- Vihisishi
- Vivumishi
- Viunganishi
- Viulizi
- Vielezi
- Ngeli pamoja Na Kirejeshi Amba
- Kirejeshi-amba
- Matumizi ya -ndi
- Matumizi ya -si
- Matumizi ya Na
- Matumizi ya katika, Ni, kwenye
- Usemi Halisi na Taarifa
- Mnyambuliko wa vitenzi
- Ukubwa na Udogo
Vihisishi
Kuelezea maana ya vihisishi
Hutumiwa kuonyesha hisi au hisia ya msemaji kidhihirisha
- Furaha
- Mshangao
- Mshtuko
- Hasira
- Uchungu
- Maumivu
- Uchovu
- Huruma
- Dharau
- Wito
- Laana
Kutunga sentensi akitumia vihisishi alivyopatiwa
Vivumishi
Vivumishi ni maneno yanayotumiwa kuelezea zaidi kuhusu nomino
Aina za Vivumishi
- A -Unganifu
- Sifa
- Pekee
- Viulizi
- Idadi
- Vimilikishi
- Viashiria
Viunganishi
Neno linalotumiwa kuunganisha neno na neno, sentensi na sentensi, wazo na wazo
Kutoa mifano tofauti ya viunganishi
- Kasoro-lakini, bali
- Kusalia kitu kimoja-ila, isipokuwa
- Kinyume na matarajio-ingawa, ijapo, ilhali
- Kulinganisha kuonyesha tofauti
- Kuongezea-aidha, mbali na, licha ya
- Kuwaongoza kutunga sentensi
A - Unganifu
Kijineno kinachotokana na kuambatanisha A na herufi tofauti kwa kutegemea ngeli
Jedwali
Ngeli A-unganifu
A – WA wa - wa
KI – VI cha - vya
LI – YA la - ya
U – I wa - ya
U – ZI wa- za
I – I ya - ya
U – U wa - wa
U – YA wa - ya
YA – YA ya - ya
I – ZI ya - zi
KU kwa - kwa
PAKUMU pa – pa , kwa – kwa, mwa - mwa
Mkato wa Maneno
Huhusu nomino pamoja na vimilikishi vyote vitatu
Mifano
Baba + yake = babake
Dada + yake =n dadake
Nyanya + yenu = nyanyenu
Shangazi + yake = shangaziye
Kaka + yako = kakako
Mjomba + yake = mjombake
Viulizi
Maneno yanayotumiwa kuuliza maswali
Mifano
- Nani: hutumika katika ngeli ya A – WA kujua cheo, jina , ukoo wa watu
- Nini: kujua ni kitu cha aina gani
Hutumika katika ngeli zote isipokuwa ya A - WA - Gani:kujua aina , jamii, hali au tabia
- Lini: kiulizi cha siku au wakati
Hutumiwa kutaka kujua kipindi, siku au wakati wa tukio - Wapi:ni kiulizi cha mahali
- Vipi:kiulizi cha namna gani
Je ni neno la kuanzisha swali - Ngapi:kuuliza idadi kamili ya vitu , vyombo katika jumla
- Pi: kubainisha kati ya nyingi ili kupata kihusika au mhusika Fulani mahususi
Vielezi
Neno linaloeleza jinsi kitendo kilivyotendeka au kufafanua zaidi kuhusu kitendo
Aina za vielezi
- Wakati
- Namna
- Jinsi
- Mahali
- Idadi
- Vuhusishi
- Tanakali
- Takriri
- Tashbihi
Hutumika kwa - Lini- wakati
- Wapi – mahali
- Vipi – jinsi au namna
- Kiasi gani- idadi
Mifano
Wakati mahali namna
Leo nyumbani taratibu
Kesho darasani harakaharaka
Juma ijayo Nairobi ghafla
Mtondogoo machoni kivivu
Vielezi vya Mkazo
Takriri au shadda ni maneno yanayotumiwa kutilia mkazo au kusisitiza jambo
mifano ya takriri
- salama salimini
- bure bilashi
- raha na buraha
- kufa kupona
- liwalo liwe
- haambiliki hasemezeki
- fanya juu chini
- si wa uji si wa maji
- daima dawamu
- buheri wa afya
- hakubali hakatai
- hawashi hazimi
Ngeli pamoja Na Kirejeshi Amba
amba ni kitenzi kisaidizi kinachorejelea mtendwa au mtendaji kwa kutambulisha ama kueleza zaidi ya jambo fulani
kirejeshi –o hutumika badala ya AMBA
o-rejeshi na AMBA havitumiki pamoja
mfano
Kuku ambaye alitaga ni mkubwa
Nomino | Ngeli | Amba- | o-rejeshi |
Kuku |
A-WA |
Ambaye-ambao |
Ye-o Cho-vyo Lo-yo O-yo Yo-zo O-zo Yo-yo O-oO -yo Yo -yo Ko Po Ko MO |
Kirejeshi –amba
Kirejeshi –o cha awali na kirejessho o- cha tamati
Kufafanua jinsi ya kuambisha o rejeshi tamati na awali
