzuri
Nwele zake za nyufa., kiuno cha nyigu, meno ya mchele, pangika kama lulu
Sauti nyororo kama ya ninga/mwewe/kinanda/hurulaini wa peponi
Mwendo wa dalji/twiga wa savanna
Kutosikia nasaha
Juhudi zangu za kumwonya/kumnasihi ______________________
Ziligonga mwaba/paramia mwamba/ambulia pang’anda/tupwa kapuni
Udekezaji – alimwengaenga/alimlea kwa tunu na tamasha
Kumwasa motto kulikuwa jambo tukizi/nadra/dimu
Akawa haskii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
Akatia maskio komango/nta/pamba
Kuwa sikio la kufa lisilosikia dawa/cha kuvunja ambacho hakina rubani

Methali Zinazoonya Kuhusu Tamaa na Uzuri wa Nje

Tamaa
Hamu kubwa ya kupata kitu, jambo, au hali Fulani
Visawe – uchu, ashiki, shauku, hamu, ari, nia, hanjamu, nyege, ukware, ghaidhi,
raghba

Methali za tamaa
Tamaa mbele mauti nyuma
Mkamia maji hayanywi, akiyanywa humsakama koo
Mwenye pupa hadiriki kula tamu
Mpanda farasi wawili hupasuka msaba/mwaranda
njia mbili zilimshinda fisi
Mwangata mbili moja humponyoka
Mchovya asli hachovyi mara moja
Mtaka yote huksa yote
Usiache mbachao kwa msala upitiapo

Methali za uzuri wa nje
Uzuri wa mkakasi ndanikipande cha mti
Sihadaike na rangi tamu ya chai ni sukari
Nyumba nzuri si mlango, ingia ndani
Kikulacho ki nguoni mwako
Ibilisi wa mtu ni mtu
Uzuri wa kuya ndani mabuu
Vyote viowevu si maji


Maudhui
Marafiki hadaa – ndumakuwili/mzandiki
Kutoaminiana katika ndoa
Ahadi za uongo – mchezo wa karata
Urembo ambao ni handaa



Insha ya Mjadala

Mjadala ni mazungumzo baina ya watu kuhusu mada au hoja kuu upande mmoja hupinga huku mwingine ukiunga mkono
Huhusu mazungumzo juu ya mada Fulani
Mfano:

  • Maisha ya mashambani ni bora kuliko y mjini
  • Teknolojia ina madhara mengi kuliko faida

Huhitaji mtahiniwa kuunga mkono hoja moja na kasha kuipinga katika aya inayofuata au kuunga mkono na baadaye kuzipinga hoja zake.
Kuna sehemu nne kuu

  • mada
  • utangulizi
  • mwili
  • tamati-kutoa kauli na ushauri

Mada huandikwa kwa herufi kubwa kulingana na swali
Utangulizi huhusu kufafanua mada na kutolea mifano
Mwili huhitaji kufafanuliwa kwa hoja
Kila hoja iwe katika aya yake
Hitimisho mtahiniwa huhitajikakutoa changamoto au ushauri

Kuna namna tatu za kuandika insha hii

  • kuunga na kupinga katika aya moja
  • kuunga mada mkono na baadaye kuipinga
  • kuipinga mada na baadaye kuiunga mkono

Usiandike chini ya hoja sita
Toa msimamo wako kwa mwandishi
Insha hizi hutumia viunganishi vya kuongezea

  • Licha ya
  • Aidha
  • Fauka ya
  • Zaidi ya
  • Pia

TEKNOLOJIA
Ni maarifa ya kisayansi yaliyowekwa katika matumizi ya vifaa, vyombo, mitambo na zana mbalimbali.
Teknolojia inaweza kutumika kwa njia ainati

  • Mawasiliano
  • Utafiti wa kisayansi
  • Usafi na afya ya mwili
  • Usafiri
  • Kilimo na ufugaji
  • Michezo na mashindano
  • Elimu
  • Biashara
  • Kutalii anga za juu

Mawasiliano

Vyombo vya mawasiliano kama tarakilishi, magazeti, simu

  • Hutupasha habari
  • Hutuepusha na maafa
  • Kuelimisha na kutumbuiza Kiingiacho mjini si haramu Kipya kinyemi kingawa kidonda

Utafiti

Wataalamu wamevumbua/wamegundua dawa za dwele
Mashine/mitambona vyombo vya kurahisisha kazi
Mitambo ya kuchunguza hali ya anga
Dawa za kuzuia mimba
Ukiona vyaelea vimeundwa

