Wednesday, 29 March 2023 13:23

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 5

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi, umepewa majibu manne.
Chagua jibu lifaalo zaidi. 

Laiti angalimaizi, abadan katan ............1...............katika  ............2...............  ............3............... Ilikuwa  ............4............... kwao wavyele wake kumhimiza  ............5............... juhudi,  ............6...............sikio la kufa halisikii ............7............... Kilio cha mtima ndicho  ............8............... kila uchao. Alipanda pankwisha akavuna 

 ............9............... 

  1.                        
    1. angalizembea
    2. asingelizembea
    3. angezembea
    4. asingalizembea
  2.                
    1. somo
    2. masomoni
    3. ujiva
    4. masomo
  3.                      
    1. zao
    2. yake
    3. yao
    4. wake
  4.                
    1. mwelekeo
    2. kaida 
    3. kusudi
    4. nia
  5.                
    1. kutojali
    2. kujibali na
    3. kutoasi
    4. kuasi
  6.              
    1. bali
    2. seuze
    3. mbali 
    4. licha ya
  7.              
    1. yeyote
    2. uneni
    3. madawa
    4. dawa
  8.                  
    1. anakiamkia
    2. wanachokilalia
    3. anakilalia
    4. anachokilalia
  9.                    
    1. pankwisha
    2. ayami
    3. pantosha 
    4. kiishicho 

Hakika misitu  ............10...............umuhimu chungu  ............11...............  ............12...............uhifadhi  ............13............... ni jambo  ............14............... kuzungumziwa na kutiliwa mkazo  ............15............... kumbi na mikutano iliyopangwa na itakayopangwa kote duniani. 

  1.                
    1.  inazo
    2. inalo
    3. inao 
    4. inayo
  2.              
    1. mzima
    2. nzima
    3. zima
    4. nomi
  3.                  
    1. Kwa sababu
    2. Hata hivyo
    3. Kwa mintarafu
    4. Kwa hivyo
  4.              
    1. wazo
    2. wayo
    3. wapo
    4. wao
  5.                
    1. linalobidi
    2. linaobidi
    3. linaostahili
    4. lisilostahili
  6.                      
    1. kwa
    2. si
    3. pasipo
    4. katika 

Kutoka swali la 16 mpaka 30, jibu kila swali ukifuata maagizo uliyopewa. 

  1. Ni orodha gani ya nomino za ngeli ya U-YA pekee?
    1. Mabua, mauaji, mawele, maumbo
    2. Uuaji, ulezi, ubao, ugonjwa
    3. Upishi, malezi, mawele, makelele
    4. Magonjwa, maua, mapishi
  2. Ni sentensi gani kati ya hizi imetumia methali?
    1. Mtoto alilala fofofo
    2. Usipoziba ufa utajenga ukuta
    3. Swali hili lilikuwa mboga
    4. Amina ni mwoga kama kunguru 
  3. Ipi si maana ya neno "chuma"?
    1. Pata pesa nyingi
    2. Toa matunda kutoka mtini
    3. Mtu asiye na nguvu
    4. Aina ya madini
  4. Tegua kitendawili:-
    Kina mkono na uso lakini hakina uhai
    1. jua 
    2. Nyota
    3. saa 
    4. sahani
  5. Kinyume cha sentensi:-
    Shangazi anaondoka nje anarudi ndani ni
    1. Mjomba anarudi ndani kutoka nje
    2. Shangazi anarudi ndani kutoka nje
    3. Mjomba anarudi nje kutoka ndani.
    4. Shangazi anarudi nje kutoka ndani
  6. Kulia ni kwa machozi, jeraha ni kwa
    1. kamasi
    2. matongo
    3. damu
    4. usaha
  7. Malipo anayopatiwa mtu aliyekwazwa ili kuondoa hasira yake ni
    1.  kilemba
    2. honoraria
    3. mapoza 
    4. marabaha 
  8. Mwalimu yule aliyekuja jioni ni jirani yangu.
    Maneno yaliyopigiwa mstari ni
    1. kielezi, kiwakilishi, kivumishi
    2. kivumishi, kielezi, kiwakilishi
    3. kiwakilishi, kivumishi, kielezi
    4. kivumishi, kielezi, kivumishi
  9. Kati ya wafanyakazi hawa, ni yupi anayeuza bidhaa rejareja mnadani?
    1. Dalali 
    2. Nokoa
    3. Hamali
    4. Mchuuzi
  10. Chagua sentensi ambayo ni sahihi kisarufi
    1. Wamezificha funguo kabatini ile
    2. Moshi anafuka chumbani mle penye wageni
    3. Barasteni penyewe kumelimwa tena
    4. Moyoni mwake ndimo mlimoficha siri
  11. Jaza vihasho kwa maneno sahihi:-
    Alimwinda .....................................na jioni aka ...................................mchuzi mkali kama...................................
    1. siki, unga, sigi
    2. sigi, uga, siki
    3. sigi, unga, siki
    4. unga, siki, sigi
  12. Andika kauli ya taarifa ya:-
    "Mbona unayachafua mazingira hivi?” aliuliza
    1. Alitaka kujua mbona ulikuwa ukichafua mazingira hivyo
    2. Alitaka kujua mbona alikuwa akichafua mazingira vile
    3. Aliuliza sababu ya kuchafua mazingira hivi
    4. Aliuliza mbona unachafua mazingira hivyo
  13. Chagua jibu lisilo sahihi
    1. Maktaba: YA-YA
    2. Nyanya: 1-ZI
    3. Uyoga: U-U
    4. Unyasi: U-ZI
  14. Kilinge ni cha wachawi ilhali .......................................ni kwa vitabu,
    1. bunda 
    2. matopa
    3. furushi
    4. mtungo 
  15. Kiingilio hutolewa kuingilia chumba cha burudani.
    Malipo au zawadi inayotolewa kwa mtu aliyeona au kuokota kitu kilichopotea ni
    1. ada 
    2. fidia
    3. utotole
    4. kiokote 

