Wednesday, 29 March 2023 13:32

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 7

Share via Whatsapp

MASWALI

Vihosho vifuatavyo vina nafasi 1-15. Vikamilishe ukitumia kiteuzi mwafaka.

Kuna sauti kadhaa za Kiswahili. Sauti za Kiswahili...................1......................na...................2......................zinazopatikana katika ...................3...................... yenyewe. Konsonanti moja ikiambatanishwa na ...................4...................... moja huunda silabi ...................5...................... Wakati  ...................6...................... silabi zinaunganishwa, zinaunda neno. Mwanafunzi ..................7...................... kuhusu utaratibu huu ni ..................8......................anoe swali kuhusu mada inayorejelewa.

  1.                      
    1. zinatokana
    2. zinatoka
    3. zikitoka
    4. inatokana
  2.                        
    1. mizani
    2. silabi
    3. mapigo
    4. herufi
  3.              
    1. akrabu
    2. abjadi
    3. akraba
    4. abadi
  4.                            
    1. neno
    2. sauti
    3. vokali
    4. tamko
  5.                            
    1. sahili
    2. mwambatano
    3. changamano
    4. soghuna
  6.                  
    1. ambalo
    2. ambapo
    3. ambayo
    4. ambao
  7.            
    1. akieleweka
    2. aliyeeleweshwa
    3. alielewa
    4. anayejielewa
  8.            
    1. mgumu
    2. ngumu
    3. sharti
    4. vigumu

Mwalimu alipotuomba ..................9.....................katika makundi..................10......................nilitatizika sana. Alisema kuwa alitaka ..................11......................au kuimba shairi la majibizano..................12......................kama ..................13...................... Nilitatizika mawazoni ..................14...................... sijawahi kuwa na ujasiri wa kusimama kadamnasi ..................15......................watu.

  1.                          
    1. tugawanwe
    2. tujigawe
    3. tugawanyishwe
    4. tutengane
  2.                    
    1. viwili
    2. mbili
    3. mawili
    4. ya pili.
  3.                
    1. tukariri
    2. tughani
    3. tusome
    4. tujifunze
  4.                  
    1. inayojulikana
    2. Unayojulikana
    3. inaojulikana
    4. linalojulikana
  5.                
    1. ngonjera
    2. tarbia
    3. utenzi
    4. thuluthi
  6.              
    1. ilhali
    2. wala
    3. maadamu
    4. yaani
  7.                
    1. kwa.
    2. ya
    3. mwa
    4. la

Kuanzia swali la 16 hadi 30, jibu kulingana na maagizo

  1. "Mlango ulinikodolea macho." Eleza tamathali ya lugha iliyotumika katika kauli hii.
    1. Utohozi
    2. Tashihisi
    3. Kinaya
    4. Chuku
  2. Kaka ni, ganda tupu la yai au konokono.
    Kaka pia ni;
    1. ndugu yangu wa kiume
    2. sehemu ya juu ya mdomo huko ndani
    3. kifaa cha kutobolea mashimo kwenye mbao au chuma
    4. mbwa asiyekuwa na mahali maalumu pa kuishi
  3. Jiriwa ni kwa seremala kama vile chungu ni kwa:-
    1. mfinyanzi
    2. sonara
    3. mnajimu
    4. mkalimani
  4. Ni ipi kati ya sentensi zifuatazo imeakifishwa vizuri?
    1. Unajua kusoma vizuri!
    2. Unajua kusoma vizuri.
    3. Unajua kusoma, vizuri.
    4. Unajua kusoma vizuri
  5. Ukizidisha nusu kwa thuluthi utapata nini.
    1. Sudusi
    2. Ushuri
    3. Humusi
    4. Tusui
  6. Chagua malipo yenye maelezo sahi
    1. Malipo ya kuoa ni fola.
    2. Malipo ya kuingia kweny, sherehe ni mahari.
    3. Malipo ya kuokota itu kilichopotea ni kosi.
    4. Malipo ya kiyesha shukrani ni duhuli.
  7. Baba yangu atamwitaje dada wa mama yangu?
    1. Mlamu
    2. Shemeji
    3. Mwanyumba
    4. Mkwemwana
  8. Chagua sentensi iliyotumia kiingizi kwa usahihi.
    1. Shime! Wamefiwa na nyanya yao wampendaye mno!
    2. Simile! Ama nitakuangukia na mzigo!
    3. Maskini! Amezoa alama sheshe mtihanini!
    4. Naam! Hatimaye anaugua kifuakikuu!
  9. Ni kauli gani inaonyesha kwamba mtu hachagui?
    1. Naomba tunda jingine tamu nilile 
    2. Maisha yenyewe yamekuwa magumu siyamudu
    3. Kitabu chochote cha hadithi kikisomwa kitafaidi
    4. Moyo wake wote ulijaa baridi ukahaki harafu
  10. Chagua jozi ambayo haina visawe
    1. Asali              uki
    2. Kilimo           zaraa
    3. Barabara      taliki
    4. Wasiwasi     wahaka
  11. Kanusha kauli hii. Mama aliyejifungulia barasteni amelazwa katika hospitali ya rufaa.
    1. Mama aliyejifungulia barasteni hatalazwa katika hospitali ya rufaa
    2. Mama asiyejifungulia barasteni hatalazwa katika hospitali ya rufaa 
    3. Mama aliyejifungulia barasteni hakulazwa katika hospitali ya rufaa
    4. Mama asiyejifungulia barasteni hakulazwa katika hospitali ya rufaa
  12. Chagua sentensi ambayo inaonyesha majuto.
    1. Mama alikuja akala akatazama taarifa akaingia chumbani.
    2. Wasichana hawajamudu kusukwa maana hawana pesa
    3. Ukiinama ovyooovyo utauumiza mgongo wako tena
    4. Lucia angalijiandikisha angaliibuka mshindi
  13. Onyesha mahali ambapo kiambishi 'wa' kimetumika kuonyesha kutendewa.
    1. Wamefua nguo
    2. Wamefuliana nguo
    3. Wamefuliwa nguo
    4. Wamewafulia nguo
  14. Chagua Kiunganishi ambacho kimetumika kwa usahihi katika sentensi.
    1. Wasichana wala wavulana wamekula matunda
    2. Walimu ila wanafunzi wamechelewa 
    3. Walimu na wanafunzi wameenda ziarani
    4. Wanafunzi isipokuwa walimu wanakula wali.
  15. Andika katika hali ya wingi. Mtume ametumwa dukani kununua yai.
    1. Mime wametumwa dukani kunum mayai.
    2. Watume wametumwa madukani kununua mays
    3. Watume wametun, wa dukani kununua mayai.
    4. Mitume wametumwa madukani kununua mayai.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu swali la 31-40,

