Thursday, 13 April 2023 07:38

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo, Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila pengo umepewa majibu manne. Chagua Jawabu lifaalo zaidi.

Binadarau ..................1................ kwa njia nyingi. ...................2............... njia  ................3.................. ni jinsi  ...............4................... mazingira yake kiholela. Hulka hiyo  .................5................. mapema, yeye mwenyewe, ...................6.......................... kwani ..............7................. Shughuli ya kutunza mazingira ni ...............8................... wetu sote ...............9................... hatutaki kuhasirika.

  1.                          
    1. amejipalia makaa
    2. amejitia hamnazo
    3. amekula njama
    4. amejipikia majungu
  2.                  
    1. Mojawapo wa
    2. Mojayapo ya
    3. Mojawapo ya
    4. Mojayapo wa
  3.                
    1. hiyo
    2. hizo
    3. hilo
    4. hayo
  4.              
    1. anayoyachafua
    2. anaoyachafua
    3. anapoyachafua
    4. anavyoyachafua
  5.            
    1. isingekomeshwa
    2. isiyokomeshwa
    3. isipokomeshwa
    4. ikikomeshwa
  6.                  
    1. ndiye atakayeathirika
    2. ndiwe ataathirika
    3. ndio atakayeathirika
    4. ndiyo atakayeathirika
  7.                
    1. mchelea mwana kulia hulia yeye
    2. mchimba kisima huingia mwenyewe
    3. majuto ni mjukuu huja baadaye
    4. mchuma janga hula na wa kwao
  8.                      
    1. mujibu
    2. jukumu
    3. dhima
    4. wajibu
  9.                
    1. ili
    2. japo
    3. iwapo
    4. ilhali

Ukuaji wa lugha ..................10.................... kutumia neno moja kuzalisha  ................11...................... Kwa mfano, kivumishi 'mwaminifu' kinaweza kutupatia nomino  ................12...................... Ukitaka kuwa  ....................13.................. katika lugha, ni .................14.....................  ujifunze kutumia upatanisho ufaao wa kisarufi. Maneno kama  .................15..................... huorodheshwa katika ngeli ya I-I.

  1.                    
    1. inahusu
    2. kunahusu
    3. unahusu
    4. zinahusu
  2.                
    1. nyingine
    2. jingine
    3. kingine
    4. kwingine
  3.                      
    1. uaminifu
    2. waaminifu
    3. kuaminifu
    4. aminika
  4.                
    1. mhodari
    2. jasiri
    3. mjuba
    4. stadi
  5.                
    1. kawaida kama sheria
    2. hakika kama mauti
    3. lazima kama ibada
    4. nadra kama kupatwa kwa jua
  6.              
    1. mikunga, mijusi na mijomba
    2. asali, miwani na amani
    3. mate, maziwa na mazingira
    4. mikoba, mibibo na mifumo