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 31-40. 

Siku ya chete hungojewa kwa hamu na hamumu katika mji wa Leteraha. Hii ndiyo siku watu wa mbali na karibu hutangamana kwa madhumuni tofauti. Kunao wanaoleta bidhaa mbalimbali kuziuza. Kunao wengine ambao hutangaza huduma hizi au zile ilhali kunao wanaokuja kununua. Mara nyingi ununuzi si ununuzi tu bali ni ununuzi kwelikweli. Kwa vile wanunuzi wengi wanafahamu fika kuwa itawachukua siku saba ndipo wafike sokoni tena, inabidi basi wanunue bidhaa za kudumu siku zote hizo. 

Nao wauzaji huhakikisha kwamba wanakidhi mahitaji ya wateja wao maana wasingependa wao waende mbali kutafuta bidhaa au huduma hizo. Basi mimi na sahibu yangu Mwendwa tulilizuru soko hilo la kwetu siku ya chete Jumamosi iliyopita. Baada ya pitapita za hapa na pale na ununuzi wa vitu hivi na vile tuliona tumeridhisha haja zetu. Tukawa tunajiandaa kuambua nyayo kurudi makwetu. 

Ghafla ustahi ulisikika kutoka karibu na tulipokuwa tukifungia mzigo wetu. Ustahi huo ulitatiza na kutatiza kelele zilizokuwa zikiendelea pale sokoni. Wacha mtafuruku upande moto. Ni kupita kwa watu waliokuwa karibu mno na tukio la mkasa ndipo tulipata fununu ya mambo. 

Mwendawazimu mmoja alitokea kudai kuwa mwanamume fulani aliyekuwa amevalia nadhifu kuwa ni mumewe. Yule mwanamke mwendawazimu aliyejulikana sana pale sokoni aliitwa Wamnara. Alimshika maskini mwanamume wa watu na kukatalia ungedhani dondora. Juhudi za mwanamume huyo kujaribu kujinasua zilimjadirisha tu Wamnara. Wehu ukampanda maradufu kama zaibaki kwenye kipimajoto. Sauti kali iliendelea kumtoka huku akitaka yule mwanamume amwambie mbona alimwacha pale sokoni na kutoweka. 

Kioja hicho kilivuta na kuvutia lukuki ya watu. Baadhi yao walimwonea huruma mwanaume yule huku wengine wakimsihi Wamnara kumwacha. 

  1. Watu wengi huitazamia siku ya chete kwa kuwa
    1. kunazo jamii zilizoendeleza elimu ua kujenga nyumba
    2. kila jamii ilifunza elimu ya kupaka kuta rangi
    3. ni siku ya kutangamana
    4. ni siku ya kuleta bidhaa tele sokoni
  2. Mnunuzi huitwa mteja au
    1. mhudumu 
    2. mshitiri
    3. dalali
    4. mwuzaji
  3. Siku ya soko pale mjini Leteraha ilitanguliwa na
    1. Alhamisi 
    2. Jumapili
    3. Ijumaa
    4. Jumanne
  4. Mwandishi na Mwendwa walidhamiria kufanya nini sokoni?
    1. kumwona mwendawazimu Namnara
    2. kununua bidhaa kadhaa pale sokoni
    3. kutongamana na wauzaji na wanunuzi
    4. kwenda kuuza bidhaa kadhaa
  5. Wanakidhi mahitaji ya wateja maana yake ni
    1. wanatosheleza matilaba ya wanunuzi
    2. wanaridhisha haja zao na za wateja pia
    3. wanawaudhi wanunuzi
    4. wanawapunja wanunuzi
  6. Kizaazaa kilisababishwa na nini pale sokoni?
    1. watu waliokuwa wakiambua nyayo
    2. tafrani za wanunuzi waliotaka kuhudumiwa haraka
    3. ukwenye uliotoka karibu na alikosimama Mwendwa
    4. moto ulioanza kuungaza vibanda sokoni
  7. Mwendwa na rafikiye hawakudhamiria
    1. kuwa miongoni mwa waliofika kutazama kioja cha sokoni
    2. kuona vioja vya pale sokoni
    3. kujua nini kilichotafirisha shughuli za sokoni
    4. kuabiri gari na kurudi makwao
  8. Kwa nini Wamnara alimganda mwanaume yule?
    1. Alidai kuwa mwanaume huyo alimrelekeza
    2. Alipendekezwa na jinsi alivyovalia maridadi
    3. Walijuana sana tangu zamani
    4. Alidai kuwa mwanamume huyo alikataa kununua bidhaa zake
  9. Vitimbi hivyo viliisha wakati
    1. polisi walifika na kumshika Namnara
    2. mwanamume alipofurukuta na kujinasua kisha akatoroka
    3. mwanamume huyo alimkubalia Namnara maombi yake
    4. watu waliingilia kati na kumsaidia mwanamume huyo
  10. Kichwa kipi kinafaa kwa habari hii?
    1. Vioja sokoni
    2. Mnunuzi ashikwa kwa kumwibia mwendawazimu
    3. Kila soko lina wendawazimu wake
    4. Wamnara na koti la mwungwana 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50. 

