Wednesday, 05 July 2023 13:00

Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 3

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Kwa kila nafasi umepewa majibu manne hapo. Jaza pengo kwa kuchagua jawabu lifaalo zaidi.

Mvua .................1.................... kidindia usiku .................2.................... Maria na ndugu .................3.................... wawili .................4.................... kuenda shambani .................5.................... walitarajia kupanda mbegu za aina mbalimbali. Kwa hakika vijana hawa hawakuwa watu wa kulaza damu .................6.................... walielewa waziwazi kuwa .................7.................... Jua lilipokuwa mtikati yaani .................8...................., walikuwa tayari wamekamilisha shughuli .................9.................... kufanya wakashika njia kurudi chengoni.

  1.                        
    1. ulikuwa unanyesha
    2. ilikuwa imenyesha
    3. ikawa ilinyesha
    4. ulikuwa ukinyesha
  2.                
    1. kuchwa
    2. kutwa
    3. yote
    4. kucha
  3.              
    1. zake
    2. yake
    3. wake
    4. wao
  4.                              
    1. walishika tariki
    2. walichana mbuga
    3. walienda nguu
    4. walikula mwande
  5.                
    1. ambalo
    2. ambayo
    3. ambako
    4. ambao
  6.                        
    1. :
    2. -
    3. ...
    4. ;
  7.                    
    1. Mwangata mbili moja humporyoka
    2. Ajizi ni nyumba ya njaa
    3. Haba na haba hujaza kibaba
    4. Usiache mbachao kwa mswala upitao
  8.                          
    1. alasiri
    2. machweo
    3. adhuhuri
    4. mawio
  9.                      
    1. walilopaswa
    2. waliopaswa
    3. walizopaswa
    4. walipopaswa

Kipindupindu au .................10.................... ni maradhi hatari ambayo husababisha .................11.................... Uele huu .................12.................... haraka huweza kusababisha kifo. .................13.................... kuzuia maambukizi yenyewe, .................14.................... kuzingatia usafi wa mazingira, kuchemsha maji ya kunywa na kuosha mboga na matunda .................15....................

  1.                        
    1. kichocho
    2. hijabu
    3. homa ya matumbo
    4. waba
  2.              
    1. kuhara damu
    2. kuendesha na kutapika
    3. kukohoa damu
    4. kuumwa kichwa na koo
  3.                      
    1. usiotibiwa
    2. usivyotibiwa
    3. usipotibiwa
    4. usingetibiwa
  4.                  
    1. Ili
    2. Lau
    3. Angaa
    4. Japo
  5.                  
    1. hawana budi
    2. tuna budi
    3. wana budi
    4. hatuna budi
  6.                    
    1. yapasavyo
    2. ifaayo
    3. ipasavyo
    4. vifaavyo