Elimu

Vyombo na vifaa vingi hutumiwa shuleni
Mitambo na vifaa vya utafiti
Matumizi ya mitandao
Kanda za video
Elimu ni bahari
Elimu haitekeki

Usalama

Zana za vita hutumiwa hutulinda dhidi ya maadui
Donge nono hupatikana baada ya kuuza vifaa
Nyua za umeme na ving’ora
Tahadhari kabla ya hatari

Kilimo na ufugaji

Pembejeo-mbegu, mbolea, dawa
Mashine za kulimia, kunyunyuzia maji
Mashine za kukama ng’ombe
Ukiona vyaelea vimeundwa
Tembe na tembe huwa mkate

Usafiri

Vyombo vya usafiri vya majini, angani na nchi kavu
Huenda kwa kasi ya umeme
Huokoa wakati
Ngoja ngoja huumiza matumbo

Madhara ya teknolojia

  • Huwafanya watu kuwa wazembe Chanzo cha mmomonyoko wa maadili
  • Hufundisha ulevi, ulanguzi wa dawa za kulevya
  • Hulemaza akili na fikira
  • Huchangia kutupilia mbali kwa tamaduni na desturi

Tamati

  • Ningependa kuwajuza kuwa ______________________
  • Ningeomba sote tupinge kwa jino na ukucha _______________________
  • Tusiwe kama chachandu kwa kujipalia makaa kwa ___________________________


Insha ya Masimulizi

Michezo

Michezo ni jumla ya shughuli za kujifurahisha, kujichangamsha,kujiburudisha au kupoteza wakati
Kuna michezo ainati kama vile

  • Kandanda
  • Mpira wa vikapu
  • Voliboli
  • Naga
  • Magongo
  • Riadha
  • Sarakasi/viroja

Riadha

Ni jumla ya michezo ya viungo vya mwili kama kukimbia, kuruka
Kuna mbio za masafa

  • Mafupi-mita 100, 200, 400
  • Kadiri-mita 800, 1500, 3000
  • Marefu-5000, 10,000, na mbio za nyika
  • Kuruka viunzi na maji
  • Kutupa tufe/kijisahani
  • Kubururana kwa kamba

Msamiati

  • Tufe
  • Mzingo
  • Nusu mzingo
  • Vijiti
  • Safu za kukimbilia
  • Wapasua hewa

Kandanda/kambumbu/soka /gozi/mpira wa miguu

  • Hushirikisha timu mbili
  • Mavazi ya wachezaji-jezi, kaptura, soksi
  • Viatu vya wachezaji-ndaruga, njumu
  • Uwanja wa michezo unaitwa uga/uchanjaa
  • Golikipa-mlinda lango/ mdakaji/mnyakati
  • Wachezaji wa ngome-walinzi/defense
  • Wachezaji wa kiungo
  • Kipindi cha lala salama/cha pili
  • Kadi ya manjano/nyekundu
  • Mshindi/mshinde
  • Mchuano/kinyang’anyiro/kindumbwendumbwe

Mapambo na maumbo

  • Uwanja/uga/uchanjaa ulijaa/ulifurika
  • Jiwe lisingeanguka ardhini
  • Shangwe, vifijo, vigelegele na nderemo vilihinikiza hewani
  • Ngome yao ilikuwa dhabiti mithili ya ukuta uliojengwa kwa zege
  • Wapasua hewa walihema na kutweta
  • Mithili ya mbwa aliyenusurika kumezwa na chatu
  • Kikorombwe cha mwisho kilipopulizwa
  • Alipiga zinga kimo
  • Cha mbuzi hadi ______________
  • Nilimvisha kanzu/kupiga tobwe
  • Mpira ulianza kwa kasi ya umeme
  • Mpira uludanadana wavuni

Methali

  • Hayawi hayawi huwa
  • Hauchi hauchi unakucha
  • Kutangulia si kufika
  • Subira huvuta heri

Mada

  • KINYANG’ANYIRO CHA KUKATA NA SHOKA
  • MECHI YA KUSISIMUA
  • KIPUTA CHA KIPEKEE
  • MECHI YA KUKUMBUKWA

Mikasa

Mikasa ni matukio au mambo ya kutisha yanayotokea kwa ghafal pasi ya kutarajiwa
Matukio haya yanaweza kuleta maafa, masaibu na majonzi
Mikasa hii inaweza kuwa ya moto, milipuko ya bomu, zilizala, mafuriko, ajali barabarani, mlipuko wa volkano na maporomoko ya ardhi
Yanayopaswa kuzingatiwa kwa masimulizi ni

