Thursday, 13 April 2023 07:41

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 3

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza kila pengo kwa kuchagua Jawabu lifaalo zaidi.

Ni muhimu kwa mtu kujaribu kadri ...............1................kuwa na uhusiano....................2......................na wenzake popote alipo. Hata akipatwa na shida, ajue kuwa  ....................3.....................  ....................4..................... jamaa zake ....................5..................... watakaomfaa ....................6.....................  wale walio karibu naye. Jambo la ajabu ni kuwa watu wengi ....................7..................... na wenzao lakini hujipata wakikimbia kuwalilia hali pindi tu, ....................8..................... na maafa. Jamii yenye watu, ....................9..................... utangamano hupiga hatua kwa urahisi.

  1.                          
    1. awezalo
    2. awezavyo
    3. awezapo
    4. awezayo
  2.                                    
    1. wema
    2. njema
    3. jema
    4. mwema
  3.              
    1. Hamadi ni iliyo kibindoni
    2. Kwa mwoga huenda kicheko kwa shujaa huenda kilio
    3. Mkataa wengi ni mchawi
    4. Imara ya jembe kaingoje shambani
  4.                              
    1. :
    2. ;
    3. ,
    4. -
  5.                      
    1. ndio
    2. siyo
    3. sio
    4. sizo
  6.                          
    1. wala
    2. ingawa
    3. japo
    4. bali
  7.              
    1. hujitenga
    2. huwatenga
    3. hukutenga
    4. humtenga
  8.                
    1. wangefikwa
    2. wamefikwa
    3. wakifikwa
    4. wanafikwa
  9.                  
    1. wanaoudhamini
    2. wanaoithamini
    3. wanaoidhamini
    4. wanaouthamini

Hamu yangu ya kulielewa zaidi somo la kiswahili, .....................10...................  nimwendee mwalimu .....................11................... msaada. Nilimkuta .....................12................... akisahihisha madaftari ya wanafunzi nikamwomba nafasi ya kunena naye. Alianza kwa kunifunza kutenga silabi katika maneno. Kwa mfano, neno iliyojumlishwa lina silabi .....................13................... Pia, mwalimu aliniongoza kutambua vielezi kama vile: .....................14................... Hivi sasa nimeweza kutumia tamathali za usemi kama sitiari ninapoandika insha. Mfano wa sitiari ni .....................15...................

  1.                  
    1. ndilo lililonifanya
    2. ndio ilionifanya
    3. ndicho kilichonifanya
    4. ndiyo iliyonifanya
  2.              
    1. wa
    2. kwa
    3. na
    4. katika
  3.                
    1. maliwatoni
    2. pambajioni
    3. majilisini
    4. handakini
  4.                        
    1. 7
    2. 13
    3. 8
    4. 6
  5.                    
    1. gani, bora, laini
    2. dhidi ya, mithili, lau
    3. kiasi, tena, kwao
    4. yule, kama, kando
  6.                    
    1. Yakobo anatia akitoa
    2. Selemani ni lumbwi
    3. gari lilibingirika bingiribingiri
    4. miguu yangu imegomea safari

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, chagua jibu lifaalo zaidi.