Mwanafunzi asiyeelewa kile ambacho mwalimu anafunza darasani hupatwa na mzongo sana. Saa nyingine huhisi kukata tamaa asiendelee kujishughulisha na somo hilo tena. Hata akianguka hajali tena. Mwalimu naye asipomwelewa amvumilie na kumfunza mwanafunzi huyo taratibu, kwa kweli mtoto huyo atapotea kabisa. Pengine hata atakamilisha masomo ya shule ya msingi bila kujua utaratibu wa ngeli. Ina maana kwamba akipata maswali kuhusiana na sehemu asiyoielewa ataanguka mtihani huo.

Lakini kwa nini mwanafunzi asielewe mwalimu anapofunza? Sababu ni kochokocho kama mchanga ufuoni pa bahari. Pengine kuna matatizo ya kinyumbani ambayo humjia mawazoni mwalimu anapofunza. Labda wazazi wanazozana, kuna mtu mgonjwa, kufiwa na mpendwa au pengine mmoja wa wazazi ni mlevi aletaye vurugu nyumbani kila siku. Sababu nyingine ni njia ya walimu kufundisha. Walimu wengine hufunza vibayavihaya hata mwanafunzi haelewi lolote. Walimu wanaopenda kuwachekesha tu wanafunzi darasani, ama wana athari ya lugiiamama ama wanazembea tu darasani, hawawezi kuwafaa wanafunzi.

Kuna wanafunzi ambao hali haiwaruhusu kupata vitabu vya kiada na madaftari ya kufanya ziada zao. Wanategemea wenzao wenye vitabu ambao saa nyingine huwanyima. Mwanafunzi kama huyu hataweza kujisomea zaidi katika muda wake wa ziada. Kama mwalimu hakumpa nakala za kurejelea, atadurusa vipi? Vilevile kuna wanafunzi ambao hawakujaliwa na akili nyepesi ya kuyaelewa mamb, haraka. Hata kama mwalimu atarudia masa mia na moja, bado hawataambua chochote! Walimu wasiotumia vifaa halisi kufundisha pia hutati kuelewa kwa wanafunzi. Mara nyingi wakiona unachozungumzia na kukigusa, kusahau kutakuwa vigumu.

Pia kuna wanafunzi walio na mtazamo hasi kuhusu somo fulani. Utawasikia wakisema, "sisi kwetu hatupiti Hisabati, au Kiswahili." Nami nauliza, kuna watu ambao wameandikiwa kuwa hawawezi kulipita somo fulani kwa sababu fulani? Ninaamini kwamba yeyote akijitolea, anaweza kufaulu katika chochote akifanyacho.