Siku za hivi karibuni, mambo ni kana kwamba kaenda segemnege katika taifa fulani liitwalo Kenya. "Watazamaji leo tungependa kuanzia kwa habari za tanzia. Abiria watano kaitwa rehemani baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani. Wenzao manusura si hayati si mamati na wamo hospitalini" Runinga moja katika taifa hili ilipeperusha habari. 

Wadau wa sekta ya uchukuzi katika taifa la Kenya kutwa kucha vichwa wajipata kongamanoni kukitegua kitendawili hiki sugu "Wakuu wa trafiki, wasimaminzi wa barabara na wahusika wengine, sabalkheri? Ningependa kunena kuwa ajali nyingi taifani zinasababishwa na baadhi ya haya. Madereva wengine baada ya kubugia ya mgema hujipata usukani. Magari mengine huwa ni yale ambayo spana ziwe tayari. Silatini si kwao kwema. Imemaizika kuwa magari mengine huendeshwa kwa kasi ghaya. Bila shaka kasi hii ya duma huyaleta maafa yaso kinaya. Baraste zingine huwa na mashimo yasokarabatiwa. 

Magari yanapoyagonga pengine hujipata kabingiria bingiribingiri. Abiria" Wengine wasibahatike kutoyaona mauko." Ukumbi wote hakuna aliyesinasina wala kukohoa. Walimkazia macho aliyekuwa mkabala. Hoja zake ziliwaingia akilini na kuwapa kero. Basi tufanye nini kuyaokoa aushi ya maskini abiria na waendashaji wa magari, bodaboda na tuk-tuk?.......? 

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza
    1. mambo hayakuwa vyema
    2. risala za heri zilitumwa na mtangazaji
    3. habari runingani ilitamiwa
    4. utulivu kafurahiwa Kenya
  2. Tambua jibu lisilo na maana ya kwenda segemnege.
    Kwenda
    1. mvange
    2. kasi
    3. kombo
    4. mrama
  3. Kulingana na kifungu,
    1. nia yao ilikuwa kuvikuna vichwa
    2. wadau walikuwa ajizi
    3. walijitia hamnazo kuhusu ajali
    4. walichemsha bongo kuhusu kero lao
  4. Ni kweli kulingana na kifungu kuwa kongamano
    1. Lilitia nanga macheo
    2. Liling'oa nanga asubuhi
    3. Halikuanza katu
    4. Lilisitishwa asubuhi
  5. Ajali katika nchi husika
    1. ubugia tembo si hoja
    2. zaadimika
    3. ni nadra 
    4. visababishi ni ayami 
  6. Magari, spana ziwe tayari kama ilivyotumika katika ufahamu ina maana
    1. magari yenye spana
    2. spana kuwa tayari
    3. makanika wawe tayari
    4. magari mabovu
  7. Tambua neno lisilo kisawe cha silatini
    1. barabarani
    2. barasteni 
    3. manzilini
    4. njiani
  8. Tambua matumizi ya............bingiribingiri.
    1. chuku
    2. nahau
    3. tanakali za sauti
    4. tashbihi
  9. Kulingana na kifungu, aya ya tatu ukumbini mwa kongamano
    1. hali ilikuwa shwari
    2. kimya kilitamalaki
    3. watu walifurika
    4. hatibu alisimama kando 
  10. Tambua maana ya maskini kama iliyotumika kifunguni
    1. fakiri
    2. hohehahe
    3. akina yahe
    4. waathiriwa 

MAJIBU

swa ms

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. 
Andika insha ya kusisimua ukianzia kwa maneno haya :- 

Ilikuwa siku ya ziara. Tulikuwa tumeingoja kwa hamu na ghamu.........................................................................................................................................................

..............................................................................................................................................................................................................................................................

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 5.

Tap Here to Download for 30/-

Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students