o-rejeshi awali hutokea kabla ya mzizi wa kitenzi –o- rejeshi tamati hutokea mwishoni mwa sentensi
Kitenzi | o-rejeshi awali | o- rejeshi tamati |
Kimbia Kula Kuwa Kua |
Anayekimbia Anayekula Anayekuwa Anayekua |
Akimbiaye Alaye Awaye Akuwaye |
Matumizi ya –ndi
Kiainishi –ndi ni kishirikishi cha kukubali kwa msisitizo
Huambatanishwa na viwakilishi nafsi au virejeshi ili kutilia mkazo
Hutumia o-rejeshi kwenye vitenzi
Nafsi
Ndi + mimi = ndimi
Ndi + wewe = ndiwe
Ndi + yeye = ndiye
Ndi + si = ndisi
Ndi + nyinyi = ndinyi
Ndi + wao = ndio
o- rejeshi
ndi + ye = ndiye
ndi + o = ndio
Matumizi ya –si
Ni kiainishi cha kutilia mkazo
Huambatanishwa na viwakilishi nafsi au virejeshi ili kuleta msisitizo wa kukanusha
Nafsi
Si + mimi = simi
Si + wewe = siwe
Si + yeye = siye
Si + sisi = sisie
Si + wao = sio
o- Rejeshi
A –WA si + yeye = siye si + o = sio
KI – VI si + cho = sicho si+ vyo = sivyo
Matumizi ‘na’
Kiunganishi NA huambatanishwa na kiwakilishi nafsi kuonyesha PIA NA PAMOJA NA
Hutumiwa pamoja na 0-rejeshi
Nafsi
Ngeli Na + o- rejeshi
A – WA na+ye = naye nao
KI –VI na + cho = nacho navyo
LI –YA na + lo = nalo nayo
U – I na + o = nao nayo
U – ZI na + o = nao nazo
I – I na+ yo = nayo nayo
U – U na + o = nao nao
U – YA na + o= nao nayo
YA – YA na +yo = nayo nayo
I – ZI na + yo = nayo nazo
KU na + ko = nako
PAKUMU na+po na+ko na+mo
Matumizi ya ‘katika’, ‘ni’ , ‘kwenye’
Hivi ni vihusishi vya mahali
Hutumiwa kuonyesha kuwapo kwa kitu kilichotajwa mahali Fulani
Ngeli hubadilika hadi PA KU MU
Kuhimiza kuwa ni kosa kutumia hivi vihusishi pamoja
Kuambatanisha nomino na vivumishi
Vivumishi | Darasa | darasani |
Viashiria Vimilikishi Ote Oote Enyewe Enye Ingine Sifa |
Hili, hilo, lile Langu, lako,lake Lote Lolote Lenyewe Lenye Jingine Zuri, jema, baya Eupe, eusi Halina |
Hapa, hapo, pale |
Usemi Halisi na Taarifa
Usemi halisi ni maneno yalivyotarajiwa na msemaji mwenyewe
Usemi taarifa ni ripoti au maelezo yakitolewa na mtu mwengine kutoka kwa msemaji halisi
Kueleza jinsi ya kubadilisha usemi
Usemi halisi usemi taarifa
leo siku hiyo
Jana siku iliyopita/tangulia
Kesho siku ijayo
Viashiria hapa hapo au pale
Vimilikishi vya karibu ake
Mbali kidogo ako
Nafsi ya kwanza ni nafsi ya tatu
Wakati ta, ki nge
Mnyambuliko wa vitenzi
Kunyambua ni kurefusha mwisho wa vitenzi katika hali tofauti
- Tendeka
- Tendesha
- Tendeshwa
Katika kauli ya kutendeka vitenzi humalizika kwa ‘ka’
Kitenzi kauli ya kutendeka
Vuka vukika
Sahau sahaulika
Maliza malizika
Bomoa bomoka
Kula kulika
Lala lalika
Lima limika
Pika pikika
Soma someka
Fagia fagilika
Kitenzi tendesha kauli ya kutendeshwa
Lala laza lazwa
Pika pikisha pikishwa
Kimbia kimbiza kimbizwa
Rudi rudisha rudishwa
Toa toza tozwa
Ota otesha oteshwa
Oa oza ozwa
Soma somesha someshwa
Ukubwa na Udogo
Maneno katika hali ya ukubwa huwa ni kukipa kitu ukubwa usio wa kawaida na pia maneno katika hali ya udogo ni kukidunisha kitu kuliko hali ya kawaida
Ngeli pia hubadilika katika hali ya ukubwa na kuwa LI- YA ,na katika hali ya udogo huwa KI – VI
Njia tofauti za kubadili maneno katika ukubwa na udogo
Kudodosha – mw, ny na kutia j
Mfano
- ng’ombe – gombe
- Mkono – kono
- Ndama – dama
Kudodosha herufi moja na kutia ji
Mfano
- Mji – jiji
Kudodosha ki na kutia ji
Mfano
- Kisu – jisu
Kuongeza ji bila kudodoa chochote
Mfano
- Jicho – jijicho
Kutia j kwa nomino zinazoanza kwa irabu
Mfano
- uso – juso
- Uta – juta