Kutoka swali 16-30, chagua jibu sahihi kulingana na maagizo

  1. Chagua sentensi yenye kiwakilishi cha idadi.
    1. Wanafunzi wote thelathini wamefaulu mtihani huo.
    2. Miji mingine ilikuwa na vurugu bali hii miwili ilikuwa na utulivu.
    3. Vijana wanapenda michezo ingawa wale wanapenda kuchora sana.
    4. Wengi hawakuamini kuwa mwimbaji yule alikuwa binamu yangu.
  2. Ni kifaa kipi anachotumia seremala kushikia vitu imara wakati anapofanya kazi?
    1. Jiriwa
    2. Timazi
    3. Kekee
    4. Mvukuto.
  3. Andika wingi wa sentensi ifuatayo. Waadhi uliopewa na buda huyo ulikufaa sana.
    1. Waadhi mliopewa na buda hao uliwafaa sana.
    2. Nyaadhi mliyopewa na buda hao iliwafaa sana.
    3. Nyaadhi mlizopewa na mabuda hao ziliwafaa sana.
    4. Waadhi mliopewa na mabuda hao uliwafaa sana.
  4. Bainisha matumizi ya kiambishi 'ka' katika sentensi.
    Badi alienda shambani akapanda miche. 
    1. Kuonyesha kufuatana kwa vitendo.
    2. Kuonyesha kuendelea kwa kitendo. 
    3. Kuonyesha kukamilika kwa vitendo.
    4. Kuonyesha kusudi la kitendo.
  5. Nahau ipi imeambatanishwa ipasavyo na maana yake?
    1. Fanya msirimbo-Fanya jambo kwa utaratibu.
    2. Fumba maneno - Weka siri.
    3. Piga vijembe Fanyia mtu ishara ya dharau.
    4. Iva macho-Ona aibu.
  6. Kanusha sentensi ifuatayo.
    Kamanda ametumwa nyumbani akamlete mzazi.
    1. Kamanda hakutumwa nyumbani akamlete mzazi.
    2. Kamanda hajatumwa nyumbani wala kumleta mzazi.
    3. Kamanda hatumwi hajamleta mzazi.
    4. Kamanda hajatumwa nyumbani akamlete mzazi.
  7. Chagua udogo wa senteni ifuatayo.
    Mtoto aliumia mkono alipogongwa na ukuta
    1. Toto liliumia kono lilipogongwa na kuta
    2. Kitoto kiliumia mkono kilipogongwa na kijikuta.
    3. Kitoto aliumia kikono alipogongwa na kijikuta
    4. Kitoto kiliumia kikono kilipogongwa na kijikuta.
  8. Tegua kitendawili kifuatacho. Mchana kutwa yupo ananizomea tu..
    1. Upepo
    2. Nzi 
    3. Jua
    4. Kivuli.
  9. Neno 'waliokosoana' lina silabi ngapi?
    1. 7
    2. 6
    3. 12
    4. 11
  10. Koko ni miti inayomea baharini. Koko pia ni
    1. vuta kirungu ili kuweka risasi ndani ya bunduki
    2. kinywaji kinachotokana na unga wa mbegu za mkakau
    3. mbegu ngumu iliyo ndani ya tunda
    4. kuondoa punje za mahindi kwenye kigunzi.
  11. Chagua sentensi iliyo katika nafsi ya pili wingi.
    1. Mtoto wako ametoroka.
    2. Nyadhifa zenu zimehifadhiwa.
    3. Wajapo kwetu tutawaelekeza. 
    4. Walimu wetu wameenda likizo.
  12. Jibu lipi linaonyesha aina za mashairi?
    1. Ngonjera, kibwagizo
    2. Utao, mloto
    3. Utenzi, takhmisa
    4. Tarbia, urari.
  13. Milima, mabonde, mito na bahari, vyote ni
    1. malighafi
    2. mandhari 
    3. madini
    4. maliasili.
  14. Chagua methali yenye maana sawa na
    'Usiache mbachao kwa mswala upitao
    1. Afadhali dooteni kama ambari kutanda.
    2. Kipya kinyemi kingawa kidonda. 
    3. Mfumai cha ndugu hufa maskini. 
    4. Mwanzo wa ngoma ni lele.
  15. Ikiwa mtondogoo itakuwa Jumanne, juzi ilikuwa siku gani?
    1. Jumatano 
    2. Jumatatu
    3. Jumapili 
    4. Alhamisi.

 Soma ufahamu kwa makini kisha ujibu maswali 31-40

Ama kukuli kuntu, imepita takriban miongo sita tangu taifa letu lilipojinyakulia uhuru mikononi mwa mabeberu. Maisha kabla ya uhuru yalikuwa usiku wa giza totoro. Mwafrika hakuidhinishwa kufaidi rasilimali za nchi wala kusoma elimu ya kumfaidi maishani. Kile kilichoitwa elimu wakati ule ni maneno machache yaliyonuiwa kumwezesha Mwafrika kupokea amri kutoka kwa mzungu. Mambo yalipomfika Mwafrika huyo kooni, aliamua mno ni mno, tangu hapo ikawa amani haiji ila kwa ncha ya upanga.

Mabeberu walipofunganya virago vyao na Mwafrika kutwaa hatamu za uongozi, nuru ya matumaini iliangaza kote nchini. Mwafrika alisadiki kuwa dhiki zake sasa ni mambo yaliyofukiwa katika kaburi la sahau. Wimbo wa amani, umoja na udugu ulitungwa ukaimbwa kwa mahadhi yaliyopokelewa vyema na raia wote. Ahadi nyingi zilitolewa na viongozi wa wakati huo. Hizi ni pamoja na elimu bora, kuangamiza maradhi na kuangamiza umaskini. Hata hivyo, ahadi hizi zimesalia katika vitabu vya kumbukumbu tu. Je, ni nini hasa kilichokwamisha juhudi za kufikia mafanikio hayo?