  1. Chagua sentensi iliyotumia kiambishi ka kuonyesha kusudi la kufanya jambo
    1. Baba alienda shambani akalima kutwa nzima.
    2. Wavuvi wameenda baharini wakavue samaki.
    3. Alipika chajio akapakua akala akalala.
    4. "Jua limewaka sana msimu huu," akasema.
  2. Ni jozi ipi iliyo tofauti na nyingine?
    1. legeza - kaza
    2. nenda- rudi
    3. tii-kaidi
    4. tulia - nyamaza
  3. Andika ukubwa wa sentensi:
    Ndovu huyo ana mkonga mrefu.
    1. Jidovu hilo lina jikonga refu
    2. Dovu huyo ana mkonga mrefu 
    3. Dovu hilo lina konga refu
    4. Jidovu hilo linakonga lirefu
  4. Kipi ni kivumishi kilichoundwa kutokana na nomino?
    1. angalia - uangalifu
    2. mwangaza - angavu 
    3. aminika mwaminifu
    4. ucheshi kicheko
  5. Mtu akitaka kupishwa njia husemaje?
    1. simile
    2. kunradhi
    3. ashakum
    4. alamsiki
  6. Tambua nomino za ngeli ya U-YA pekee
    1. wimbi, mawele
    2. ugomvi, wasiwasi
    3. ua, ufito
    4. mabele, magonjwa
  7. Nini maana ya sentensi 'Angalijua unakoishi angalikuja kukutembelea.' 
    1. Alikuja kukutembelea lakini hakujua unakoishi
    2. Kutojua unakoishi ndiko kulikomfanya. asikutembelee
    3. Licha ya kujua unakoishi hakuja kukutembelea
    4. Akijua unakoishi atakuja kukutembelea 
  8. Chagua nahau iliyoambatanishwa ipasavyo na maana yake.
    1. Lilia ngoa - onea wivu
    2. Vilka kilemba cha ukoka - sema mtu kwa mafumbo
    3. Tia mrija - kumpa mtu msaada
    4. Mkono birika - kupenda kutoa msaada bila malipo
  9. Tegua kitendawili: Chepesi chavunja hata majengo.
    1. jiwe
    2. upepo
    3. nyundo
    4. kisu
  10. Andika usemi wa taarifa wa sentensi: Zela: Mwanangu, ukisoma kwa bidii utasaidia jamaa yetu kukabiliana na uchochole.
    1. Zela aliagizwa asome kwa bidii ili aisaidie jamaa yao kukabiliana na uchochole.
    2. Zela alimwambia mwanawe kuwa akisoma kwa bidii atasaidia jamaa yao kukabiliana na uchochole.
    3. Zela alimwambia mwanawe kuwa iwapo angesoma kwa bidii angesaidia jamaa yao kukabiliana na uchochole.
    4. Zela aliambiwa kuwa iwapo angesoma kwa bidii angesaidia jamaa yao kukabiliana na uchochole.
  11. Mkungu ni kwa ndizi lakini mkururo ni kwa ..............................................
    1. Watoto
    2. nyota
    3. waasi
    4. maembe
  12. Chagua kielezi katika sentensi ifuatayo. watoto watiifu na wapole aghalabu huwafurahisha wazazi wao.
    1. watiifu
    2. wapole
    3. wao
    4. aghalabu
  13. Ni maelezo yapi yaliyo sahihi?
    1. Mbia ni mshirika wa kibiashara lakini bia ni kinywaji kinacholevya.
    2. Vumba ni wayo wa mnyama lakini fumba ni harufu mbaya
    3. Daka ni kushika kitu kilichorushwa lakini taka ni kutoa yai katika kiloaka.
    4. Dhamana ni ubora wa kitu lakini thamani ni malipo atolewayo mtu ili apokee huduma.
  14. Chagua sentensi changamano kati ya hizi.
    1. Tuliwapelekea.
    2. Kasisi anaongoza ibada kanisani.
    3. Tuliwakaribisha kwetu lakini hawakuja.
    4. Daraja lililojengwa pale limeanza kutumika.
  15. Ni vyema mtu kuridhika na kile ambacho amejaliwa kupata badala ya kuvitamani vya wenzake.
    Chagua methali inayoambatana na kauli hii.
    1. Mwenye shoka hakosi kuni.
    2. Achanikaye kwenye mpini hafi njaa.
    3. Bura yangu sibadili na rehani.
    4. Mtumai cha ndugu hufa maskini. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 31-40

Bara la Afrika limejaliwa maliasili chungu nzima. Haya ni pamoja na mito, maanguko ya maji, wanyama pori, misitu, milima, madini na kadhalika. Si ajabu kwamba mabara mengi hulihusudu bara hili kutokana na ukwasi huu ambao wenyeji wake hawajaulalia wala kuuamkia. Je, kwa nini bara hili bado linaselelea katika lindi la ufukara licha ya ukwasi huo wote? Au ni yale ya kozi mwanamadada kulala njaa kupenda?

Ukosefu wa uongozi bora katika mengi ya mataifa haya ni kiini kimojawapo cha hali hii. Aghalabu, viongozi wengi huwa wamba ngozi wasiojali maslahi ya wakazi hata kidogo. Viongozi wa aina hii huchumia vibindo vyao tu bila kujali uchochole unaowaguguna wakazi wengine wa mataifa hayo. Viongozi wao hao hukwamilia madarakani huku wakitaka kutawala kwa miaka na dahari. Matokeo yake ni kudorora kwa hali ya kiuchumi katika mataifa husika.

Ukoloni mamboleo aidha umechangia kudhulumiwa kwa mataifa mengi kiuchumi. 'Misaada' hutolewa katika nchi hizi, huku masharti makali yakiwekwa ndiposa 'usaidizi' uweze kupatikana. Kati ya masharti hayo ni kwamba kampuni za kuchimba madini lazima zitoke katika mataifa ya wafadhili. Tujuavyo ni kuwa uso wa kufadhiliwa u chini na tangu hapo, wenyeji wa mataifa haya maskini huwa hawana lao ila tu kufuata maagizo yanayotolewa. Wakati mwingine viongozi hupakwa mafuta viganjani ili wapitishe sera zitakazoleta manufaa kwa wenye nguvu.