Kuanzia nambari 16 mpaka 30, jibu kila swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Chagua sentensi yenye kivumishi.
    1. Migodi ya dhahabu imefunguliwa kijijini.
    2. Shangazi alijifungua salama salimini.
    3. Wageni waliotarajiwa watafika baadaye.
    4. Kilichopotea jana kimepatikana.
  2. Andika wingi wa sentensi: Uwanja utakaochezewa mechi hiyo umeandaliwa.
    1. Viwanja vitakavyochezewa mechi hiyo umeandaliwa.
    2. Nyanja itakayochezewa mechi hizo imeandaliwa.
    3. Uwanja utakaochezewa mechi hizo umeandaliwa.
    4. Nyanja zitakazochezewa mechi hizo zimeandaliwa.
  3. Ni sentensi ipi iliyo katika hali timilifu?
    1. Naenda sokoni kununua mboga.
    2. Vijana hawajawapuuza wazee wao.
    3. Gari unaloliona haliendi mjini.
    4. Mjomba angenihitaji angenipigia simu.
  4. Mahali mahakamani anaposimama mshtakiwa wakati wa kesi huitwaje?
    1. Rumande.
    2. Dungu.
    3. Kizimba.
    4. Seli.
  5. Bainisha sentensi yenye na ya kiunganishi.
    1. Nguo ya mtoto ilifuliwa na kijakazi.
    2. Waashi wanaiczeka nyumba nyingine mtaani.
    3. Kidake ana kitabu kipya cha hadithi.
    4. Kasisi na waumini watakutana kwa ibada kesho.
  6. Andika kinyume cha sentensi hii: Mjomba amemnunua mtamba mkubwa.
    1. Mjomba amemwuza mtamba mdogo.
    2. Shangazi amemnunua fahali mkubwa.
    3. Ilalati amemwuza fahali mdogo."
    4. Shangazi amemnunua mtamba mdogo.
  7. Sentensi Amina amepigiwa simu' ina maana mbili. Zichague.
    1. Simu imepigwa kwa Amina. Simu iliyopigwa ni ya Amina.
    2. Simu ya Amina imetumika kumpigia. Simu imepigwa na Amina na mwenzake.
    3. Simu imepigwa kwa niaba ya Amina. Simu imepigwa ili kuwasiliana na Amina.
    4. Simu ya Amina imepigwa. Amina amempigia mwingine simu.
  8. Legea ni kwa legevu kama vile cheka ni kwa
    1. kicheko.
    2. chekesha.
    3. ucheshi.
    4. mcheshi.
  9. Unganisha: Kiatu kilikuwa kizuri. Kiatu hakikumtoshea.
    1. Licha ya kiatu kuwa kizuri hakikumtoshea.
    2. Aghalabu kiatu kilikuwa kizuri hakikumtoshea.
    3. Kiatu kilikuwa kizuri maadamu hakikumtoshea.
    4. Angaa kiatu kilikuwa kizuri hakikumtoshea.
  10.  Nomino ipi ya makundi ni sahihi?
    1. Seti ya nafaka.
    2. Jopo la mwandishi.
    3. Korija ya mvua.
    4. Kaumu ya sungura.
  11. Kanusha: Sayo alikimbia kwa kasi akashinda mbio hizo.
    1. Sayo hakukimbia kwa kasi wala hakushinda mbio hizo.
    2. Sayo hajakimbia kwa kasi wala kushinda mbio hizo.
    3. Sayo hakukimbia kwa kasi wala kushinda mbio hizo.
    4. Sayo hakukimbia kwa kasi wala hajashinda mbio hizo.
  12. Ipi ni tashbihi?
    1. Mwadime anatia akitoa.
    2. Mnyoofu kama kondoo.
    3. Shikuku ni sungura.
    4. Mwili wangu ulikataa kuenda
  13. Mtu anayefua visu huitwaje?
    1. Sogora.
    2. Mhunzi.
    3. Mjume.
    4. Mjumu.
  14. Chagua sentensi iliyoakifishwa ipasavyo.
    1. Bwana Juma - yule mwalimu mgeni - amepandishwa cheo.
    2. Twende (akasema rafiki yangu) lau sivyo tutachelewa.
    3. Aisha, dada, yangu mkubwa amefanya harusi.
    4. Je? Mzazi wako amefika mkutanoni?
  15. Ni methali zipi zilizo na maana sawa kati ya hizi?
    1. Maji ya kifuu ni bahari ya chungu. 
    2. Konzi ya maji yamkifu mtoto.
    3. Papo kwa papo kamba kukata jiwe.
    4. Maji yaliyotulia yana kina kirefu.
      1. (i), (iv)
      2. (i), (ii) 
      3. (iii), (iv)
      4. (ii), (iv) 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali kuanzia 31 mpaka 40
Naikumbuka siku hiyo vizuri kana kwamba ilikuwa ni jana au juzi tu. Kama kawaida, mama alikuwa ameenda cheteni kuuza mboga na matunda. Baba naye alikuwa ameandama shughuli zake za uashi katika jengo moja huko mjini. Ilikuwa kawaida yangu kubaki na mnuna wangu. Basi siku ile, ilivyokuwa ada, nilimlisha, nikamwosha na kumvika yale tuliyoita mavazi japo hayakusetiri viungo vyetu barabara. Hata hivyo mtaa wetu ulisheheni watoto kufu yetu, wengine hata hali zao za kiafya, mavazi na mtindo wa maisha kwa jumla zilikuwa mbaya zaidi.

Mabanda tuliyoita nyumbani yalisongamana sana. Mara nyingi, sisi watoto tulienda kuchezea katika eneo moja wazi lililokuwa katikati ya reli na barabara moja pale mtaani. Eneo hili lilikuwa na jaa lililohanikiza uvundo wa kila aina. Hapo ungewaona walalahoi waliozumbua riziki yao kwa kusaka vyuma, fnakombo na chupa za plastiki mumo humo jaani. Waling'ang'ania nafasi hii na nguruwe, mbuzi, ng'ombe na ndege wa porini kama kunguru. Wageni nao walichepukia mbali kidogo huku wakiziba pua zao kujisetiri na uvundo huo uliokirihi. Ajabu ni kuwa kile kilichoonekana kama taka na wengine kiligeuka chanzo cha kupata riziki kwa idadi kubwa ya viumbe.