  • Wakati wa mkasa
  • Mahali pa tukio
  • Jinsi tukio lilivyotokea
  • Kushiriki kwa msimulizi
  • Shughuli za uokozi

Msamiati na mapambo

Kelele-mayowe, kamsa, usiahi
Mlipuko-mfyatuko, mwatuko, mshindo, ngurumo
Vilio-shake, kusinana, kikweukweu, kwikwikwi, mayowr
Mochari-makafani, ufuoni,
Ving’ora vya ambulensi na makarandinga
Vifusi na majivu katika majengo
Manusura na majeruhi
Huduma ya dharura
Vukuto la moto
Helikopta za kijeshi na shirika la msalaba mwekundu
Mabehewa(mabogi) yalitapakaa
Gari liliyumba yumba/lilipiga danadana
Taharuki na hekaheka
Kuuputa moto kwa matagaa
Cheche za moto zilitanda kama fataki
Paparazi walizuka/walitokea ghafla bin vu kama mizuka
Upepo ulivuma kwa ghamidha na ghadhabu
Waja walipiga mbizi ili kujinusuru
Gari liligeuzwa likawa ganda tu
Ngeu ilitapakaa na kuzagaa kote
Mizigo ilfyatuka na kuwalenga wapiti njia
Ving’ora vilihinikiza/vilitanda/vilishamiri kote
Mavundevunde ya moshi yalitanda kote
Joto lilisambaa na kuzagaa
Vilikuwa vilio si vilio, majonzi si majonzi, zogo si zogo

Methali

  • Chelewa chelewa utampata mwana si wako
  • Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
  • Ngoja ngoja huumiza matumbo
  • Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo
  • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
  • Juhudi si pato

Vihisishi vya majuto na mshangao

La haula la kwata !
Yarabi maskini!
Ole wangu!
Masaalale!
Lo!

Uasidizi

Walitupiga jeki
Niliwatilia upendo
Niliwapa mkono
Tulisaidiana kama kiko na digali
Maiti na jeneza
Kinu na mchi

Tamati
Hakika, hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
Daima dawamu sitalisahautukio hilo
Matukio hayo hayatafutika kutoka tafakulini mwangu
Ninapokumbuka kisa hicho, machozi hunitiririka njia mbilimbili

Huzuni

Insha humhitaji kuelezea kisa kinachoonyesha huzuni na woga

Insha nyingi huhusu mikasa au masaibu kwa watu
Visawe vya mikasa ni balaa, janga , balaa, baa, visanga
Mikasa yote hutokea kama ajali

  • Zilizala
  • Ajali barabarani au angani
  • Mlipuko wa bomu
  • Ukame
  • Maporomoko ya ardhi
  • Moto Ugaidi

Yanayozingatiwa mahali pa mkasa

  • Jinsi tukio lilivyotukia
  • Kushiriki kwako
  • Uchunguzi na matokeo

Tanbihi : mahali pa tukio – hotelini , mwituni, ofisini, kituo cha mafuta, kiwandani,
shuleni, dukakuu, barabarani, ufuoni mwa bahari, chumba cha maabara

Mapambo
Mlipuko – mfyatuko, mwatuko, mngurumo,
Ulikuwa mlipuko wa kuatua moyo/mtima, kushtua, kuogofya, kutisha
Ulikuwa mlipuko wa jiko la gesi/umeme/gari/bomba la mafuta
Kelele: usiahi, unyonge, kamsa, ukwezi, mayowe, ukwenje
Vilio vya –kusinasina, cha shake, kikweukweu kwikwikwi
Iwapo ni bomu, moto, ajali ya ndege
Moto ulirindima na kutatarisha majengo
Mabiwi/mashungi ya moto
Mavunde/mawingu ya moshi yalitanda kote
Vukuto la moto liliongezeka badala ya upepo kuvuma kwa hasira/ghamidha/hamaki/ghadhabu
Nilijitoma ndani ya nyumba kuwanusuru
Nahodha hodari haogopi moto
Kwa muda wa bana banua sehemu ile ikawa kama tanuri/joko/jehanamu
Jingo hilo liligeuzwa na kuwa majivu
Moto/nari ilifakamia majengo kama nzige wavamiavyo shamba la mihigo
Muda si muda, muda kiduchu, kutia na kutoa, fumbo fumbua,bana banua, kuku
kumeza
Punje paka kunawia mate, punda kunawia mavumbi,
Wengine walichomeka kiasi cha kutotambulika
Vilio vilinywea na sauti kuwapwelea
Tulipirikana na kupitana katika juhudi/hekaheka/pilikapilika za kuuputa moto
kuwaokoa wahasiriwa
Huzuni