Tunaweza kusema kwamba aliondoka mkoloni wa kizungu akaja mkoloni wa kiafrika. Tuliodhani kuwa wakombozi wetu waligeuka kuwa wamba ngoma waliovuta ngozi kwao. Badala ya kuleta mwamko mpya, waliendeleza sera zilezile za watangulizi wao. Rasilimali za umma ziliporwa kwa manufaa ya watu binafsi. Wachache waliojaribu kupinga uhalifu huo

walinyamazishwa milele. Uligeuka kuwa ulirnwengu, wa mnyonge kupata haki ni mwenye nguvu kupenda.

Hatua nyingi zimependekezwa kama njia mwafaka ya kukabiliana na hali hii. Hizi ni pamoja na kuzinduliwa kwa katiba mpya, kubuniwa kwa sera mbalimbali na kufanyiwa marekebisho kwa asasi kama vile polisi na mahakama. Harakati za hivi punde zilihusiana na kubadilishwa kwa mfumo wa elimu kwa azma ya kuwawezesha wengi kujitegemea badala ya kutafuta kazi za ajira tu. Hata hivyo, juhudi kama hizi zitabaki ngoma gova iwapo mambo yanayokwamisha maendeleo hayatatafutiwa suluhisho la kudumu.

Kwanza, ni lazima rasilimali za nchi ziondolewe mikononi mwa watu binafsi ili zilifaidi taifa kwa jumla. Iweje madini yamfaidi mtu binafsi huku wazalendo wengine wakiambulia patupu? Halikadhalika, ufisadi ambao umekithiri kote nchini uangamizwe kwa njia inayofaa. Idara ya mahakama isitekwe na watu binafsi kwa lengo la kubadili mkondo wa sheria.

Tumewaona washukiwa wengi wa ufisadi wakikimbilia mahakamani ili wapewe vibali vya kuzuilia kutiwa mbaroni kwao. Iweje asasi inayopaswa kuzuia ufisadi ndiyo inayowasetiri mafisadi?

Ustawi wa jamii yetu utapatikana tu iwapo sote tutaukumbatia uzalendo. Raia mzalendo huwa tayari kuitetea nchi yake kwa hali na mali. Yeye na maovu huwa wamebaidika mithili ya ardhi na mbingu. Hana tamaa wala ubinafsi. Yeye huwajali ndugu zake bila kujali dini, jinsia, kabila wala tabaka. Huo ndio moyo tunaohitaji ili kulijenga taifa thabiti.

  1. Kulingana na aya ya kwanza, ni kweli kuwa
    1. ni zaidi ya miaka sitini tangu taifa lianze kujitawala
    2. ni karibu miaka sitini tangu taifa lianze kujitawala
    3. taifa lilitawaliwa na mabeberu kwa miongo sita
    4. taifa lilitawaliwa na mabeberu kwa takriban miongo sita.
  2. Si kweli kusema kuwa
    1. awali mwafrika hakupata elimu yoyote
    2. wakati wa ukoloni maisha ya mwafrika yaligubikwa na dhiki
    3. mwafrika alipata elimu duni wakati wa ukoloni
    4. wakoloni walitumia rasilimali za bara letu kujifaidi.
  3. Uhuru unaozungumziwa ulipatikana kwa njia ya
    1. maridhiano
    2. bahati nasibu
    3. maafikiano
    4. makabiliano.
  4. Maneno 'ahadi hizi zimesalia katika vitabu vya kumbukumbu tu' yana maana kuwa
    1. Mwafrika hakusomewa ahadi zilizowekwa
    2. ahadi zilizingatiwa muda mrefu uliopita
    3. ahadi zilizowekwa hazikutimizwa kamwe
    4. yaliwekwa malengo makubwa yasiyowezekana.
  5. Kilichozuia ustawi baada ya uhuru hasa ni
    1. ubinafsi wa wale waliotwaa madaraka 
    2. umaskini ambao tuliachiwa na mabeberu
    3. ukosefu wa maarifa wa wananchi wenyewe
    4. uhaba wa rasilimali katika taifa letu.
  6. Mfumo wa elimu ulibadilishwa ili 
    1. nafasi za ajira ziweze kuongezeka 
    2. watu binafsi wabuni njia za kujiimarisha kiuchumi
    3. kupunguza mzigo wa masomo kwa wanafunzi
    4. kuondoa mfumo duni tulioachiwa na wakoloni.
  7. Zitabaki ngoma gova' ndiko kusema
    1. hazitakuwa na manufaa 
    2. zitatufaidi ipasavyo
    3. zitapingwa na wananchi
    4. zitashabikiwa na wengi.
  8. Watu wanaokimbilia mahakamani kwa mujibu wa kifungu huwa na lengo lipi? 
    1. Kuwashtaki mafisadi.
    2. Kuepuka dhuluma za polisi.
    3. Kuepuka kukamatwa kutokana na uhalifu wao.
    4. Kuchukua vibali vya kushiriki njama za ufisadi.
  9. Kifungu yamebaidika mithili ya ardhi na mbingu' kimetumia tamathali gani ya usemi?
    1. Sitiari
    2. Chuku
    3. Kinaya
    4. Tashbihi.
  10. Aya ya mwisho inadokeza kwamba mzalendo
    1. huwajali watu wa taifa lake tu
    2. hana ubaguzi kwa yeyote
    3. hajali lolote kuhusu ufisadi
    4. huwatetea hata wanaolipuja taifa. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 41 hadi 50.