  1. Kwa kawaida, ikiwa mwanafunzi haelewi kile ambacho anafunzwa:-
    1. anamchukia mwalimu anayemfunza
    2. anaenda kutafuta ushauri kwa mwalimu
    3. anatatizika kimawazo na kukosa utulivu
    4. anahofia kuchukiwa na mwalimu wake
  2. Ikiwa mwanafunzi anashindwa kuelewa kile ambacho amefunzwa, mwalimu:- 
    1. anafaa kubadilisha vitabu anavyovitumia
    2. anafaa kumvumila na kumfunza tena polepole
    3. anafaa kumwadhibu ili aelewe
    4. kumkalisha karibu na ubao na kumpa kazi nyingi ya ziada
  3. Ni yapi si matatizo ya kinyumbani?
    1. Kuugua kwa mtu wa jamaa.
    2. Baadhi ya wazazi kutumia mihadarati.
    3. Migogoro baina ya wazazi
    4. Akili inayochukua muda kuelewa mambo
  4. Ni kweli kwamba mwanafunzi ataambulia alama mbaya iwapo mwalimu:-
    1. hafanyi uzembe darasani
    2. hatumii muda wa masomo kuwaburudisha wanafunzi
    3. anaepuka athari za lughamama
    4. hatajibidiisha katika kuyatekeleza majukumu yake ipasavyo
  5. Badala ya kutamka 'sasa' mtu akitamka 'thatha' husemwa kwamba ana; 
    1. kigugumizi 
    2. kithembe
    3. ububu
    4. zusitasita
  6. Kukataa kumwazima mwenzako kitabu anapokuomba
    1. tukatika kutunza bidhaa zako zisipotee
    2. ni dalili ya uchoyo na ubinafsi
    3. humtia moyo kujikaza na kidogo alicho nacho
    4. kunawafanya wazazi wake wamnunulie vitabu vingine
  7. Ni kweli kwa mujibu wa habari kwamba:-
    1. mwanafunzi anafaa kujitengenezea nakala baada ya kufunzwa
    2. mwanafunzi hahitaji vitabu au nakala ili kufaulu masomoni 
    3. mwanafunzi akiwa na nakala, zinaweza kumfaa kudurusu akapita mtihani wake
    4. kama mwalimu amefunza, si lazima awape wanafunzi nakala
  8. Mwalimu anapendekezewa kutumia nyenzo kufunza ili;
    1. asisumbuke kuandikia wanafunzi nakala
    2. kurahisisha kuelewa na kutosahau kwa wanafunzi
    3. kuweza kufundisha haraka bila shida
    4. watoto wasiokuwa na vitabu vya ziada na kiada wafaidike
  9. Mtazamo hasi ni kinyume cha mtazamo
    1. chanya
    2. tasa
    3. shufwa
    4. witiri
  10. "Ninaamini kwamba yeyote akijitolea, anaweza kufaulu katika chochote akifanyacho." Kauli hii inaunga mkono usemi kwamba:-
    1. penye nia pana njia.
    2. mchagua jembe si mkulima.
    3. lisemwalo lipo njiani laja.
    4. asiyejali hupata hatari.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 41-50

Je umewahi kujiuliza, ama unajua mwandani ni nani? Mwandani ni mtu wa ndani, rafiki ambaye pia huitwa msena au msiri. Ni mtu wa kuambia mambo ya siri au pengine mambo ya ndani ambayo hayafai kuambiwa mtu mwingine hivihivi. Ni mtu ambaye kwa muda umemkagua na kumjua kuwa mtu wa kuaminika. Kufikia kumfungulia mambo yako ya ndani ina maana kwamba umemsoma kama msahafu na kuwa na Imani kuwa hutakuwa umekosea kuchukua funguo za moyo wako ukamwekea wazi mambo ya ndani kabisa.

Hata hivyo siku hizi dunia i...ebadilika kabisa! Imebadilika kama hali ya anga ilivyobadilika, kiangazi kikageuka kipupwe au pengine masika yakageuka vuli! Ni vigumu kumpata mtu wa kumwamini hasa ikizingatiwa ile methali ya wahenga kwamba hapana siri ya watu wawili. Ukitaka iwe siri, basi heri uizike katika moyo wako na kuifunikia hadi kifo. Marafiki wa siku hizi ni kama wanawashwa na midomo, ukiwaambia jambo, mara tu watokapo kadamnasi yako, wanamtafuta mtu wa kumpasha habari motomoto.