Mikasa kwa jumla
Milio ya ving’ora vya makaradinga ya polisi, ambulensi, magari ya zima moto _____ tanda/tamalaki/tawala anga
Manusura/mahututi/majeruhi walipelekwa hospitalini/zahanatini
Walipewa hudum ya kwanza/ya dharura
Wafu walipelekwa mochari/ufuoni/makafari
Paparazi walizuka kama mizuka na kupeperusha picha sawia na matukio
Wanahabari walitangaza matukio ya mkasa redioni/runingani/magazetini
Wengine walisali/walipiga dua zisizoeleweka
Kwa nyota ya jaha/bahati ya mtende/kwa sudi wasamaria wema msalaba mwekundu wanajeshi zimamoto wakasaidia kuokoa
Basi lilipiga danadana na kuanguka bondeni ziwani/baharini
Tulifanya wanguwangu/himahima/chapu chapu/yosa yosa/ hala hala/mwendo wa arubili
Bila shaka tukio hilo halitafutika moyoni/sitalisahau daima dawamu
Niltamani ardi inimeze mzima mzima
Nilitamani kulia nikacheka nikalia
Machozi yaligoma

Methali
Ngoja ngoja huumiza matumbo
Chelewa chelewa utampata mwana si wako
Fimbo ya mbali haiui nyoka
Heri jirani wa karibu kuliko ndugu wa mbali
Akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki
Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo
Mja hakatai wito hukataa aitiwalo
Ajali haina kinga wala kafara
Tahadhari kabla ya hatari
Nahodha hodari haogopi moto

Furaha

Furaha inaweza kutokana na matukio mbalimbali kama vile

  • Sherehe –harusi
  • Siku ya kuzaliwa
  • Mahafali
  • Siku kuu ya krismasi
  • Kwenda ughaibuni
  • Matokeo mazuri ya mtihani

Mada
Siku ya siku
Akidi ya kufana
Sherehe ya kukata na shoka
Siku ya ndovu kumla mwanawe
Shamrashamra za
Msamiati na mapambo
Maua ya kila nui/ainati – asmini ,mawaridi afu, nangisi
Ukumbi wa mahema , jumba kubwa ,uwanja
Vipasa sauti/mikrofoni –vilihinikiza /sheheni
Muziki wa kuongoa ongoa ulitamalaki katika anga
Vyakula – mapochopocho/maakuli yaliyotishia kuangusha meza
Vinywaji vya kila jamii yalipenyeza kisirisiri
Mkalimani/mtarijumani alitafsiri haya yote
Kiume – mtanashati
Kike – mlibwede, spoti , mrembo kama mbega
Binti alikuwa mrembo mithili ya hurulaini aliyeasi/toka peponi
Alitembea kwa mwendo wa dalji/mwendo wa twiga wa savanna
Mwanaume mrefu njorinjori /mrefu kama unju/weusi kama kaniki
Udohoudoho , chipsi, bisi, kripsi
Waja walisakata rumba/dansi/tibwirika kwa miondoko
Msafara /mlolongo wa mashangingi
Walikula kiapo/yamini/vishana pete huku shangwe
Walipigana pambaja
Pofushwa na vimulimuli vya wapiga picha
Waja walijaa furifuri
Ilikuwa dhahiri shahiri kuwa ningefua dafu
Nilidamka wanguwangu kwa kuubwaga mgolole wangu na kuanza hamsini zangu
Kuche kusiche hatimaye kulikucha
Amka bukrata kichea
Niliamka asubuhi ya Mungu
Waja walisalimiana kwa furaha na farahani
Furaha sufufu ilinitinga si kidogo
Vyakula vya kunoga na kuhomolewa viliandaliwa na wapishi wajuzi
Vicheko vilipamba moto jari moja
Watu walichangamka na kukaramka kwa bashasha
Nilivalia meli zangu mpya zilizometameta kama mbalamwezi
Utamu wa malaji ungemfanya mtu kuramba viwiko vya mkono