Makeke alikuwa mwanamume wa makamo. Hakuna mtu ambaye hakumfahamu kijijini kwa vitimbi vyake. La kushangaza ni kuwa ukimwuliza mwanakijiji yeyote, atakuambia kuwa hakuwahi kumwona Makeke akiwa si mlevi. Alizovaa hazikuwa nguo bali mararu tu. Ukija kwenye usafi wa mwili wake, msalie mtume tu! Uvundo aliotoa ulikithiri. Nzi, chawa, viroboto na mafunza walipata mazingira mwafaka katika mwili wake. Kwa bahati nzuri, alijijengea kijumba cha msonge nje ya makao ya mke na wanawe ili kuepuka kile alichoitwa 'udhia wa watoto na wanawake. Kwa njia hiyo aliwaepusha na wageni hao ambao hawakumbanduka mwilini mwake.

Familia hii ilikuwa na wana kumi na mmoja. Kati yao, hakuna aliyewahi kuliona lango la shule. Walikuwa kama vibarua wa kulihudumia shamba la Makeke. Awali, shamba hilo, ambalo Makeke alirithi kutoka kwa baba yake, lilikuwa kubwa. Hata hivyo, alianza kulipiga bei polepole ili apate darahima za kukinaisha hamu yake ya ugimbi. Mwishowe kilibaki kikataa kidogo tu. Kipato chote hiki kilimiminwa mifukoni mwa wagemaji haramu kijijini.

Kila asubuhi, Makeke aligawa majukumu kwa mkewe na wanawe. Wapo waliohitajika kumtafutia ng'ombe malisho, wa kulima na kupalilia miche shambani au kumwandalia uji wa wimbi ambao aliupenda sana. Meno yake yalidhoofika kiasi cha kutoweza kutafuna chakula kigumu. Macho yake nayo yalidhoofika yakabaki na nuru hafifu kama ya kikongwe aliyechungulia kuzimuni. Ilikuwa wazi kwamba uraibu wake ulimwacha taabani. Juhudi za mkewe za kujaribu kumwasa apunguze ulevi huo zilijibiwa kwa kipigo na matusi makali huku akionywa asimletec Makeke 'upuuzi wa wanawake. Tangu hapo, mkewe lake likawa jicho tu. Wanakijiji waliposhuhudia dhiki za watoto hawa ambao walivalia mavazi duni na kudhoofika kwa kukosa lishe bora, waliamua kuchukua hatua zifaazo. Walishika njia hadi kwa chifu wakamshtakia hali. Chifu naye aliandamana na wanakijiji hadi kwa Bwana Makeke. Walipofika, waliwakuta watoto wakifanya kazi shambani. Wakati huo, Makeke mwenyewe alikuwa ameshayoyomea zake ulevini. Chifu aliwaagiza askari wake wamsake kokote alikokuwa amlete kadamnasi.

Makeke alipofika na kuupata umati kwake, alikuja juu kama moto wa kifuu. Alitaka kujua aliyewapa kibali cha kumwingilia kwake bila idhini. Wananchi walijawa na hamaki wakataka kumtia adabu lakini Bwana chifu akawatahadharisha dhidi ya kuchukua sheria mikononi mwao.

Afisa wa maslahi ya watoto aliyekuwa miongoni mwa wanakijiji wale alimwelimisha Makeke na wale waliokuwepo kuhusu haki za watoto. Aliwaeleza kuwa ni jukumu sio tu la kila mzazi bali wananchi wote kuhakikisha kuwa mtoto anatimiziwa haki hizo. Haki zenyewe ni pamoja na lishe bora, mavazi, makazi, huduma za afya na elimu ya msingi miongoni mwa nyingine. Yeyote aliyepatikana na hatia ya kumdhulumu mtoto haki hizo alipaswa kukabiliwa na mkono mrefu wa sheria. Hayo yalimwacha Makeke akigwaya kwa hofu. Papo hapo, aliomba radhi kwa wote waliokuwepo. Akaahidi kutupa jongoo na mti wake.