Elimu duni wanayopata wenyeji aidha hufanya viwanda viadimike kama wali wa daku. Katika hali hiyo, wenyeji hawana mahali pa kupeleka malighafi ila tu kuuza nje kwa bei ya kutupa. Hili nalo hutomelewa zaidi na wanunuzi wa bidhaa katika mataifa maskini ambao wana kasumba kwamba chochote kiagizwacho kutoka ughaibuni ni bora kuliko kilichoundiwa nchini. Kwa hivyo, wachache wanaodiriki kuanzisha viwanda nchini huambulia patupu kwa kukosa wateja wa bidhaa zao. Lakini tukichunguza kwa kina tutapata kuwa hivyo vilivyotoka katika mataifa ya kigeni ni vya hali ya chini zaidi.

Viwango vya juu vya ushuru ni tatizo jingine sugu kwa wawekezaji wa humu nchini na wale kigeni. Jambo hili hasa ndilo husababisha gharama ya bidhaa zilizoundiwa nchini kuwa juu kuliko zile zinazotolewa nje. Serikali inapaswa kuwapunguzia mzigo huu wawekezaji ikiwa wanatarajiwa kukabiliana na ushindani wa bidhaa kutoka nje.

Ni muhimu wananchi wawachague viongozi waadilifu ambao wana maono ya kuyaokoa mataifa yao. Voingozi kama hawa wataanzisha miradi ya kuzalisha nguvu za umeme, kuchimba na kutumia madini, kulinda mbuga za wanyama na kuepuka misaada na mikopo inayoambatana na masharti kandamizi. Vijana nao wahimizwe kutilia maanani elimu yao ili waje kufaidika wao na mataifa yao kwa jumla.

Huu ni wakati mwafaka wa mwafrika kujistahi Asipumbazwe na imani potovu kwamba ustaarabu hutoka tu uzunguni na kuwa chochote afanyacho mwafrika ni ushenzi. Yafaa sisi wenyewe tubuni na kutumia vyetu; tukishajitosheleza tuwauzie wao hao wageni ili tupate pesa za kigeni.

  1. Kulingana na aya ya kwanza,
    1. Maliasili ni utajiri unaopatikana pasipo na gharama yoyote.
    2. Afrika imezalisha maliasili kwa wingi kuliko mabara mengine.
    3. Maliasili ya kipekee hupatikana barani Afrika
    4. Afrika imeendelea kiasi cha kuonewa gere na mabara mengi.
  2. Viongozi wanalaumiwa katika kifungu kwa;
    1. ukosefu wa maarifa
    2. kutumia mabavu
    3. ubinafsi walio nao
    4. kutawala kwa muda mrefu
  3. Kauli 'uchochole unaowaguguna wakazi' imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. Kinaya
    2. tashhisi
    3. sitiari
    4. chuku
  4. Misaada inayotolewa na nchi za kigeni,
    1. haijalisaidia bara Afrika kwa vyovyote vile.
    2. inakashifiwa kwa viwango vya juu vya riba.
    3. yote hutolewa kwa nia ya kulifaidi bara hili.
    4. Mara nyingi huandamana na masharti ya kuwadhulumu wafadhiliwa.
  5. NI kweli kusema kuwa;
    1. mtu hujichagulia mwenyewe msaada atakaopata
    2. Kuwekewa vikwazo huwafanya wengi kukataa msaada
    3. Mtu anapotaka hisani huwa kama mtumwa asiye na uhuru
    4. Msaada hauwezi kumsaidia mtu kuinuka kiuchumi
  6. Hupakwa mafuta viganjani katika kifungu ni sawa na:
    1. kupumbazwa kwa maneno matamu
    2. kuhongwa
    3. kukashifiwa
    4. kutishiwa hali ya maisha
  7. Imani potovu anayozungumzia mwandishi katika kifungu ni kuwa;
    1. viwango vya elimu vinavyotolewa ni vya chini.
    2. bidhaa bora ni zile zinazonunuliwa nje ya nchi.
    3. malighafi yanafaa kutumika katika viwanda vya nchi.
    4. malighafi yanayouzwa nje hayaleti faida ifaayo.
  8. Kwa nini wawekezaji wanatatizika kuendesha shuguli zao nchini?
    1. Ushuru mkali nchini unawazuia kushindana na bidhaa zinazoagizwa kutoka nje.
    2. Bidhaa kutoka nje ya nchi zinatozwa ushuru wa juu zaidi.
    3. Wamekosa maarifa ya kuendesha shuguli zao ipasavyo.
    4. Nchi nyingi hazina nafasi zifaazo za kutumiwa na wawekezaji.
  9. Mwito wa mwandishi wa makala haya kwa mwafrika ni kuwa;
    1. ajiheshimu na kuwajibika ipasavyo
    2. aachane kabisa na ustaarabu wa kigeni 
    3. atumie rasilimali zake kikamilifu chochote kisitoke nje
    4. abadili mtindo wa kufanya mambo ili aige ya kizungu
  10. Neno 'hulihusudu' kulingana na muktadha lina maana ya
    1. kushangazwa na hali yake
    2. kujivunia hali yake
    3. kuvutiwa na hali yake
    4. kutamaushwa na hali yake. 