Methali
Hauchi hauchi huwa
Hayawi hayawi huwa
Siku njema huonekana asubuhi
Baada ya dhiki, faraja
Mtu ni watu
Mgaagaa na upwa hali wali mkavu

Tashbihi
Shirikiana kama kinu na mchi, kiko na digali, soksi na kiatu
Lazima kama ibada
Kawaida kama sharia
Bidii kama mchwa ajengaye kichuguu/kishirazi/kidurusi
Bidii za msumeno ukerezao mbao
Bidii ni duduvule agatoye gogo la mti



Kumbukumbu

Kumbukumbu ni taarifa au rekodi zilizoandikwa na kuhifadhiwa
Anayeandika ni katibu au karani
Kiongozi wa mkutano huwa mwenyekiti au naibu wa mwenyekiti
Kumbukumbu ni maoni ya wote;hivyo basi katibu hafai kutoa hisia zake mwenyewe
Sehemu muhimu za kumbukumbu ni

  • Mada/kichwa
  • Mahudhurio
  • Ajenda za mikutano
  • Thibitisho

Mada/kichwa

  • Huwa na jina rasmi linalotambulisha shirika, kundi, kampuni
  • Huwa na tarehe, mahali na wakati(saa)
  • Kichwa kindikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari
    Mfano
    KUMBUKUMBU ZA MKUTANO WA CHAMA CHA MAZINGIRA WA TAREHE 2 MEI 2010 KATIKA
    UKUMBI WA HOTELI YA MAJIMBO SAA MBILI ASUBUHI

Mahudhurio

  • Huonyesha majina ya waliohudhuria, waliokosa kuhudhuria na waliotuma udhuru(sababu) ya kutohudhuria
  • Huonyesha walioalikwa
  • Majina ya wanajopo/wanakamati/wanachama yafuate vyeo
  • Baadhi ya vyeo ni kama vile
    • Mwenyekiti au naibu mwenye kiti
    • Karani au naibu/katibu
    • Katibu mwandamizi/mratibu
    • Mhazini-anayetunza mali ya shirika au kampuni

Ajenda

  • Hizi ni hoja muhimu zinazojadiliwa k.v kufunguliwa kwa mkutano
  • Kusomwa kwa kumbukumbu za mkutano uliotangulia
  • Hoja nyinginezo zitategemea nia ya mkutano au shirika
  • Kufungwa kwa mkutano-taja anayeomba na wakati

Mapambo

  • Mkutano ulifahamishwa kwamba _______________
  • Ripoti ilitolewa kuwa ___________________
  • Mwenyekiti aliwaarifu/aliwajuza kuwa _____________________
  • Mkutano uliamua kwamba ___________________
  • Walipatana kwamba __________________
  • Kikao kilielezwa kuwa ____________________

Thibitisho
Sehemu hii huwa na sahihi na tarehe

Baada ya kumbukumbu kusomwa na kuthibitishwa katika mkutano unaofuata mwenyekiti na katibu hutia sahihi

Umbo la kumbukumbu

Mada:herufi kubwa
Waliohudhuria
_____________________
_____________________
_____________________

Waliotuma udhuru
_____________________
_____________________
_____________________

Wasiotuma udhuru
_____________________
_____________________

Waalikwa
_____________________
_____________________

Ajenda
_____________________
_____________________
_____________________

KUMB CCM1 1/02:

KUMB CCM 2 1/02:

Thibitisha
Mwenyekiti ________________________ (sahihi)
Tarehe ___________________________
Katibu ____________________________(sahihi)
Tarehe ___________________________



Insha ya Mazungumzo

Mazungumzo ni maongezi mahojiano au malumbano baina ya mtu na mwingine au kundi moja na jingine

Mazungumzo haya yanaweza kuwa
Poroja/soga/domo-ni mazungumzo ya kupitisha wakati
Kutafuta ujumbe maalum-hufanyika kwa njia ya mahojiano
Kumdadisi au kumwelekeza mtu-baina ya mtu aliye na tajriba na Yule anayetaka msaada