Tulipiga milundi, tukavuka mitaro ya majitaka na kujipenyeza katikati ya mabanda. Hatimaye tulifika kwenye eneo lile la kuchezea. Mara kwa mara nilimshika ndugu yangu mkono, asije kubwagwa na mahamali ambao aghalabu walipita bila simile. Tuliwakuta wenzetu ambao aghalabu walicheza katika makundi. Michezo ilipangwa kulingana na hirimu ya wachezaji wenyewe. Wadogo wetu walishiriki kibe, gungwi na kibafute miongoni mwa michezo mingine. Kwa upande wetu, tulitumia karatasi kujitengenezea mipira ili angaa tushiriki kipute.

Mchezo ulipokuwa umetunogea, nilisikia Rindo kikali si mbali sana kutoka pale tulipokuwa. Shughuli zote zilisitishwa ghafla kila mmoja adaposhikulikoshuhudiwa kishindo kile. Akili zangu ziliduru mara moja kwani sikumbha mugu Sijui nilikopata nguvu kama za buldoza nikausukuma umati hadi pale katikati. Mnung vangura kuwa amelala kingalingali huku akivuja damu kwa wingi. Alikuwa katika hali ya kutisha Wenzake walikuwa wakijaribu kumpangusa ngeu ile huku wakimwita licha ya umri wao mdogo.

Nilikimbia huku na kule nikilia kama mwchu. Kwa nyota ya jaha, msamariamwema mmoja alisimamisha gari akamchukua majeruhi. Mama mmoja alinishika mkono tukaingia garini huku likiondoka kwa kasi. Safari yetu ilitia nanga katika hospitali moja ya kibinafsi. Wahudumu walishikilia kuwa ndugu yangu asingehudumiwa minghairi ya kutoa arbuni. "Vipi nyinyi! Yaani mnathamini fulusi zaidi ya uhai wa binadamu? Mbona hivi lakini.?" Msamariamwema yule alisaili kwa ukali.

Hali ilipozidi kutokota, alitoa kitambulisho chake cha kazi. Kumbe alikuwa mhariri mkuu katika idhaa moja ya runinga. Wauguzi na matabibu walipoyaona haya, walimchukua mnuna wangu kwa haraka na kumpeleka katika chumba cha matibabu ya dharura. Yamkini waliogopa kuwa uozo na ubaguzi katika utoaji huduma pale hospitalini ungemulikwa na kuisambaratisha biashara yao.

Mkurugenzi wa hospitali ile alimwita chemba msaidizi wetu. Sijui walijadiliana kuhusu nini. Hatimaye niliruhusiwa kuingia katika wodi kumwona mdogo wangu ambaye alikuwa amelala na kutulia baada ya kupewa dawa ya kupunguza maumivu. Kule nje, shughuli ziliendelea kana kwamba hakuna lolote lililojiri. Kwa wengine, mkasa uliotusibu haukuwahusu ndewe wala sikio.

Mbio za sakafuni huishia ukingoni. Muda mfupi baadaye, polisi walifika na kueleza kwamba walishamtia nguvuni dereva aliyesababisha ajali kwa kuendesha gari kwa kasi huku amepiga maji. Waliomba idhini ya kunihoji ili wapate taarifa zaidi. Hata sikumbuki niliyowaambia kwani akili yangu ilikuwa kwa mnuna wangu wakati huo wote.