Soma makala yafuatayo kisha uilbu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50

Mapuya alitembea taratibu, akapiga kisogo makazi yake kuelekea kwenye kituo cha karibu cha kibiashara. Makazi haya aliyoita kwake sasa yalishageuka mahame baada ya mkewe kuwachukua wanawe wawili akarudi kwao kijijini alikotoka. Mapuya mwenyewe alipatikana pale kwa nadra mithili ya kupatwa kwa jua. Kila siku, alikuwa kiguu na njia kusaka ugimbi ambao tangu hapo ulikuwa ada yake. Hata unadhifu na kutafuta lishe bora sasa ni mambo aliyoyatia kapuni kabisa. Ukimsaili kini cha hali hii, jibu ni lile lile maisha hayana huruma kwake, ameenda nguu kabisa.

Siku hiyo, kinyume na ada yake, Mapuya alihisi hofu na ukiwa wa kipekee. Hakusita kujiuliza kiini cha hali hiyo kwani hakuwa mwanagenzi kamwe katika mchezo wa kupiga maji; kubugia kopo baada ya kopo. Alitulia kidogo nje ya banda milimouziwa pombe tumbo likanguruma kumkumbusha kuwa nalo lilikuwa likidai haki yako. Hapo alijiambia kuwa hata kileo chenyewe ni halall ya tumbo kwa hivyo hana haja ya kujali. Mara hiyo akajitoma bandani kwa vishindo.

Mie ndani, Mapuya alijibanza kwenye kona, akawatazama waliokuwemo kana kwamba ndipo anawaona kwa mara ya kwanza. Mwenzake mmoja aliduwezwa na hali ya Mapuya. akapaza sauti akamwuliza, Vipi leo mwenzangu ama huna chochote umekuja kurondea kama ilivyo ada? Wateja wengine mie bandani walivunjika mbavu huku moyo ukimwuma Mapuya kama aliyepigwa mshale wa sumu. Alivuta taswira akaiona hali yake ya kisogoni hadi kufikia hapo. Akajuta na kusikitika. Kwa hakika maisha yalikuwa yamempiga dharuba kali kiasi kisichosemeka.

Aliyakunjua maisha yake akaona siku zile alipokuwa akifanya kazi katika shirika moja la kuuza mitambo ya kielektroniki. Siku hizo, alivalia suti nadhifu zilizopigwa pasi zikanyoka mithili ya mwanzi. Mshahara wake ulikuwa wa kugugumiwa mate. Hili hasa lilitokana na kisomo chake kilichompa wadhifa wa juu katika shirika hilo. Alikuwa na kilakitu. Wanawe walisomea katika shule za kifahari. Mkewe alipaliliwa vyema kwa mavazi na mitindo aali ya nywele. Majirani walimwonea gere nao wanawe wakamwonea fahari.

Magwiji wa lugha waliamba kuwa pavumapo palilie si kazi kudamirika. Maisha yalipozidi kumtononokea Mapuya, alipata starehe mpya ya vileo na disko. Kwake, aliona hii ni njia mwafaka ya kulifuta jasho lake. Polepole, alianza kuzama kwenye kinamasi mzimamzima. Ulevi wake ulipokidhiri, wasimamizi wake walimwonya mara kadhaa. Hatimaye akaambiwa shirika hilo alione paa.

Baada ya kumwaga unga, shida zilimwandama Mapuya akaingilia uraibu wa pombe haramu ili kujipurukusha. Hivi ndivyo alivyojipata katika hali yake hii. Wakati haya yalipokuwa yakimpitia Mapuya akilini, alisikia mayowe makali kutoka kwa walevi mle bandani. Awali alidhani ni utani lakini mayowe yalipoongezeka huku wengine wakianguka na kutokwa povu midomoni ndipo alipokelewa nususi ya mambo. Dakika chache baadaye, wawili walikata roho wachache wakapofuka huku manusura wakibaki katika hali mahututi.