Habari hizo sharti wanazitia chumvi ili ziwe tamu masikioni mwa yule anayepokezwa! Sasa chukulia kwa mfano umemweleza rafiki yako kuhusu migogoro inayoendelea katika familia yako. Pengine wazazi wako wanazozana au pengine mmoja katika familia yenu anaugua ugonjwa wa UKIMWI. Ama pengine mmefungiwa nyumba kwa sababu ya kukawia kulipa pango. Halafu keshoye ukifika shuleni unashangaa kuona waangaliwa na kuchekwa kisirisiri. Ukichunguza unapata kwamba tayari siri yako imetembea kama moto kwenye kichaka kikavu, Je hilo litakuchoma maini kiasi gani?

Wosia wangu kwa marafiki ni kwamba, wanafaa kuwa wa ukweli, ama waache kabisa kujiita marafiki ilhali mioyo yao imejaa uadui. Kumbuka kuujenga urafiki huchukua muda mrefu lakini kuuvunja ni kazi ya chini ya sekunde tano. Nani angependa kuchukua muda kujenga uhusiano ambao hautadumu? Hata watu wakikusikia kuwa u mtu wa sampuli hiyo, unafikiri yupo ambaye angependa kuhusiana na wewe? Hakutakuwa na haja ya wewe kuhesabiwa kama rafiki maana utakuwa hufai lolote la haja. Akufaaye kwa dhiki ndiye awezaye tu kuitwa rafiki.

  1. Kabla ya kumchagua rafiki:-
    1. unakuwa umesifiwa na wengine kumhusu
    2. unakuwa umesikia kuhusu wema wake
    3. unakuwa umemchunguza na kumkagua
    4. anakuwa amejipendekeza sana kwako
  2. Kwa kawaida rafiki:-
    1. huambiwa mambo wanayoambiwa wenzake
    2. haambiwi mambo wanayoambiwa wenzake
    3. hana tofauti na watu wengine wa kawaida
    4. hufunuliwa mambo waliyofichwa wengine
  3. Neno msahafu kama lilivyotumika katika ufahamu liria maana ya:-
    1. gazeti lililoandikiwa watu kusoma
    2. daftari lenye maneno mengi ya kusomwa
    3. kitabu kitakatifu
    4. kitabu kinachopendwa na wengi
  4. Ni msimu gani uliolinganishwa sawa na maelezo yake? 
    1. Vuli - Majira ya joto jingi
    2. Kiangazi - Wakati wa matope mengi 
    3. Kipupwe - Msimu wa baridi kali
    4. Masika - Msimu wa rasharasha za mvua
  5. Ukilinganisha siku hizi na za zamani, ni wazi kwamba:-
    1. hapo zamani ilikuwa vigumu kupata mtu wa kukutunzia siri. 
    2. watu wengi siku hizi wamejifunza kuwa wasiri kama usiku.
    3. si rahisi kupata mtu wa kumwamini na mambo yako siku hizi.
    4. watu wa zamani walitangaza sana mambo ya wenzao.
  6. Rafiki anapotoboa siri yako kwa wengine:-
    1. hakosi kuiongeza utamu kwa maneno yasiyokuwa kweli
    2. humwambia huyo anayeambiwa aitunze siri hiyo
    3. huwa lengo lake ni kukuaibisha usiwahi kumpa siri nyingine
    4. anapata sifa na marafiki wapya
  7. Mara nyingi siri zinazoambiwa wengine
    1. hazihusiani na vurugu katika jamaa 
    2. hazihusiani na mafanikio au ushindi nyumbani
    3. si kuhusu maradhi ya aibu
    4. hazina lolote la kweli bali uongo mtupu tu
  8. Je, ni nini maana ya UKIMWI? 
    1. Upungufu wa Kinga Mwilini 
    2. Ukondefu wa Kinga Mwilini 
    3. Usafi wa Kinga Mwilini
    4. Ukosefu wa Kinga Mwilini
  9. Mtu hujuaje kwamba siri yake. imewafikia wengine?
    1. Rafiki mwenyewe anaenda kujishtaki
    2. Wanaoambiwa wanakuja kumwambia
    3. Jinsi wanavyomwangalia wakimwona
    4. Anakisia tu bila kuwa na hakika
  10. Kauli ya mwandishi anapomalizia makala katika aya ya mwisho ni kwamba:-
    1. ni kazi ngumu kuuanza urafiki lakini kuuharibu hakuhitaji muda 
    2. kujenga urafiki ni rahisi kuliko kuuvunja
    3. kuuanza na kuumaliza urafiki si kazi rahisi
    4. unapotangaza siri za wengine unajisaidia ili usiletewe umbeya Zaidi

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika Insha yako.

Endeleza isha ifuatayo:-

Baada ya kufunga shule Novemba mwaka jana, nilienda mashambani kumtembelea nyanya yangu. Nilipofika huko......................................

MAJIBU

swa

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Mid Term Exams Term 1 2023 Set 7.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students