  1. Chagua jibu lililo sahihi.
    1. Matukio ya kifungu yalifanyika siku chache zilizopita.
    2. Wazazi wa mwandishi walifanya. kazi za kijungujiko.
    3. Mama wa msimulizi alikuwa mchuuzi.
    4. Baba alikuwa akiijengea familia nyumba yao mtaani.
  2. Mwandishi anasema kuwa;"
    1. kunao waliokuwa na hali mbaya zaidi yake mtaani.
    2. wote walioishi katika mtaa wao walikuwa katika hali sawa.
    3. familia yao ndiyo iliyokuwa na mavazi bora mtaani.
    4. hali yao ilikuwa mbaya kuliko jamaa nyingine mtaani.
  3. Jaa linalozungumziwa
    1. lilitatiza usafiri katika barabara na reli.
    2. lilitumiwa na wakazi wote kujitafutia riziki.
    3. lilikuwa sehemu ya watoto kuchezea kote mtaani.
    4. liliwafaidi wengi licha ya madhara kwa wengine.
  4. Kile kilichoonekana kama taka na wengine kiligeuka chanzo cha kupata riziki kwa idadi kubwa ya viumbe.'
    Chagua methali inayolandana na kifungu hiki cha maneno.
    1. Mkulima ni mmoja walaji ni wengi.
    2. Ganda la muwa la jana chungu kaona kivumo.
    3. Lake mtu halimtapishi bali humchefusha.
    4. Mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
  5. Michezo walioshiriki watoto,
    1. ilitegemea umri wa washiriki na vifaa katika mazingira.
    2. ilichezwa na watoto wadogo huku wakubwa wao wakiwalinda.
    3. ilikatizwa mara kwa mara na tishio la usalama.
    4. iliwabagua waliokuwa wadogo kiumri.
  6. Yamkini kishindo walichosikia msimulizi na wenzake kilisababishwa ha;
    1. kupita kwa garimoshi hapo karibu. 
    2. kupigwa dafrau kwa mnuna wake.
    3. michezo waliyoshiriki watoto - uwanjani.
    4. kupita kwa gari katika mwendo wa kasi.
  7. Si kweli kusema kuwa;
    1. Watoto walijaribu kumpa mwenzao msaada.
    2. Wahusika katika kifungu walijaliana maslahi.
    3. Msimulizi alimpata nduguye akiwa amelalia mgongo.
    4. Mwandishi alijulikana kwa nguvit zake za buldoza.
  8. Hatimaye wahudumu walimshughulikia nduguye msimulizi kwa kuwa.
    1. ada iliyohitajika ililipiwa kikamilifi 
    2. waliamrishwa kufanya hivyo na mkurugenzi wao.
    3. walihofia uovu wao kufichuliwa katika vyombo vya habari.
    4. walihofia vitisho alivyovitoa msamaria mwema.
  9. Maana ya alimwita chemba ni kuwa
    1. alizungumza naye hadharani.
    2. alimwomba radhi.
    3. alisema naye faraghani.
    4. alimpigia simu.
  10. Msimulizi anasema kwamba hajui alivyowajibu askari kwa kuwa:
    1. alikuwa mdogo sana.
    2. aliwaogopa polisi.
    3. amesahau mambo mengi.
    4. alitatizwa na hali ya nduguye. 

Soma kifungu hiki kisha ujibu maswali kuanzia nambari 41 mpaka 50
Malezi ya watoto yamekumbwa na changamoto anuwai. Hali hii inatishia mustakabali wa jamii kwani huenda tukakosa wa kupokeza usukani wakati utendakazi wetu utakapodidimizwa na umri. Hatua za dharura na za hakika hazina budi kuchukuliwa ikiwa tunataka kuliokoa jahazi letu kabla halijagonga mwamba. Lau sivyo, tutaishia kujiuma kidole mambo yakituendea mrama.

Hapo zamani, jukumu la kuwatunza watoto lilikuwa la jamii nzima. Hakika ilijulikana na wote kuwa mkono mmoja haumlci mwana. Hata pale wazazi wa mtoto walipotangulia mbele ya haki kabla mtoto mwenyewe hajakomaa na kuwa mtu mzima, walezi wengine walichipuka miongoni mwa familia, majirani au hata jamaa wengine ambao hawakuhusiana na mtoto huyo kwa damu wala usaha. Kwa njia hiyo, watoto wote walipata malezi yafhayo katika jamii.

Siku hizi mambo yamebadilika sana. Wavycle wengi wanawajali tu wanao huku wakiwapuuza mayatima na watoto. Kwa kukosa walezi wa kuwatunza, watoto wengine wasiobahatika katika jamii. Si ajabu kumwona mtoto akifanya mambo ya kuhatarisha maisha yake au wanajamii wengine huku watu wazima wamemkodolea macho tu na kujitia hamnazo. Ukiwasaili kuhusu kiini cha hali hiyo, watakujibu kuwa wanaogopa kubwekewa na wazazi wa mtoto huyo au 'Kila mmoja ajibcbee mzigo wake'. Wasilolijua watu kama hawa ni kuwa mtego wa panya huwanasa waliokuwemo na wasiokuwemo. Athari za matendo mabaya katika jamii hazichagui ni nani atakayehasirika.