  • Kila mmoja hupewa nafasi ya kuzungumza
  • Mhusika mmoja asichukue nafasi kubwa
  • Tumia alama za uakifishaji ainati
  • Sharti pawe na hali ya kuchachawiza
  • Vitendo viweze kuandikwa katika alama za mabano
  • Fani za lugha zitumuke ili kuleta uhondo katika mazungumzo
  • Lazima pawe na maagano au maelewano
  • Tangaza msimamo iwapo ni mahojiano
  • Hatua

Mada/kichwa
Huandikwa kwa herufi kubwa na kupigiwa ,mstari
Mfano

MAZUNGUMZO BAINA YA DAKTARI NA MGONJWA
Maudhui-hili ni lengo au kusudi la mazungumzo
Msamiati utategemea lengo la mazungumzo
Vitendo na ishara-haya yataandikwa katika mabano mfano: (akiketi, akilia, wakibisha, akicheka)
Alama za uakifishaji
Koloni( : )huandikwa baada ya jina au cheo cha mtu
Alama za dukuduku ( -------------)kwamba mazungumzo yanaendelea
Parandesi au mabano ()
Kubana maneno ambayo hayatasemwa
Alama ya hisi ( ! ) hutumiwa pamoja na viingizi kuonyesha hisia
Mfano: yarabi maskini!



Insha ya Maelezo au Wasifu

Hii ni insha inayotoa maelezokuhusu jambo, mahali au kitu Fulani

  • Insha hii hueleza, huarifu, huburudisha au hutahadharisha
  • Mwandishi asiandike chini ya hoja sita
  • Tumia viunganishi unapounganisha mawazo katika aya au unapoaanza aya nyingine
  • Tiririsha mawazo ili pawena mtiririko na mshikamano
  • Katika tamati toa ushauri kwa makundi mbalimbali
  • Mwandishi anaweza kutoa msimamo wake kuhusu hoja Fulani

FAIDA ZA ELIMU

  • Elimu ni taaluma au mfuo wa mafunzo yanayofundishwa katika jamii zetu
  • Elimu inazo faida anuwai
  • Elimu huondoa ujinga akilini
  • Mja hupata maarifa, ujuzi na hekima
  • Mwanafunzi hutambua mambo tofauti
  • Humakinika katika mambo ayafanyayo
  • Elimu ni bahari na pia habari
  • Aliyeelimika huweza kuishi na wengine
  • Mtu hujiheshimu na kuheshimu wengine
  • Husaidia kudumisha amani, umoja na upendo baina ya watu
  • Kichango kuchangizana
  • Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu
  • Ni daraja la kutuvusha katika umaskini
  • Waja hutia bidii za mchwa ili kufaulu maishani
  • Humwezesha mtu kuhitimu katika taaluma Fulani
  • Uhawinde hutokomea kama umande nyasini wakati wa jua la asubuhi
  • Hurahisisha mawasiliano Baina ya mtu mmoja na mwingine au baina ya mataifa
  • Hujifunza mengi kwani kuishi kwingi kuona mengi
  • Aliyesoma hutalii nchi nyingi
  • Kuhifadhi siri
    Elimu humwezesha mja kusoma uumbe kutoka katika barua au arafa akiwa pekee
  • Huchangia kuwepo kwa maendeleo
  • Serikali hujenga shule,vyuo na miundo msingi mingineyo ya elimu
  • Taasisi mbalimbali huboresha mitaala ya ufundishaji
  • Hufanikisha utafiti, utumiaji wa teknolpjia mpya na mitambo mbalimbali

Elimu ni irithi

Elimu ni mali ambayo haiteki
Ni almasi inayostahili kuchibwa na mtoto yeyote mwandilifu
Zamani watu waliridhi mashamba na mifugo
Elimu ni silaha na nguzo muhimu na madhubuti

Methali

Elimu ni bahari
Elimu ni taa, gizani huzagaa
Elimu ni ali ambayo adui hawezi kuiteka
Elimu maisha si vitabu

Viunganishi na mapambo

Isitoshe, elimu ni ,ali ambayo adui hawezi _____________________
Zaidi ya hayo, humwezesha mja kuhitimu _____________________
Hata hivyo, kuna wale wanaoitumia __________________________
Aidha, limu hurahisisha mawasilia ___________________________

Nahau

Tujifunge masombo/nira/kibwebwe ili ________________________
Tujikaze kisabuni _________________________
Tusiwe pweza wa kujipalia makaa kwa kutoelimika _________________________
Tujifunge masombo mithili ya _____________________ duduvule atoboaye gogo/mchwa ajengaye kichuguu

