Friday, 28 October 2022 12:16

Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End of Term 3 November 2022 Exams Set 2

Share via Whatsapp

MASWALI

Soma mazungumzo yafuatayo kisha ujibu maswali 1-5.
(Ni wakati wa mapumziko mafupi. Koi na Rao wameketi chini ya mti wakiwatazama wenzao wakicheza uwanjani.)

Koi: Sijui ni kwa nini siku hizi maradhi yanayohusiana na vyakula vichafu yamekuwa mengi hivi. Licha ya Roda, hata Hamisi anaendesha. (Akirusha jiwe dogo mbali kidogo)

Rao: (Akionyesha uso wa mshangao.) Ala! Hata Hamisi anaugua? Ndiyo maana hawakuja shuleni leo.(Muda unapita)Lakini kuna njia kadhaa za kupambana na magonjwa ya tumbo.

Koi: Ni kweli Rao. Kabla ya kula, ni sharti tuinawe mikono ili kuondoa uchafu. Mikono aidha hustahili kusafishwa kila baada ya kutoka msalani kujisaidia.

Rao: Naam, vyakula viliwavyo bila kupikwa kama vile matunda hustahili kuoshwa vizuri kabla ya kula. (Wamezama katika mawazo)

Koi: Nakumbuka pia mwalimu Kazamoyo akitushauri kupika vyakula kama vile nyama hadi viive vizuri.

Rao: Kwa nini Koi? (Akimsogelea)

Koi: Nyama ambayo haijapikwa ikapikika huweza kuwa na viini hatari vinavyoweza kusababisha maradhi mabaya ya tumbo.

Rao: Lo! Nitazingatia haya yote ili niwe salama. Sitaki kukaa nyumbani kwa ajili ya ugonjwa ilhali mtihani unakaribia. (Kengele inakirizwa. Wanaamka kuelekea
darasani mwao)

Koi: Leo jioni baada ya masomo, tupitie kwa kina Roda na Hamisi ili kuwajulia hali, sawa? (Rao anakubali kwa ishara ya kichwa)

  1. Moja kati ya magonjwa yanayozungumziwa hapa ni
    1. malaria. 
    2. UKIMWI. 
    3. kuendesha. 
    4. kifafa.
  2. Wanafunzi wanaougua ni 
    1. Koi na Hamisi.
    2. Rao na Koi. 
    3. Roda na Rao. 
    4. Hamisi na Roda.
  3. Inawezekana kuwa msalani ni 
    1. chooni. 
    2. shuleni. 
    3. darasani. 
    4. uwanjani.
  4. Kulingana na mazungumzo haya, nyama ambayo haijapikwa vizuri huweza kuwa na · 
    1. ladha ya kuvutia.
    2. viini hatari. 
    3. rangi ya kuvutia. 
    4. harufu nzuri mno.
  5. Baada ya kengele kukirizwa, Rao na Koi 
    1. waliwatembelea Roda na Hamisi. 
    2. walielekea uwanjani. 
    3. walikaa chini ya mti. 
    4. walielekea darasani. 

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 6 hadi 8.
Mimi na familia yangu tunaishi katika nyumba kubwa sana. Mimi ndimi mtoto wa pekee katika familia yangu, yaani, sina dada wala kaka. Baba yangu ni mwalimu katika shule ya msingi ya Nyotanjema naye mama yangu ni mwuguzi katika hospitali ya Ponaupesi. Baba yangu anayo magari mawili, moja jekundu na jingine jeusi. Hata hivyo, mara nyingi yeye hulitumia lile jeusi. Yeye hunipeleka shuleni kila asubuhi.
Ninaye mbwa nimpendaye. Mbwa huyo anaitwa Papi. Kila Jumamosi, mimi humwosha na kuyachana manyoya yake. Ingawa mimi ndimi mtoto wa pekee, sijihisi mpweke. Ninao wazazi na mbwa ambao huwa nami ninapowahitaji.

  1. Kulingana na taarifa, si kweli kusema kuwa 
    1. mwandishi hana dada. 
    2. katika nyumba hiyo, kunao watu watatu tu.
    3. mwandishi humsafisha mbwa wake kila siku. 
    4. mwandishi hajihisi mpweke.
  2. Baba wa mwandishi ana
    1. magari mawili na nyumba kubwa. 
    2. gari moja jeusi na mbwa mmoja.
    3. mbwa na gari jekundu. 
    4. nyumba kubwa na mbwa.
  3. Papi ni
    1. paka wa mwandishi. 
    2. mbwa. 
    3. rafiki wa mwandishi. 
    4. mama wa mwandishi.
  4. Ni nani huwa na mwandishi anapokuwa mpweke? 
    1. Marafiki zake. 
    2. Watu wa ukoo wake. 
    3. Mbwa wake na wazazi wake. 
    4. Mbwa wake.

Soma kifungu kafuatacho kisha ujibu maswali 10 hadi 12.
Jumamosi hiyo ni moja kati ya zile ambazo siwezi kuzisahau. Ilikuwa asubuhi angavu. ve joto kiasi na upepo uliovuma kwa maringo ya tausi jike. Huko juu, ndege waliimba na kuruka ovyo kutoka tawi hadi tawi. Hakika, ilikuwa ni siku ambayo wenyeji wa Kokotoa walikuwa wameisubiri kwa hamu.
Chaurembo na Ramadhani wangefunga ndoa. Harusi yenyewe ilikuwa katika kanisa la Hosana. Maarusi walipofika, watu walikusanyika wakiimba na kucheza kwa furaha. Baada ya harusi, wageni walikula na kunywa kwa furaha. Baadaye, kila mmoja alijiendea zake akiwa na furaha tele.