Wanakijiji walipendekeza watoto wale wanunuliwe mavazi na nyenzo nyingine kutokana na hazina ya kustawisha kijiji ili waende shuleni. Chifu na Afisa wa maslahi ya watoto waliahidi kufuatilia kwa karibu malezi ya wana hawa. Makeke alionywa kuwa iwapo angeendeleza ukaidi wake asingeepuka mkono wa sheria.

Watoto walienda shuleni wakainukia kuwa wenye vichwa vyepesi. Waliendelea kuwasaidia wazazi baada ya masomo na wakati wa likizo. Hatimaye, walihitimu wakapata kazi katika sekta mbalimbali. Familia hii iliimarika sana kihali na kiuchumi. Ama kweli kuinamako ndiko kuinukako.

  1. Chagua maelezo sahihi kulingana na kifungu
    1. Ulevi ndio uliomfanya Makeke awe maarufu zaidi.
    2. Makeke alijulikana kutokana na vitendo vyake vya hila.
    3. Watu walimjua Makeke kwa umaskini wake.
    4. Wanakijiji walishangaa walipogundua ulevi wa Makeke.
  2. Madhara ya ulevi kwa jumla kulingana na kifungu ni
    1. kupunguza uwajibikaji
    2. kukaribisha vimelea
    3. kudhulumu familia
    4. kudhoofisha afya.
  3. Kwa nini Makeke hakuwapeleka wanawe shuleni?
    1. Elimu haikutiliwa maanani siku hizo.
    2. Yeye na mkewe hawakujua maana ya elimu.
    3. Alitaka wabaki nyumbani ili wafanye kazi.
    4. Umaskini ulimfanya ashindwe kuwapa mahitaji.
  4. Mkewe Makeke ni mwenye busara kwa kuwa
    1. alivumilia licha ya vitimbi vya mumewe
    2. aliwafahamisha wanakijiji hali ilipokithiri
    3. alijitenga ili asiathiriwe na vimelea kama mumewe
    4. alijaribu kumnasihi mumewe dhidi ya ulevi.
  5. Haki za watoto zilizokiukwa katika kifungu ni
    1. elimu na utangamano
    2. afya na makazi
    3. lishe bora na mavazi
    4. upendo na matibabu.
  6. Jambo lililomkera Bwana Makeke alipofika ni
    1. watoto kuacha kazi aliyawapa
    2. watu kufika kwake bila ruhusa
    3. kuitwa ulevini kabla ya kujitosheleza
    4. kutishiwa kuchukuliwa hatua na wanakijiji.
  7. Bwana Chifu aliagiza Makeke asakwe kokote alikokuwa aletwe kadamnasi. Hali hii inaonyesha kuwa
    1. serikali ina mkono mrefu
    2. watu walijua aliko Makeke
    3. chifu hakuwa na huruma
    4. hakutaka kuwaudhi wanakijiji.
  8. Funzo alilotoa Afisa wa maslahi ya watoto ni kwamba
    1. jukumu la kulinda haki za watoto ni la wazazi
    2. siku hizi watu hawakiuki haki za watoto kiholela
    3. watu wengi hawana habari kuhusu haki za watoto
    4. kila mwananchi ana jukumu la kulinda haki za watoto.
  9. Sifa za wanakijiji zinazojitokeza katika kifungu ni
    1. ukali na uwajibikaji
    2. ushirikiano na kujaliana maslahi
    3. uaminifu na maridhiano
    4. upendo na uvumilivu.
  10. Methali 'Kuinamako ndiko kuinukako' ina maana kuwa
    1. mahali kwenye mabonde kunaweza kubadilika na kuwa na mwinuko
    2. mtu mwovu anaweza kubadilika mwenendo akawa mwadilifu
    3. hali ya wanyonge inaweza kubadilika wawe wenye uwezo
    4. watu wanaozozana wanaweza kumaliza tofauti zao wakapatana.

 INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako.

Andika insha isiyopungua ukurasa mmoja na nusu ukifuata maagizo uliyopewa. Andika insha ya kusisimua itakayomalizika kwa maneno yafuatayo.

...................................................................................Alitimiza ahadi yake akayaacha maovu na kuwa mtu wa kutegemewa na jamii yake.

MAJIBU

swa cdadad

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students