Tamati
Ningependa kukunja jamvi kwa ____________________________
Ninapofikia tamati
Jua linapoaga mikalatusi
Ninatia kitone nikitoa lulu kuwa



Barua Rasmi

Pia huitwa barua ya kiofisi
Huandikwa kuhusu jambo rasmi
Huandikwa ili

  • Kuomba nafasi ya kazi
  • Kuomba nafasi za masomo shuleni au chuoni
  • Maombi ya msaada kutoka kwa serikali
  • Kuomba msamaha au radhi
  • Malalamishi kuhusu jambo Fulani

Barua rasmi ina sehemu zufuatazo

  • Anwani
  • Anwani mbili – ya mwandishi na ya mwandikiwa
  • Anwani ya mwandishi huandikwa tarehe
  • Kianzio
    Sehemu hii huandikwa bwana (BW) au bibi (BI), Mkurugenzi mkuuu, mwalimu mkuu
    Mtajo
    Ni kichwa cha barua ambacho huashiria lengo au madhumuni kwa ufupi
    Kumbukumbu – KUMB
    Mintarafu – MINT
    Kusudi – KUS
    Kuhusu – KUH
    Yahusu – YAH
    Kichwa cha barua rasmi hupigiwa mstari
  • Mwili
    Huelezea zaidi kuhusu kusudi ya barua na lengo hasa kuandika barua
    Mtahiniwa huhitajika kuelezea kuhusu Elimu yake
    Wasifukwani haambatanishi stakabadhi zozote zile
    Tanbihi
    Insha yoyote ile lazima itimize ukurasa na nusu
  • Tamati/mwisho
    Humalizwa kwa
    Wako mwaminifu
    Sahihi
    Jina

Mtindo wa barua rasmi

SHULE YA MSINGI
YA LIZAR,
S.L.P 93,
NAIVASHA,
NOVEMBA 18, 2015.

MWALIMU MKUU,
SHULE YA UPILI YA ALLIANCE,
S.L.P 2003,
KIKUYU.
Kwa Bwana/Bi – kianzo

mtajo-MINT: NAFASI YA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA

mwili

hitimisho –
wako mwaminifu

Msamiati

Nina furaha kukuandikia __________________
Ninasikitika ninapokuandikia waraka _________________
Ningependa kuchukua fursa hii _____________
Kwa mujibu wa ilani ______________________ katika gazeti, runinga, mabango
Shule yako imetajwa na kutajika katika _________________ michezo, elimu, bidhaa bora
Shirika/kampuni imeipa kipaombela swala la _____________________
Nina nidhamu na taadhima ya hali ya juu
Vyeti vyangu pamoja na wasifu vimeambatanishwa na waraka
Nitakuwa kielelezo dhabiti kwa wenzangu
Nina talanta katika fani ya riadha _____________________
Ni matumaini yangu kuwa utaupokea waraka huu ________________________________

Barua Ya Kirafiki ama Kindugu

Huhusu kupatiana mwaliko, kujuliana hali, kufahamisha au kuarifu kuhusu jambo
Sehemu muhimu za barua hii ni

  • Anwani ya mwandishi
    Huandikwa pembeni kabisa upande wa kulia sehemu ya juu
    Huwa na jina la mwandishi , mahali anakoishi, sanduku laposta na tarehe
    Kianzio
    Hudhihirisha Yule anayeandikiwa
    Hubainisha uhusiano wake na mwandishi
    Mfano
    • Kwa mpendwa
    • Kwa mwanangu mpendwa
    • Kwa mpenzi wangu
    • Kwa sahibu/muhibu
  • Utangulizi
    Haya ni maamkizi kwa yule anayeandikiwa
    Mfano
    • Pokea salamu – sufufu, furifuri, tolatola nyingi kama nyota angani, mchanga
    • Mimi ni bugeri wa afya
    • Mzima kama chuma cha pua / ngarange za mvule
    • Nina buraha na furaha/furaha na bashasha
    • Nina imana kuwa Mola/Mkawini/Jalali
    • Nina matumaini kama tai kuwa u buheri wa afya/siha/zihi.rai
  • Methali
    • Ama kweli/yakini/waama
    • Waraka ni nusu ya kuonana
    • Afya ni bora kuliko mali
  • Mwili
    Sehemu – hii hubeba ujumbe wa mwandishi
    Wema – ninaomba unitendee fadhila/jamala
    Ninashukuru kwa wema ulionitendea
    Utiifu – ninakuhakikishia kwamba nitakuwa na utiifu, nidhamu na bidii
    Lengo au azma ya kukuandikia waraka huu ni
    Waraka huu ni kukujulisha kuwa
    Ningependa kukujuza kuwa
  • Tamati
    Ningependa kutia nanga kwa kukuelezea kuwa _______________
    Kwa kuwa wasaa umenitia kumbu/muda 
    Umenipa kisogo, ningependa kutia kitone
    Ninakunja jamvi kwa msemo usemao _______________________
    Kalamu yangu inalilia wino ____________________
    Ndimi mzazi wako ____________________
    Wako wa moyoni _____________________________
    ni wako mpendwa ______________________
    Ndimi mwana wako mpendwa