  1. Kulingana na kifungu, harusi hii ilikuwa lini? 
    1. Jumapili. 
    2. Jumamosi. 
    3. Jumatatu. 
    4. Ijumaa.
  2. Mwandishi wa taarifa hii ana maana gani anaposema huko juu
    1. Mtini. 
    2. Majini.
    3. Kanisani. 
    4. Nyumbani.
  3. Watu walikusanyika, kuimba na kucheza 
    1. baada ya kula na kunywa. 
    2. wakienda nyumbani. 
    3. maarusi walipoingia.
    4. nyumbani kwao. 

Soma kifungu kafuatacho kisha ujibu maswali 13 hadi 15.
Dukakuu la Tulizo liko katika kaunti ya Konambaya. Ingawa kunayo madukakuu mengine, Tulizo ndilo kubwa zaidi. Limejengwa kando ya barabara kuu ya Jogoo katikati ya kituo cha polisi cha Pingu na soko la Malimali. Mwenye duka hilo anaitwa bwana Sahara. Bwana Sahara amewaajiri wafanyakazi sita. Wengi wao ni wanaume. Hata hivyo, wanawake wachache waliomo hufanya kazi nyepesi nyepesi tu.
Bwana Sahara huhakikisha kuwa wateja wote wamehudumiwa vyema. Huwataka waende wakiwa wameridhika, Wakazi wengi hulipenda duka hili la bwana Sahara kwa sababu humo, wao hupata kila wanachohitaji kutoka unga hadi matunda

  1. Kulingana na habari, ni kweli kusema kuwa
    1. kunayo maduka mengine makubwa Konambaya. 
    2. barabara ya Jogoo iko kati ya soko na kituo cha polisi. 
    3. bwana Sahara hawezi kufanya kazi peke yake dukani mle. 
    4. kuna bidhaa chache dukani Tulizo.
  2. Dukakuu la Tulizo limejengwa 
    1. kando ya barabara kuu ya Jogoo. 
    2. nyuma ya soko la Malimali. 
    3. mbele ya kituo cha poliso cha Pingu. 
    4. juu ya kaunti ya Konambaya.
  3. Wakazi wanalipenda duka hili kwa kuwa 
    1. bidhaa huuzwa kwa bei rahisi. 
    2. wanunuzi hupata bidhaa wanazohitaji.
    3. bwana Sahara hupenda wateja wake wakifurahi. 
    4. kuna unga na matunda kwa wingi. 

Soma kifungu kifuatacho. Chagua jibu lifaalo zaidi kati ya yale uliyopewa tamu ilinukia.

Fisi _____16_____ na njaa, aliamua kuelekea sehemu ambayo harufu ya _____17_____ yake, Alipofika katika njiapanda, hakujua aelekee kushoto au_____18_____ .Kwa ajili ya _____19_____ aliamua kuzifuata njia zote mbili. Hapo ndipo alipasuka na_____20_____ papo hapo.

  1.                  
    1. alipozidi
    2. alizidisha
    3. alipozidishwa
    4. alipozidiwa
  2.            
    1. chakula
    2. mate
    3. nyama
    4. viazi
  3.                 
    1.  kulia
    2. kucheka
    3. katikati
    4. nyuma
  4.                  
    1. bidii 
    2. tamaa
    3. utamu
    4. kutamani
  5.            
    1. kula
    2. kushiba
    3. kufufuka
    4. kufa

Katika suala 21-30. jibu swali kulingana na maagizo uliyopewa.

  1. Kitenzi shinda katika kauli ya kutendwa huwa 
    1. shindana.
    2. shindwa.
    3. shindika.
    4. shindiwa.
  2. Chagua orodha ya wanyama wa porini pekee. 
    1. Ngiri, kifaru, twiga.
    2. Punda, ngiri, mbogo. 
    3. Paa, ndovu, ngamia.
    4. Nguruwe, paka, mbwa.
  3. Shida ni kwa tatizo kama vile televisheni ni kwa
    1. redio.
    2. rununu.
    3. runinga.
    4. barua
  4. Ni upi wingi wa: Kiazi kilipikwa kikaiva? 
    1. Viazi zilipikwa zikaiva. 
    2. Viazi vilipikwa vikaiva. 
    3. Kiazi zilipikwa zikaiva. 
    4. Viazi ilipikwa ikaiva.
  5. Chagua neno ambalo halipo katika ngeli ya LI-LI. 
    1. Jani.
    2. Joto!
    3. Jua
    4. Jasho.
  6. Mchungwa huzaa machungwa. Mnazi huzaa
    1. nanasi.
    2. minazi
    3. mnanasi.
    4. nazi
  7. Kamilisha methali ifuatayo: Mtoto umleavyo ndivyo
    1. akuavyo. 
    2. akuwapo
    3. achezavyo.
    4. aliavyo
  8. Bendera ya taifa letu inazo rangi ngapi? 
    1. Tano.
    2. Nne
    3. Tatu.
    4. Mbili
  9. Mstari mmoja katika ubeti wa shairi huitwa
    1. mshororo
    2. sentensi
    3. mizani
    4. kibwagizo
  10. Wazazi wachache tu ndio waliofika mkutanoni. Neno lililopigiwa mstari ni
    1. kielezi.
    2. kiunganishi.
    3. kiwakilishi
    4. kivumishi.

MARKING SCHEME

swa ms timer

Join our whatsapp group for latest updates

Download Kiswahili Questions and Answers - Grade 4 End of Term 3 November 2022 Exams Set 2.


Tap Here to Download for 30/-




Why download?

  • ✔ To read offline at any time.
  • ✔ To Print at your convenience
  • ✔ Share Easily with Friends / Students