Baada ya kushuhudia hali ile, Mapuya alinyanyuka akachapuka chapuchapu kuelekea manzilini. Akilini alijikumbusha kauli ya wahenga kwamba, Fisi akimla mwele, mzima funga mlango. Aliamua kutupa jongoo na mti wake. Ingebidi atafute kazi angaa ya kijungujiko almradi we halali. Ikiwezekana, angemwendea mkewe amwangukie miguuni angaa ainusuru aila yake kabla mambo hayajaharibika kabisa.

  1. Chagua maelezo yaliyo sahihi.
    1. Mapuya na aila yake waliishi katika mahame
    2. Mapuya alifanya kazi katika kituo cha kibiashara hapo karibu
    3. Mapuya alikuwa akishiriki ulevi wa pombe kila siku
    4. Mapuya aliingilia ulevi pindi tu shida zilipomkabili
  2. Madhara ya pombe kulingana na kifungu hiki ni,
    1. Kukosa kula na ubovu wa mavazi 
    2. kuwa kiguu na njia, kukata tamaa 
    3. kuathirika kiafya, ukosefu wa mavazi 
    4. kukosa kuwajibika,kusambaratika kwa familia
  3. Mnamo siku ya tukio:
    1. Mapuya alikuwa na uhakika kuwa mambo yangeenda mrama
    2. Huzuni ya Mapuya iliongezeka kwa kuachwa na mke
    3. Mapuya alikosa utulivu akashindwa hata kutembea
    4. Hisia za Mapuya zilikuwa kinyume na jinsi alivyozoea
  4. Kwa nini Mapuya aliamua kutokula chakula?
    1. Kwa maoni yake, pombe ingemshibisha kama chakula
    2. Hakuwa na pesa za kununulia chakula chochote
    3. Ulevi aliozoea ulimmalizia hamu ya chakula
    4. Hakuwa na wakati wa kula kwani alikuwa ulevini wakati wote
  5. Ni kweli kuwa Mapuya,
    1. alikuwa afisa wa ngazi ya juu zaidi kazini
    2. awali aliwajibika katika kutunza familia 
    3. alipikiwa majungu na wakubwa wake akafutwa kazi
    4. aliacha kazi kwa hiari ili ashiriki ulevi 
  6. Mambo yafuatayo yanaonyesha jinsi Mapuya alivyokuwa na maisha mazuri ila, 
    1. suti nadhifu zilizopigwa pasi
    2. mshahara wa kugugumiwa mate 
    3. shirika lililouza mitambo ya kielekroniki
    4. wanawe kusomea katika shule za Kifahari
  7. Maana ya shirika hilo alione paa ni kuwa;
    1. alionywa dhidi ya ulevi
    2. alifukuzwa kazini
    3. alikumbushwa majukumu yake
    4. alitazama paa la shirika.
  8. Aya ya sita inadokeza kuwa:
    1. Mapuya alishiriki ulevi haramu ili kujisahaulisha madhila yake
    2. ulevi uliwafanya wenzake Mapuya wapige mayowe
    3. kushuhudia madhara ya wenzao kuliwafanya wengi wachanganyikiwe
    4. kuongezeka kwa mayowe kuliwafanya wengi wakate roho
  9. Methali 'Fisi akimla mwele, mzima funga mlango' inatuhimiza;
    1. wenzetu wakifikwa na shida tujiandae kwa zizo hizo
    2. wengine wanapohasirika tushukuru kwa kunusurika
    3. udhaifu wa wenzetu uwe njia yetu ya kujitetea
    4. wenzetu wakiingia taabani tuweke mikakati bora ya kujilinda
  10. Kulingana na kifungu hiki;
    1. Mapuya aliamua kufanya kazi yoyote hata kama haikubaliki
    2. Mapuya ameamua kuyarekebisha makosa yake kwa vyovyote vile
    3. Mapuya ameshindwa kabisa kukabiliana na hali yake
    4. Mapuya yuko radhi kufanya kazi yoyote inayohitaji nguvu nyingi

INSHA

SEHEMU B: KISWAHILI INSHA

Wewe ni kiranja mkuu katika shule yenu. Umechaguliwa kutoa hotuba kuhusu JINSI YA KUIMARISHA AFYA MAISHANI.

Andika hotuba hiyo.............................................

MWONGOZO

swa da 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 End Term Exams Term 1 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students