Sampuli
BIDII FAULU,
S.L.P 93,
NAIVASHA.

18-11-2015

Kwa sahibu yangu, fundi msanifu ,
Utangulizi ______________________________
Mwili
Hatima
Ni mimi wako,
Jina la mwandishi



Insha ya Hotuba

Hotuba ni maelezo yanayotolewa ili kupitisha ujumbe Fulani
Anayetoa hotuba huitwa katibu
Umati unaosikiliza huitwa hadhira
Huanza kwa mlahaka/salamu kwa kutambua vyeo kuanzia wa juu mpaka wa chini ,
sababu ya mkutano
Alama za kunukuu hutumiwa
Hotuba inaweza kuwa ya

  • Mwanafunzi akihutubia shuleni
  • Mwalimu
  • Mwalimu mkuu wa wazazi shuleni
  • Daktari au afisa wa afya
  • Rais wakati wa maadhimisho ya mashujaa
  • Waziri wa usala, afya na ugatuzi

Mfano wa utangulizi
“mgeni wa heshima, mkuu wa elimu gatuzini, mkaguzi wa elimu, mwenyekiti na
maafisa wa elimu na wanafunzi, hamjambo?
‘Mwalimu mkuu, naibu wa mwalimu mkuu, walimu wenzangu, viranja na wanafunzi,
sabalkheri?

Mapambo
ninazo bashasha/furaha/buraha
Nimesimama kidete/tisti/imara kama chuma
Cha pua/ngarange za mvule/kiini cha mpingo
Nitawandondolea hoja zangukuanzia utando hadi ukoko,shinani hadi kileleni
Rejelea hadhira mara kwa mara – nanyi, enyi wazazi, nasi wanafunzi

Tamati
Ningependa kutia kitone/nanga/kukunja jamvi kwa msemo usemao
Ninawamiminia shukrani tolatola/fokofoko
Kwa kutulia kama maji mtungini/maziwa kitomani
Kwa kuwa lililo na mwanzo halina budi kuwa na mwisho
Ninawatakia Baraka njema za Mualana/ninawatakia mbawazi za mkawini mbingu



Dawa za Kulevya

Ni kitu chochote kinachoathiri fahamu za mwili na afya ya mja
Mifano

  • Kokeini
  • Mandraksi
  • Bangi
  • Ganja
  • Miraa au mirungi
  • Tumbako

Athari za dawa za kulevya

  • Kuvuruga akili
  • Mtumiaji hugeuka na kuwa mkia wa mbuzi/juha/kalulu
  • Kupata ujasira bandia
  • Mja huwa katili
  • Hujiingiza katika visanga kama wizi
  • Hudhuru afya
  • Mhasiriwa kama ng’onda/kimbaumbau mwiko wa pilau
  • Sura huumbuka na kusawijika
  • Husababisha saratani
  • Kuenea kwa magonjwa ya zinaa

Methali
Kinga ni bora kuliko tiba
Tahadhari kabla ya hatari

utovu wa nidhamu
watumiaji husheheni matusi
hutabawali kadamnasi
kuvalia mavazi mafupi

Methali
mwacha mila ni mtumwa
usiache mbachao kwa msala upitao
kuzorota kwa uchumi
mtu binafsi hutumia njenje zote
watoto hawatimiziwi mahitaji
filisha mja- akabaki hana mbele wala nyuma
uchumi wa nchi huzorotabaada ya kutumia pesa kuwatibu wahasiriwa
husababisha uraibu
huleta wizi
husababisha uzembe
madereva kusababisha ajali
kupata magonjwa

Join our whatsapp group for latest updates

Download Insha - Class 8 Kiswahili Revision Notes.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students