Kuwanyima watoto malezi yafaayo kumewasababishia dhiki chungu nzima katika jamii. Kati ya dhiki hizo ni ajira ya watoto wenyewe hutafuta ajira za kijungujiko ili kujikimu. Wengi wa hawa hufanyishwa kazi za sulubu ambazo huwaathiri kiafya na ukuaji wao kwa jumla. Ilali hii aidha huendeleza ukuaji zaidi kwani hawapati fursa ya kubugia elimu ambayo ingewabadilishia mustakabali wao.

Kuna wale ambao huangukia mikono ya watu katili ambao huwaingiza katika ndoa za mapema, mila potovu kama vile wizi wa mifugo na dhuluma za kimapenzi. Madhalimu hao hawabagui umri wala jinsia bali huwakandamiza watoto hao bila kujali.

Jamii haina budi kuchukua hatua zifaazo kuhusiana na malezi ya watoto. Hili likipuuzwa, huenda tukaishia kujenga ukuta baada ya kupuuza kuziba ufa. Yeyote. asijipakatic mikono, na kusema 'kila mtoto ana mzazi au jamaa zake Tujue kuwa walezi wa kweli ni mimi na wewe. Tujali maslahi ya watoto na kuwalindia haki zao.

  1. Changamoto anuwai ni sawa na
    1. matatizo ya aina nyingi. 
    2. dhiki mbaya zaidi.
    3. vishawishi vya kushangaza.
    4. madhila madogomadogo.
  2. Tatizo linaloikodolea macho jamii kulingana na aya ya kwanza ni;
    1. kudhoofika kwa watendakazi 
    2. kukosa warithi.
    3. kukosa watoto
    4. kuvurugika kwa malezi.
  3. Mwandishi anasema kwamba hapo zamani;
    1. kila mzazi aliwalea wanawe tu ipasavyo.
    2. mayatima hawakuwa wengi ilivyo sasa.
    3. watoto waliwaogopa watu wazima kote.
    4. wanajamii walishirikiana katika malezi ya wana.
  4. Mtoto kufanya maovu machoni pa watu wazima bila kukanywa ni ishara ya;.
    1. dhuluma wanazofanyiwa watoto.
    2. kupotoka kwa vijana wasiojali maonyo.
    3. ubaguzi wa baadhi ya watu katika malezi.
    4. hofu waliyo nayo watu dhidi ya watoto wa majirani.
  5. Msemo kujitia hamnazo unarejelea tabia ya wanajamii ya;
    1. kujitia hatarini.
    2. kujifanya hawana habari
    3. kujifanya wanajua mengi.
    4. kujitia moyo kwenye tatizo.
  6. Ni kweli kusema kuwa,
    1. wapo wazazi wanaopinga kukosolewa kwa wanao.
    2. jukumu la kumrekebisha mtoto ni la mzazi pekee.
    3. shida zinazowakabili watoto wote ni za kujiletea.
    4. zamani hakukuwa na mayatima kama ilivyo sasa.
  7. Mwandishi anatuonya dhidi ya kupuuza matendo mabaya ya baadhi ya watoto kwa kuwa,
    1. shida ikitokea tutalaumiwa sote. 
    2. watoto wakiachwa wataharibika wote.
    3. maovu yakitendeka atawaathiri wahusika peke yao.
    4. madhara yakitokea tutaathirika sote.
  8. Madhara ya ajira ya watoto ni pamoja
    1. kulipwa mshahara duni, kupunguza umaskini.
    2. kudumaza ukuaji, maradhi ya kuambukiza.
    3. kuathirika kiafya, kuwanyima haki Sala ya elimu.
    4. kazi za sulubu, kuimarisha utangamano.
  9. Dhuluma want zopitia watoto si pamoja na;
    1. kudhalilishwa kingono.
    2. kuozwa wakiwa wachanga.
    3. kushirikishwa katika uhalifu. 
    4. kupewa ajira ya kuwakimu.
  10. Kichwa kifaacho zaidi kwa makala haya ni:
    1. Ajira ya watoto
    2. Haki za watoto
    3. Usipoziba u fa utajenga ukuta
    4. Tamaa mbele mauti nyuma. 

INSHA

Umepewa dakika 40 kuandika insha yako. Malizia insha kwa maneno yafuatayo huku ukiifanya iwe ya kusisimua zaidi.

............................................................................................................. bNilimshukuru Mungu nilipoamka na kugundua kuwa ilikuwa ni ndoto tu.

MWONGOZO

swa 3

 

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Class 8 Opener Exams Term 2 2023 Set 3.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students